Agano Jipya 2023
Aprili 3–9. Pasaka: “Ee Kaburi, U Wapi Ushindi Wako?”


“Aprili 3–9. Pasaka: ‘Ee Kaburi, U Wapi Ushindi Wako?,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2023 (2022)

“Aprili 3–9. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Kaburi la Bustani.

Aprili 3–9

Pasaka

“Ee Kaburi, U Wapi Ushindi Wako?”

Unaposoma shuhuda juu ya ufufuko wa Mwokozi katika muhtasari huu, andika hisia na misukumo inayokujia kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Andika Misukumo Yako

Wakati wa wiki ya mwisho ya maisha ya Mwokozi, Wayahudi wengi waliomzunguka walikuwa wakishiriki katika tamaduni za Pasaka. Waliandaa vyakula, wakaimba nyimbo, na kukusanyika pamoja ili kukumbuka ukombozi wa nyumba ya Israeli kutoka utumwani kwa Wamisri. Familia zilisikiliza hadithi ya malaika muangamizaji akipita juu ya nyumba za mababu zao ambao waliweka alama milango yao kwa damu ya kondoo. Katikati ya sherehe hizi zilizojaa ishara nyingi za ukombozi, wachache tu walikuwa wakielewa kwamba Yesu Kristo, Mwanakondoo wa Mungu, alikuwa karibu kuwakomboa kutoka utumwa wa dhambi na kifo—kupitia mateso Yake, kifo Chake, na Ufufuko Wake. Hata hivyo, kuna wale waliomtambua Yesu kama ndiye Masiya wao aliyeahidiwa, Mkombozi wao wa milele. Toka wakati huo na kuendelea, wafuasi wa Yesu Kristo wametoa ushahidi kwa ulimwengu wote “kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu …; na kwamba alizikwa, na kwamba alifufuka tena siku ya tatu” (1 Wakorintho 15:3–4).

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mathayo 21–28

Yesu Kristo ananikomboa kutokana na dhambi na kifo, ananiimarisha mimi katika udhaifu wangu, na ananifariji katika majaribu yangu.

Njia moja ya kuzingatia kwenye baraka za Upatanisho wa Mwokozi wiki hii ni kutumia muda kila siku kusoma kuhusu wiki ya mwisho ya maisha ya Mwokozi (ratiba ya kusoma inayowezekana inafuata). Ni nini unapata katika sura hizi kinachokusaidia wewe kuhisi upendo wa Mwokozi? Tafakari sura hizi zinakufundisha nini kuhusu jinsi Yeye anavyoweza kukukomboa kutoka katika dhambi, kifo, majaribu, na udhaifu. Ni kwa jinsi gani unaifanya imani katika nguvu Zake za ukombozi?

Ona pia Easter.ComeuntoChrist.org.

Yesu msalabani

Kusulubiwa, na Louise Parker

Mathayo 28:1–10; Luka 24:13–35; Yohana 20:19–29; 1 Wakorintho 15:1–8, 55

Mashahidi wengi wanashuhudia juu ya Ufufuko wa Yesu Kristo.

Fikiria jinsi ambavyo ilikuwa kwa wanafunzi kumwangalia Yesu akifanyiwa mzaha, akisumbuliwa, na kusulubiwa. Walikuwa wameshuhudia nguvu Zake, wameona ukweli wa mafundisho Yake, na walikuwa na imani kwamba Yeye alikuwa Mwana wa Mungu. Kushuhudia kifo Chake lazima kulisababisha wanafunzi Wake kuhuzunika na kukanganyikiwa. Lakini punde walikuwa mashahidi wa muujiza mkuu wa Ufufuko Wake.

Ni nini unaweza kujifunza kutoka kwenye maelezo ya wale walioshuhudia Ufufuko wa Mwokozi? Wekea alama au andika uzoefu wa kila mtu katika Mathayo 28:1–10; Luka 24:13–35; Yohana 20:19–29; na 1 Wakorintho 15:1–8, 55. (Mashahidi wengine wa Kristo aliyefufuka wanaweza kupatikana katika 3 Nefi 11; Mormoni 1:15; Etheri 12:38–39; Mafundisho na Maagano 76:19–24; 110:1–10; na Historia ya—Joseph Smith 1:15–17.) Ni nini kinachokuvutia kuhusu shuhuda za mashahidi hawa? Baada ya Ufufuko wa Mwokozi, watu wengine walifufuka na kuwatokea wengi (ona Mathayo 27:52–53; 3 Nefi 23:9). Je, ni jinsi gani imani yako katika Mwokozi na ahadi ya ufufuko vinashawishi namna unavyoishi?

