Njoo, Unifuate
Agosti 12–18. Warumi 7–16: ‘Ushinde Ubaya kwa Wema’


Agosti 12–18. Warumi 7–16: ‘Ushinde Ubaya kwa Wema’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

Agosti 12–18. Warumi 7–16,“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Roma

Agosti 12–18

Warumi 7–16

“Ushinde Ubaya kwa Wema”

Unaposoma Warumi 7–16, andika mawazo yo yote unayopokea kuhusu jinsi gani unavyoweza kuwafundisha watoto ukweli uliomo katika sura hizi.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waulize watoto kama walishiriki na familia zao kitu fulani walichojifunza darasa la msingi wiki iliyopita. (Unaweza kuhitaji kwa kifupi kurejea somo la wiki iliyopita.) Kama ni hivyo, walishiriki nini?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Warumi 8:35–39

Baba yangu wa Mbinguni ananipenda.

Unawezaje kutumia maneno ya Paulo kuwafundisha watoto kwamba Baba wa Mbinguni siku zote atawapenda?

Picha
baba akicheza dansi na binti

Mungu wa Mbinguni anawapenda watoto Wake wote.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kukariri kirai “[Hakuna kinachoweza] kututenganisha sisi kutoka upendo wa Mungu” (Warumi 8:39). Kuonyesha ukweli huu, pigilia misumari mbao mbili pamoja, na mojawapo weka alama “sisi” na nyingine “upendo wa Mungu.” Waache watoto waone kama wanaweza kutenganisha hizo mbao.

  • Wapeleke watoto nje kuhisi mwanga wa jua au waonyeshe picha ya jua. Ni kwa jinsi gani jua linafanana na upendo wa Baba wa Mbinguni? Wasaidie kuona kwamba ingawa jua liko mbali sana, linaweza kutusaidia kuhisi joto. Tunaweza kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni wakati wote, ingawa hayupo nasi kimwili. Mnaweza pia kuimba pamoja “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29).

Warumi 10:17

Imani huja kwa kusikia neno la Mungu.

Watoto wanaposikia neno la Mungu na kulisikiliza kwa makini imani yao katika Mungu itakua. Unawezaje kuwasaidia waelewe umuhimu wa kusikiliza neno la Mungu?

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto Warumi 10:17, na uwaonyeshe picha za hali ambazo wanaweza kusikia neno la Mungu (kama vile kujifunza maandiko kifamilia, Kanisani, au Mkutano Mkuu; ona ukurasa wa shughuli za wiki hii). Waulize watoto ni lini walisikia neno la Mungu.

  • Simulia hadithi kuhusu mtoto anayesikiliza neno la Mungu katika njia mbalimbali. Wakati unaposimulia hadithi, puliza puto kidogo kidogo kuonyesha jinsi imani ya mtoto inavyokua kila wakati anaposikia neno la Mungu.

  • Kuwasaidia watoto kuelewa kwamba imani yao inaweza kukua, wasaidie kuimba “Imani” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96–97). Wanapoimba, waombe wajifanye kuwa mbegu kwa kuchuchumaa chini. Kila wakati wanapoimba neno imani, waambie wainuke kidogo kama mmea unaokua.

  • Ficha katika darasa seti ya maandiko, picha ya Rais wa Kanisa, na nakala ya majarida ya the Friend au Liahona . Waombe watoto watafute vitu hivi na kushiriki jinsi kila kimoja kinavyofanya iwezekane kwa sisi kusikia neno la Mungu.

Warumi 16:1–4

Ninaweza kusema asante kwa hao wanaonisaidia.

Paulo alikuwa na shukrani kwa watu waliomsaidia. Unaweza kuwasaidia watoto kutambua mambo ya ukarimu watu wengine wanayofanya kwa ajili yao na kukumbuka kuwashukuru.

Shughuli Yamkini

  • Eleza kwamba Paulo alikuwa na shukrani kwa msaada alioupata kutoka kwa mwanamke aliyeitwa Fibi na wanandoa walioitwa Prisila na Akila (ona Warumi 16:1–4). Waombe watoto wachore picha za Paulo na watu hawa watatu unaposhiriki maneno na virai kutoka kwenye aya.

  • Muombe kila mtoto ashiriki kitu fulani kizuri ambacho mtu fulani alikifanya kwa ajili yake hivi karibuni. Wasaidie watoto kutengeneza kadi za asante sana kwa ajili ya watu hao.

  • Wasaidie watoto kujifunza jinsi ya kusema asante sana katika lugha tofauti. Wimbo “Children All Over the World” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 16–17) unaweza kusaidia.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Warumi 8:16–18

Baba wa Mbinguni ananitaka mimi kujitayarisha kupokea vyote ambavyo anavyo.

