Agano Jipya 2023
Mei 1–7. Luka 12–17; Yohana 11: “Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea”


“Mei 1–7. Luka 12–17; Yohana 11: ‘Furahini Pamoja Nami, kwa Kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Mei 1–7. Luka 12–17: Yohana 11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

mtu akimkumbatia mwanaye

Mwana Mpotevu, na Liz Lemon Swindle

Mei 1–7

Luka 12–17; Yohana 11

“Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea”

Kwa maombi soma Luka 12–17 na Yohana 11, ukitafuta jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kweli zilizopo katika sura hizi na kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni.

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wakumbushe watoto baadhi ya mafumbo na hadithi zilizopo katika Luka 12–17 na Yohana 11, na waalike kushiriki kile wanachokijua kuhusu hadithi hizi.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Luka 15

Baba wa Mbinguni Anawataka watoto Wake wote warudi Kwake.

Fikiria kuhusu watoto katika darasa lako, ikijumuisha wale ambao hawahudhurii mara kwa mara. Unawezaje kuwasaidia kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwashawishi watoto unaowafundisha ili wakusaidie kuwafikia hao wengine kwa upendo?

Shughuli Yamkini

  • Mpe sarafu mtoto mmoja, mwingine picha ya kondoo, na mtoto mwingine picha ya mwana mpotevu (ona ChurchofJesusChrist.org au ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Simulia mafumbo haya tatu yanayopatikana katika Luka 15 na waalike watoto kuinua juu sarafu au picha zao wakati unapozitaja. Unaweza kuwaalika watoto kuelezeana tena mafumbo hayo mmoja na mwingine kwa maneno yao wenyewe.

  • Waombe watoto washiriki uzoefu wao wakati walipokuwa wamepoteza kitu. Ni kwa jinsi gani walikipata? Eleza kuwa watu wanaweza kupotea kiroho wakati wanapokuwa hawamfuati Baba wa Mbinguni. Shuhudia kwamba Mungu anataka watu waliopotea waje Kwake, na sisi tunaweza kuwasaidia.

  • Waalike watoto kufikiria watoto wengine ambao hawaji kwenye Msingi. Wasaidie kupaka rangi au waandike ujumbe ukiwaalika watoto hawa kuhudhuria Msingi au shughuli ya Msingi. Kwa namna gani nyingine tunaweza kuwasaidia watoto kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni kwao?

Luka 17:11–19

Ninaweza kuonyesha upendo wangu kwa Baba wa Mbinguni kwa kuwa mwenye shukrani kwa baraka zangu.

Ni kwa namna gani hadithi ya wakoma kumi inahimiza watoto kuwa wenye shukrani?

Shughuli Yamkini

  • Simulia hadithi ya wakoma kumi walioponywa na Yesu. Onyesha picha iliyopo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na waalike watoto kuhesabu hadi kumi katika vidole vyao. Kisha waambie kushusha chini vidole tisa ili kuonyesha ni mkoma mmoja tu ndiye aliyemshukuru Yesu. Wasaidie watoto kufikiria mtu ambaye wangemshukuru kwa tendo la ukarimu au la msaada.

  • Alika kila mtoto kufanya kitu kinachoashiria shukrani zao kwa hicho kitu na waombe watoto wengine kukisia kitu hicho ni nini. Waombe watoto kushiriki njia ambazo tunaweza kumwonyesha Baba wa Mbinguni kuwa tunashukuru kwa ajili ya baraka zetu.

Yohana 11:1–46

Tunaamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

Martha, ambaye alikuwa dada wa Lazaro, aliyemwambia Yesu: “Ninaamini kwamba Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu” (Yohana 11:27). Hadithi ya Mariamu, Martha, na Lazaro inaweza kuimarisha ushuhuda wa watoto juu ya Yesu Kristo.

Shughuli Yamkini

  • Fanya muhtasari hadithi ya Yesu akimfufua Lazaro kutoka kwa wafu (ona pia “Sura ya 43: Yesu Anamfufua Lazaro,” katika Hadithi za Agano Jipya, 107–9, au video inayofanana nayo katika ChurchofJesusChrist.org). Waoneshe watoto tawi lililokufa na mmea ulio hai, na waulize kipi kimekufa na kipi kilicho hai. Toa ushuhuda wako kwamba kwa sababu ya uwezo wa Yesu Kristo, watu waliokufa watafufuliwa na kuishi milele.

  • Wasaidie watoto kukariri kirai ambacho Yesu alikisema kwa Martha: “Mimi Ndimi huo ufufuo, na uzima” (Yohana 11:25). Elezea kwamba kwa sababu ya Ufufuko wa Mwokozi, tutawaona tena wapendwa wetu waliofariki.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Luka 15

Mimi ninaweza kumsaidia Yesu kumtafuta kondoo Wake aliyepotea.

