Agano Jipya 2023
Juni 12–18. Luka 22; Yohana 18: “Si Mapenzi Yangu, bali Yako, Yatimizwe”


“Juni 12–18. Luka 22; Yohana 18: ‘Si Mapenzi Yangu, bali Yako, Yatimizwe,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Juni 12-18. Luka 22; Yohana 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Kristo na wafuasi Gethsemane

Kijisitu cha Gethsemane, na Derek Hegsted

Juni 12–18

Luka 22; Yohana 18

“Si Mapenzi Yangu, bali Yako, Yatimizwe”

Kujifunza kutoka Luka 22 na Yohana 18 pamoja na watoto ni fursa ya kuwasaidia kuzidisha kwa kina upendo wao kwa Yesu Kristo na imani yao Kwake. Kwa sala tafakari jinsi unavyoweza kufanya hili.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha za matukio katika sura hizi, kama vile Kristo akiwa Gethsemane (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 56) na picha katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waalike watoto kueleza nini kinatokea katika picha hizi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Luka 22:39–46

Yesu aliteseka kwa ajili yangu kwa sababu Yeye ananipenda.

Fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kuhisi upendo wa Yesu unapojadili hadithi ya mateso Yake katika Gethsemane.

Shughuli Yamkini

  • Simulia hadithi ya Luka 22:39–46 kwa watoto, pengine kwa kutumia “Sura ya 51: Yesu Anateseka katika Bustani ya Gethsemane” (katika Hadithi za Agano Jipya, 129–32, au video zinazoambatana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Elezea kwamba Yesu alisikia maumivu yote na huzuni ambayo kila mtu aliwahi kuisikia. Waulize watoto nini kinaweza kuwafanya wasikie huzuni, maumivu, au kufadhaika. Shuhudia kwamba Yesu anaweza kutusaidia sisi kuhisi vyema tunapokuwa tunahisi kwa njia hizi.

  • Pitisha picha darasani ya Mwokozi akiwa Gethsemane (kama ili iliyoko katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Kila mtoto anapoishika picha, sema, “Yesu aliteseka kwa sababu Yeye anampenda [jina la mtoto].” Waalike watoto kurudia maneno haya pamoja na wewe.

  • Imba wimbo pamoja watoto kuhusu upendo wa Yesu kwetu sisi, kama vile “I Feel My Savior’s Love” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75). Wasaidie kufikiria njia ambazo wamewahi kuhisi upendo wa Yesu.

Luka 22:41–43

Ninaweza kuomba ninapohitaji msaada.

Wakati Yesu aliposali huko Gethsemane, malaika alimtokea kumuimarisha. Je, unawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kwamba wao pia wanaweza kuomba kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya nguvu?

Shughuli Yamkini

  • Fanya muhtasari wa Luka 22:41–43 kwa ajili ya watoto. Shiriki uzoefu ambapo uliomba kwa ajili ya kupata usaidizi na Baba wa Mbinguni akakuimarisha kwa njia ya Roho Mtakatifu au kwa kumtuma mtu ili akusaidie.

  • Kwenye mshipi waa karatasi, andika baadhi ya mambo ambayo tunaweza kuyasema katika sala, kama vile “Baba wa Mbinguni,” “ninakushukuru,” “ninakuomba,” na “katika jina la Yesu Kristo, amina.” Weka kamba hizo sakafuni bila mpangilio, na wasaidie watoto kuziweka katika mpangilio ambao tunaweza kuyasema katika sala. Tunaweza kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa vitu gani? Tunaweza kufanya nini kingine Kwake? Shuhudia kwamba watoto wanaweza kusali kwa Baba wa Mbinguni mahali po pote na wakati wo wote.

Picha
Kristo akiomba katika Gethsemane

Kristo Anasali katika Bustani ya Gethsemane,na Hermann Clementz

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Luka 22:39–46

Katika Gethsemane, Yesu Kristo alijichukulia juu yake Yeye mwenyewe dhambi zangu na maumivu.

