Agano Jipya 2023
Aprili 3–9. Pasaka: “Ee Kaburi, U Wapi Ushindi Wako?”


Aprili 3–9. Pasaka: ‘Ee Kaburi, U Wapi Ushindi Wako?,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2023 (2022)

Aprili 3–9. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Kaburi la Bustani.

Aprili 3–9

Pasaka

“Ee Kaburi, U Wapi Ushindi Wako?”

Tumia muda wako na watoto kuwasaidia kuona pasaka kama kipindi cha kufurahia katika Mwokozi na kuongeza shukrani zao kwa dhabihu Yake. Mawazo katika muhtasari huu yanaweza kutoholewa ili kukusaidia kufundisha watoto wa rika lolote.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha za Mwokozi akiwa Gethsemane, juu ya msalaba, na baada ya Ufufuko Wake (ona picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 56–60). Waombe watoto kushiriki kitu wanachojua kuhusu matukio ya kwenye picha.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Yesu Kristo ni Mwokozi wangu.

Unaposoma kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo, tafakari ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuhisi ni kiasi gani Yesu Anawapenda.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya Yesu, na uwaalike watoto kushiriki kile wanachokijua kuhusu kile alichokifanya kwa ajili yetu sisi. Shiriki ushuhuda wako juu ya upendo wa Mwokozi na uwezo Wake wa kutuokoa kutoka dhambini. Inua kioo juu, na uwaache watoto waje kwa zamu kukiangalia. Kila mtoto anapotazama, sema, “Yesu anakupenda [jina la mtoto], na Anaweza kukusaidia [jina la mtoto] kuishi na Baba wa Mbinguni tena.”

  • Onyesha picha Yesu Akisali katika Gethsemane (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 56) unaposimulia hadithi ya Yesu akiteseka katika Gethsemane kwa ajili ya dhambi za ulimwengu (ona Mathayo 26:36–46; Luka 22:39–44). Shuhudia kwamba kwa sababu ya mateso Yake, tunaweza kusamehewa tukifanya uchaguzi usio sahihi. Unaweza pia kutumia “Sura ya 51: Yesu Akiteseka katika Bustani ya Gethsemane” (katika Hadithi za Agano Jipya, 129–32, au video zinazofanana katika ChurchofJesusChrist.org).

  • Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu upendo, kama vile “I Feel My Savior’s Love” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75). Wasaidie watoto kutambua maneno katika wimbo ambayo yanauelezea upendo wa Mwokozi. Je, nini kinatusaidia sisi kuhisi upendo Wake? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wengine kuhisi upendo Wake?

Picha
Yesu na Mariamu katika kaburi tupu

Amefufuka, na Greg Olsen

Kwa sababu Yesu alikufa na kufufuka, mimi nitaishi tena.

Unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo, sisi na wapendwa wetu tutafufuka siku moja?

Shughuli Yamkini

  • Wafundishe watoto hadithi ya Pasaka kwa kutumia picha ya Kristo katika Gethsemane, juu ya msalaba, na baada ya ufufuko Wake (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 56–60 na ukurasa mzima katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waache watoto wachache washikilie picha wakati unasimulia hadithi. Waeleze watoto kuhusu watu waliomuona Yesu baada ya kufufuka, kama vile Mariamu (ona Yohana 20:1–18) au Tomaso (ona Yohana 20:24–29).

  • Waulize watoto kwa nini tunasherehekea Pasaka. Eleza kwamba katika Pasaka tunasherehekea siku Yesu Kristo alifufuka. Uliza kama watoto wangependa kushiriki kile familia zao hufanya ili kukumbuka Ufufuo wa Yesu Kristo.

  • Eleza kwamba kufufuka inamaana kuishi tena baada wa kufa kwetu. Toa ushuhuda wako kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo, sisi tutafufuliwa—tutaishi tena baada ya kufa, na katu hatutakufa tena.