Mpango wa Baba wa Mbinguni unafanya iwezekane kwa ajili yetu kuwa kama Yeye na kurithi vyote ambavyo anavyo. Ukweli huu unaweza kuvutia watoto unaowafundisha kuishi injili kwa imani zaidi.

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Warumi 8:16–18. Tunajifunza nini kutoka kwenye aya hizi kuhusu sisi ni kina nani na tunaweza kuwa nani? Eleza kwamba “mrithi” ni mtu anayerithi, au kupokea, kile wazazi wake walichonacho. Andika ubaoni Tunahitaji kufanya nini ili kurithi vyote ambavyo Baba yetu wa Mbinguni anavyo? Imbeni pamoja wimbo kuhusu utiifu, kama vile “I will Follow God’s Plan for Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto 164–165)), mkitafuta majibu. Ni majibu gani mengine watoto wanaweza kufikiria?

  • Waombe watoto kufikiria kuhusu mfalme anayetaka wana na mabinti zake kutawala katika himaya yake siku moja. Elezea kwamba Baba wa Mbinguni ni kama mfalme, na sisi ni wana na mabinti zake wa kifalme. Unaweza kushiriki hadithi ya mwana wa Mfalme Louis wa XVI wa Ufaransa, inayopatikana katika hotuba ya Dada Elaine S. Dalton “Kumbuka Wewe ni Nani!” (Ensign au Liahona, Mei 2010, 121). Je, ni kwa jinsi gani kuweza kukumbuka kwamba sisi ni watoto wa Baba wa Mbinguni na tumezaliwa ili siku moja tuwe kama Yeye kunatusaidia kuishi kwa haki hapa duniani? (Kwa taarifa zaidi, ona True to the Faith, 74–76.)

Warumi 10:17

Imani huja kwa kusikia neno la Mungu.

Watoto wana nafasi nyingi za kusikia neno la Mungu. Wasaidie kuona namna gani kusikia neno la Mungu kunaweza kuimarisha imani yao.

Shughuli Yamkini

  • Andika sentensi ifuatayo ubaoni: chanzo chake ni , na huja kwa la . Waombe watoto wajaze mapengo baada ya kusoma Warumi 10:17. Shiriki muda ambapo mtu fulani alipofundisha ukweli wa injili ambao ulisaidia kuimarisha imani yako—labda ungeshiriki maandiko unayoyapenda au nukuu kutoka mkutano mkuu. Waalike watoto kushiriki uzoefu wao.

  • Weka alama glasi kadhaa za maji kwa vitu ambavyo kwavyo tunapata neno la Mungu (kama maandiko, mikutano ya Kanisa, na mkutano mkuu). Jadili ni kwa jinsi gani neno la Mungu linaongeza imani yetu unapomimina kila glasi katika chombo chenye kitambulisho “Imani.”

  • Mpe mtoto mmoja picha ya Mwokozi akimponya mtu bila kuruhusu watoto wengine kuona picha hiyo. Muombe mtoto kutoa ishara kuwasaidia watoto wengine kukisia picha inaonyesha nini. Tunawezaje kushiriki na wengine nini tunajua kuhusu Mwokozi ili waweze kuwa na imani katika Yeye?

Warumi 14:10, 13

“Acha tusizidi … kuhukumiana.”

Wakati watoto wanaongea na wengine wanaofanya chaguzi tofauti kuliko wanavyofanya wao, wanaweza kushawishiwa kuwa watoa hukumu. Fikiria jinsi ushauri wa Paulo kwa Warumi unaweza kuwasaidia kuepuka hukumu kama hiyo.

Shughuli Yamkini

  • Mwalike mtoto asome Warumi 14, 13. Waombe watoto wengine kuhesabu ni mara ngapi Paulo alitumia neno hukumu. Nini maana ya kumhukumu mtu? Kwa nini tunapaswa kuepuka kuwahukumu wengine?

  • Onyesha picha ya mtu, na waulize watoto sisi tunajua nini kuhusu mtu huyu kwa kutazama picha yake tu. Je, baadhi ya vitu gani sisi hatuvijui kumhusu yeye? Kwa nini Bwana ni mtu sahihi zaidi kumhukumu mtu huyu? (Ona 1 Samweli 16:7).

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waombe watoto wachague shughuli moja mliyofanya kama darasa na waifanye pamoja na familia zao. Waambie kwamba wiki ijayo wanaweza kushiriki kile walichofanya.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Washirikishe watoto katika majadiliano ya injili. Unaweza ukataka kufikiria juu ya kutengeneza njia za ubunifu za kuwashirikisha watoto wadogo katika majadiliano ya injili. Wakati mwingine unaweza kufanya kitu fulani kidogo kama kualika watoto kukaa kwenye duara sakafuni badala ya kwenye viti vyao.

Chapisha