Njoo, Unifuate
Novemba 18–24. Yakobo: ‘Iweni Watendaji wa Neno, wala Si Wasikiaji tu’


Novemba 18–24. Yakobo ’Iweni Watendaji wa Neno, wala Si Wasikiaji tu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

Novemba 18–24. Yakobo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Ibrahimu akisali nje ya hema yake

Ibrahimu kwenye Nyanda za Mamre, na Grant Romney Clawson

Novemba 18–24

Yakobo

“Iweni Watendaji wa Neno, wala Si Wasikiaji tu”

Waraka wa Yakobo una kweli nyingi ambazo zinaweza kuwabariki watoto unaowafundisha. Mfuate Roho ili kuamua kweli zipi utashiriki nao. Mawazo yaliyoko katika muhtasari huu yanaweza pia kusaidia.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kutaja kanuni ya injili wanayokumbuka kujifunza pamoja na familia zao wakati wa wiki iliyopita au kutoka darasa lao la Msingi Jumapili iliyopita. Baada ya kila mtoto kutaja, muombe mtoto mwingine katika darasa kufanya muhtasari wa yale waliyoshiriki.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Yakobo 1:5–6.

Ninaweza kumwomba Baba wa Mbinguni kunisaidia kujifunza kile kilicho cha kweli.

Wasaidie watoto unaowafundisha kuelewa kwamba wanaweza kumgeukia Baba wa Mbinguni kwa ajili ya hekima. Kufanya hivyo kutawabariki sana wanapokabiliana na maswali magumu.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kujifunza kirai “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu”(Yakobo 1:5). Je, tunamwulizaje Mungu maswali? Je, Yeye hutujibu kwa namna gani?

  • Onyesha picha ya Ono la Kwanza (Kitabu cha sanaa za Injili, na. 90), na elezea namna gani kusoma Yakobo 1:5 kulimshawishi Joseph Smith kumwuliza Baba wa Mbinguni ili amsaidie na swali hilo (ona Joseph Smith—Historia ya 1:1-15). Toa ushuhuda wako kwamba Mungu hujibu maombi, na ushuhudie kwamba watoto wanaweza kuomba Kwake wakati wakiwa na maswali. Waache watoto wachore picha zao wenyewe za Joseph Smith akisoma Yakobo 1:5 na akiomba kwa Baba wa Mbinguni.

Yakobo 3:1–13

Naweza kusema mambo mazuri.

Kama Yakobo alivyoshuhudia, kujifunza kusema maneno ya ukarimu tu kwa wengine kutatusaidia kuwa kama Yesu Kristo (ona Yakobo 3:2).

Shughuli Yamkini

  • Lete kitu kitamu na kitu kichachu kwa ajili ya watoto kuonja. Wasaidie kuelewa kwamba hatuna budi kutumia ndimi zetu kusema mambo matamu (au ya ukarimu) na kutosema machachu (au ukatili) (ona Yakobo 3:10). Wasaidie kufikiria juu ya mifano ya mambo mazuri tunayoweza kusema kwa wengine.

  • Mpe kila mtoto mchoro wa kawaida wa mtu akizungumza. Waalike watoto wauinue juu unaposema jambo zuri tunaloweza kufanya na ndimi zetu (kama vile kusema ukweli, tunaposifia, na kutoa msaada kwa mtu fulani) na kuuweka chini unaposema kitu ambacho hatutakiwi kufanya na ndimi zetu (kama vile kusema uongo, kuwasema vibaya watu, na kukataa kutii mzazi).

  • Imarisha ujumbe wa Yakobo 3:1–13 kwa kuimba pamoja wimbo kuhusu kuwa mkarimu, kama vile “Huruma Huanza Nami” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 145). Pendekeza kwamba watoto watengeneze “chupa kubwa ya ukarimu” wanaweza kuijaza na changarawe au vitu vingine vidogo wakati wowote wanaposema kitu fulani kizuri kwa mtu fulani.

Yakobo 5:7–11.

Baadhi ya baraka za Mungu zinahitaji subira.

Subira siku zote haiji yenyewe, hususani kwa watoto. Fikiria jinsi unavyoweza kuutumia ushauri wa Yakobo ili kuwasaidia watoto unaowafundisha kujifunza subira.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kufikiria nyakati walipokuwa hawana budi kusubiri kitu fulani ambacho kwa hakika walikitaka. Waeleze kwamba kusubiri kitu fulani tunachokitaka bila kulalamika huitwa kuwa na subira.

  • Fanya muhtasari wa Yakobo 5:7 kwa maneno yako, na onyesha picha ya mbegu au mche. Kwa nini tunahitaji subira tunapopanda mmea? Ni nini kingetokea kama tungejaribu kuuvuta mche kuufanya ukue haraka? Shuhudia kwamba Mungu ana baraka nyingi kwa ajili yetu, lakini baadhi yake zinahitaji subira.