  • Tumia glavu kufundisha watoto kwamba sisi sote tuna mwili (ukiwakilishwa na glavu) na roho (ikiwakilishwa na mkono). Tunapokufa, roho na miili yetu hutengena. Roho zetu zinaendelea kuishi, lakini miili yetu haiishi. Tunapofufuliwa, roho na miili yetu huungana tena. Acha watoto wachukue zamu kuvaa na kuvua glavu.

  • Imbeni pamoja wimbo wa pasaka, kama vile “Did Jesus Really Live Again?” au “Jesus Has Risen” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64, 70) na waonyeshe watoto picha za Yesu baada ya kufufuka (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.59-61).

  • Onyesha picha ya mtu fulani unayemjua kuwa alifariki. Shiriki ushuhuda wako kwamba yeye atafufuka sababu ya Upatanisho na Ufufuko wa Yesu Kristo.

  • Tazameni pamoja video ya “Jesus Is Resurrected” au “The Risen Lord Appears to the Apostles” (ChurchofJesusChrist.org). Au onyesha video nyingine ya Pasaka inayopatikana katika Easter.ComeuntoChrist.org.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Yesu Kristo aliteseka kwa ajili yangu huko Gethsemane na juu ya msalaba.

Unapojifunza maandiko wiki hii, tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kujenga imani yao katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake.

Shughuli Yamkini

  • Soma pamoja na watoto Luka 22:39–44 na mistari iliyochaguliwa kutoka Mathayo 27:29–50. Waalike kutafuta maneno ambayo yanawasaidia kuelewa kile Mwokozi alipitia katika Gethsemane na juu ya msalaba.

  • Wasaidie watoto kukariri makala ya tatu ya imani. Toa ushuhuda wako kwamba Yesu Kristo ana uwezo wa kutuokoa kutoka katika dhambi na kifo.

  • Wasaidie watoto kuandaa mahubiri mafupi kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo ambayo wataweza kushiriki na wengine. Wahimize kujumuisha maandiko na shuhuda zao katika mahubiri yao. Kama wanahitaji msaada wa ziada, wangeweza kusoma “Lipia Dhambi, Upatanisho” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org).

Kwa sababu Yesu alikufa na kufufuka, mimi nitaishi tena.

Watoto unaowafundisha siku moja watakumbwa na kifo cha mpendwa wao kama bado hawajakumbwa. Wasaidie kujua kwamba kwa sababu Yesu Kristo alifufuka, sisi sote tutafufuliwa.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha na. 57–59 katika Kitabu cha Sanaa ya Injili, na waombe watoto kulinganisha picha na vipengele vinavyofuata: Mathayo 27:29–38, 59–60; Yohana 20:10–18.

  • Waalike watoto kila mmoja binafsi kusoma “Ufufuo” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org) na watafute kitu ambacho wangetaka kufundisha familia zao. Wape muda watoto kushiriki kile walichokipata.

  • Wasaidie watoto kuangalia katika kielezo cha mada cha Kitabu cha Nyimbo za Watoto ili kupata wimbo ambao wangetaka kuimba kuhusu Yesu Kristo au Ufufuko. Imbeni wimbo huo pamoja, na waulize wanajifunza nini kutoka kwenye wimbo huu.

  • Onyesha video ya “Jesus Is Resurrected” (ChurchofJesusChrist.org), na waalike watoto wachache kutoa shuhuda zao kuhusu Upatanisho na Ufufuko wa Mwokozi. (Unaweza kuwauliza watoto hawa kufanya hivyo siku chache kabla ya darasa ili waweze kujiandaa.) Waalike watoto kuandika chini shuhuda zao na kuzitoa nyumbani.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwasaidia watoto kushiriki kile walichojifunza na familia zao, wahimize kuimba nyumbani wimbo kuhusu Yesu Kristo wiki hii.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto wananufaika kutokana na marudio. Usiogope kurudia shughuli mara nyingi, hususan na watoto wadogo. Marudio yatawasaidia watoto kukumbuka kile unachofundisha.

Chapisha