Agano Jipya 2023
Aprili 10–16. Mathayo 15–17; Marko 7–9: “Wewe Ndiwe Kristo”


Aprili 10–16. Mathayo 15–17; Marko 7–9: “Wewe ndiwe Kristo” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

Aprili 10–16. Mathayo 15–17; Marko 7–9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Kugeuka Sura kwa Kristo

Kugeuka Sura kwa Kristo, na Carl Heinrich Bloch

Aprili 10–16

Mathayo 15–17; Marko 7–9

“Wewe Ndiwe Kristo”

Unapotafakari Mathayo 15–17 na Marko 7–9, kuwa makini na misukumo ya kiroho ambayo inaweza kukusaidia kujua kile watoto katika darasa lako wanahitaji.

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto washiriki ni kwa nini wana shukrani kwa ajili ya viongozi katika Kanisa, ikijumuisha nabii na mitume na viongozi wa eneo husika. Je, hivi karibuni tumewasikia wakifundisha nini?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mathayo 16:13–17

Ninaweza kupata ushuhuda kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

Fikiria jinsi unavyoweza kutumia ushuhuda wa Petro na majibu ya Yesu kufundisha watoto juu ya ushuhuda ni nini na kuwashawishi kutafuta ushuhuda wao wenyewe.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wasikilize kile Petro alichosema unaposoma Mathayo 16:15–17. (Ona pia “Sura ya 32: Petro Akishuhudia juu ya Kristo,” katika Hadithi za Agano Jipya, 76–77, au video inayofanana nayo katika ChurchofJesusChrist.org.) Elezea kwamba Petro alikuwa akitoa ushuhuda wake juu ya Yesu Kristo. Soma mistari huo tena. (Au onyesha video hiyo tena.) Wakati huu waombe watoto kusikiliza ni nani alimwambia Petro kwamba Yesu Alikuwa Mwana wa Mungu.

  • Toa ushuhuda wako juu ya Yesu Kristo, na ueleze jinsi ulivyoupokea. Waalike watoto kutafuta ushuhuda wao wenyewe kutoka kwa Baba wa Mbinguni.

Mathayo 16:15–19

Yesu Kristo anawapa manabii na mitume funguo za ukuhani ili kuliongoza Kanisa Lake.

Mwokozi anafananisha ufunuo na mwamba, mamlaka ya ukuhani na funguo. Je, unawezaje kutumia milinganisho hii ili kuwasaidia watoto kuwa na imani kwa wale wanaoliongoza Kanisa Lake?

Shughuli Yamkini

  • Onyesha watoto mwamba unaposoma Mathayo 16:18 pamoja nao. Rudia pamoja nao kirai “juu ya mwamba huu Nitalijenga Kanisa Langu,” ukiongezea vitendo sambamba na maneno. Eleza kwamba Kanisa limejengwa juu ya “mwamba” wa ufunuo.

  • Onyesha watoto baadhi ya funguo, na waulize tunatumia funguo kufanya nini. Elezea kwamba Petro na Mitume wengine walipokea funguo za ukuhani kutoka kwa Yesu. Funguo hizi “zinafungua” baraka kwetu na zinafungua njia ya kwenda mbinguni. Kwa mfano, funguo za ukuhani zinaturuhusu sisi kubatizwa na kupokea sakramenti. Wapatie watoto funguo za karatasi, wafanye waandike baadhi ya baraka ambazo funguo za ukuhani “zinafungua”

  • Onyesha picha ya Rais wa Kanisa, na toa ushuhuda wako kwamba anashikilia funguo zote za ukuhani leo, kama vile Petro alivyofanya.

sanamu ya Petro akiwa ameshikilia funguo

Funguo za ukuhani ni mamlaka ya kuelekeza matumizi ya ukuhani.

Mathayo 17:19–20

Imani yangu inaweza kutenda miujiza.

Tunaposoma ahadi ya Yesu kwamba imani ni kama punje ya mbegu ya haradali inaweza kuhamisha mlima, ni misukumo gani unayopokea kuhusu watoto unaowafundisha?

Shughuli Yamkini

  • Soma Mathayo 17:19–20 pamoja na watoto. Waalike kufanya zamu kuchora milima mikubwa na mbegu ndogo ubaoni. Elezea kwamba milima ni kama mambo ambayo ni magumu kwetu sisi kuyafanya. Ni mambo gani ambayo yanaweza kuonekana kama milima kwetu sisi? Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kufikiria kuhusu jinsi imani inavyoweza kuwasaidia kufanya mambo ambayo Mungu anawataka wafanye.

