Agano Jipya 2023
Aprili 24–30. Yohana 7–10: “Mimi Ndimi Mchungaji Mwema”


Aprili 24–30. Yohana 7–10: ‘Mimi Ndimi Mchungaji Mwema’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

Aprili 24–30. Yohana 7–10.“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Yesu na mwanamke aliyeanguka chini

Hata Mimi Sikuhukumu, by Eva Koleva Timothy

Aprili 24–30

Yohana 7–10

“Mimi Ndimi Mchungaji Mwema”

Unaposoma Yohana 7–10, fikiria kuhusu watoto unaowafundisha. Mawazo mengi kwa ajili ya watoto wakubwa katika muhtasari huu yanaweza pia kutoholewa kwa ajili ya watoto wadogo au kinyume chake.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wakumbushe watoto juu ya kitu ambacho uliwaalika kukifanya katika somo lililopita. Waombe kushiriki kile walichokitenda ili kufanyia kazi mwaliko ule.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Yohana 7:14–17

Kuzishika amri kutanisaidia mimi kujua kuwa ni za kweli.

Yesu alifundisha kwamba tunaweza kupata ushuhuda wa kweli alizoshiriki tunapoziishi. Amani tunayojisikia wakati tunatii amri inatusaidia kujua kuwa ni za kweli. Zingatia jinsi unavyoweza kuwafundisha watoto ukweli huu

Shughuli Yamkini

  • Fupisha Yohana 7:17 katika maneno ambayo watoto wataelewa. Wasaidie wao kujua kwamba kutii amri kunatusaidia sisi kuhisi kuwa karibu zaidi na Yesu Kristo. Kwa mfano, mngeweza kuimba pamoja wimbo kama “Keep the Commandments” au “Choose the Right Way” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47, 160–61). Waombe watoto wasikilize ni jinsi gani tutabarikiwa tunapotii amri.

  • Shiriki uzoefu ulipopata ushuhuda kwamba amri hiyo ilitoka kwa Mungu kwa sababu uliishi amri hiyo, kama vile kulipa zaka au kumsamehe mtu asiye kuwa mkarimu. Waalike watoto kufikiria juu ya uzoefu waliopata wakati walipotii amri. Waalike washiriki jinsi walivyojisikia wakati walipotii.

  • Waalike watoto wajichore wao wenyewe wakitii amri. (Wasaidie kufikiria juu ya mifano.) Waalike kushiriki na wengine hizo picha zao na wazungumze kuhusu furaha wanayopata kutokana na kutii amri hiyo.

Yohana 8:29

Yesu alimtii Baba Yake.

Yesu Kristo daima Alifanya mambo yaliyompendeza Baba Yake wa Mbinguni. Ni kwa jinsi gani wewe unaweza kuwasaidia watoto kutafuta njia za kufuata mfano Wake?

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kurudia kile Yesu Alichosema kuhusu Baba wa Mbinguni katika Yohana 8:29: “Nafanya siku zote yale yampendezayo.” Waombe washiriki mambo Yesu aliyofanya ambayo yalimfanya Baba wa Mbinguni afurahi. Waonyeshe baadhi ya picha kutoka katika Kitabu cha Sanaa ya Injili ili kuwapa mawazo.

  • Waulize watoto ni nini huwafanya kuwa na furaha. Au mwalike mzazi wa mmoja wa watoto kushiriki uzoefu ambapo mtoto alifanya kitu ambacho kilimfanya mzazi aridhike au afurahi. Tunaweza kufanya nini ili kumfanya Baba wa Mbinguni afurahi? Waalike watoto kuchora picha zao binafsi wakifanya hizo shughuli ili wazipeleke nyumbani na ziwakumbushe.

Yohana 10:1–16

Yesu ananijua na ananipenda.

Fumbo la mchungaji mwema linaweza kuwasaidia watoto kuelewa kwamba Yesu anawapenda na anajua kuwa wao ni akina nani.

Shughuli Yamkini

  • Wape watoto picha ambazo zinawakilisha kitu fulani katika fumbo la mchungaji mwema, kama kondoo, mchungaji, au mbwa mwitu. Chagua baadhi ya mistari kutoka Yohana 10:1–16 ya kuwasomea watoto, na waombe kuzinyanyua juu picha zao wakati wanapokusikia ukisoma kuhusu vitu katika picha zao. Wasaidie watoto kufikiria juu ya njia ambazo Yesu ni kama mchungaji wetu. Toa ushuhuda wako kwamba Mwokozi anatupenda na atatuongoza kuelekea Kwake.

