Agano Jipya 2023
Juni 5–11. Yohana 14–17: “Kaeni katika Pendo Langu”


“Juni 5–11. Yohana 14–17: ‘Kaeni Katika Pendo Langu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Juni 5–11. Yohana 14–17.“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Karamu ya Mwisho

Karamu ya Mwisho, na William Henry Margetson

Juni 5–11

Yohana 14–17

“Kaeni Katika Pendo Langu”

Sali ili kujua mahitaji ya watoto unaowafundisha unaposoma Yohana 14–17. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia katika kujifunza kwako, na muhtasari huu unaweza kukupa mawazo kuhusu jinsi ya kuwafundisha watoto katika darasa lako.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwasaidia watoto kushiriki kile wanachojifunza nyumbani, acha kila mtoto achukue zamu ya kushikilia moyo wa karatasi na kushiriki kitu ambacho yeye hufanya ili kuonyesha upendo kwa wengine.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Yohana 14:15

Ninaonyesha upendo wangu kwa Yesu kwa kushika amri Zake.

Wasaidie watoto kuelewa kwamba wanaweza kumwonyesha Mwokozi kwamba wanampenda kwa kushika amri Zake.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kukariri Yohana 14:15. Waombe waseme “Kama unanipenda” unapoinua moyo wa karatasi juu. Waombe waseme “Shikeni amri zangu” unaponyanyua maandiko juu.

  • Wasaidie watoto kufikiria baadhi ya amri za Yesu. Waalike wapendekeze njia wanazoweza kushika kila amri. Shuhudia kwamba kwa kufanya mambo haya inaonyesha upendo wetu kwa Yesu Kristo.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu amri, kama vile “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47).

  • Cheza mchezo ulioko katika ukurasa wa shughuli ya wiki hii pamoja na watoto.

Yohana 14:26–27; 15:26; 16:13–14

Roho Mtakatifu hunisaidia mimi.

Yesu aliwafundisha wanafunzi Wake ukweli muhimu kuhusu Roho Mtakatifu? Fikiria ni kwa jinsi gani ukweli huu ungeweza kuwabariki watoto unaowafundisha.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha Karamu ya Mwisho (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 54). Waeleze watoto kwamba katika Karamu ya Mwisho, Yesu aliwafundisha wanafunzi Wake kuhusu Roho Mtakatifu. Shiriki baadhi ya kweli hizi Yeye alizofundisha katika Yohana 14:26–27; 15:26; 16:13–14.

    Picha
    Yesu akizungumza na wanafunzi

    Karamu ya Mwisho, na Clark Kelley Price

  • Shiriki uzoefu wakati Roho Mtakatifu alipokufariji, alipokuongoza, au alipokusaidia kujua ukweli. Shuhudia kwamba Roho Mtakatifu anaweza kuwasaidia watoto kwa njia hizo hizo.

  • Pamoja na watoto, imbeni wimbo kuhusu Roho Mtakatifu, kama vile “The Holy Ghost” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 105). Waalike wao wasikilize mambo yanayotajwa katika wimbo ambayo Roho Mtakatifu anayafanya.

Yohana 17:3

Ninaweza kuwajua Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Yesu alifundisha kwamba “uzima wa milele” ni kumjua Mungu pekee wa kweli na Yesu Kristo.” Watoto unaowafundisha wanapokuja kuwajua Wao, watapata nguvu za kiroho ambazo zitawabariki kwa maisha yao yote na zitawasaidia kupata uzima wa milele.

Shughuli Yamkini

  • Soma Yohana 17:3, na waombe watoto wasikilize yule ambaye Yesu anataka sisi tumjue. Onyesha picha chache ambazo zinawakilisha njia tunazoweza kuja kumjua Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, kama vile picha za Maandiko, familia ikijifunza pamoja na mtu mmoja akimhudumia mwingine. Weka picha uso ukiangalia chini, na waalike watoto kuchukua zamu wakizigeuza na kuelezea kilichoko katika picha hizo. Ni kwa jinsi gani vitu hivi vinatusaidia kuwajua Baba wa Mbinguni na Yesu?