Kujua kuhusu kile Yesu alifanya kwa ajili yetu katika Gethsemane kunaweza kuwasaidia watoto kutubu kwa ajili ya dhambi zao na kumrudia Mwokozi wakati wanapopitia majaribu magumu.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wasome Luka 22: 39-46, wakiangalia maneno au virai ambavyo vinaeleza jinsi Yesu alivyohisi akiwa Gethsemane. Je, ni kitu gani Yesu alikuwa akikipitia ambacho kilisababisha Yeye ahisi hivyo? (ona Mafundisho na Maagano 19:16–19). Wape watoto nafasi ya kushiriki hisia zao kuhusu Yesu na dhabihu Yake kwa ajili yetu.

  • Waalike watoto washiriki wakati ambapo walikuwa na huzuni au katika maumivu. Waulize kama wanamjua yeyote ambaye amewahi kuhisi kitu kama hicho. Waalike wasome Alma 7:11–12. Je, mistari hii inatufundisha nini kuhusu Yesu Kristo na mateso Yake kwa ajili yetu sisi?

  • Mpe mtoto fimbo ambayo ni ndefu kuliko upana wa mlango wa darasa, na muombe kuishika kimlalo na ajaribu kutembea kupita mlango. Elezea kwamba fimbo inawakilisha dhambi zetu, ambazo zinatuzuia kuingia ufalme wa Mungu. Ondoa fimbo kuonyesha kwamba Yesu alijichukulia Yeye mwenyewe dhambi zetu ili kwamba tuweze kusamehewa tunapotubu.

Luka 22:39–44

Ninaweza kufuata mfano wa Yesu kwa kuwa mtiifu kwa Baba wa Mbinguni.

Yesu alionyesha utiifu kwa Baba wakati Aliposema, “Walakini si mapenzi yangu bali yako yatendeke” (Luka 22:42). Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujifunza kutokana na mfano wa Yesu?

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kukariri kirai “Walakini sio mapenzi yangu, bali yako yatendeke” (Luka 22:42) na jadili hii inamaanisha nini. Tunaweza kufanya nini ili kutii mapenzi ya Baba wa Mbinguni?

  • Wasaidie watoto kutambua baadhi ya sababu kwa nini ni vigumu wakati mwingine kufanya kitu ambacho Baba wa Mbinguni anataka. Je, ni baraka gani tulizopokea kwa kuwa watiifu kwa Baba wa Mbinguni, hata ilipokuwa vigumu?

Luka 22:50–51

Yesu aliwapenda maadui Zake.

Kujifunza jinsi ya kuwa wapatanishi siyo rahisi, hususani wakati watu wengine wanapokuwa siyo wakarimu kwetu? Ni kwa jinsi gani hadithi katika Luka 22:50–51 inawashawishi watoto unaowafundisha kuwa wakarimu katika kila hali?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kusoma Luka 22: 50–-51. Je, tunajifunza nini kuhusu Yesu kutokana na hadithi hii? Katikati ya wiki, waombe baadhi ya wazazi wa watoto wakuambie kuhusu nyakati ambapo watoto wao walionyesha ukarimu, hata ilipokuwa ni vigumu. Shiriki hadithi hizo na darasa. (Wakumbushe watoto kwamba kuwa wakarimu haimaanishi kuruhusu watu wengine kuwaumiza; wanapaswa siku zote kuwaeleza wazazi wao au mtu mzima mwingine anayeaminika kama mtu fulani anawaumiza.)

  • Imbeni wimbo kuhusu kuwa mkarimu, kama vile “Kindness Begins with Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 145). Wimbo huu unafundisha nini kuhusu ukarimu? Tunawezaje kuonyesha ukarimu kwa wengine kama Mwokozi alivyofanya?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike vijana kushiriki shuhuda zao juu ya Mwokozi na familia zao. Wangeweza pia kuwaomba wanafamilia wao kushiriki shuhuda zao juu Yake.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Waalike Watoto washiriki kile wanachojua. “Waombe [watoto] washiriki nawe fikira zao, hisia, na uzoefu unaohusiana na kanuni unazofundisha. Utagundua kwamba wanao umaizi ambao ni rahisi, safi, na wenye nguvu” (Kufundisha katika njia ya Mwokozi26).

Chapisha