  • Onyesha picha ya Yesu na wanakondoo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Tunajuaje kwamba Yesu Kristo anawapenda wanakondoo? Tunawezaje kuelezea kwamba wanakondoo wanampenda Yesu? Ni kwa jinsi gani tunaweza kumwonyesha Yesu kwamba tunampenda Yeye?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Yohana 7:14–17

Kuzishika amri kutanisaidia mimi kujua kuwa ni za kweli.

Wewe na watoto unaowafundisha mnaweza kuwa na uzoefu katika kuishi kweli za injili na kujifunza kuwa ni za kweli. Unawezaje kujenga juu ya uzoefu huo unapofundisha?

Shughuli Yamkini

  • Andika kila mstari wa Yohana 7:14–17 katika vipande tofauti vya karatasi na vionyeshe katika mpangilio usio na utaratibu. Waombe watoto waziweke katika mpangilio sahihi na kuangalia Yohana 7:14–17 kuona kama ziko sahihi. Waalike watoto kugawanyika katika jozi na kushiriki uelewa wao wa kila mstari na mwenzake. Ni kwa jinsi gani utii kwa amri za Mungu umewasaidia kujua kuwa amri ni za kweli?

  • Shiriki mifano kutoka katika maandiko ukionyesha jinsi gani watu walibarikiwa kwa kuishi kweli za injili, kama vile (ona Danieli 6) au Elizabeti (ona Luka 1:5–14). Je! Ni baraka gani tumepewa kutokana na kutii amri?

  • Siku chache kabla ya darasa, mwalike mmoja wa watoto kuandika kuhusu wakati ambapo alipata ushuhuda juu ya amri kwa kuiishi. Wakati wa darasa, muulize mtoto huyo kushiriki alichoandika.

Yohana 8:31–36

Ukweli unaweza kunifanya kuwa huru.

Baadhi ya watu hufikiri kuwa kuishi injili kuwazuia. Je, unawezaje kutumia Yohana 8:31–36 ili kuwasaidia watoto kuelewa kwamba kuishi injili kwa kweli kunatufanya tuwe huru?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kusoma Yohana 8:31–36 na kushiriki kile wanachofikiria kinamaanisha kuwa mtumwa wa dhambi. Ni kwa jinsi gani mafundisho ya Yesu hutusaidia kuwa huru?

  • Onyesha kufuli ili kuwakilisha dhambi na ufunguo kuwakilisha jinsi ukweli wa Injili unavyoweza kutufanya kuwa huru. Kwa mfano, kujua kuhusu Upatanisho wa Mwokozi kunaweza kutupa uhuru wa kutubu na kusamehewa dhambi zetu. Au kujua kuhusu Neno la Hekima kunaweza kutupa uhuru kuepukana na mazoea mabaya.

Picha
Yesu Akifundisha Hekaluni

Yesu alifundisha, “Kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32).

Yohana 10:1–18

Yesu ni kama mchungaji wangu.

Unaposoma fumbo la mchungaji mwema, tafuta kweli zinazofundisha kuhusu uhusiano wetu na Mwokozi. Ni kwa jinsi gani kujua kweli hizi hubariki watoto?

Shughuli Yamkini

  • Andika mchungaji mwema na kibarua katika ubao. Eleza kwamba kibarua ni mtu anayekodiwa kufanya kazi kwa malipo ya pesa. Waombe watoto kuorodhesha tofauti wanazozipata katika Yohana 10:1–18 kati ya mchungaji mwema na kibarua. Kwa nini ungehitaji kumfuata mchungaji mwema kuliko kibarua? Ni kwa jinsi gani Yesu ni kama mchungaji kwetu?

  • Chora au onyesha picha ya mlango. Someni pamoja Yohana 10:7–9, na waulize watoto ni kwa jinsi gani Yesu ni kama mlango. Kulingana na mstari wa 9, ni baraka gani zinazokuja kwa wale “wanaoingia katika” mlango? Tunaingiaje kwenye mlango ambao Yesu Kristo anatupatia?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wasaidie watoto kufikiria juu ya amri wanayoweza kutii kikamilifu zaidi. Waombe kujaribu kutii amri hiyo wakati wa wiki ijayo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Uliza maswali yenye msukumo. Uliza maswali yanayoalika watoto unaowafundisha kusonga mbele badala ya kutoa taarifa ya mambo. Badala yake, wahimize kushiriki shuhuda zao za kweli juu ya injili. Kwa mfano, kama unajadili amri, unaweza kuwauliza watoto kushiriki ni kwa jinsi gani kutii amri kumewabariki wao.

Chapisha