Njoo, Unifuate
Julai 29–Agosti 4. Matendo ya Mitume 22–28: ‘Mtumishi na Shahidi’


“Julai 29–Agosti 4. Matendo ya Mitume 22–28: ‘Mtumishi na Shahidi’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Julai 29–Agosti 4. Matendo ya Mitume 22-28,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Paulo gerezani

Julai 29–Agosti 4

Matendo ya Mitume 22–28

“Mtumishi na Shahidi”

Unaposoma maelezo kutoka utumishi wa Mtume Paulo katika Matendo ya Mitume 22–28, tafuta kanuni ambazo zitakuwa na maana kwa watoto unaowafundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha za chumba cha gereza, boti, na nyoka. Waalike watoto kushiriki hadithi zozote wanazojua kuhusu Paulo zinazohusiana na picha hizi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Matendo ya Mitume 23:10–11

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanajali kuhusu mimi na watanisaidia wakati wa shida.

Kujifunza kuhusu jinsi Mwokozi alivyomsaidia Paulo kunaweza kuwasaidia watoto kujua kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanawajali.

Shughuli Yamkini

  • Shiriki hadithi katika Matendo ya Mitume 23:10–11 ya Mwokozi akimtembelea Paulo gerezani. Au onyesha video “Uwe na Moyo Mkuu” (LDS.org), ambayo inasimulia hadithi hii. Simulia wakati ambapo ulikuwa na majaribu na ukapokea mwongozo na faraja kutoka kwa Mungu. Waombe watoto kushiriki nyakati walipohisi kufarijiwa na Mungu.

  • Wasaidie watoto kukariri kile Yesu alichosema kwa Paulo: “Uwe na moyo mkuu.” Waombe watoto kufikiria juu ya mtu ambaye wanaweza kumwalika kuwa na moyo mkuu—labda mtu fulani ambaye ana huzuni au wasiwasi.

Matendo ya Mitume 26:1—29

Naweza kushiriki ushuhuda wangu pamoja na wengine.

Kurudia ushuhuda wa Paulo mbele ya Mfalme Agripa kunaweza kuwasaidia watoto kujifunza jinsi ya kushiriki kile wanachojua kuwa ni kweli.

Shughuli Yamkini

  • Lete taji darasani na mwache mtoto aivae na ajifanye kuwa Mfalme Agripa. Mwalike mtoto mwingine asimame mbele ya mfalme kumwakilisha Paulo unapofanya muhtasari wa ushuhuda wa Paulo na majibu ya Mfalme Agripa, yanayopatikana katika Matendo ya Mitume 26:1—29 (ona ”Sura 63: Paulo anamaliza utumishi wake,” Hadithi za Agano Jipya, 162—66, au video inayofanana katika LDS.org). Elezea kwamba tunaweza kushiriki shuhuda zetu na wengine, kama alivyofanya Paulo.

  • Waombe watoto kusikiliza wakati unaimba au kusoma wimbo kuhusu ushuhuda , kama vile aya ya 2 ya “Ushuhuda (Nyimbo no. 137) au Najua Baba Yangu Anaishi” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 5). Waalike watoto wainue mikono yao wanaposikia kitu wanachoweza kukitolea ushuhuda. Unaweza kutaka kuimba wimbo mara kadhaa; waalike watoto kujiunga mawe mara wanapoyazoea maneno yake. Waombe kushiriki baadhi ya vitu kuhusu injili ambavyo wanajua ni vya kweli.

  • Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kufikiria kuhusu kitu wanachoweza kusema wakati wanatoa ushuhuda wao. Waalike kushiriki ushuhuda wao na mtu fulani katika familia yao.

Matendo ya Mitume 27

Manabii wananionya juu ya hatari

Fikiria jinsi hadithi ya Paulo ya maangamizi ya meli baharini yanavyoweza kufundisha watoto kwamba manabii wanaona hatari ambazo sisi hatuwezi kuziona.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wajifanye kwamba wapo ndani ya meli ambayo inaangamia katika dhoruba. Soma onyo la Paulo kwa watu, linalopatikana katika Matendo ya Mitume 27:9—10, na shiriki hadithi ya maangamizi ya meli baharini ambayo yalitokea kwa sababu hawakusikiliza onyo lake (ona aya 11, 39—44). Onyesha picha ya Rais wa Kanisa. Je, ni aina gani ya maonyo anayotupa sisi?

  • Weka picha kadhaa au vitu chumba kizima ambavyo vinawakilisha vitu ambavyo manabii wametufundisha kufanya, kama vile kuhudhuria Kanisani au kubatizwa. Kama darasa, tembeeni kuzunguka chumba, mkisimama kwenye kila picha au kitu ili kuzungumzia kuhusu jinsi gani kufuata mafundisho ya nabii kunatusaidia kutuweka salama.

Picha
Rais Thomas S. Monson

Kufuata mafundisho ya nabii kunasaidia kutuweka salama.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Matendo ya Mitume 23:10—11; 27:18—26; 28:1—6

Wakati ninapokabiliana na dhiki Mungu hanitelekezi.

Wakati wote wa majaribu ambayo Paulo alipitia, Bwana alikuwa pamoja naye. Je, unawezaje kuwasaidia watoto kulinganisha uzoefu wa Paulo na maisha yao?

