Agano Jipya 2023
Machi 20–26. Mathayo 13; Luka 8; 13: “Mwenye Masikio na Asikie”


“Machi 20–26. Mathayo 13; Luka 8:13: ‘Mwenye Masikio na Asikie’’’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Machi 20–26. Mathayo 13; Luka 8:13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
ngano tayari kuvunwa

Machi 20–26

Mathayo 13; Luka 813

“Mwenye Masikio, na Asikie”

Mafumbo ni hadithi rahisi zinazoweza kuwavutia watoto. Muhtasari huu na Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia vinaweza kukusaidia kutumia mafumbo ya Mwokozi ili kuwafundisha watoto kweli muhimu.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Lete vitu kadhaa ambavyo vitawasaidia watoto kukumbuka baadhi ya mafumbo katika Mathayo 13, kama vile mbegu, lulu, au sanduku la hazina. Waalike watoto kushiriki kile wanachokumbuka kuhusu mafumbo haya.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mathayo 13:1–23

Nahitaji kujiandaa kujifunza mafundisho ya Yesu.

Watoto wadogo wanaweza wasielewe ishara zote kwenye fumbo la mpanzi, lakini wanaweza kujifunza ukweli wa injili rahisi linalofundisha. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kuelewa vizuri jinsi fumbo hili linavyohusiana nao?

Shughuli Yamkini

  • Onyesha aina mbali mbali za udongo (au picha za udongo) unapofanya muhtasari Mathayo 13:3–8. Mpe kila mtoto mbegu, na uulize wangeweza kufanya nini ili kusaidia mbegu hiyo ikue. Eleza kwamba shuhuda zetu ni kama mbegu. Ni kwa jinsi gani tunasaidia shuhuda zetu “mbegu” kukua?

  • Tumia ukurasa wa shughuli wa wiki hii ili kuwasaidia watoto kuelewa kile kila aina ya udongo ulioelezwa katika Mathayo 13 unafundisha kuhusu mioyo yetu. Waulize watoto ni aina gani ya moyo Yesu anawataka kuwa nao ili kujifunza mafundisho Yake.

  • Soma Mathayo 13:9, 15, na uwaalike watoto kuonyesha sehemu mbalimbali za mwili wao wakati wakisikia zimetajwa. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia sehemu hizi za mwili kujifunza mafundisho ya Yesu?

Mathayo 13:24–30, 36–43, 47–48

Baba wa Mbinguni ananitaka nifanye chaguo sahihi.

Baadhi ya mafumbo ya Yesu yanafundisha kwamba siku ya mwisho, Mungu atawatenga waovu kutoka kwa wenye haki. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia mafumbo kuwashawishi watoto kuchagua kile kilicho sahihi?

Shughuli Yamkini

  • Waache watoto waigize fumbo la ngano na magugu (ona Mathayo 13:24–30). Elezea kwamba ngano inawakilisha watu wanaofanya chaguo sahihi na magugu (majani hatari) yanawakilisha watu ambao hawafanyi hivyo. Siku moja, Baba wa Mbinguni atawakusanya watu wenye haki kuishi Naye.

  • Wape watoto baadhi ya mifano ya chaguzi nzuri na mbaya. Waombe watoto kusema “chaguo la ngano” wakati unapoelezea uchaguzi sahihi “chaguo la magugu” wakati unapoelezea uchaguo mbaya.

  • Lete picha za mabua ya ngano, na waache watoto wachore katika picha baadhi ya njia wanaweza kuwa wenye haki.

Mathayo 13:44–46

Uumini wangu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni hazina.

Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia taswira ya hazina na lulu za thamani ili kuwasaidia watoto kuelewa thamani ya kuwa wa Kanisa la Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Ficha picha za kasha la hazina na lulu katika chumba, na waache watoto wazitafute. Tumia picha kufundisha kuhusu mafumbo katika Mathayo 13:44–46. Zungumza kuhusu kwa nini mtu anaweza kuacha kila kitu walichonacho kwa ajili ya lulu nzuri au hazina katika shamba. Elezea kwamba wakati mwingine tunatoa kitu kizuri kwa ajili ya kitu kilicho bora zaidi. Waambie watoto kwa nini injili ni ya thamani kwako.

