“Februari 20–26. Mathayo 6–7: ‘Alikuwa Akiwafundisha kama Mtu Mwenye Mamlaka’’’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)
“Februari 20-26. Mathayo 6–7,“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023
Februari 20–26
Mathayo 6–7
“Aliwafundisha kama Mtu Mwenye Mamlaka”
Anza kwa kusoma Mathayo 6–7, ukiwa unafikiria kuhusu watoto unaowafundisha. Ni jumbe gani kutoka katika sura hizi wanahitaji kusikia? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na muhtasari huu unaweza kusaidia kukupa mawazo ya kufundisha kama inavyohitajika.
Alika Kushiriki
Waombe watoto kushiriki kile walichofanya wiki iliyopita ili kuwa nuru au mfano kwa mtu fulani.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Mimi naweza kuomba kwa Baba yangu wa Mbinguni kama Yesu alivyofanya.
Watoto wanaweza kujifunza kusali kwa kusikiliza sala za wengine. Unawezaje kuwasaidia wao kujifunza kutoka katika sala ya Yesu Kristo katika mistari hii?
Shughuli Yamkini
-
Pitia tena mafundisho ya Yesu kuhusu sala yapatikanayo katika Mathayo 6:5–13. Unaweza kutumia “Sura ya 20: Yesu Anafundisha kuhusu Sala” (katika Hadithi za Agano Jipya, 51–52, au video inayofanana nayo kwenye ChurchofJesusChrist.org).
NaN:NaN -
Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kukumbuka sehemu tofauti za sala.
-
Chora mikono ya kila mtoto kwenye kipande cha karatasi. Sema kuhusu kile tunachopaswa kufanya na mikono wakati tunaposali. Katika kila mchoro, andika kitu tufanyacho kuonyesha staha wakati tunasali (kwa mfano, kuinamisha vichwa vyetu, kufumba macho yetu, na kadhalika).
-
Imba wimbo kuhusu sala pamoja na watoto (kama vile “We Bow Our Heads” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 25), na toa ushuhuda wako juu ya nguvu ya sala. Waalike watoto kushiriki uzoefu wao juu ya sala.
Ninapaswa kuwatendea wengine jinsi ninavyotaka kutendewa.
Yesu anafundisha katika Mathayo 7:12—pia inafahamika kama Sheria ya Dhahabu—hutoa mwongozo rahisi wa jinsi ya kuwatendea wengine. Ni nini kitachowasaidia watoto unaowafundisha waishi kanuni hii?
Shughuli Yamkini
-
Soma Mathayo 7:12, na ufafanue kwa maneno rahisi ambayo watoto wanaweza kuelewa. Wasaidie watoto kufikiria njia tofauti tofauti ili kumalizia sentensi kama ifuatayo: “Ninapenda wakati wengine wanapo kwa ajili yangu.” Kila baada ya kila sentensi, waalike kurudia pamoja nawe, “Hivyo ninapaswa kwa wengine.”
-
Imba pamoja na watoto wimbo ambao unahisi unaimarisha Mathayo 7:12, kama vile “Jesus Said Love Everyone” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 61). Fanya matendo rahisi ili kuendana na wimbo. Waulize watoto kile wanachojifunza kuhusu jinsi tunavyopaswa kuwatendea wengine kutoka katika mfano wa Mwokozi.
-
Waalike watoto kuorodhesha mambo mazuri wazazi wao au wanafamilia wengine wanawafanyia. Soma Mathayo 7:12, na waalike watoto kutaja mambo mazuri wanayoweza kuzifanyia familia zao.
Ninaweza kujenga juu ya msingi imara kwa kumfuata Yesu.
Kwa kutumia mfano wa Mwokozi kuhusu kujenga nyumba juu ya mchanga au kwenye mwamba kunaweza kuwa njia ya kukumbukwa kuwafundisha watoto kuhusu umuhimu wa kutenda juu ya kile tunachojifunza.
Shughuli Yamkini
-
Imba pamoja na watoto “The Wise Man and the Foolish Man” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 281), na fanya vitendo kuongozana na maneno ya wimbo.
-
Tumia Mathayo 7:24–27 kufundisha kuhusu tofauti kati ya mtu mwenye hekima na mtu mpumbavu. Waalike watoto kujifanya wanajenga nyumba. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama mtu mwenye hekima?
