“Machi 13–19. Mathayo 11–12; Luka 11: ‘Nami Nitawapumzisha’’’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)
“Machi 13–19. Mathayo 11–12; Luka 11, “ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023
Machi 13–19
Mathayo 11–12; Luka 11
“Nami Nitawapumzisha”
Mawazo ya kufundisha katika muhtasari huu yamekusudia kusaidia kutoa msukumo kwenye ubunifu wako wenyewe. Hisi kuwa huru kuyatohoa kukidhi mahitaji ya watoto unaowafundisha.
Alika Kushiriki
Wahimize watoto kushiriki kile wanachoweza kufanya ili kumwabudu Bwana siku ya Sabato.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Yesu Atanisaidia ninapokuja Kwake.
Watoto wanaweza kuhisi kufarijika wakijua kwamba Yesu Atawasaidia na mizigo yao watakapokuja Kwake.
Shughuli Yamkini
-
Soma Mathayo 11:28–30, na uonyeshe picha ya ng’ombe maksai waliotiwa nira katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waombe watoto waoneshe kwa kidole ng’ombe maksai na nira yake. Elezea kwamba hao ng’ombe maksai waliotiwa nira kwa pamoja wanaweza kuvuta mzigo mkubwa zaidi kuliko kama wakivuta kila mmoja peke yake. Shuhudia kwamba tunapojisikia vibaya, wasiwasi, au woga, tunaweza kumtafuta Yesu na Yeye atatusaidia.
-
Muombe mtoto kunyanyua kitu kizito. Wakati anapohangaika, jitolee kumsaida. Ni kwa jinsi gani Yesu hutusaidia kufanya mambo magumu? Shiriki uzoefu wako ambapo wewe ulihisi Yesu anakusaidia kufanya jambo gumu, na waombe watoto washiriki uzoefu wao wenyewe.
Ninaweza kuishika kitakatifu siku ya Sabato.
Je, ni njia gani za kujifurahisha ambazo unaweza kuwafundisha watoto kuhusu siku ya Sabato na kwa nini tunaishika kitakatifu?
Shughuli Yamkini
-
Soma Mathayo 12:10–13 kwa sauti. Waalike watoto kusimama na kukaa kila wakati unaposema “Sabato,” na rudia pamoja nao kirai “Ni [sahihi] kufanya vyema katika siku za Sabato” (Mathayo 12:12). Wanafikiri hiyo ina maana gani?
-
Onyesha kalenda kwa watoto na angazia siku ya Sabato kwa ajili yao. Tunafanya kitu gani katika siku zingine za wiki? Tunaweza kufanya nini katika kuifanya Sabato iwe tofauti na siku zingine (ona Isaya 58:13–14).
-
Waombe watoto wachore mambo mazuri wanayoweza kufanya katika siku ya Sabato (ona ukurasa wa shughuli ya wiki).
-
Waalike watoto wabuni vitendo vya kuwasaidia kukumbuka njia tunayoweza kuwa tayari kwa Sabato wanapoimba wimbo “Saturday” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 196).
-
Chora macho, masikio, mdomo, na mikono katika ubao. Waombe watoto kukuambia ni kitu gani kila sehemu ya miili yetu inaweza kufanya ili kuishika siku ya Sabato kitakatifu.
Baba wa Mbinguni hutupa zawadi nzuri.
Mafundisho ya Mwokozi katika Luka 11:11–13 yanaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda na anataka kuwabariki.
Shughuli Yamkini
-
Tumia somo la vitendo kuelezea mafundisho ya Mwokozi katika Luka11:11–13. Kwa mfano, kuweka jiwe ndani ya mfuko wa mkate au weka picha ya nge ndani ya katoni ya mayai. Waulize watoto wabashiri ni kitu gani kilicho ndani, kisha waonyeshe. Waalike kubadilisha jiwe au picha ya nge na kipande cha mkate au yai. Soma Luka 11:11–13, na shiriki ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbinguni anatupenda, anajibu sala zetu na anatupatia baraka nyingi kupitia Roho Wake.
-
Imbeni pamoja wimbo kuhusu upendo wa Mungu, kama vile “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,, 228–29). Ni zipi baadhi ya zawadi nzuri ambazo Yeye ametupatia sisi? Waombe watoto kuchora picha za baraka kutoka kwa Baba wa Mbinguni ambazo kwazo wao wana shukrani.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Yesu Atanisaidia ninapokuja Kwake.
Unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa kwamba Mwokozi Atawapatia pumziko kutokana na changamoto zao wanapokuja Kwake?
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto washiriki nyakati walipokuwa na woga au wasiwasi kuhusu jambo fulani. Waalike wapekue Mathayo 11:28–30 kwa ajili ya ushauri ambao unaweza kuwasaidia katika hali kama hizo. Mwokozi “anatupumzishaje [sisi]”? (mstari wa 28).
-
Waalike watoto wachore picha za vitu wanavyovifanya ili kuja kwa Yesu na kujifunza juu Yake.
-
Wasaidie watoto kukariri makala ya imani ya nne. Zungumza nao kuhusu jinsi gani kila moja ya kanuni na ibada za kwanza za injili zinatusaidia kukubali mwaliko wa Yesu wa, “Njooni kwangu” (Mathayo 11:28).
Sabato ni siku ya kufanya mambo mema ambayo hunileta karibu zaidi na Mungu.
Watoto unaowafundisha wataimarika unaposisitizia malengo na baraka za kuishika siku ya Sabato kitakatifu.
Shughuli Yamkini
-
Mwalike mtoto aigize kama mtu yule ambaye mkono wake uliponywa na Mwokozi (ona Mathayo 12:10–13). Mtoto mwingine anaweza kumwuliza maswali kuhusu uzoefu huo.
-
Someni pamoja Mathayo 12:12. Je, ni mambo gani mazuri tunaweza kufanya katika Sabato? Waache watoto wachore mawazo yao katika ukurasa wa shughuli ya wiki hii, kata vipande, na fanyeni zamu katika kuweka kila chemsha bongo ya moja na mwingine pamoja.
-
Ficha picha kadhaa za watu wakifanya mambo yanayoonyesha upendo kwa Baba wa Mbinguni katika siku ya Sabato. Waombe watoto kutafuta picha hizo na kushiriki jinsi kufanya vitu vilivyomo katika picha huonyesha upendo wetu kwa Mungu.
Vyote viwili, matendo yangu na moyo wangu lazima viwe safi.
Mwokozi alifundisha kwamba haitoshi kuonekana mwenye haki kwa wengine. Mawazo yetu, hisia, na matendo ya sirini lazima pia yawe safi.
Shughuli Yamkini
-
Ili kufafanua mistari hii inafundisha nini, waonyeshe watoto kikombe au chombo kingine ambacho kiko safi kwa nje lakini kichafu ndani. Wasaidie kufikiri kuhusu “nje ya kikombe” inaweza kuwakilisha nini. Je, “sehemu ya ndani” inawakilisha nini? Kwa nini ni muhimu kusafisha kote nje na ndani?
-
Someni pamoja baadhi ya maandiko ambayo yanasisitiza uadilifu kote ndani ya mioyo yetu na matendo yetu—kwa mfano, Zaburi 24:3–5; Mathayo 15:7–8; Moroni 7:6–9. Jadili kwa nini Mwokozi anataka mioyo yetu na matendo yetu binafsi kuwa safi kiroho.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wahimize watoto kushiriki na familia zao mawazo ya kuishika siku ya Sabato kitakatifu.