Agano Jipya 2023
Mei 15–21. Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12: “Tazama, Mfalme Wako Anakuja”


“Mei 15–21. Mathayo 21–23; Marko 11: Luka 19–20: Yohana 12: ‘Tazama, Mfalme Wako Anakuja’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Mei 15–21. Mathayo 21–23; Marko 11: Luka 19–20: Yohana 12.” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

mtu juu ya mti wakati Yesu akikaribia

Zakayo juu ya Mti wa Mkuyu, na James Tissot

Mei 15–21

Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12

“Tazama, Mfalme Wako Anakuja”

Unaposoma Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; na Yohana 12, tilia maanani misukumo unayopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu. Rejelea “Kukidhi Mahitaji ya Watoto Wadogo” mwanzoni mwa nyenzo hii kwa ajili ya mambo ya kukumbuka wakati ukifundisha kanuni hizi.

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha iliyopo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, na waalike watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu kinachotokea katika picha.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Luka 19:1–10

Baba wa Mbinguni na Yesu wananijua mimi kwa jina.

Unaposoma juu ya mwingiliano wa Mwokozi na Zakayo, ni ujumbe gani unaoupata ambao unaweza kuwabariki watoto unaowafundisha?

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha Zakayo juu ya Mkuyu (katika muhtasari huu au kwenye ChurchofJesusChrist.org). Wasaidie watoto wampate Zakayo na kusema jina lake. Buni vitendo vya watoto kufanya wakati unaposimulia hadithi ya Zakayo na Yesu—kwa mfano, wasimame kwa vidole vyao ili kuona juu ya umati au kujifanya kupanda mti. Eleza kwamba Mwokozi alimuona Zakayo na akamwita kwa jina. Shuhudia kwamba Mwokozi pia anamjua kila mmoja wa watoto na majina yao.

  • Leta fremu tupu ya picha kwenye darasa, au utengeneze moja kwa kutumia karatasi. Mwalike kila mtoto kuchukua zamu kushika fremu kuzunguka uso wake wakati wanadarasa wengine wakisema, “Baba wa Mbinguni na Yesu wanakujua [jina la mtoto].”

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu upendo wa Mungu, kama vile “I am a Child of God” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3). Waalike watoto wachore picha za vitu vinavyowasaidia kujua Baba wa Mbinguni anawapenda.

Mathayo 21:12–14

Hekaluni ni mahali patakatifu.

Staha ya Yesu kwa hekalu, kama inavyoelezewa katika mistari hii inaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kwamba hekaluni ni mahali patakatifu.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha Yesu Akisafisha Hekalu (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 51), na simulia hadithi kama ilivyoandikwa katika Mathayo 21:12–14. Wasaidie watoto kutafuta pesa na wanyama katika picha. Kisha jadili kwa nini Mwokozi aliwataka wabadilisha pesa na watu wauzao wanyama kuondoka hekaluni.

  • Onyesha picha za mahekalu (kwa mfano, ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.117-19), na waombe watoto kushiriki jinsi wanavyojisikia walionapo hekalu. Unaweza kueleza kwamba hekaluni ni mahali tunapokwenda kufanya ahadi na Mungu, kutafuta majibu ya sala, na kujisikia kuwa karibu na Mungu. Wasaidie watoto kutambua hisia kutoka kwa Roho Mtakatifu akiwaambia kwamba hekaluni ni sehemu maalum. Waombe watoto kuigiza vile ambavyo wangefanya kama wangekuwa ndani ya hekalu. Kwa mfano, wangezungumza kwa kunong’ona na kukaa kwa staha.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu hekalu, kama vile “I Love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95), na waalike watoto kufanya lengo la kuingia ndani ya hekalu siku moja.

Hekalu la Fort Collins, Colorado

Hekalu ni nyumba ya Bwana.

Mathayo 21:28–32

Mimi ninaweza kuwa mtiifu.

Baba wa Mbinguni anataka tuwe watiifu. Fumbo la wana wawili ni fursa ya kufundisha kuhusu umuhimu wa utiifu.

Shughuli Yamkini

  • Chora picha ya wana wawili ubaoni, na tumia michoro unapopitia fumbo katika Mathayo 21:28–32. Mwana yupi alifanya uamuzi sahihi mwishoni? Waombe ili watoto kutaja vitu wanavyoweza kufanya ili kuwa watiifu nyumbani. Waache wachore picha zao wenyewe wakifanya mojawapo ya mambo hayo.

  • Waalike watoto kushiriki uzoefu walioupata kwa kuwa watiifu kwa wazazi wao. Walibarikiwaje kwa kuwa watiifu?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Luka 19:1–10

Nikimtafuta Mwokozi, Nitampata.