  • Weka picha ya mlima kwenye upande mmoja wa chumba. Waombe watoto kutaja baadhi ya mambo wanayoweza kufanya ili kupata imani zaidi katika Yesu Kristo. Acha kila mtoto anayetaja kitu fulani ahamishe mlima karibu na upande mwingine wa chumba. Soma Mathayo 5:19–20, na ushuhudie juu ya nguvu ya imani katika maisha yako.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu imani, kama vile “Faith” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96). Mpe kila mtoto mbegu aende nayo nyumbani. Waalike wapande mbegu hiyo na kuiweka mahali ambapo wanaweza kuiona ikikua ili kuwasaidia kukumbuka kuwa na imani katika Baba na Mbinguni na Yesu Kristo.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mathayo 16:13–17

Ushuhuda juu ya Yesu Kristo unakuja kwa ufunuo.

Ni kwa jinsi gani ushuhuda wa Petro katika Mathayo 16:13–17 unawasaidia watoto wanapojenga shuhuda zao?

Shughuli za Yakini

  • Waulize watoto wao wangesema nini kama mtu angewauliza, “Yesu ni nani?” Alika watoto wasome Mathayo 16:13–17 ili kupata ni jinsi gani Petro alijibu swali hilo. Aliupataje ushuhuda wake juu ya Yesu? Tunaweza kufanya nini ili kuimarisha shuhuda zetu?

  • Wasaidie watoto kulinganisha njia tunayojua kweli za kiroho na jinsi tunavyojua kweli nyinginezo. Kwa mfano, tunajuaje mtu ni mrefu kiasi gani au hali ya hewa ikoje? Tunajuaje kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu? Waambie watoto jinsi Roho Mtakatifu alivyoshuhudia kwako juu ya Mwokozi.

  • Toa ushuhuda wako juu ya Yesu Kristo, na wape changamoto watoto ya kupata au kuimarisha shuhuda zao juu Yake.

Mathayo 16:15–19

Kanisa la Yesu Kristo linaongozwa na wale wanaoshikilia funguo za ukuhani.

Kujifunza Mathayo 16 :15–19 kunaweza kujenga imani ya watoto kwamba Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni urejesho wa Kanisa lile lile ambalo Yesu alilianzisha wakati Yeye alipokuwa akiishi duniani.

Shughuli za Yakini

  • Andika Mathayo 16:19 kwenye ubao, ukiacha maneno machache, likiwemo neno “funguo.” Waombe watoto kutafuta maneno yanayokosekana.

  • Onyesha video ya “Wherefore Are the Keys?” (ChurchofJesusChrist.org), au rejelea “Funguo za Ukuhani” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Funguo za ukuhani ni nini? Ni kwa jinsi gani funguo za ukuhani ni kama funguo halisi?

  • Wasaidie watoto kuorodhesha kwenye ubao baadhi ya watu wenye funguo za ukuhani. “Funguo za Ukuhani” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org) kuna orodha ambayo inaweza kuwasaidia. Alika mtu kwenye kata yako ambaye anashikilia funguo za ukuhani kushiriki kwa kifupi na darasa kwa nini funguo za ukuhani ni muhimu.

  • Ficha funguo kadhaa (au picha za funguo) kote chumbani, na alika watoto kuzitafuta. Baada ya kila ufunguo kupatikana, wasaidie watoto kufikiria juu ya baraka tunazofurahia kwa sababu ya funguo za ukuhani (kwa mfano, familia za milele, ubatizo, na sakramenti).

Mathayo 17:1–9

Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.

Aya hizi zinaelezea moja ya nyakati chache katika maandiko wakati sauti ya Mungu Baba iliposikika ikishuhudia juu ya Mwanawe Mpendwa. Kujifunza tukio hili pamoja na watoto kunaweza kujenga imani yao katika Yesu Kristo.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto wachore picha za tukio lililoelezewa katika Mathayo 17:1–9. Waombe kuelezeana picha zao wao kwa wao. (Ona “Sura ya 33: Akionekana katika Utukufu: Kugeuka Sura,” katika Hadithi za Agano Jipya, 78–79, au video inayofanana nayo kwenye ChurchofJesusChrist.org.)

  • Wape watoto muda kutafakari kuwa hadithi hii katika Mathayo 17:1–9 inawafundisha nini kuhusu Yesu Kristo. Waalike kuandika mawazo yao ubaoni. Alika kushiriki jinsi wanavyojua kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Alika watoto kuwauliza wazazi wao au wanafamilia wengine jinsi gani walipata shuhuda zao juu ya Yesu Kristo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia muziki. Nyimbo za msingi na nyimbo za dini zinaweza kuwasaidia watoto wa rika zote kuelewa na kukumbuka kweli za injili. Kuimba pia kunaweza kuwafanya watoto kuwa wachangamfu katika kujifunza. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi22.)