-
Waache watoto wachore picha za mfano wa mtu mwenye hekima na mtu mpumbavu.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Mahubiri ya Mlimani yana ujumbe kwangu.
Sura hizi zina ujumbe mwingi ambao unaweza kuwafaa watoto unaowafundisha. Zisome ukiwafikiria watoto akilini. Ni nini kinachokuvutia wewe?
Shughuli Yamkini
-
Wakumbushe watoto kwamba wamekuwa wakijifunza kuhusu kile Yesu alichofundisha wakati wa Mahubiri ya Mlimani. Kweli gani wanaweza kukumbuka kujifunza kuhusu wiki ya mwisho?
-
Andika kwenye ubao baadhi ya virai kutoka kwenye Mahubiri ya Mlimani na vifungu vingine ambavyo haviko katika maandiko. Waalike watoto kutambua ni virai gani vinavyotokea kwenye Mahubiri ya Mlimani na kushiriki wanachojifunza kutokana virai hivyo. Waombe washiriki kile wanachojifunza kutoka katika mafundisho haya.
-
Chagua mistari kadhaa kutoka Mathayo 6–7 ambayo unahisi itakuwa na maana kwa watoto. Andika marejeleo ya maandiko katika kadi, na zifiche kote chumbani. Waache watoto wazitafute, wasome mistari, na kuelezea kwa nini mafundisho haya ni muhimu kwao.
-
Shiriki moja ya vifungu unachokipenda kutoka katika Mathayo 6–7, na elezea kwa nini unakipenda. Ikiwa watoto wana kifungu wanachokipenda, waalike kushiriki kwa nini wanakipenda na kile wanachojifunza kutokana na hicho kifungu.
-
Imba pamoja watoto wimbo kuhusu Mwokozi na mafundisho Yake, kama vile “I’m Trying to Be like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79). Simamisha wimbo unapofika kwenye kifungu cha maneno kinachohusiana na kanuni inayofundishwa katika Mathayo 6–7. Wasaidie watoto kufanya miunganiko na mambo wanayojifunza kutoka katika sura hizi.
Baba wa Mbinguni atasikia na kunijibu ninaposali.
Unapojifunza Mathayo 6:5–13; 7:7–11, unahisi watoto wanapaswa kuelewa nini kuhusu sala?
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto wasome Mathayo 6:9-13 kwa sauti na kisha kuorodhesha mambo Mwokozi Aliyosema katika sala Yake. Je, tunawezaje kufuata mfano Wake tunaposali?
-
Imba wimbo kuhusu sala pamoja na watoto, kama vile “Did You Think to Pray?” (Nyimbo, na. 140). Wasaidie watoto kupekua mashairi ya wimbo ili kupata sababu za kuomba na baraka ambazo zinazotokana na sala.
-
Wasaidie watoto kukariri Mathayo 7:7 kwa kucheza mchezo kama ufuatao: Mtoto mmoja anakariri neno la kwanza au maneno kutoka kwenye aya hiyo na kisha kurusha mpira kwa mtoto mwingine, ambaye kisha anakariri neno au kirai kinachofuata.
-
Igiza Mathayo 7:9–10 pamoja na watoto kwa kutumia vifaa rahisi. Waombe watoto washiriki kile hiki kinawafundisha nini wao kuhusu sala.
-
Shiriki wakati ulipohisi kwamba sala zako zilijibiwa.
Ninaweza kutafuta hazina za milele badala ya hazina za kidunia.
Ni kwa jinsi gani unaweza kusaidia watoto unaowafundisha kuthamini zaidi vitu vya milele kuliko vitu vya kiulimwengu?
Shughuli Yamkini
-
Leta sanduku la “hazina” likiwa limejaa vitu au picha ambazo zinawakilisha vitu ambavyo ulimwengu huthamini—kwa mfano, pesa au mwanasesere. Someni Mathayo 6:19–21 pamoja, na halafu waulize watoto kukusaidia kufikiria juu ya hazina za mbinguni ambazo zinaweza kuchukua nafasi ya vitu vya kidunia katika sanduku.
-
Waalike watoto kutaja au kuchora baadhi ya mambo wanayoweza kufanya ili “kuweka … hazina mbinguni” (Mathayo 6:20).
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kushiriki na familia zao mafundisho wanayoyapenda kutoka katika Mahubiri ya Mlimani.