Unaweza kutumia hadithi ya Zakayo kuwasaidia watoto kufikiria mambo wanayoweza kufanya kuja karibu zaidi kwa Mwokozi.

Shughuli Yamkini

  • Soma Luka 19:1–10, ukitua kila mistari michache ili kujadili tunajifunza nini kuhusu Zakayo. Je, Zakayo alifanya nini ili aweze kumwona Yesu? Ni kwa jinsi gani alijibu wakati Yesu alipomwambia kushuka chini kutoka mtini? Mwombe kila mtoto atoe sababu moja ya kwa nini wangependa kumwona Yesu. Kama Mwokozi angekuja kwenye mji wetu, tungefanya nini ili kujiandaa?

  • Waalike watoto kufikiria juu ya watu wanaowafahamu ambao, kama Zakayo, wanaweza kuwa wanamtafuta Mwokozi. Waulize watoto wangeweza kufanya nini ili kumsaidia mtu mwingine kujifunza kuhusu Mwokozi.

  • Waalike watoto kushiriki uzoefu wakati walipohisi kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo waliwajua na waliwapenda.

Mathayo 21:12–14

Hekalu ni mahali patakatifu ambapo ninapaswa kupaheshimu.

Ni kwa jinsi gani hadithi ya Mwokozi akisafisha hekalu inakusaidia wewe kuwafundisha watoto kuhusu utakatifu wa mahekalu?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kusoma Mathayo 21:12–14. Onyesha picha Yesu Akisafisha Hekalu (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 51), na waulize ni mstari gani unaoonyeshwa katika picha.

  • Waalike watoto kushiriki jinsi walivyojisikia wakati walipoingia ndani ya hekalu, walipotembelea viwanja vya hekalu, au walipoangalia picha za mahekalu. Ni nini kiliwasaidia kujua kuwa hekalu ni mahali patakatifu? Unaweza kushiriki na watoto kwa nini wewe unalipenda hekalu. Kwa nini ni takatifu kwako?

  • Alika kijana mmoja au zaidi kuja katika darasa na kuongea kuhusu jinsi walivyojiandaa kuingia hekaluni. Kama wamewahi kuwa hekaluni, waombe waongee kuhusu jinsi walivyohisi wakati walipokuwa humo.

  • Kata picha ya hekalu katika vipande vya chemsha bongo, na mpe kila mtoto kipande kimoja. Waombe watoto kuandika nyuma ya kipande cha chemsha bongo kitu kimoja wanachoweza kufanya ili kujiandaa kuingia hekaluni. Pale kila mtoto anaposhiriki wazo, ongeza kipande chake kwenye chemsha bongo.

  • Ubaoni, andika yafuatayo: anaweza kunisaidia kujiandaa kuhudumu hekaluni. Alika watoto kupendekeza njia za kukamilisha sentensi hizi. Baadhi ya mawazo yanaweza kujumuisha “Kushika maagano yangu ya ubatizo” au “Roho Mtakatifu.”

Mathayo 23:25–28

Yesu ananitaka mimi kuwa mwenye haki katika matendo yangu na tamaa zangu.

Yesu aliwafundisha waandishi na Mafarisayo kuhusu umuhimu wa kuishi injili kwa dhati—siyo tu kujifanya kuwa mwenye haki. Ni nini kingeweza kuwasaidia watoto kuelewa ukweli huu?

Shughuli Yamkini

  • Unaposoma Mathayo 23:25–28 pamoja na watoto, fikiria kushiriki maana hii ya unafiki kutoka kwenye Kamusi ya Biblia: “mtu ambaye anajifanya kuwa mshika dini wakati siyo.” Kwa nini ni vibaya kuwa mnafiki?

  • Onyesha watoto kikombe ambacho ni kisafi kwa nje lakini kichafu ndani ili kusaidia kuonyesha mfano katika Mathayo 23:25. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuhakikisha tu wasafi na tusio na doa kwa ndani?

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wasaidie watoto kufikiria juu ya kitu kimoja walichojifunza wakati wa darasa ambacho wanaweza kushiriki pamoja na familia zao nyumbani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie wazazi wa watoto. “Wazazi ni walimu muhimu sana wa injili kwa watoto wao—wana vyote jukumu kuu na nguvu kubwa zaidi ya kuwashawishi watoto wao (ona Kumbukumbu la Torati 6:6–7). Unapowafundisha watoto kanisani, kwa maombi tafuta njia za kuwasaidia wazazi wao katika jukumu lao hili muhimu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi25).