Mafundisho na Maagano 2021
Maelekezo kwa ajili ya Wakati wa Kuimba


“Maelekezo kwa ajili ya Wakati wa Kuimba na Maonyesho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Maelekezo kwa ajili ya Wakati wa Kuimba,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi: 2021

Picha
watoto wakiimba

Maelekezo kwa ajili ya Wakati wa Kuimba na Maonyesho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti

Wapendwa Marais wa Msingi na Viongozi wa Muziki,

Nyimbo za watoto wa Msingi ni zana yenye nguvu sana katika kuwasaidia watoto kujifunza kuhusu mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni na ni kweli za msingi za injili ya Yesu Kristo. Wakati watoto wanaimba kuhusu kanuni za injili, Roho Mtakatifu atashuhudia juu ya ukweli wa kanuni hizo. Maneno na muziki vitakaa katika akili na mioyo ya watoto maisha yao yote.

Tafuta msaada wa Roho unapojiandaa kufundisha injili kupitia muziki. Toa ushuhuda wako juu ya kweli mnazoziimba. Wasaidie watoto kuona jinsi muziki unavyoshabihiana na kile wanachopitia na kujifunza nyumbani na katika madarasa ya Msingi. Watoto na familia zao watabarikiwa kwa juhudi zako za dhati.

Tunawapenda na tunatoa shukrani zetu kwa huduma ya kujitolea ambayo mnatoa ili kuwaimarisha na kuwalinda watoto wetu wa thamani.

Urais Mkuu wa Msingi

Maelekezo kwa ajili ya Maonyesho Kwenye Mkutano wa Sakramenti

Chini ya uelekezi wa askofu, maonyesho ya watoto kwenye mkutano wa sakramenti kwa kawaida hufanyika katika robo ya nne ya mwaka. Urais wa Msingi na kiongozi wa muziki, wanapanga kukutana mapema katika mwaka pamoja na mshauri katika uaskofu mwenye kusimamia Msingi ili kuanza kujadili mipango ya maonyesho. Unapomaliza mipango, pata ruhusa yake kwa ajili ya maonyesho hayo.

Maonyesho yanapaswa kuwaruhusu watoto kuonesha kile ambacho wao na familia zao wamejifunza kuhusu injili ya Yesu Kristo kutoka katika Mafundisho na Maagano nyumbani na katika Msingi, ikijumuisha nyimbo za Msingi walizoimba katika kipindi chote cha mwaka. Kwa sala fikiria kanuni zipi za injili na nyimbo zinasaidia kile ambacho wamejifunza. Katika mwaka mzima, weka kumbukumbu ya hotuba za watoto na matukio binafsi kwa ajili ya matumizi wakati wa maonyesho. Waalike watoto kushiriki maandiko, hadithi, na shuhuda zao za Mwokozi na injili Yake katika maonyesho hayo. Wakati ukipanga maonyesho, fikiria njia ambazo maonyesho yanaweza kusaidia mkusanyiko kulenga kwa Mwokozi na kweli Alizorejesha katika siku za mwisho.

Matawi yenye idadi ndogo ya watoto yanaweza kufikiria njia ambazo wanafamilia wanaweza kushiriki pamoja na watoto wao. Mshiriki wa uaskofu anaweza kuhitimisha mkutano kwa hotuba fupi.

Wakati ukiandaa maonyesho, kumbuka mwongozo ufuatao:

  • Mazoezi yasichukue muda usio wa lazima kutoka kwenye madarasa ya Msingi au familia.

  • Vitu vya kuona, mavazi ya maonyesho, na njia za mawasiliano havifai kwa ajili ya mkutano wa sakramenti

Ona Handbook 2: Administering the Church, 11.5.3, ChurchofJesusChrist.org.

