Njoo, Unifuate
Novemba 11–17. Waebrania, 7–13: ‘Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo’


“Novemba 11–17. Waebrania 7–13: ‘Kuhani mkuu wa Mambo Mema yatakayokuwapo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Novemba 11–17. Waebrania 7–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Melkizedeki akitoa baraka kwa Abramu

Melkizedeki anambariki Abramu, na Walter Rane

Novemba 11–17

Waebrania 7–13

“Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo”

Unapopitia upya na kutafakari muhtasari huu, sikiliza kwa makini vishawishi unavyopokea kuhusu watoto unaowafundisha. Roho atakusaidia kupata habari kwa ajili yao katika Waebrania 7–13.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waombe watoto kushiriki vitu wao na familia zao wanafanya kujifunza injili nyumbani. Waombe kushiriki baadhi ya uzoefu wao wanaoupenda wa kujifunza injili na familia zao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Waebrania 7:1–6

Ukuhani unaweza kutusaidia katika njia nyingi.

Waebrania 7:1–6 inaweza kutoa nafasi kuwasilisha kwa watoto baraka za ukuhani.

Shughuli za Yakini

  • Kwa kifupi elezea Ibrahimu alikuwa nani, na kisha tumia Waebrania 7:1–6 na Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:36–40 (katika kiambatanisho cha Biblia) kufundisha kwamba Ibrahimu alilipa zaka kwa Melkizedeki. Eleza kwamba Melkizedeki alikuwa na ukuhani Mkuu, ambao ni uwezo wa Mungu uliopewa kwa wanadamu duniani, na aliutumia kumbariki Ibrahimu. Watoto wanaweza kufurahi kuigiza hadithi kwa ‘vitu rahisi vya kubeba’ kama taji na bahasha ya zaka.

  • Mualike mwenye ukuhani wa Haruni na Melkizedeki kutembelea darasa na wawaelezee watoto jinsi walivyotumia ukuhani kubariki wengine. Kisha waoneshe watoto picha tofauti za ibada za ukuhani (kwa mfano, ona Picha 103–8 katika Kitabu cha Sanaa za Injili). Wasaidie watoto kuamua ukuhani gani unahitajika kwa kila ibada na toa picha ile kwa mwenye ukuhani anayefaa kuishika.

Waebrania 11:1–32

Imani ni kusadiki katika mambo ambayo hatuwezi kuyaona.

Hata kama hawawezi kumwona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo au kupata uzoefu wote wa baraka za injili, wanafunzi unaowafundisha wanaweza kukuza imani kwa kujifunza kutoka mifano katika Waebrania 11.

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha ya Yesu. Weka kote chumbani vitu kadha kuwakilisha “ushahidi” kwamba Yeye ni halisi hata kama hatuwezi kumwona (kama vile maandiko, picha ya Ono la Kwanza, na picha ya dunia). Waombe watoto kuonyesha vitu, na kisha shiriki pamoja nao jinsi kila kitu kinatusaidia kuwa na imani kwamba Yesu yu hai.

  • Leta feni, na waache watoto kuchukua zamu kuhisi feni ikipuliza hewa kupitia nyuso zao. Wafundishe kwamba hatuwezi kuona hewa, lakini tunaweza kuihisi. Vilevile, hatuwezi kumwona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, lakini tunaweza kuhisi upendo wao na kuwa na imani ambayo ni ya kweli.

  • Shiriki hadithi za mmoja au watu zaidi waliotajwa katika Waebrania 11:4–32. Fikiria kutumia Hadithi za Agano la Kale (ona sura ya 4–6, 8–10, 15–17, 23 na 28). Watu hawa walifanya nini kuonyesha walikuwa na imani katika kitu fulani wasichokiona? Shiriki baadhi ya baraka ulizopokea kwa sababu ya imani yako.

Waebrania 13:5–6

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo watatusaidia na kamwe hawatatuacha.

Ni majaribu gani watoto wanaweza kuwa wanayapitia? Ni kwa jinsi gani ujumbe wa Waebrania 13:5–6 unaweza kuwasaidia?

Shughuli za Yakini

  • Rudia upya baadhi ya hadithi za Agano Jipya watoto walizojifunza mwaka huu ambapo Mwokozi aliwasaidia wengine, kama vile wakati alipomponya mtu kwenye kifafa (ona Luka 5:18–26) au kuwalisha 5,000 (ona Mathayo 14:15–21). Wasaidie watoto kujifunza msemo “Bwana ni msaada wangu” (Waebrania 13:6).

