“Februari 13–19. Mathayo 5: Luka 6: ‘Heri Ninyi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)
“Februari 13–19. Mathayo 5: Luka 6, “ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023
Februari 13–19
Mathayo 5; Luka 6
“Heri Ninyi ”
Fursa yako ya kufundisha watoto ni ya thamani. Unapojiandaa mwenyewe kiroho, Bwana atakuongoza.
Alika Kushiriki
Waombe watoto wazungumze kuhusu kitu walichokifanya wiki hii ili kushiriki nuru ya Bwana na mtu mwingine—pengine kwa kuwa mfano mwema au kuonyesha upendo na ukarimu.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Ninaweza kuwa mpatanishi.
Watoto unaowafundisha wanaweza kuwa na ushawishi mkubwa nyumbani wanapowatendea wengine kwa upendo na ukarimu.
Shughuli Yamkini
-
Wasomee Mathayo 5:9 watoto, na uelezee kwamba wapatanishi hufanya sehemu yoyote kuwa mahali penye amani, pasipo kujali ni wapi walipo. Andika katika mishipi ya karatasi baadhi ya mifano ya hali ngumu ambazo watoto wanaweza kukabiliana nazo (kwa mfano, ndugu wanapigania mwanasesere). Mwalike kila mtoto kuchukua mshipi wa karatasi. Unaposoma matukio, waombe watoto washiriki jinsi wanavyoweza kuwa wapatanishi katika hali hiyo. Au shiriki matukio machache yasiyo halisi, na uwasaidie watoto kutambua kama watu husika ni wapatanishi.
-
Waalike wazazi wachache wa watoto kutembelea darasa lako na kushiriki mifano ya nyakati watoto wao walikuwa wapatanishi nyumbani.
Yesu anataka mimi niwe nuru kwa wengine.
Watoto wadogo wanaweza kuwa na ushawishi mkubwa wa mema kwa wengine. Unawezaje kuwahamasisha ili nuru zao ziangaze?
Shughuli Yamkini
-
Onyesha watoto vitu kadhaa vinavyotoa mwanga, na uonyeshe ya picha ya watoto. Soma Mathayo 5:14–16, na uwaambie watoto kwamba mifano yao miema inaweza kuwa nuru kwa wengine ili waone. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia nuru yetu kuwaleta wengine kwa Mungu?
-
Angaza tochi kuzunguka chumba, na waalike watoto kufuata nuru kwa macho yao. Tumia nuru kuongoza macho yao hadi kwenye picha ya Mwokozi. Nuru unatusaidiaje sisi? Tunawezaje kuwa nuru kwa ulimwengu? Ziba tochi. Ni nini hutokea kama hatushiriki nuru yetu au kama tunaificha?
-
Ficha tochi chumbani, na uzime taa. Waache watoto wajaribu kuitafuta. Rejelea Mathayo 5:15, na uzungumzie kuhusu kwa nini hatupaswi kuficha nuru yetu.
-
Wasaidie watoto kutafuta na kupaka rangi mishumaa iliyofichwa katika ukurasa wa shughuli ya wiki hii.
-
Imba wimbo pamoja na watoto kuhusu kuwa nuru kwa wengine, kama vile “Jesus Wants Me for a Sunbeam,” “Shine On,” au“I Am like a Star” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 60–61, 144, 163).
Yesu Kristo anataka nimpende kila mmoja.
Watoto wadogo wanaweza kuanza sasa kufanya mazoezi ya kuonyesha upendo, hata wakati wapotendewa visivyo na wenzao au ndugu zao. Unaposoma Mathayo 5:44–45, fikiria jinsi mafundisho ya Mwokozi yanavyotumika kwa watoto unaowafundisha.
Shughuli Yamkini
-
Rudia tena Mathayo 5;44 kwa kutumia maneno na hali ambazo watoto wataelewa na kuzihusisha. Waombe watoto kushiriki nyakati walipoonyesha upendo kwa mtu mmoja ingawa ilikuwa ni vigumu. Ni kwa jinsi gani uzoefu huu uliwafanya wajisikie?
-
Kama darasa, imbeni wimbo kuhusu kuwapenda wengine, kama vile “Jesus Said Love Everyone” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 136). Ni nini tunajifunza kutoka kwenye wimbo huu kuhusu kuwapenda wengine?