Maelekezo kwa ajili ya Wakati wa Kuimba

Dakika 5 (Urais wa Msingi): Sala ya kufungua, andiko au makala ya imani, na hotuba moja

Dakika 20 (kiongozi wa muziki): Muda wa kuimba

Makusudi ya wakati wa kuimba ni kuwasaidia watoto kuongeza imani yao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa njia ya Muziki. Urais wa Msingi na kiongozi wa muziki huchagua nyimbo kwa ajili ya kila mwezi wakiwa na kusudi hilo akilini mwao. Nyimbo hizo zinapaswa ziimarishe kanuni ambazo watoto wanajifunza kuhusu injili ya Yesu Kristo katika madarasa yao na nyumbani. Orodha ya nyimbo ambazo zinaimarisha kanuni hizi imejumuishwa katika mwongozo huu. Nyimbo hizi pia zimependekezwa katika mihtasari kwenye Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Unapofundisha nyimbo kwa watoto, waalike kuelezea kile ambacho tayari wamejifunza kuhusu hadithi na kanuni za mafundisho zifundishwazo na nyimbo. Ukitaka unaweza kurejea mihutasari ya Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi ambayo watoto wanajifunza katika madarasa yao. Hii itakusaidia kuzijua hadithi na kanuni ambazo wanajifunza ili kwamba uweze kufikiria jinsi ya kuwasaidia kujifunza kupitia muziki.

Wakati wa kuimba, unaweza pia kurejea nyimbo ambazo watoto walishajifunza hapo awali na nyimbo wanazofurahia kuziimba. Wakati ukifanya marejeo, waalike watoto kutoa mawazo na hisia zao kuhusu kweli zinazopatikana katika nyimbo.

Kitabu cha Nyimbo za Watoto ni nyenzo ya msingi ya muziki katika Msingi. Nyimbo kutoka kitabu cha nyimbo za Kanisa na nyimbo kutoka kwenye gazeti la Friend na Liahona pia zinafaa. Mara chache watoto wanaweza kuimba nyimbo za kizalendo au za sikukuu ambazo zinafaa kwa ajili ya Jumapili na kwa umri wa watoto. Matumizi ya muziki wowote tofauti kwenye Msingi lazima yaidhinishwe na uaskofu (ona Handbook 2: Administering the Church, 11.2.4).

Picha
watoto wakiimba katika mkutano wa sakramenti

Muhtasari wa Msingi

Kila wiki, Msingi hujumuisha:

Muda wa kuimba:Dakika 25

Mapumziko:Dakika 5

Madarasa:Dakika 20

Viongozi wa Msingi wenye idadi kubwa ya watoto wanaweza kuwagawa katika makundi mawili na kuwa na kundi moja katika madarasa ya Msingi wakati kundi lingine wakiwa katika wakati wa kuimba. Kisha makundi mawili haya yangeweza kubadilishana nafasi. Katika hali kama hiyo, viongozi wa darasa la Msingi wanaweza kuhitaji kubadilisha muda uliooneshwa hapo juu ili kuendana na hali yao.

Muziki kwa ajili ya Wakati wa Kuimba

Januari

  • Sala ya Kwanza ya Joseph Smith,” Nyimbo za Kanisa, na. 26

  • Search, Ponder, and Pray,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109

  • Family History—I Am Doing It,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 94

Februari

  • I Want to Be a Missionary Now,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 168

  • The Priesthood Is Restored,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 89

  • I Stand All Amazed,” Nyimbo za Kanisa, na. 193

Machi

  • The Church of Jesus Christ,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77

  • When I Am Baptized,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103

  • When He Comes Again,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83

Aprili

  • Jesus Has Risen,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 70

  • I Want to Be a Missionary Now,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 168

  • Jesus Said Love Everyone,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 61

Mei

Juni

  • I’m Trying to Be like Jesus,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79

  • Reverence Is Love,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 31

  • Help Me, Dear Father,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 99

Julai

Agosti

  • The Priesthood Is Restored,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 89

  • The Holy Ghost,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 105

  • I am a Child of God,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3

Septemba

  • Reverently, Quietly,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 26

  • I Am like a Star,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 163

  • I Will Be Valiant,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 162

Oktoba

  • The Spirit of God,” Nyimbo za Kanisa, na. 2

  • I Love to See the Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95

  • The Church of Jesus Christ,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77

Novemba

  • Family History—I Am Doing It,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 94

  • Families Can Be Together Forever,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188

  • Praise to the Man,” Nyimbo za Kanisa, na. 27

Desemba

  • I Will Follow God’s Plan,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 164–65

  • He Sent His Son,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35

  • Hark! The Herald Angels SingNyimbo za Kanisa, na. 209

Kutumia Muziki ili Kufundisha Mafundisho

Kumbuka kwamba makusudi ya wakati wa kuimba sio tu kuwafundisha watoto jinsi ya kuimba, bali ni kutumia muziki ili kuwasaidia kuongeza imani yao katika Mungu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Mawazo yafuatayo yanaweza kukupa mwongozo wa kiungu wakati ukipanga njia za kufanya hili.