Shughuli Yamkini

  • Ukitumia Matendo ya Mitume 23:10, eleza kwamba Paulo aliwekwa gerezani kwa sababu aliwafundisha watu kuhusu Yesu. Kisha soma Matendo ya Mitume 23:11 pamoja na watoto. Au onyesha video “Uwe na Moyo Mkuu” (LDS.org), ambayo inasimulia hadithi hii. Kwa nini Paulo “angekuwa na moyo mkuu” hata kama alikuwa gerezani?

  • Andika ubaoni Matendo ya Mitume 23:10—11; Matendo ya Mitume 27:18—26; na Matendo ya Mitume 28:1—6. Onyesha picha za gereza, meli, na nyoka, na waalike watoto kurejea aya hizi na kuzifananisha na picha. Katika kila moja ya maelezo haya, Bwana alimwonesha vipi Paulo kwamba Alikuwa pamoja naye?

  • Mwombe mtu fulani kutoka kwenye kata kushiriki uzoefu wakati Bwana alikuwa pamoja naye wakati wa matatizo. Pengine wewe au watoto mnaweza pia kushiriki uzoefu wenu.

Matendo ya Mitume 26:1—29

Ninaweza kutoa kwa ujasiri ushuhuda wangu juu ya Yesu Kristo.

Ujasiri wa Paulo katika kushiriki ushuhuda wake unaweza kuwasaidia watoto kuwa wajasiri wakati wanaposhiriki shuhuda zao.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kusoma Matendo ya Mitume 26:1—29 na kuzitafuta baadhi ya kweli za injili ambazo Paulo alimfundisha Mfalme Agripa. Kwa nini ingeweza kuogofya kwa Paulo kushiriki vitu hivi mbele ya Mfalme? Waalike watoto kuorodhesha baadhi ya kanuni za injili wanazojua kuwa za kweli. Waombe wamfikirie mtu fulani wanayemjua anayehitaji kusikia ushuhuda wao juu ya kweli hizi.

  • Waalike watoto kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuandika kitu ambacho wangeweza kusema katika ushuhuda wao.

Matendo ya Mitume 27

Manabii wananionya juu ya hatari.

Watoto wanaweza kusikiliza jumbe za manabii wa sasa na kutambua maonyo yao. Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujifunza jinsi ya kusikiliza maonyo hayo?

Shughuli Yamkini

  • Kata vipande vya karatasi vyenye umbo kama meli katika vipande vya fumbo. Waalike watoto kuandika maonyo ya Paulo katika Matendo ya Mitume 27:9–11 kwenye vipande hivyo na kuweka fumbo pamoja. Kwa nini watu hawakumsikiliza Paulo? (ona aya ya 11). Waalike watoto wasome aya ya 18—20 na 40—44 ili kujua kile kilichotokea kama matokeo. (Eleza kwamba kwa sababu watu walifuata ushauri wa mwisho wa Paulo kubaki kwenye meli, hakuna hata mmoja aliyekufa katika maangamizi hayo ya meli baharini; ona aya ya 30—32.) Ni nini tunaweza kujifunza kutoka kwenye uzoefu huu kuhusu kumfuata nabii.

  • Leta ujumbe wa hivi karibuni wa mkutano mkuu wa Rais wa Kanisa na shiriki pamoja na watoto maonyo yoyote au ushauri alioutoa. Waalike watoto kufikiria njia wanazoweza kumfuata nabii.

  • Onyesha video “Waliobarikiwa na Wenye Heri ni Wale Wanaoshika Amri za Mungu” (LDS.org). Ni kwa jinsi gani manabii ni kama mtu mwenye darubini?

  • Andika shughuli chache kwa watoto wanazoweza kufanya ambazo zitawasaidia kujifunza kuhusu wajibu wa nabii—kwa mfano, “Soma Mafundisho na Maagano 21:4–7” au “Imba ‘Mfuate Nabii’” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11, au tumia wimbo mwingine kuhusu manabii). Tundika orodha ya shughuli nje ya darasa, na mwalike mtoto mmoja asimame mlangoni na kusoma shughuli moja moja kwa watoto wote darasani, ukiwaruhusu kukamilisha shughuli kabla ya kusoma nyingine. Eleza kwamba jinsi mtoto mmoja alivyoweza kutoa maelekezo kwa wengine, viyo hivyo nabii anatufundisha kile ambacho Mungu angependa sisi tufanye. Waombe watoto kushiriki kile walichojifunza kuhusu manabii kutoka kwenye shughuli hizo.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waombe watoto kutumia kile walichojifunza kuhusu Paulo ili kuzihimiza familia zao kujifunza ujumbe wa nabii wa hivi karibuni na kujadili jinsi wanavyoweza kufuata ushauri wake.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Husisha milango ya hisi. “Watoto wengi (na watu wazima) wanajifunza vyema zaidi wakati milango mingi ya hisi inapohusishwa. Tafuta mbinu za kuwasaidia watoto watumie mlango wa kuona, kusikia, na kugusa wanapojifunza. Katika hali zingine, unaweza hata kupata njia za kujumuisha mlango wa kunusa na kuonja!” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

Chapisha