  • Zungumza na watoto kuhusu mambo wanayofanya ili kuwajua marafiki zao vizuri zaidi. Je, tunapataje kuwajua vyema Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo? Shiriki njia tunazoyafanya haya.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Yohana 14:15; 15:10–14

Ninaonyesha upendo wangu kwa Yesu Kristo kwa kushika amri Zake.

Unaposoma vipengele hivi katika kujifunza kwako binafsi, fikiria kuhusu watoto unaowafundisha. Watabarikiwaje wanapoelewa kwamba utiifu wao kwa Mwokozi ni ishara ya upendo wao Kwake?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kushiriki njia Yesu alizoonyesha kuwa Yeye alikuwa mtiifu kwa Baba wa Mbinguni. Onyesha picha kutoka katika maisha ya Mwokozi ili kuwasaidia (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 34–35, 56–57). Waombe watoto kuzungumza kuhusu wakati walipomtii Baba wa Mbinguni.

  • Mwalike mtoto asome Yohana 14:15. Acha watoto wachue zamu kuchora picha ambazo zinazomwakilisha mtu akishika amri, wakati watoto wengine wote wakibahatisha kile mtoto huyu anakichora. Kwa mifano ya amri, ona Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana kijitabu (2022). Ni kwa jinsi gani kushika amri hizi humwonyesha Mwokozi kwamba sisi tunampenda Yeye?

Yohana 14:26; 15:26; 16:13

Roho Mtakatifu huongoza, hufariji na hushuhudia ukweli.

Je, watoto unaowafundisha wamepokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Wanajua nini kuhusu jinsi Roho Mtakatifu anavyoweza kuwasaidia? Fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa vyema nafasi ya Roho Mtakatifu.

Shughuli Yamkini

  • Wapatie watoto mistari ifuatayo wasome katika jozi: Yohana 14:26; 15:26; na 16:13. Waombe watafute maneno ambayo yanawafundisha kile Roho Mtakatifu hufanya. Andika maneno hayo ubaoni.

  • Shiriki uzoefu wakati Roho Mtakatifu alikuongoza, alikufariji, alikuonya, au kushuhudia ukweli kwako. Waalike watoto kushiriki uzoefu wowote waliokuwa nao. Walitambuaje ushawishi wa Roho Mtakatifu?

  • Mwalike kila mtoto kuchora sura yake katika mfuko wa karatasi. Angaza kwa tochi, ikiwakilisha Roho Mtakatifu, ndani ya kila mfuko. Kisha weka vitu katika mifuko vitakavyozuia mwanga, kama vile vipande vya nguo, kuwafundisha kwamba chaguzi zetu mbaya zinaweza kuzuia ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Waache watoto watoe vitu vilivyomo katika mifuko yao kuwakilisha toba.

Yohana 15:1–9; 17:3

Baba wa Mbinguni na Yesu wananitaka mimi niwajue Wao.

Utabariki maisha ya watoto kwa kuwasaidia kuja kumjua vyema Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha mmea (au picha ya mmea) pale watoto wanapochukua zamu kusoma mistari katika Yohana 15:1-9. Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo ni kama mzabibu? Je, sisi tunakuwaje kama matawi? Ni nini tunaweza kufanya ili “kukaa ndani” au kukaa karibu, na Mwokozi?

  • Soma kwa sauti Yohana 17:3. Waulize watoto ni kitu gani wanachokifanya ili kumjua Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Shiriki ni kwa jinsi unakuja kuwajua Wao.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kushiriki na familia zao wimbo ambao hivi karibuni wamejifunza darasani au wakati wa kuimba.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tohoa shughuli. Kama unafundisha watoto wadogo, unaweza kupata mawazo ya ziada ambayo unaweza kutumia kwa darasa lako katika sehemu ya muhtasari huu kwa watoto wakubwa. Vivyo hivyo, shughuli kwa watoto wadogo zinaweza kutoholewa kufundisha watoto wakubwa.

Chapisha