Jifunze juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Waalike watoto kuelezea kile wanachojifunza kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kutokana na nyimbo mnazoimba. Waalike watoto kutaja maneno yao wayapendayo kutoka kwenye wimbo unao mwelezea Mungu na Mwokozi.

Soma maandiko yanayohusiana. Kwa nyimbo nyingi katika Kitabu cha Nyimbo za Watoto na kitabu cha nyimbo za kanisa, marejeleo kwa ajili ya maandiko yameorodheshwa. Wasaidie watoto kusoma kipengele cha maandiko, na kuzungumza kuhusu jinsi kinavyohusiana na wimbo mnaoimba. Ungeweza pia kuorodhesha marejeleo machache ya maandiko ubaoni na waalike watoto kulinganisha kila rejeleo na wimbo au mstari kutoka kwenye wimbo.

Jaza nafasi zilizo wazi. Andika mstari wa wimbo ubaoni kwa kuacha baadhi ya maneno muhimu. Kisha waombe watoto kuimba wimbo, na kusikiliza maneno ambayo yatajaza nafasi zilizoachwa wazi. Wakati wakijaza kila nafasi iliyo wazi, jadili kanuni zipi za injili mnajifunza kutokana na maneno yanayokosekana.

Picha
watoto wakiimba katika mkutano wa sakramenti

Dondoo kutoka kwa Viongozi wa Kanisa. Waalike watoto kusikiliza dondoo kutoka kwa kiongozi wa Kanisa ambayo hufundisha kanuni sawa ya injili kama ile iliyoko kwenye wimbo wa Msingi. Waombe kunyanyua mikono yao wakati wanaposikia kitu ambacho huwasaidia wao kuelewa ukweli ambao wanauimba. Waalike kuelezea kile walichosikia.

Toa ushuhuda. Toa ushuhuda mfupi kwa watoto kuhusu kweli za injili zinaopatikana kwenye wimbo wa Msingi. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kuimba ni njia mojawapo wanayoweza kutoa ushuhuda na kumhisi Roho.

Simama kama shahidi. Waalike watoto kufanya zamu kusimama na kuelezea kile wanachojifunza kutoka kwenye wimbo wanaoimba au jinsi wanavyohisi kuhusu kweli zilizofundishwa katika wimbo. Waulize wanahisi vipi wakati wanapoimba wimbo, na wasaidie kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu.

Tumia picha. Waombe watoto wakusaidie kupata au kutengeneza picha ambazo zinaendana na maneno muhimu au vifungu vya maneno katika wimbo. Waalike kueleza ni jinsi gani picha zinahusiana na wimbo na kile ambacho wimbo unafundisha. Kwa mfano, kama unafundisha wimbo “When He Comes Again” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83), ungeweka picha kote chumbani ambazo zinaonesha maneno muhimu kutoka kwenye wimbo (kama vile malaika, theluji, na nyota). Waombe watoto kukusanya picha na kuzinyanyua juu katika utaratibu sahihi wakati mkiimba wimbo kwa pamoja.

Shiriki somo la vitendo. Ungeweza kutumia vitendo ili kuhamasisha mjadala kuhusu wimbo. Kwa mfano, wimbo “When I Am Baptized” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103) unataja mvua. Ungeweza kuwaonesha watoto picha ya mvua au glasi ya maji na ongelea kuhusu jinsi ubatizo na Roho Mtakatifu vinavyosafisha roho zetu kama maji ya mvua yanavyosafisha dunia; hii ingeweza kuongoza kwenye mjadala kuhusu kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Alika kuelezea uzoefu binafsi. Wasaidie watoto kuunganisha kanuni zilizofundishwa kwenye wimbo na uzoefu ambao wamekuwa nao wa kanuni hizo. Kwa mfano, kabla ya kuimba “I Love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95), ungeweza kuwaomba watoto kuinua mikono yao kama wamewahi kuona hekalu. Waalike kufikiria wakati wakiimba kuhusu jinsi wanavyoweza kuhisi wanapoliona hekalu.

