Agano Jipya 2023
Aprili 24–30. Yohana 7–10: “Mimi Ndimi Mchungaji Mwema”


“Aprili 24–30. Yohana7–10: ‘Mimi Ndimi Mchungaji Mwema’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Aprili 24–30. Yohana 7–10,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
Yesu na mwanamke aliyeanguka chini.

Wala Mimi Sikuhukumu, na Eva Koleva Timothy

Aprili 24–30

Yohana 7–10

“Mimi Ndimi Mchungaji Mwema”

Unaposoma Yohana 7–10, unaweza kupokea mawazo kutoka kwa Roho Mtakatifu kuhusu kanuni za mafundisho ya injili zilizoko katika sura hizi. Kuandika misukumo yako kunaweza kukusaidia kuweka mpango ya kuifanyia kazi.

Andika Misukumo Yako

Japokuwa Yesu Kristo alikuja kuleta “amani [na] mapenzi mema kwa watu wote” (Luka 2:14), kulikuwa na “matengano katika mkutano kwa ajili yake” (Yohana 7:43). Watu walioshuhudia matukio hayo hayo walifikia maazimio tofauti kabisa kuhusu Yesu alikuwa nani. Baadhi walihitimisha, “Ni mtu mwema,” na wengine wakasema, “Anawadanganya makutano” (Yohana 7:12). Alipomponya mtu asiyeona siku ya Sabato, baadhi walisisitiza, “Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki siku ya sabato,” wakati wengine waliuliza, “Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo?” (Yohana 9:16). Bado licha ya mkanganyiko wote huu, wale waliotafuta ukweli walitambua nguvu katika maneno Yake, kwani “hajanena kamwe mtu yeyote kama huyu anavyonena” (Yohana 7:46). Wakati Wayahudi walipomuomba Yesu “tuambie wazi” kama alikuwa ndiye Kristo, Alifunua kanuni ambayo inaweza kutusaidia sisi kutofautisha kati ya ukweli na uongo: “Kondoo wangu waisikia sauti yangu,” Alisema, “nami nawajua, nao wanifuata” (Yohana 10:24, 27).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Yohana 7:14–17

Ninapoishi kweli zilizofundishwa na Yesu Kristo, nitakuja kujua kwamba ni za kweli.

Wayahudi walishangaa kwamba Yesu alijua mengi, wakati hajasoma (ona mstari wa 15)—angalau, siyo katika njia walizozifahamu. Katika jibu la Yesu, Yeye alifundisha njia tofauti ya kujua ukweli ambayo ipo kwa kila mmoja, bila kujali elimu au historia ya mtu. Kwa mujibu wa Yohana 7:14–17, je, ni kwa jinsi gani unaweza kujua kwamba mafundisho ambayo Yesu alifundisha ni ya kweli? Je, ni kwa jinsi gani mchakato huu umekusaidia wewe kukuza ushuhuda wako juu ya injili?

Yohana 8:2–11

Rehema ya Mwokozi ipo kwa wote.

Wakati akizungumza kuhusu mchangamano wa Mwokozi na mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, Mzee Dale G. Renlund alisema: “Hakika, Mwokozi hakusamehe uzinzi. Lakini Yeye pia hakumhukumu yule mwanamke. Alimtia moyo kubadilisha maisha yake. Alihamasika kubadilika kwa sababu ya huruma na rehema Yake. Tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia inathibitisha matokeo ya ufuasi wake: ‘Na mwanamke alimtukuza Mungu kutoka saa ile, na kuamini katika jina lake’ [ona Yohana 8:11, tanbihi c]” (“Mchungaji Wetu Mwema,” Liahona, Mei 2017, 30).

Je, ni lini umehisi kama mwanamke yule, kupokea rehema badala ya hukumu kutoka kwa Mwokozi? Je, ni lini umekuwa kama waandishi na Mafarisayo, kushitaki au kuhukumu wengine hata ukiwa ungali una dhambi? (ona Yonana 8:7). Je, ni nini kingine unachoweza kujifunza kutokana na jinsi Mwokozi alivyochangamana na waandishi na Mafarisayo na mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi? Je, ni nini unajifunza kuhusu msamaha wa Mwokozi unaposoma mistari hii?

Ona pia (video) “Go and Sin No More” , ChurchofJesusChrist.org.

Yohana 9

Kama tuna imani, Mungu anaweza kujionyesha Mwenyewe katika mateso yetu.