Ona pia (video) “Jesus Is Resurrected,” “The Risen Lord Appears to the Apostles,” “Blessed Are They That Have Not Seen, and Yet Have Believed”, ChurchofJesusChrist.org.

2:19
2:29

1 Petro 1:3–11

Yesu Kristo hunipa tumaini na shangwe.

Ni maneno au vishazi gani katika 1 Petro 1:3–11 vinakupa tumaini kwa sababu ya Yesu Kristo? Ni lini umehisi tumaini hilo?

Mzee Gerrit W. Gong alishuhudia kwamba Ufufuko “unatoa matumaini kwa wale waliopoteza viungo; wale waliopeteza uwezo wa kuona, kusikia, au kutembea; au wale walifikiriwa wamepotelea kwenye magonjwa yasiyo na huruma, ugonjwa wa akili, au uwezo mwingine hafifu. Yeye anatutafuta sisi. Yeye anatuponya. … [Pia] kwa sababu ‘Mungu mwenyewe alilipia dhambi za ulimwengu’ [Alma 42:15], … Yeye anaweza, kwa rehema, kutusaidia kulingana na madhaifu yetu. … Tunatubu na kutenda yote tunayoweza. Yeye anatuzingira milele ‘katika mikono ya upendo wake’ [2 Nefi 1:15]” (“Hosana na Haleluya—Yesu Kristo Aliye Hai: Moyo wa Urejesho na Pasaka,” Liahona, Mei 2020, 54).

Ona pia Alma 27:28; 36:1–24; 3 Nefi 9:11–17; Moroni 7:40–41.

ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

ComeuntoChrist.org.Easter.ComeuntoChrist.org inajumuisha ratiba ya wakati na maelezo ya kila kilichotendeka katika kila siku ya wiki ya mwisho ya maisha ya Mwokozi. Kila siku ya wiki, familia yako inaweza kupitia upya maelezo haya ili kuona Mwokozi alifanya nini siku hiyo, au mnaweza kusoma kuhusu wiki Yake ya mwisho katika maandiko kama familia (ona orodha iliyopendekezwa kwenye “Mawazo ya Kujifunza Binafsi Maandiko”).

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za WatotoFikiria kuimba nyimbo pamoja kuhusu Upatanisho wa Mwokozi na Ufufuko wiki hii, ikijumuisha baadhi ambazo hazijulikani sana kwenu. (Ona kielezo cha mada cha Nyimbo za Kanisa au Kitabu cha nyimbo za Watoto, chini ya mada kama vile “Upatanisho,” “Pasaka,” au “Ufufuko”). Kuwasaidia wanafamilia kujifunza nyimbo, unaweza kuonyesha picha ambazo zinaendana na maneno hayo.

“Yesu Kristo” mkusanyiko katika Maktaba ya Injili.Mkusanyiko wa Maktaba ya Injili wenye kichwa cha habari “Yesu Kristo” ukijumuisha video, kazi za sanaa, na muziki ambao unaweza kuisaidia familia yako kusherekea Ufufuko wa Mwokozi katika Pasaka hii.

“Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume.”Kama familia, someni “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume” (ChurchofJesusChrist.org). Alika kila mwanafamilia kuchagua ujumbe wa Pasaka kutoka katika ushuhuda huu ili kuuelezea kwa wengine. Kwa mfano, unaweza kutengeneza mabango ya kuweka kwenye mtandao wa kijamii, juu ya mlango wako wa mbele, au katika nyumba yenu.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Jesus Has Risen,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 70.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Weka malengo yanayowezekana. Kutumia hata dakika chache katika siku kujifunza maandiko kunaweza kubariki maisha yako. Jiwekee sharti la kujifunza kila siku, tafuta njia ya kujikumbusha mwenyewe ahadi yako, na fanya kwa uwezo wako wote kuifuata. Kama ukisahau, usikate tamaa. Anza tu tena.

Kristo katika Gethsemane

Gethsemane, na Adam Abram