Agano Jipya 2023
Mei 29–Juni 4. Mathayo 26; Marko 14; Yohana 13: “Kwa Ukumbusho”


“Mei 29–Juni 4. Mathayo 26; Marko 14; Yohana 13: ‘Kwa Ukumbusho’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Mei 29–Juni 4. Mathayo 26; Marko 14; Yohana 13,“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Chakula cha Mwisho

Kwa Ukumbusho Wangu, na Walter Rane

Mei 29–Juni 4.

Mathayo 26; Marko 14; Yohana 13

“Kwa Ukumbusho”

Unaposoma Mathayo 26; Marko 14; na Yohana 13, angalia kanuni ambazo unahisi zitawabariki watoto unaowafundisha.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha za matukio kwenye sura hizi, kama vile Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 54–55, na waalike watoto waseme kile kinachotendeka kwenye picha.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mathayo 26:26–29; Marko 2:22–24

Sakramenti hunisaidia kufikiria juu ya Yesu.

Wasaidie watoto kuelewa kwamba kupokea sakramenti ni nafasi ya kukumbuka kile Yesu alichotufanyia.

Shughuli Yamkini

  • Fanya muhtasari hadithi ya Yesu akianzisha sakramenti. Unaweza kutumia “Sura ya 49: Sakramenti ya Kwanza” (katika Hadithi za Agano Jipya, 124–26, au video inayofanana nayo kwenye ChurchofJesusChrist.org), au video ya “Sacrament” (ChurchofJesusChrist.org). Je, kwa nini tunapokea sakramenti? Wasaidie watoto kuelewa kwamba tunamkumbuka Yesu wakati wa sakramenti.

  • Waoneshe watoto picha ya mkate na kikombe cha maji. Waulize watoto kama wanafahamu mkate wa sakramenti na maji vinasimama nini. Elezea kwamba ishara hizi zinatusaidia kukumbuka kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu na kufufuka kutoka kwa wafu.

  • Waombe watoto wafunge macho yao na kufikiria juu ya mtu wanayempenda, na kisha waalike kukusimulia kuhusu mtu huyo. Waombe kufunga macho yao tena, na kufikiria juu ya Mwokozi, na kushiriki vitu wanavyofahamu kumhusu Yeye. Wahimize kufikiria kuhusu Yesu wakati wa sakramenti kila wiki.

  • Waalike watoto kukuonyesha wanaweza kufanya nini ili kumkumbuka Yesu na kuwa na staha wakati wa sakramenti. Wasaidie watoto kutengeneza kijitabu kilichoelezwa katika ukurasa wa shughuli ya wiki hii na kukitumia ili kuwasaidia wao kufikiria kuhusu Yesu wakati wa sakramenti. Au waache wapekue baadhi ya Magazeti ya Kanisa kupata picha za Yesu na watengeneze kolagi wanayoweza kuangalia wakati wa sakramenti.

Yohana 13:34–35

Ninaweza kuwapenda wengine kama Yesu alivyofanya.

Yesu alionyesha upendo Wake kwa kuwajali wale waliomzunguka. Je, watoto unaowafundisha wanazo fursa gani za kuonyesha upendo wao kwa wengine?

Shughuli Yamkini

  • Waoneshe picha za hadithi ambazo watoto wamejifunza mwaka huu wakati Yesu alipoonyesha upendo wake kwa wengine (ona mihutasari iliyopita katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Soma Yohana 13:34–35, na wasaidie watoto kurudia kirai “Kama Nilivyowapenda ninyi, … nanyi pendaneni.” Je, tunawezaje kuonyesha upendo kwa familia zetu na marafiki?

  • Mwalike mtoto kushikilia picha ya Mwokozi wakati darasa likiimba wimbo kuhusu upendo wa Mwokozi, kama vile “Love One Another” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 136). Wape watoto mioyo ya karatasi na waalike kuchora juu ya mioyo picha ya wao wenyewe wakifanya kitu kinachoonyesha upendo wao kwa mtu mwingine.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mathayo 26:26–29; Marko 2:22–24

Sakramenti inanisaidia kumkumbuka Yesu Kristo na dhabihu Yake aliyotoa kwa ajili yangu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuwa na uzoefu wa maana katika sakramenti?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kufanya zamu kusoma mistari hii katika Mathayo 26:26–29 au Marko 14:22–24 (ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, Marko 14:20–24 [katika kiambatisho cha Biblia]) na Mafundisho na Maagano 20:75–79. Ni maneno gani na mawazo gani yanafanana katika hivi vifungu viwili?