  • Waombe watoto kuchora picha ya wakati walipohisi woga. Wasomee Waebrania 13:5–6, na kushuhudia kwamba Baba wa Mbinguni atatusaidia na kamwe hatatuacha. Wasaidie watoto kukata karatasi zenye umbo la moyo mkubwa kutosha kufunika michoro. Ni baadhi ya vitu gani ambavyo vinatusaidia kujisikia karibu zaidi kwa Baba wa Mbinguni? Andika baadhi ya mambo haya juu ya mioyo.

  • Wafundishe watoto mstari wa pili wa “Tell Me Dear Lord” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 176). Kulingana na wimbo, ni msaada gani tunaweza kupokea wakati Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wakiwa karibu nasi? Zungumzia kuhusu wakati Baba wa Mbinguni alipokuwa karibu nawe na akakusaidia.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Waebrania 7:1–4

Wenye ukuhani wanaostahili humfuata Mwokozi.

Unawezaje kutumia mistari hii kuwasaidia watoto kuelewa kwamba wale wenye ukuhani wanatakiwa wawe waaminifu na kuwahudumia wengine kama Mwokozi alivyofanya?

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kuorodhesha mambo wanayojua kuhusu wenye ukuhani wawili mashuhuri Ibrahimu na Melkizedeki. Wanaweza kupata msaada katika Waebrania 7:1–4; Ibrahimu 1:1–2; na Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:25–40 (katika kiambatisho cha Biblia). Ni sifa zipi za kama Kristo watu hawa wanazo ambazo ziliwasaidia kuuheshimu ukuhani?

  • Waombe watoto wasome Mathayo 7:1–2 na kutafuta vyeo vilivyotumika kumwelezea Melkizedeki. Je, ni kwa jinsi gani vyeo hivi vinatukumbusha juu ya Yesu Kristo. Wasaidie kufikiri juu ya njia ambazo Yesu alikuwa “Mfalme wa amani.” Je, wanafahamu juu ya wenye ukuhani wengine wowote ambao pia ni mfano wa kumfuata Mwokozi?

  • Elezea tukio ambalo kwalo mwenye ukuhani mwadilifu alikusaidia kuja karibu na Mwokozi. Wasaidie watoto kufikiri juu ya njia ambazo huduma za ukuhani zimewabariki wao.

Waebrania 11

Baba wa Mbinguni huwazawadia wale walio na imani.

Waebrania 11 ina mifano mingi ya watu ambao walibarikiwa walipotenda kwa imani. Hadithi zipi zitawavutia zaidi au zenye msaada kwa watoto unaowafundisha?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kuorodhesha ubaoni vitu wanavyojifunza kuhusu imani katika Waebrania 11:1–3 6. Mpe kila mmojawapo wa watoto jina la mtu fulani aliyetajwa katika Waebrania 11, na waalike wasome mistari inayohusiana na yule mtu. Waombe kushiriki ishara kuhusu yule mtu ili kwamba watoto wengine waweze kukisia ni nani huyo. Watu hawa walionyeshaje imani, na jinsi gani Baba wa Mbinguni aliwazawadia? (Kwa picha za watu hawa, ona sehemu ya Agano la Kale ya Kitabu cha sanaa za injili).

  • Baada ya kusoma kuhusu baadhi ya mifano ya imani katika Waebrania 11, waombe watoto kuandika kuhusu mtu wanayemjua ambae alionesha imani. Waalike wanafunzi kadhaa kushiriki mifano yao pamoja na darasa.

Waebrania 12:5–11

Bwana huwarudi wale anaowapenda.

Mistari hii inaweza kuwasaidia watoto kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni, wazazi wao, na wengine wanawarekebisha kwa sababu wanawapenda na wanawataka wajifunze kutoka makosa yao.

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Waebrania 12:5–11, na uwaombe watoto kutafuta kwa nini Baba wa Mbinguni anaturudi (anaturekebisha au kututia nidhamu). Hii inatufundisha nini sisi kuhusu kwa nini wazazi wa kidunia pia wanawarekebisha watoto wao? Je, ni kwa jinsi gani tunapaswa kukubali marekebisho ya upendo?

  • Shiriki mifano ya watu katika maandiko waliorudiwa na Bwana na wakatubu (kwa mfano, ona 1 Nefi 16:25–27; Etheri 2:13–15). Je, ni kwa jinsi gani wanakuwa mifano mizuri ya kanuni katika Waebrania 12:5–11?

  • Baada ya kusoma Waebrania 12:5–11, waalike watoto kuandika mambo machache watakayojaribu kukumbuka wakati wanarudiwa kwa ajili ya makosa yao.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuandika au kuchora picha ya kitu wanachohisi kuwa ni kitu muhimu sana walichojifunza katika darasa. Wahimizi kuelezea kile walichojifunza pamoja na familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia kurasa za shughuli. Watoto wanapokamilisha kurasa za shughuli wakati wa darasa, tumia muda huo kupitia upya kanuni kutoka katika somo.

Chapisha