Agano Jipya 2023
Februari 27–Machi 5. Mathayo 8; Marko 2–4; Luka 7: “Imani Yako Imekuokoa”


“Februari 27–Machi 5. Mathayo 8–9; Marko 2–4: ‘Imani Yako Imekuokoa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Februari 27–Machi 5. Mathayo 8; Marko 2–4: Luka 7,“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Yesu anamwinua mwanaume kutoka kitandani

Februari 27–Machi 5

Mathayo 8; Marko 2–4; Luka 7

“Imani Yako Imekuokoa”

Unaposoma Mathayo 8; Marko 2–4; na Luka 7 wiki hii, fikiria kuhusu watoto unaowafundisha. Sali kwamba Roho Mtakatifu akuongoze wewe kwa mawazo yatakayowasaidia kugundua kweli katika sura hizi.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waombe watoto washiriki hadithi ya Yesu akifanya muujiza (ona orodha ya miujiza katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Nifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia). Unaweza pia kuonyesha picha zinazohusiana (kama vile Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 40).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mathayo 8; Marko 2–3; Luka 7

Yesu ana nguvu ya kutenda miujiza.

Wakati unaposoma kuhusu miujiza ya uponyaji ya Mwokozi, tafakari miujiza gani ya kushiriki. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kazi ya imani katika miujiza ambayo Yesu aliitenda?

Shughuli Yamkini

  • Shiriki hadithi ya mtu mwenye kupooza kutoka Marko 2:1–12. Kwa msaada, ona “Sura ya 23: Mtu Ambaye Hakuweza Kutembea” (katika Hadithi za Agano Jipya, 57–58, au video zinazofanana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Eleza kwamba mtu mwenye kupooza hakuweza kutembea. Wasaidie kutambua kwamba mtu huyu aliponywa na Mwokozi.

  • Waalike waelezee kuhusu wakati walipokuwa wagonjwa. Simulia moja ya hadithi za Yesu akimponya mgonjwa, kama vile Mathayo 8:1–4, 5–13, 14–15; Marko 3:1–5; Luka 7:11–16. Waalike watoto kusimilia tena hadithi hii kwa maneno yao wenyewe. Shuhudia kwamba nguvu ya Yesu inaweza kuponya, kubariki, na kutufariji.

Mathayo 8; Marko 2–3; Luka 7

Ninaweza kuonyesha upendo kwa wengine kama Yesu alivyofanya.

Yesu alionyesha upendo mkuu kwa kuponya wenye magonjwa na walioathirika. Tafakari jinsi unavyoweza kuwafundisha watoto kuonyesha huruma kwa watu wenye shida.

Shughuli Yamkini

  • Chagua hadithi moja au zaidi za Yesu akionyesha upendo kwa mtu aliye katika shida, kama vile zile zilizoko katika Mathayo 8:1–4, 5–13, 14–15; Marko 2:1–12; 3:1–5; Luka 7:11–16. (Ona pia video “Widow of Nain” kwenye ChurchofJesusChrist.org.) Elezea juu ya wakati ambapo mtu alionyesha upendo kwako wewe katika wakati wa shida na jinsi ulivyojisikia. Waalike watoto kushiriki uzoefu wao.

  • Onyesha video “Gordon Hinckley: Lessons I Learned as a Boy” au “The Coat” (ChurchofJesusChrist.org). Ni kwa jinsi gani watoto kwenye video hizi wanafuata mfano wa Yesu? Waalike watoto kushiriki hali zingine wakati mtu anaweza kuwa na mahitaji. Nini tunaweza kufanya kuwasaidia?

  • Imbeni wimbo kuhusu kuonyesha upendo na ukarimu kwa wengine, kama vile “Kindness Begins with Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,145).

Picha
Yesu ndani ya mashua akituliza dhoruba

Kutoka Nuru hadi Imani, na Howard Lyon

Marko 4:35–41

Wakati ninapokuwa na woga au hatarini, Yesu anaweza kunisaidia nijisikie amani.

Tukio la Yesu akituliza dhoruba linaweza kuwasaidia watoto kujua kwamba Anaweza kuwapatia amani wakati wanahisi hofu.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto wafikirie kwamba wapo kwenye meli unaposoma Marko 4:35–41. (Ona pia “Sura 21: Yesu Anaamuru Upepo na Mawimbi,” katika Hadithi za Agano Jipya, 53, au video inayofanana katika ChurchofJesusChrist.org.) Waombe watoto kuelezea jinsi ambavyo wangejisikia kama wangekuwa pale. Je, ni lini watoto waliogopa? Ni kwa jinsi gani walipata faraja?

  • Waalike watoto kutoa sauti ya dhoruba na kuacha wakati mmoja wao anaposema “Nyamaza, utulie.” Shuhudia kwamba kama vile Yesu anaweza kuleta amani wakati kuna dhoruba nje, Anaweza kutuletea amani mioyoni mwetu tunapojisikia vibaya ndani yetu.

