Agano Jipya 2023
Mei 22–28. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; Luka 21: “Mwana wa Adamu Atakuja”


“Mei 22–28. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; Luka 21: ‘Mwana wa Adamu Atakuja’’’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Mei 22–28. Joseph Smith— Mathayo 1: Mathayo 24–25: Marko 12–13; Luka 21,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Ujio wa Pili

Ujio wa Pili, na Harry Anderson

Mei 22–28

Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; Luka 21

“Mwana wa Adamu Atakuja”

Tafakari watoto unaowafundisha wanahitaji nini ili kujifunza kutoka Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; na Luka 21. Jisikie huru kutohoa mawazo haya kwa ajili ya watoto wakubwa katika muhtasari huu kwa watoto wadogo au kinyume chake.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Leta darasani kitu au picha inayohusiana na moja ya mafumbo au hadithi katika usomaji wa wiki hii (kama vile mafuta yakiwakilisha wanawali kumi au sarafu kuwakilisha vipaji au senti za mjane. Waombe watoto washiriki kile wanachokijua kuhusiana na fumbo au hadithi hii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Joseph Smith—Mathayo 1:31

Kabla Yesu hajaja tena, injili itahubiriwa duniani kote.

Ishara moja kwamba Yesu atarudi karibuni ni kwamba injili Yake inahubiriwa kote ulimwenguni. Watoto wanaweza kusaidia kutimiza unabii huu kwa kushiriki injili.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha ramani, tufe, au picha ya dunia (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.3) wasaidie watoto kusema, “Injili hii … itahubiriwa ulimwenguni kote” (Joseph Smith—Mathayo 1:31). Kwa nini Mungu anataka watoto Wake wote kusikia Injili Yake?

  • Waalike watoto kutembea papo hapo mnapoimba pamoja wimbo kuhusu kushiriki injili, kama vile “I Want to Be a Missionary Now” au “Called to Serve” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 168, 174).

  • Onyesha video “I’ll Go Where You Want Me to Go” (ChurchofJesusChrist.org). Watoto wanapoangalia, wasaidie kuhesabu njia ambazo wanazoweza kushiriki injili katika video hii. Ni njia gani zingine watoto wanaweza kufikiria?

Picha
dunia kutoka angani

Injili itahubiriwa ulimwengu kote. Picha kwa hisani ya NASA Kituo cha Anga cha Johnson

Mathayo 25:14–30

Ninaweza kutumia vipawa alivyonipatia Mungu.

Watoto wadogo wanatambua vipawa na uwezo wao. Wasaidie kuelewa kwamba vipawa hivi na uwezo huja kutoka kwa Baba wa Mbinguni.

Shughuli Yamkini

  • Leta sarafu kadhaa za kutumia unapoelezea fumbo wa talanta, lipatikanalo katika Mathayo 25:14–30. Unaweza kuwaomba watoto watatu kuwakilisha watumishi watatu. Eleza kwamba katika siku ya Yesu, talanta ilijulikana kama pesa, lakini leo talanta inaweza kumaanisha vipawa na uwezo wetu.

  • Waombe watoto wataje njia ambazo wazazi wao, ndugu, walimu, au marafiki wamewasaidia wao. Watu hawa wana talanta gani ambazo zinawasaidia kuwahudumia wengine?

  • Andika ujumbe mfupi kwa watoto ukiwaambia kila mmoja wao kuhusu vipawa na uwezo uliogundua ndani yao. Unaposhiriki na kila mmoja wa watoto vipawa unavyoviona ndani yao, wahimize kuboresha vipawa vyao na wavitumie kuwahudumia wengine.

Mathayo 25:31–46

Yesu ananitaka niwahudumie wengine.

Tunamtumikia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa kuwatumikia watu wanaotuzunguka. Wasaidie watoto kufikiria njia wanazoweza kuwatumikia wengine.

Shughuli Yamkini

  • Fanya muhtasari wa fumbo katika Mathayo 25:34–46. Wasaidie watoto kuelewa kwamba wakati tunapowatumikia wengine, tunamtumikia Yesu.

  • Nyanyua juu picha ya mtoto pamoja na picha ya Yesu iliyofichwa nyuma yake. Nini tunaweza kufanya ili kumtumikia mtoto huyu? Ondoa picha ya mtoto na elezea kwamba wakati tunapotumikiana, tunamtumikia Yesu.

  • Waalike watoto kuchora picha zao wenyewe wakiwatumikia wengine katika njia aliyoeleza Mwokozi katika Mathayo 25:35–36. Waombe watoto wengine kubashiri hawa wanachora nini.

