“Machi 27–Aprili2. Mathayo 14; Marko 6; Yohana 5–6: ‘Usiogope’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)
“Machi 27–Aprili2. Mathayo 14; Marko 6; Yohana 5–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023
Machi 28–Aprili 2
Mathayo 14; Marko 6; Yohana 5–6
“Msiogope”
Unapojiandaa kufundisha kutoka Mathayo 14; Marko 6; na Yohana 5–6, angalia jumbe ambazo zinafaa kwenye maisha ya watoto unaowafundisha. Nini unafikiri kinaweza kuwasaidia kuelewa jumbe hizi? Muhtasari huu unaweza kukupatia baadhi ya mawazo.
Alika Kushiriki
Onyesha picha ya Yesu akitembea juu ya maji (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia au Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 43), na waombe watoto kushiriki kile wanachokijua kuhusu hadithi hii.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Yesu Kristo anajua kitu ninachohitaji na anaweza kunisaidia.
Fikiria hadithi ya Yesu akimponya mtu kwenye bwawa la Bethzatha. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuona kile hadithi inafundisha kuhusu wema wa Yesu, upendo, na sifa nyingine?
Shughuli Yamkini
-
Tumia picha Kristo Akiponya Wagonjwa Bethzatha (Kitabu cha Sanaa ya Injili,, na.42) ili kuwasimulia watoto hadithi katika Yohana 5:1–9. Au onyesha video “Jesus Heals a Man on the Sabbath” (ChurchofJesusChrist.org). Waambie watoto waweke dhana kwamba wao ni mtu ambaye Yesu alimponya. Ni kwa jinsi gani wangejisikia kama Yesu angewaponya?
3:3 -
Waombe watoto wataje baadhi ya mambo ambayo ni magumu kwao au yale yenye kuwahuzunisha. Waambie kuhusu wakati katika maisha yako ulipopokea msaada kutoka kwa Kristo kipindi cha jaribio gumu. Shuhudia kwamba Yesu anajua kuhusu matatizo yetu yote na anataka kutusaidia.
Ninafuata mfano wa Yesu wakati ninapokuwa mkarimu kwa wengine.
Njia moja Yesu alionyesha upendo ilikuwa ni kuwalisha wafuasi Wake walipokuwa na njaa. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujifunza kuhudumia wengine kama Yesu alivyofanya?
Shughuli Yamkini
-
Onyesha watoto kikapu na mkate unapowasimulia hadithi katika Mathayo 14:13–21. Elezea kwamba ingawa Yesu alikuwa amejaribu kupata mahali pa kuwa peke yake, watu walitaka kuwa karibu na Yeye. Shiriki hadithi yote na watoto, na uwaombe wasikilize kile Yesu alichofanya ili kuonyesha ukarimu na upendo watu wale.
-
Waombe watoto kushiriki njia ambazo mtu fulani amekuwa mkarimu kwao. Kisha wasaidie kufikiria njia wanazoweza kuwa wakarimu kwa wengine. Kwa kila jibu wanalotoa, chora mkate au samaki katika ubao. Waambie watoto kwamba wanapofanya vitu hivi, wanafuata mfano wa Yesu aliotoa wakati alipowalisha watu elfu tano waliokuwa na njaa.
Imani katika Yesu Kristo inaweza kunisaidia kutoogopa.
Petro alionyesha imani kubwa wakati alipotembea juu ya maji kumwelekea Yesu. Masomo gani yanayoweza kuwa kwa ajili ya watoto katika hadithi hii?
Shughuli Yamkini
-
Onyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia (ona pia Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 43) unaposimulia hadithi kutoka Mathayo 14:22–33 kwa maneno yako. Fikiria kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kukusimulia wewe hadithi hiyo. Unaweza pia kuleta bakuli dogo la maji na waalike watoto kujifanya “kutembea” kwa vidole vyao kwenye uso wa maji.
-
Onyesha video ya “Wherefore Didst Thou Doubt?” (ChurchofJesusChrist.org), na waulize watoto kwa nini Petro aliogopa. Kisha waombe wasimulie kuhusu nyakati ambazo wamehisi uoga na kushiriki kile kilichowasaidia. Wasaidie kuona kwamba imani katika Yesu Kristo inatusaidia kushinda hofu.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Yesu Kristo ananifundisha kuhusu Baba wa Mbinguni.