-
Wape watoto mioyo ya karatasi iliyoandikwa kwa maneno “Nitaonyesha upendo wangu kwa kila mtu.” Waombe waipambe mioyo na kuining’iniza nyumbani mwao kama ukumbusho wa kuwapenda wengine.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Ninaweza kuwa na furaha ninapoishi kama Yesu Alivyofundisha.
Unaposoma Mathayo 5:3–12, ni maneno na virai gani vinakuvutia? Ni kwa jinsi gani mafundisho haya yatabadilisha maisha ya watoto unaowafundisha?
Shughuli Yamkini
-
Unda chati kwenye bodi yenye nguzo mbili, zilizoandikwa Heri wale … na Baraka. Waalike watoto kupekua Mathayo 5:3–12 wakitafuta sifa za wale ambao Yesu alisema wangebarikiwa na baraka Aliyowaahidi. Kisha jaza katika chati kile walichokipata. Jadili na watoto kile kila sifa na baraka inayoendana nayo inamaanisha.
-
Andika kila sifa kutokana na mistari hii kwenye kadi na baraka zake juu ya kadi hiyo. Kwa mfano, kadi moja ingesema “mpole” na nyingine ingesema “watairithi nchi” (mstari wa 5). Waache watoto kuoanisha sifa na baraka. Waombe watoto kuchagua moja ya sifa katika mistari hii ambayo wanahitaji kuiendeleza.
Ninaweza kuwa mpatanishi.
Yesu Alifundisha kwamba wapatanishi maana wataitwa watoto wa Mungu. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwahamasisha watoto kuwa wapatanishi?
Shughuli Yamkini
-
Mwalike mtoto asome Mathayo 5:9 kwa sauti. Mpatanishi ni nani? Ni kwa njia zipi tunaweza kuwa wapatanishi kwa familia zetu na marafiki? (Kwa baadhi ya mawazo, ona mistari 21–24, 38–47.)
-
Muombe kila mtoto kufikiria hali ambayo itahitaji msaada wa mpatanishi. Je, mpatanishi angefanya nini katika hiyo hali?
-
Waalike watoto kushiriki nyakati ambapo walionyesha upendo kwa mtu fulani, hata kama mtu huyo alikuwa tofauti nao au alikuwa vigumu kupendwa.
Mfano wangu unaweza kuangaza njia kwa wengine kumfuata Yesu.
Wengi wa watoto unaowafundisha wamefanya maagano ya ubatizo. Fikiria kuhusu jinsi maneno ya Mwokozi katika Mathayo 5:14–16 yanavyohusiana na maagano yao. Ni jumbe gani Bwana Angeweza kuwa nazo katika kifungu hiki cha maneno kwa ajili ya watoto unaowafundisha?
Shughuli Yamkini
-
Wasaidie watoto kukariri Mathayo 5:16. Andika mstari ubaoni. Someni pamoja mara kadhaa, mkifuta maneno machache kila mara. Waalike watoto kuchora vitu wanavyoweza kufanya ili kuwa nuru kwa wengine. Zungumzeni kuhusu jinsi kuwa nuru kwa wengine kunavyotusaidia sisi kutimiza maagano yetu ya ubatizo (ona Mosia 18:8–10).
-
Imbeni pamoja wimbo kuhusu kushiriki nuru na wengine, kama vile “Shine On” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 144). Ni kwa jinsi gani tunaweza kushiriki nuru ya Mwokozi?
-
Waombe watoto wachore vitu vinavyotupatia nuru. Soma Mathayo 5:14–16. Waulize kwa nini Yesu anatutaka sisi tuwe nuru kwa ulimwengu.
-
Waalike watoto wawili kuangaliana, na muombe mmoja kujaribu kumfanya mwingine atabasamu pasipo kumgusa. Zungumzia kuhusu uwezo walio nao watoto kuleta furaha kwa wengine.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wape changamoto watoto kumtazama mtu ambaye amekuwa mpatanishi wiki hii. Mwanzoni mwa darasa la wiki ijayo, waalike kuzungumzia kuhusu nani na kitu gani walichoona.