  • Waulize watoto wanafanya nini ili kuwasaidia kufikiria juu ya Yesu wakati wa sakramenti. Wasaidie kutafuta maandiko au maneno kutoka katika nyimbo za sakramenti ambayo wanaweza kusoma wakati wa sakramenti, na kisha kuorodhesha katika kadi ambayo watoto wanaweza kurejelea wakati mwingine wanapopokea sakramenti. Imba nyimbo chache kati ya hizi pamoja na watoto (ona Nyimbo za Dini, na. 169–97).

    Picha
    watoto wakipokea sakramenti

    Sakramenti inatusaidia sisi kumkumbuka Yesu Kristo na dhabihu Yake kwa ajili yangu.

  • Andika vifungu muhimu kutoka katika sala ya sakramenti katika ubao, na wasaidie watoto kuvikariri. Vifungu hivi vinamaanisha nini? Kwa nini ni muhimu kufanya upya maagano yetu ya ubatizo kila wiki?

  • Mwalike mtu mwenye Ukuhani wa Haruni kuwaambia watoto kuhusu uzoefu wake katika kuandaa, kubariki, au kupitisha Sakramenti. Ni kitu gani kilimsaidia yeye kujiandaa kufanya hivi? Anajisikiaje anapofanya hivyo? Ni kwa jinsi gani mkate na maji vinamkumbusha kuhusu Mwokozi?

  • Waombe watoto ambao wamebatizwa kushiriki kile wanachokumbuka kuhusu ubatizo wao. Je, walijisikiaje? Ni maagano gani walifanya? (ona Mosia 18: 18–10). Waambie kwamba kila wiki wakati wanapopokea sakramenti, inaweza kuwa kama kubatizwa tena—tunaweza kusamehewa dhambi zetu, na kuweka upya maagano yetu.

Yohana 13:1–17

Yesu alinionyesha jinsi ya kuwatumikia wengine.

Hadithi ya Mwokozi akiosha miguu ya wanafunzi Wake inaweza kuwashawishi watoto unaowafundisha kwa upendo kuwahudumia watu wanaowazunguka.

Shughuli Yamkini

  • Siku chache kabla, mwombe mmoja wa watoto kusoma Yohana 13:4–9 na ashiriki hadithi hiyo pamoja na darasa kwa mtazamo wa Petro. Je, Mwokozi alikuwa anajaribu kumfundisha nini Petro na wale Mitume wengine? Watoto wangeweza kuzungumza kuhusu kile wanachojifunza kutokana na hadithi hii kuhusu Yesu. Tunajifunza nini kuhusu kuwatumikia wengine?

  • Someni pamoja Yohana 13:12–17. Waombe watoto kila mmoja kuandika kuhusu wakati ambapo Yesu alimhudumia mtu mwingine. Wahimize kujumuisha kile wanachojifunza kutokana na mfano Wake. Kama wanahitaji msaada wanaweza kutafuta mifano katika video “Christlike Attributes” (ChurchofJesusChrist.org). Waombe waelezee kile walichoandika kwa darasa.

Yohana 13:34–35

Wanafunzi wa Yesu Kristo wanawapenda watu wengine kama Yeye alivyofanya.

Tunapobatizwa, tunafanya maagano ya kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo. Katika Yohana 13:34–35, Mwokozi anaelezea jinsi tunavyoweza kuonyesha kwamba sisi ni wanafunzi Wake.

Shughuli Yamkini

  • Andika ubaoni ne, kama vile nilivyo ninyi (Yohana 13:34). Waalike watoto kutafuta kwenye maandiko na kujaza mapengo. Tunaweza kufanya mambo gani mengine ili kuonyesha kwamba tunayo imani katika Yesu Kristo? Watoto wangeweza kufikiria maneno mengine ambayo yangekamilisha sentensi hii ubaoni, kama vile hudumu na hudumiwa au fundisha na fundishwa.

  • Waalike watoto kusoma Yohana 13:35 na kufikiria watu wanaowajua ambao ni mifano ya wanafunzi wa Yesu Kristo. Waombe kushiriki jinsi watu hawa wanavyoonyesha upendo kwa wengine kama Mwokozi alivyofanya.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Alika watoto washiriki pamoja na familia zao kitu watakachofanya kwa sababu ya kile walichojifunza darasani. Kwa mfano, wangeweza kushiriki jinsi watakavyomkumbuka Yesu Kristo wakati wa sakramenti.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa ushuhuda kwa darasani lako. Ushuhuda unaweza kuwa rahisi kama “Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni anampenda kila mmoja wenu” au “Ninajisikia vizuri ndani ninapojifunza kuhusu Yesu Kristo.”

Chapisha