Sisi sote tunamjua mtu ambaye kwa namna moja au nyingine ni kama kondoo aliyepotea, sarafu iliyopotea, au mwana mpotevu katika mafumbo yale ya Mwokozi. Fikiria jinsi unavyoweza kuwashawishi watoto hawa kuwafikia watu hawa kwa upendo.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto wasome fumbo la kondoo aliyepotea au fumbo la sarafu iliyopotea, ipatikanayo katika Luka 15:1–10, na washiriki kile walichojifunza.

  • Andika majina haya ubaoni: baba, mwana mkubwa, na mwana mdogo. Onyesha video ya “The Prodigal Son” (ChurchofJesusChrist.org) na simamisha mara kadhaa ili watoto waandike katika ubao baadhi ya hisia za watu walioorodheshwa. Je, Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanajisikiaje kuhusu wale waliotenda dhambi?

  • Muombe mtoto kutoka katika chumba wakati wengine wakiificha sarafu au kondoo wa karatasi. Muite mtoto arudi na kutafuta sarafu au kondoo. Je, ni kwa njia zipi watu wanaweza kujisikia “wamepotea” kama sarafu au kondoo? Waalike watoto kupendekeza njia ambazo wanaweza kuwafikia. Imba pamoja na watoto wimbo unaohusiana, kama vile “Dear to the Heart of the Shepherd” (Nyimbo, na.221, na shuhudia juu ya furaha inayokuja pale watu wanamrudia Mungu.

  • Elezea kwamba Yesu alitumia kondoo aliyepotea, sarafu iliyopotea, na mwana mpotevu kuwakilisha watu “waliopotea” kwa sababu hawana baraka za injili. Waalike watoto wafikirie juu ya watu wanaowafahamu ambao hawana baraka hizi katika maisha yao. Ni kitu gani wanaweza kufanya ili kuwasaidia watu hawa kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni kwao?

Yesu na kondoo

Mchungaji Mpole, na Yongsung Kim

Luka 11:11–19

Ninaweza kuonyesha upendo wangu kwa Baba wa Mbinguni kwa kuwa mwenye shukrani kwa ajili ya baraka zangu.

Hadithi ya wakoma kumi inaweza kuwa njia nzuri kuwashawishi watoto kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya baraka zao.

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja hadithi ya wakoma kumi. Ni kwa namna gani mkoma aliyetoa shukrani alibarikiwa kwa ajili ya shukrani zake? Kwa nini ni muhimu kumshukuru Mungu kwa baraka zetu?

  • Waalike watoto kuorodhesha vitu wanavyoshukuru ambavyo vinaanza na kila herufi ya jina lao.

  • Waombe watoto kuandika ujumbe wa-asante kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya baraka alizowapa. Wanaweza kutundika jumbe hizo pembeni ya vitanda vyao ili kuwakumbusha kushukuru wanaposali.

Yohana 11:1–46

Tunaamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

Unawezaje kutumia hadithi ya Mariamu, Martha, na Lazaro kuwasaidia watoto kujua, kama Martha alivyojua, kwamba Yesu ndiye “Kristo, Mwana wa Mungu”? (Yohana 11:27).

Shughuli Yamkini

  • Andika ubaoni baadhi ya kauli zilizozungumzwa na watu katika Yohana 11. Waalike watoto kutambua ni nani aliyesema kila kauli, na waalike kupekua Yohana 11 ili kuhakikisha majibu yao. Wangejisikia vipi kama wao wangelikuwa Yesu, Martha, Mariamu, au Lazaro? Ni kwa jinsi gani kuamini katika Yesu kunatusaidia wakati tunapokuwa na huzuni au hofu?

  • Soma ushuhuda wa Martha, unaopatikana katika Yohana 11:20–27. Waombe watoto watafute maneno na virai ambavyo vinaonyesha Martha alikuwa na imani katika Yesu Kristo. Tunaweza kufanya nini ili tuweze kuwa kama yeye?

  • Wasaidie watoto kukariri Yohana 11:25. Elezea kwamba kila mtu atafufuliwa, lakini ni watenda haki tu watapokea uzima wa milele na kuishi pamoja Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo tena.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wapatie watoto karatasi ambayo wanaweza kuandikia au kuchora vitu ambavyo wanashukuru katika wiki yote.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Marudio ni muhimu katika kujifunza. Watoto wananufaika kwa kusikia kanuni ya injili au kufanya shughuli zaidi ya mara moja. Jaribu kurudia shughuli katika njia tofauti tofauti.