Njoo, Unifuate
Novemba 4–10. Waebrania 1–6: ‘Yesu Kristo, ‘Sababu ya Wokovu wa Milele’’


“Novemba 4–10. Waebrania 1–6: ‘Yesu Kristo,‘Sababu ya Wokovu wa Milele’’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Novemba 4–10. Waebrania 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Kristo amesimama pamoja na msichana na mwanaume

Marhamu ya Gilead, na Anne Henrie

Novemba 4–10

Waebrania 1–6

Yesu Kristo, “Sababu ya Wokovu wa Milele”

Ni ukweli gani unaupata katika Waebrania 1–6 ambao unahisi mwongozo wa kiungu wa kuufundisha kwa watoto? Kuwa makini na ushawishi wa Roho ambao unakujia wakati unapojitayarisha, na hakikisha unaandika chini.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Je, watoto walikubali mwaliko mwishoni mwa somo la wiki iliyopita ili kutafuta mstari wa maandiko wanaoweza kushiriki? Kama ndivyo, wape muda wa kuishiriki. Kama sivyo, wasaidie kufikiria kitu kingine walichojifunza kutoka maandiko hivi karibuni ili waweze kushiriki.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Waebrania 1:2–10; 2:8–10, 17–18

Ninaamini katika Yesu Kristo.

Mistari hii inaweza kuwasaidia watoto kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo na kuimarisha uhusiano wao na Yeye.

Shughuli Yamkini

  • Ukitumia maneno yako, andika kwenye vipande vya karatasi ukweli kuhusu Yesu Kristo ambao unaupata katika Waebrania 1:2–10; 2:8–10, 17–18, na zifiche kote chumbani. Waalike watoto kuvitafuta vipande hivyo vya karatasi. Wasaidie kusoma ukweli ulioandikwa kwenye karatasi, na ongelea juu ya ukweli huo unamaanisha nini. Kama inahitajika, eleza kwamba Yesu Kristo anaitwa Mwana wa Mungu kwa sababu Baba wa Mbinguni ni baba wa vyote roho Yake na Mwili Wake.

  • Pitisha picha ya Mwokozi chumbani, na wacha kila mtoto ashiriki kwa nini yeye anamshukuru Yesu Kristo wakati anashikilia picha hiyo.

Waebrania 3:8

Baba wa Mbinguni anatutaka “kutoshupaza mioyo [yetu].”

Waebrania 3 inatoa mfano wa Waisraeli kushupaza mioyo yao na kukataa baraka za Bwana. Na pia ni onyo kwetu sote kutoshupaza mioyo yetu.

Shughuli Yamkini

  • Leta sponji (au nguo ya kufua) na jiwe darasani. Waalike watoto kugusa vitu hivyo na kuelezea jinsi wanavyohisi juu ya hivyo vitu. Weka matone machache ya maji juu ya kila kitu, na onyesha kwamba maji mengi zaidi yanalowanisha sponji kuliko jiwe. Eleza kwamba mioyo yetu inahitajika iwe laini na sio migumu ili kwamba tuweze kukubali ukweli wa Baba wa Mbunguni mioyoni mwetu.

  • Kata umbo la moyo kutoka kwenye kifaa laini, kama vile nguo, na kifaa kigumu, kama vile kadibodi. Waambie watoto kwamba tunaposikiliza na kutii tunakuwa na moyo laini na tunapokuwa hatusikilizi na hatutii tunakuwa na moyo mgumu. Katika maneno yako mwenyewe, shiriki baadhi ya mifano kutoka maandiko ya watu waliokuwa na mioyo laini au mioyo migumu (kama vile Nefi, Lamani, na Lemueli [1 Nefi 2:16–19], Paulo [Matendo ya Mitume 9:1–22], au Joseph Smith [Joseph Smith—Historia ya 1:11—20]). Unapouelezea kila mfano, waalike watoto kuonyesha moyo laini au moyo mgumu.

Musa akimtawaza kaka yake Haruni

Musa anamwita Haruni kwenye Huduma, na Harry Anderson

Waebrania 5:4

Wenye Ukuhani wameitwa na Mungu.

Waebrania 5:4 ni aya muhimu kwa sababu inaeleza wazi kwamba wenye ukuhani—na wengine wanaohudumu katika Kanisa—lazima waitwe na Mungu.

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto Waebrania 5:4. Muombe mwenye ukuhani kuelezea ukuhani ni nini na aelezee uzoefu wake wa kupokea ukuhani.

  • Wasaidie watoto kukariri virai kutoka kwenye makala ya tano ya imani. Toa ushuhuda wako kwamba watu wanaoitwa kufanya kazi ya Mungu wanaitwa na Mungu kwa njia ya ufunuo.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Waebrania 1:2–10; 2:8–10, 17–18

Ninaamini katika Yesu Kristo.

Waraka kwa Waebrania uliandikwa ili kuimarisha imani katika Yesu Kristo kwa Watakatifu Waebrania. Inaweza kufanya hivyo hivyo kwa watoto unaowafundisha.