  • Waalike watoto kushiriki uzoefu wa wakati mtu alipoonyesha huduma kama ya Kristo kwao au kwa familia zao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Joseph Smith—Mathayo 1:31

Kabla Yesu hajaja tena, injili itahubiriwa katika ulimwengu wote.

Watoto unaowafundisha wanaweza kusaidia kuhubiri injili katika ulimwengu kabla ya Ujio wa Pili wa Mwokozi.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kushiriki baraka walizopokea au watakazopokea kwa sababu wao ni waumini wa Kanisa la Kristo. Someni pamoja Joseph Smith—Mathayo 1:31, na uwaulize watoto jinsi wanavyohisi injili itakavyowabariki watoto wa Mungu ulimwenguni kote.

  • Waonyeshe watoto ramani ya dunia au ya nchi yako na wasaidie kutambua baadhi ya sehemu ambapo mwanafamilia au rafiki alihubiri injili akiwa kwenye misheni yake.

  • Waalike watoto wachache waje wakiwa wamejiandaa kushiriki ni kwa jinsi gani wanafamilia wao au mababu zao walijulishwa injili.

  • Mwombe mtoto aandike jina la mtu fulani anayeweza kuzungumza naye kuhusu Yesu Kristo au kumualika kanisani. Pia waombe watoto kuorodhesha vitu wanavyoweza kufanya ili kuwa wamisionari sasa.

Mathayo 25:1–13

Ninawajibika kwa uongofu wangu binafsi kwa Yesu Kristo.

Fumbo la wanawali kumi hufundisha kwamba hatuwezi kuazima uongofu wetu kwa Mwokozi kutoka kwa wengine. Ni kwa jinsi gani unawasaidia watoto kuwajibika kwa ajili ya uongofu wao binafsi?

Shughuli Yamkini

  • Muombe mtoto kuja akiwa amejiandaa kushiriki jinsi yeye alivyojifunza kuhusu fumbo la wanawali kumi nyumbani wiki hii.

  • Chora taa ya mafuta katika ubao, na iandike ushuhuda. Mpe kila mtoto kipande cha karatasi kilichoundwa kama tone la mafuta, na muulize kila mtoto aandike juu yake kitu atakachofanya kuongoka zaidi kwa Mwokozi. Bandika matone yao kwenye ubao kuzunguka taa.

  • Waalike watoto kukusaidia kutengeneza orodha ya vitu vya kufanya ili kujiandaa kwa ajili ya mgeni rasmi. Ni kwa jinsi gani vitu hivi vinalingana au vinatofautiana na njia tunazoweza kujiandaa kwa Ujio wa Pili wa Mwokozi?

  • Kwenye vipande vitano vya karatasi, andika vitu ambavyo haviwezi kuazimwa. Kwenye vipande vingine vitano, andika vitu vinavyoweza kuazimwa. Changanya vipande, na waombe watoto wavipange katika makundi haya mawili. Someni pamoja Mathayo 25:1–13. Kwa nini ni muhimu kutokutegemea wengine kwa ajili ya uongofu wetu kwa Yesu Kristo?

Mathayo 25:14–46

Katika Hukumu ya Mwisho, tutampa Bwana hesabu ya maisha yetu.

Baada ya Ufufuko, Mungu atatuhukumu kulingana na utiifu wetu katika amri Zake na kukubali dhabihu yake ya kulipia dhambi. Fumbo la talanta na fumbo la kondoo na mbuzi linatufundisha kuhusu hii Hukumu ya Mwisho.

Shughuli Yamkini

  • Alika nusu ya darasa isome Mathayo 25:14–30 na nusu ingine kusoma Mathayo 25:31–46. Omba makundi yaigize mafumbo kwa darasa. Je! Bwana anatuahidi nini katika mafumbo haya?

  • Waalike watoto wasome Mathayo 25:35–36 katika jozi na kutengeneza orodha ya vitu wanaweza kufanya kuonyesha upendo wao kwa Yesu Kristo.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waombe watoto kushiriki na familia zao njia wanazoweza kuwa wamisionari bora na kuongea na familia zao kuhusu watu wanaoweza kushiriki nao injili.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Isikilize au iigize hadithi. Kwa sababu watoto wanapenda hadithi, tafuta njia za kuwashirikisha katika hadithi za maandiko unazoshiriki. Wanaweza kushika picha au vitu, chora picha za hadithi, na kuigiza hadithi au kusaidia kueleza hadithi. Rudia hadithi ili kuwasaidia kutambua maelezo muhimu na mafundisho ya injili.

Chapisha