  • Elezea hadithi ya Ayubu, ambaye ametajwa katika Yakobo 5:11 kama mfano wa subira (ona “Sura ya 46: Ayubu,” Hadithi za Agano la Kale, 165–69, au video inayofanana kwenye LDS.org). Ni kwa jinsi gani Ayubu alibarikiwa kwa kuwa na subira?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Yakobo 1:5–6

Baba wa Mbinguni atanisaidia kujifunza ukweli kama nitatafuta msaada Wake.

Ingawa watoto unaowafundisha wataonekana wadogo, wako wadogo kwa miaka michache tu ukilinganisha na Joseph Smith alivyokuwa wakati aliposoma Yakobo 1:5 na alipata mwongozo wa kiungu wa kumwendea Baba wa Mbinguni katika sala. Fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kujenga imani yao kwamba Mungu atawasaidia watakapokosa hekima.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kukusimulia hadithi ya Ono la Kwanza la Joseph Smith kwa maneno yao (ona Joseph Smith—Historia ya 1:5–19; ona pia video “Ono la Kwanza la Joseph Smith” kwenye LDS.org). Je, ni kwa jinsi gani Yakobo 1:5 ilimsaidia Joseph? Wasaidie watoto kufikiria mifano ya watu wengine katika maandiko waliopokea jibu kwa sala zao kama vile Nefi [1 Nefi 11:1–6] na kaka wa Yaredi [Etheri 2:18–3:9]). Je, ni mambo gani tunaweza kumwuliza Baba wa Mbinguni katika sala?

  • Soma pamoja na watoto Joseph Smith—Historia ya 1:10-14. Waalike watoto kutafuta vitu Joseph alifanya ili kupokea majibu kwa maswali yake. Tunawezaje kufuata mfano wa Joseph wakati tunapokuwa na maswali?

Yakobo 1:22–27; 2:14–26

“Imani pasipo matendo imekufa.”

Utawezaje kuwasaidia watoto kuona uhusiano kati ya kile wanachoamini na kile wanachofanya?

Shughuli Yamkini

  • Waonyeshe watoto tochi bila betri, penseli bila risasi, au kitu kingine ambacho hakifai au “kimekufa.” Waombe watoto kusoma Yakobo 2:14–17. Ni kwa jinsi gani vitu hivi vinafafanua kwa mfano ukweli wa aya hizi?

  • Waalike watoto wasome kimya Yakobo 1:22–27; 2:14–26. Kisha waombe kushiriki kile wanachoweza kufanya kuonyesha kwamba wao ni watendaji wa neno. Kwa mfano, je, wanamfahamu mtu fulani ambaye ni mgonjwa au mpweke ambaye wanaweza kumtembelea, au wanaweza kuamua kuhudumia familia zao zaidi? Unaweza pia kuwakumbusha juu ya maneno waliyoweza kusikia katika mkutano wa sakramenti leo. Tunawezaje kuwa watendaji wa maneno haya?

Yakobo 3:1–13

Ninaweza kudhibiti maneno ninayosema.

Maneno tunayosema sisi kwa sisi yanaweza kuonekana sio muhimu, lakini kama Yakobo alivyoshuhudia, yanaweza kuwa na ushawishi mkubwa, kwa mema au mabaya.

Shughuli Yamkini

  • Je, kuna mtu yoyote katika kata, pengine mmoja wa watoto unaowafundisha, aliyewahi kufanya kazi na farasi au anajua vitu fulani kuhusu boti? Unaweza kumwalika aje kutoa umaizi kuhusu mafundisho ya Yakobo katika Yakobo 3:3–4 kuhusu kutumia maneno ya huruma, au toa baadhi ya umaizi wako mwenyewe. Tunajifunza nini kuhusu kudhibiti ndimi zetu kutokana na mifano hii?

  • Waalike watoto wasome Yakobo 3:1–13 na kuchora picha ya kitu fulani wanachopata ambacho kinafundisha kuhusu kudhibiti ndimi zetu. Wape muda wa kuelezea picha zao na kile walichojifunza.

  • Baada ya kurudia upya Yakobo 3:1–13 pamoja, rudia upya viwango vya lugha katika Kwa Nguvu ya Vijana (20-21). Wasaidie watoto kufikiria juu ya kitu fulani wanachoweza kufanya ili kuboresha jinsi wanavyozungumza na wengine, na kuwatia moyo kujiwekea malengo binafsi.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kusali kwa Baba wa Mbinguni wakiwa na swali au kujaribu kuwa na subira zaidi wakati wa wiki ijayo. Waombe kushiriki uzoefu wao katika darasa lijalo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto kuwa wachangamfu. “Unapowafundisha watoto, waruhusu kujenga, kuchora, kupaka rangi, kuandika, na kubuni. Vitu hivi ni zaidi ya shughuli za kufurahisha—ni muhimu katika kujifunza” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).