  • Weka katika sanduku au kasha vitu kadhaa au picha ambazo zinawakilisha “hazina” katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, kama vile Mwokozi, mahekalu au Kitabu cha Mormoni. Muombe kila mtoto kuchagua kitu au picha na kuzungumza kuhusu kwa nini hiyo ni hazina.

  • Imbeni pamoja “The Church of Jesus Christ” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77), na waulize watoto sababu za wao kuwa wenye shukrani kwa ajili ya Kanisa la Mwokozi. Shuhudia juu ya baraka ulizopata kwa sababu ya uumini wako katika Kanisa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mathayo 13:1–23

Nahitaji kuandaa moyo wangu kupokea mafundisho ya Yesu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kugundua umuhimu wa kuwa na moyo laini na ulio tayari ili kwamba Yesu aweze kuwafundisha?

Shughuli Yamkini

  • Mpangie kila mtoto kusoma kuhusu moja ya aina nne za udongo katika Mathayo 13:4–8. Waalike watafute na kushiriki kile kinachotokea kwa mbegu katika aina ya udongo wanaousoma. Ni kwa jinsi gani mioyo yetu inaweza kuwa kama aina hizi tofauti za udongo? (ona Mathayo 13:19–23).

  • Waonyeshe watoto picha ya bustani. Udongo unahitaji uweje ili mmea uweze kukua ndani yake? Onyesha picha ya udongo wenye mawe na wenye miiba. Kwa nini mimea itakuwa na wakati mgumu kukua katika aina hii ya udongo? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuhakikisha mioyo yetu iko kama udongo mzuri ili kwamba tuweze kupokea mafundisho ya Mwokozi?

  • Waalike watoto kusoma Mathayo 13; 15–17. Chora jicho, sikio, na moyo ubaoni. Ni kwa jinsi gani tunatumia kila moja ya vitu hivi kujifunza mafundisho ya Yesu?

Mathayo 13:24–30, 36–43

Ninaweza kuchagua kilicho sahihi hata kama wale walionizunguka hawachagui hivyo.

Unaposoma aya hizi ukiwafikiria watoto akilini, misukumo gani inakujia?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kuchora picha tofauti kutoka kwenye fumbo la ngano na magugu, lipatikanalo katika Mathayo 13:24–30, na shiriki michoro yao pamoja na darasa. Waombe waonyeshe michoro yao kwa kutumia tafsiri ya fumbo linalopatikana katika Mathayo 13:36–43. Unaweza kuhitaji kueleza kwamba magugu ni majani yenye madhara.

  • Kama inawezekana, onyesha picha ya ngano na magugu. Eleza kwamba ngano na magugu vitakua pamoja hadi mwisho mavuno (mwisho wa dunia). Hii inatufundisha kwamba tunaishi na yote mema na maovu yakituzunguka, na lazima tuwe makini ili kuchagua kilicho sahihi. Waombe watoto washiriki jinsi wanavyoweza kuelezea tofauti kati ya mema na maovu.

Mathayo 13:44–46

Uumini wangu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni hazina.

Je, watoto unaowafundisha wanaona uumini wao katika Kanisa kama na hazina ya thamani? Pengine kujadili mafumbo katika Mathayo 13:44–46 kunaweza kuwasaidia kushiriki hisia zao kuhusu Kanisa la Mwokozi.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wasome Mathayo 13:44–46 wao binafsi na kushiriki fumbo katika maneno yao wenyewe na mwanadarasa mwingine.

  • Kata duara kadhaa kuwakilisha sarafu, na uziweke katika sanduku la hazina. Waalike watoto kuchukua sarafu na kuchora au kuandika juu yake kitu kimoja wanachokipenda katika kuwa muumini wa Kanisa. Waombe watoto kushiriki kile walichokiweka katika sarafu.

  • Mwalike mshiriki wa kata kushiriki na watoto hadithi yake ya kuongoka na kusema ni kitu gani alichotoa dhabihu ili kujiunga na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Waombe watoto wazungumze kuhusu dhabihu wanazofanya kwa ajili ya Bwana na Kanisa Lake.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kufundisha familia zao kuhusu moja kati ya mafumbo waliyosoma katika Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto wanapenda kushiriki kile wanachojifunza. Ingawa ni wadogo, watoto wanaweza kuwaimarisha wanafamilia wao. Wahimize kushiriki na familia zao mambo waliyojifunza katika Msingi. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi30.)

Chapisha