Ni nini Yohana 9:1–3 inakufundisha kuhusu changamoto na mateso ya maishani? Unaposoma Yohana 9, tafakari jinsi “kazi za Mungu zilivyodhihirishwa” katika maisha ya mtu aliyezaliwa kipofu. Je, ni kwa jinsi gani zimedhihirishwa katika maisha yako—ikijumuisha katika mateso yako?

Yohana 10:1–30

Yesu Kristo ni Mchungaji Mwema.

Hata kama hauna uzoefu wa kondoo na uchungaji wa kondoo, kusoma Yohana 10, pale Mwokozi aliposema, “Mimi ndimi mchungaji mwema,” kunaweza kukufundisha kweli muhimu kumhusu Yeye. Ili kupata kweli hizi, tafuta virai ambavyo vinaelezea mchungaji mwema anavyokuwa na kisha ufikirie jinsi virai hivyo vinavyotumika kwa Mwokozi. Hapa chini kuna baadhi ya mifano:

  • Mstari wa 3: “Naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwaongoza.”

  • mstari wa 11: Yeye “huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.”

  • mstari wa 16: “Kutakuwako kundi moja, na mchungaji mmoja.”

Haya ni baadhi ya maswali ya ziada ya kukusaidia kutafakari sura hii: Ni kwa jinsi gani Yesu ni kama mlango? (ona mstari wa 7–9). Je! Yeye amekupaje wewe “uzima …uwe nao tele”? (mstari wa 10). Ni lini umehisi kuwa Yeye anakufahamu wewe binafsi? (ona mstari wa 14). Je, Unawezaje kutambua sauti ya Mchungaji Mwema? (ona mstari wa 27).

Ona pia Zaburi 23; Ezekieli 34; Alma 5:37–39; 3 Nefi 15:21–16:5; Gerrit W. Gong, “Mchungaji Mwema, Kondoo wa Mungu,” Liahona, Mei 2019, 97–101.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Yohana 7:24.Ili kuisaidia familia yako kuelewa mafundisho ya Yesu katika Yohana 7:24, ungeweza kuwaonyesha kitu fulani ambacho kinaonekana kwa njia moja upande wa nje lakini ni tofauti upande wa ndani. Au wanafamilia wangeweza kushiriki uzoefu ambao uliwafundisha wao kutohukumu kwa mwonekano wa nje. Ungeweza pia kuorodhesha sifa za kila mwanafamilia ambazo hazionekeni kwa macho (ona pia 1 Samweli 16:7; Thomas S. Monson, “Waone Wengine kama Wanavyoweza Kuja Kuwa,” Liahona, Nov. 2012, 68–71).

Yohana 8:31–36.Inamaanisha nini kuwa “mtumishi wa Ibilisi? (ona Moroni 7:11). Je, ni ukweli gani uliofundishwa na Yesu unaoweza kutufanya sisi kuwa huru?

Picha
Kristo Akimponya mtu asiyeona

Yesu Akimponya Mtu Asiyeona, na Carl Heinrich Bloch

Yohana 9.Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuisaidia familia yako kupata taswira ya tukio la Yesu akimponya mtu asiyeona katika Yohana 9? Mnaweza kuigiza hadithi pamoja au kuonyesha video “Jesus Heals a Man Born Blind” (ChurchofJesusChrist.org). Simamisha hadithi mara chache ili kwamba wanafamilia waweze kusoma mistari inayohusika kutoka Yohana 9. Waalike waandike somo lolote wanalojifunza kutoka kwenye tukio hili, kama vile kile inachomaanisha kuongoka kwenye injili ya Yesu Kristo.

Yohana 10:1–18, 27–29.Ili kuwashirikisha wanafamilia kujifunza kutoka kwenye fumbo la Mchungaji Mwema, waombe kila mmoja kuchora picha ya mojawapo ya vitu vifuatavyo: mwizi, mlango, mchungaji, mtu wa mshahara (mfanyakazi wa kukodiwa), mbwa mwitu, na kondoo. Waalike wasome Yohana 10:1–18, 27–29, na kisha jadilini kama familia Mwokozi alifundisha nini kuhusu vitu walivyochora.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “The Lord Is My Shepherd,” Nyimbo za Kanisa, na. 108.

Kuboresha Kujifunza Binafsi.

Tafuta maneno na virai vyenye mwongozo. Unaposoma, Roho anaweza kukuletea maneno au virai fulani kwenye usikivu wako ambavyo vinakupa mwongozo na hamasa au kuvifanya vionekane kana kwamba vimeandikwa kwa ajili yako. Fikiria kuandika maneno au virai vyovyote vinavyokupa mwongozo katika Yohana 7–10.

Picha
Kristo na mwanakondoo

Hakuna Kupotea Tena, na Greg K. Olsen

Chapisha