Shughuli Yamkini

  • Mpangie kila mtoto aya chache katika Waebrania 1:2–10; 2:8–10, 17–18, na waalike watoto kutafuta ukweli kuhusu Yesu Kristo katika mistari hiyo. Waache washiriki au kuandika ubaoni kile wanachokipata. Je, ni kitu gani kingine tunachokijua kuhusu Yesu Kristo? Watoto wanaweza kupata baadhi ya mawazo kutoka katika nyimbo kama vile “Najua Mkombozi Wangu Anaishi” (Wimbo, na. 136) au “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35).

  • Waalike wanafunzi kuchora picha zao wenyewe wakiwa pamoja na wazazi wao. Waombe kushiriki kile walichonacho kwa pamoja na wazazi wao. Eleza kwamba wakati Waebrania 1:3 inasema kwamba Yesu Kristo ni “sura halisi ya [Mungu] mwenyewe,” ina maana kwamba Yesu na Baba wa Mbinguni wana tabia na sifa zilezile. Shuhudia kwamba tunajifunza kuhusu Baba wa Mbinguni kwa kujifunza na kumfuata Yesu Kristo.

  • Wasaidie watoto kufikiria watu ambao wanaweza kushiriki nao shuhuda zao juu ya Yesu Kristo. Fikiria kuwaalika wao kufanya mazoezi ya kuelezea kile ambacho wangewaambia wale watu kuhusu Yesu.

Waebrania 3:7–19

Ili kupokea mwongozo na baraka za Baba wa Mbinguni, lazima “tusishupaze mioyo [yetu].”

Katika Waebrania 3, hadithi ya Waisraeli nyikani inatumika katika kufundisha umuhimu wa kutoshupaza mioyo yetu. Je, unawezaje kutumia hadithi hii ili kuwafundisha watoto katika darasa lako kanuni hii?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wafikirie juu ya vitu ambavyo ni vigumu na vilivyo laini (Unaweza kuleta baadhi ya mifano ili kuwaonyesha.) Someni pamoja Waebrania 3:8. Je, inamaanisha nini kuwa na moyo mgumu? Je, ni kwa nini Mungu anatutaka tuwe na mioyo laini?

  • Katika maneno yako mwenyewe, simulia hadithi ya Waisraeli wakishupaza mioyo yao dhidi ya Bwana huko nyikani (ona Hesabu 14:1–12; Waebrania 3:7–19). Acha watoto waigize hadithi hii. Je, ni nini kitatokea kama tukishupaza mioyo yetu dhidi ya Bwana na injili yake?

  • Waalike watoto wasome Mathayo 13:15; Waebrania 3:15; Mosia 11:29; na Musa 6:27. Waombe wachore ubaoni sehemu zilizotajwa katika mistari hii. Inamaanisha nini kuwa na masiko mazito kiroho, kipofu wa macho kiroho, na mioyo migumu? Je, sisi tunawezaje kuhakikisha kwamba masikio yetu, macho, na mioyo viko tayari kupokea baraka za Mungu?

Waebrania 5:1–4

Wenye Ukuhani wameitwa na Mungu.

Waebrania 5 inatoa nafasi ya kujadili ukuhani ni nini—uwezo na mamlaka ya kutenda katika jina la Mungu—na jinsi unavyopokelewa. Hii inaweza hususani kuwa ya msaada kwa vijana wanaojiayarisha kutawazwa kwenye ukuhani.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha Musa Anampa Haruni Ukuhani (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 15) wakati mtoto akisoma Waebrania 5:4. Inaweza kuwa na msaada kueleza kwamba kwa sababu Haruni alikuwa mtu wa kwanza kuwa na ukuhani wa Haruni, uliitwa kwa jina lake. Wasaidie watoto wafikirie kazi zinazofanywa na wenye ukuhani wa Haruni (kama vile kubatiza, kubariki na kupitisha sakramenti, na kuwaalika wengine kuja kwa Kristo).

  • Wasaidie watoto kufikiria kuhusu njia tofauti ambazo watu hupokea mamlaka. Kwa mfano, jinsi gani mwalimu, daktari, au kiongozi wa kisiasa wanapokea mamlaka? Je, ni kwa jinsi gani Mungu anatoa mamlaka yake? Waalike watoto kufikiria kuhusu swali hili wanaposoma Waebrania 5:4 na makala ya tano ya imani.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki andiko, wimbo, au shughuli waliyojifunza darasani leo pamoja na familia zao kwa ajili ya mkutano wa jioni ya familia nyumbani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto wanaweza kutambua ushawishi wa Roho. Wafundishe watoto kwamba hisia za amani, upendo, na ukunjufu walizonazo wakati wanapoongea au kuimba kuhusu Yesu Kristo na injili Yake zinatoka kwa Roho Mtakatifu. Hisia hizi zinaweza kujenga shuhuda zao.