  • Fikiria matendo yenye kuendana na mstari wa tatu wa “Tell Me the Stories of Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,, 57), na muimbe mstari huo kwa pamoja wakati mkifanya matendo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mathayo 8; Marko 2–3; Luka 7

Yesu anaweza kutenda miujiza kwenye maisha yangu kama ninakuwa na imani Kwake Yeye.

Yesu alifanya miujiza mingi wakati wa huduma Yake duniani. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuwa na ufahamu kwamba miujiza inatokea leo?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kuchagua moja ya miujiza ifuatayo ili kusoma kuhusu na kuchora: Mathayo 8:1–4, 5–13, 14–15; Marko 2:1–12; 3:1–5; Luka 7:11–16. Waalike watoto kuelezea michoro yao kwa darasa. Tunajifunza nini kuhusu Yesu kutoka katika mistari hii?

  • Waombe watoto kuigiza jinsi wanavyohisi wakati wanapokuwa wagonjwa, na huzuni, hofu, au wasiwasi. Ni kwa jinsi gani Yesu anatusaidia wakati tunapokuwa na hisia hizi? Shuhudia kwamba Yesu anaweza kuwasaidia watoto kwenye hali hizi zote.

  • Waalike watoto washiriki uzoefu wakati wao au mtu mwengine wanayemfahamu alipokea baraka ya ukuhani. Ni kwa jinsi gani aliponywa au kubarikiwa?

Marko 2:15–17; Luka 7:36–50

Yesu anatupenda hata tunapokuwa tumetenda dhambi na anataka kutusaidia tutubu.

Hadithi hii katika Marko 2:15–17 na Luka 7:36–50 inaweza kuwasaidia watoto kuelewa kwamba Yesu anatupenda hata tunapokuwa tumetenda dhambi. Anataka kutusaidia tutubu na kusogea kwake.

Shughuli Yamkini

  • Andika Je, Yesu anajisikiaje kuhusu dhambi? na Yesu anajisikiaje kuhusu sisi tunapotenda dhambi? ubaoni. Waombe watoto kufikiria kuhusu maswali haya wanaposoma kwa pamoja Marko 2: 15–17 na kisha washiriki majibu yao. (Yawezekana ukataka kusoma pamoja “Mtoza ushuru” katika Mwongozo wa Maandiko [scriptures.ChurchofJesusChrist.org].) Kwa nini ni muhimu kujua kwamba Yesu anatupenda, ingawaje sisi hatujawa wakamilifu? Kujua hili kunatusaidiaje sisi tunapohitaji kutubu?

  • Siku chache kabla ya darasa, mwalike mmoja wa watoto na mwanafamilia kuja Kanisani wakiwa wamejiandaa kushiriki hadithi iliyomo katika Luka 7:36–50. Pengine wangeweza kuchora picha yenye kuonyesha sehemu za hadithi hii ili kuionyesha kwa darasa. Jadili pamoja na watoto kile Bwana angetaka sisi kujifunza kutoka katika hadithi hii.

Marko 4:35–41

Wakati ninapokuwa na woga au hatarini, Yesu anaweza kunisaidia nijisikie amani.

Watoto wanahitaji kujua kwamba Mwokozi anaweza kuwapatia amani wakati wanapokabiliana na dhoruba za maisha—sasa na katika wakati ujao.

Shughuli Yamkini

  • Muombe mmoja wa watoto kutumia Marko 4:35–41 na picha Yesu Anatuliza Dhoruba (Kitabu cha Sanaa ya Injili,, na. 40) ili kusimulia hadithi ya Yesu Akituliza Dhoruba. Waombe watoto kuelezea jinsi ambavyo wangejisikia kama wangekuwa pale.

  • Waalike watoto waelezee matukio wakati walipojisikia amani baada ya kusali kwa ajili ya msaada. Wakumbushe kwamba amani hii inatoka kwa Mwokozi.

  • Mpatie kila mtoto karatasi ya wingu la mvua, na waombe kuandika jaribu ambalo mtu anaweza kupata. Weka mawingu yote ubaoni, yakifunika picha ya Mwokozi. Mwalike mtoto kuondoa moja ya mawingu na shauri njia ambayo tungeweza kumsaidia mtu mwenye majaribu kupata amani. Wakati mawingu yote yakishatolewa, shuhudia juu ya nguvu ya Mwokozi kutuliza dhoruba za maisha yetu.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wasaidie watoto kuandika na kuigiza huduma watakazofanya kwa mtu fulani wiki hii.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto ni wachangamfu. Wakati mwingine unaweza kuhisi kwamba uchangamfu wa watoto ni vurugu kwenye kujifunza. Lakini unaweza kujenga juu ya asili hiyo ya uchangamfu wao kwa kuwaalika kuigiza hadithi au kufanya matendo yanayofanana na matukio katika wimbo au andiko. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi25.)

Chapisha