Uliza maswali. Kuna maswali mengi ambayo unaweza kuuliza wakati mnaimba nyimbo. Kwa mfano, unaweza kuwauliza watoto wanajifunza nini kutoka kwenye kila mstari wa wimbo. Pia unaweza kuwaomba kufikiria maswali ambayo yanajibiwa na wimbo. Hii inaweza kupeleka kwenye majadiliano kuhusu kweli zinazofundishwa katika wimbo.

Sikiliza majibu. Waombe watoto kusikiliza majibu ya maswali. Kwa mfano, wimbo “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35) una maswali na majibu kadhaa. Ungeweza kuwauliza watoto maswali na kisha wasikilize majibu wakati wakiimba.

Kuwasaidia Watoto Kujifunza na Kukumbuka Nyimbo za Msingi

Watoto hujifunza wimbo kwa kusikiliza na kuimba tena na tena. Mara zote yaimbe maneno ya wimbo mpya kwa watoto—usiyasome tu au kuyakariri. Hii huwasaidia watoto kuunganisha sauti ya muziki na maneno. Baada ya wimbo kufundishwa, urejee wimbo katika njia tofauti za kufurahisha kwa mwaka mzima. Chini ni baadhi ya mawazo ya kuwasaidia watoto kujifunza na kurejea nyimbo.

Onesha kwa mfano mpangilio wa sauti. Ili kuwasaidia watoto kujifunza sauti ya muziki wa wimbo, weka mkono wako kwa upana, na wakati ukiimba maneno, peleka mkono wako juu kuonesha sauti ya juu na chini kuonesha sauti ya chini.

mwangwi. Waalike watoto kuwa mwangwi wa sauti yako kwa kurudia kile unachokiimba. Waimbie watoto kifungu kifupi cha maneno au mstari, kisha waache waimbe kwa kurudia.

Tumia njia tofauti tofauti. Imba nyimbo katika njia tofauti tofauti, kama vile kwa kunong’ona, kwa kutotoa maneno, kwa kupiga makofi mapigo ya muziki, kwa kubadilisha kasi ya muziki, au kuimba ukiwa umekaa au kusimama. Pia ungeweza kutengeneza mchemraba kwa karatasi na, kwenye kila upande wa mchemraba, andika njia tofauti ya kuimba. Mwalike mtoto kuzungusha mchemraba kuchagua njia gani watoto wataimba wimbo.

Imba katika makundi. Lipe kila darasa au mtu mmoja mmoja kifungu cha maneno cha kuimba wakati amesimama, na kisha waache wabadilishane vifungu hivyo mpaka kila darasa au kila mtu awe amepata kuimba kila kifungu cha maneno.

Tumia matendo. Waalike watoto kufikiria kuhusu matendo rahisi ili kuwasaidia kukumbuka maneno na ujumbe wa wimbo. Kwa mfano, unapoimba “Reverently, Quietly” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 26), ungeweza kuwaalika watoto kukunja mikono yao, kuinamisha vichwa vyao, na kugusa mioyo yao wakati wanapoimba mistari husika katika wimbo.

Wasichana wanaimba, wavulana wanaimba. Chora picha ya mvulana na picha ya msichana. Wakati ukiupitia upya wimbo, inua mojawapo ya picha kuonesha nani anatakiwa kuimba sehemu hiyo ya wimbo.

Kikapu cha kurushia vitu. Weka vikapu au vyombo vingine vyenye namba mbele ya darasa—vyombo vingi kulingana na idadi ya beti za wimbo fulani. Mwalike mmoja wa watoto kurusha kifuko chenye mbegu au karatasi iliyokunjwa ndani ya au karibu na chombo chenye namba. Waache watoto waimbe ubeti wenye namba sawa na ile iliyo kwenye chombo.

Oanisha picha na kifungu cha maneno. Andika kila mstari wa wimbo kwenye kipande tofauti cha karatasi, na kisha tafuta picha ambayo inawakilisha kila mstari. Weka picha kwenye upande mmoja wa chumba na karatasi upande mwingine. Imba wimbo, na waombe watoto kuoanisha picha na maneno.

Tengeneza mabango. Onesha mabango yakiwa na maneno kutoka kwenye kila mstari au picha ambayo huwakilisha maneno. Wakati watoto wakiimba, funika baadhi ya maneno au picha mpaka waweze kuimba mstari mzima bila bango. Pia unaweza kuwaalika watoto kukusaidia kutengeneza mabango.

Chapisha