Ni kwa jinsi gani mafundisho ya Yesu kuhusu Baba Yake yanawasaidia watoto kujifunza kuhusu Baba wa Mbinguni?
Shughuli Yamkini
-
Unda seti mbili za kadi zinazofanana zilizoandikwa kwa maneno ambayo Yesu aliyatumia kufundisha kuhusu Baba wa Mbinguni katika Yohana 5, kama vile upendo, uzima, na matendo (ona Yohana 5:20, 26, 36). Weka kadi kuangalia chini, na waombe watoto kutafuta zile zilizofanana kwa kugeuza kadi mbili kwa wakati mmoja. Pindi kila mfanano unapofanyika, soma mstari wenye neno, na uliza watoto kile neno hilo linatufundisha kuhusu Baba wa Mbinguni.
-
Waombe watoto wasome Yohana 5:30 na kisha kukamilisha sentensi hii: “Sitafuti mapenzi yangu, lakini …” Ni kwa jinsi gani Kristo anafanya mapenzi ya Baba Yake wa Mbinguni? Ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kufanya mapenzi ya Baba wa Mbinguni?
Matoleo yangu madogo yanaweza kuleta tofauti.
Ilikuwa ni mvulana mdogo ambaye alitoa mkate na samaki ambazo Yesu alitumia kuwalisha watu elfu tano. Ni kwa jiinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuona jinsi wanavyoweza kuchangia katika kazi ya Bwana?
Shughuli Yamkini
-
Wasaidie kufikiria watu elfu tano ni umati mkubwa kiasi gani. Ingelikuwaje kuwalisha watu hao wengi kwa mikate mitano na samaki wawili tu?
-
Alika mtoto kusimulia hadithi ya kulishwa kwa watu elfu tano kwa maneno yake mwenyewe. Sisitiza kwamba ilikuwa ni mvulana mdogo ambaye alitoa mkate na samaki ambazo Bwana alitumia kutenda walisha elfu tano. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama mvulana aliyeezewa katika Yohana 6:9? Alika watoto wachore mikate na samaki kwenye karatasi na waziandike vitu kadhaa wanaweza kumpatia Bwana kusaidia kazi Yake.
-
Wape watoto chamsha bongo ndogo kuikamilisha. Ni nini kingetokea kama mojawapo ya vipande vya chemsha bongo hakingekuwepo? Elezea kwamba sisi sote ni kama vipande vya chemsha bongo—sisi sote ni muhimu, na tunahitajiana. Wasaidie watoto kutaja sababu ya wao kuwa muhimu katika famiia zao, katika darasa lao Msingi, katika familia ya Mungu, na makundi mengineyo.
Imani katika Yesu Kristo inaweza kunisaidia kutoogopa.
Imani na hofu inachukua nafasi kubwa katika hadithi ya Yesu na Petro kutembea juu ya bahari. Ni nini watoto wanaweza kujifunza kutoka kwenye hadithi hii?
Shughuli Yamkini
-
Onyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia (ona pia Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 43). Waombe watoto watafute virai katika Mathayo 14:22 -33 ambavyo vinaielezea picha hii.
-
Waombe watoto watafute ishara za imani na ishara za hofu wanaposoma Mathayo 14:22–33. Ungeweza pia kuonyesha video ya “Wherefore Didst Thou Doubt?” (ChurchofJesusChrist.org). Inamaanisha nini kuwa na imani katika Yesu Kristo? Wasaidie watoto kufikiri juu ya nyakati ambapo imani yao iliwasaidia kushinda hofu.
2:6 -
Waombe watoto kufikiria kuwa walikuwepo na walikuwa na kamera wakati Yesu na Petro walipotembea juu ya bahari. Ni wakati gani wangechagua kuchukua picha na kwa nini? Pendekeza kwamba wapekue Mathayo 14:22–33 kwa ajili ya mawazo. Waalike wachore picha ya wakati waliouchagua, washiriki picha zao, na kueleza kwa nini walichagua wakati huo.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Kama watoto wamemaliza ukurasa wa shughuli ya wiki hii, waalike kuutumia kufundisha familia zao kile walichojifunza leo. Au wape nakala ya ukurasa huu ili wamalizie pamoja na familia zao nyumbani.