Agano Jipya 2023
Mei 8–14. Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18: “Nimepungukiwa na Nini Tena?”


“Mei 8–14. Mathayo 19–20: Marko 10: Luka 18: “Nimepungukiwa na Nini Tena?,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Mei 8–14. Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
vibarua katika shamba la mizabibu

Mei 8-14

Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18

“Nimepungukiwa na Nini Tena?”

Soma Mathayo 19–20; Marko 10; na Luka 18, ukiwa na watoto unaowafundisha akilini. Andika misukumo yo yote unayoipata. Maandalizi yako yatakusaidia kufundisha watoto kile wanachohitajika kujua kutoka kwenye sura hizi.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kushiriki chochote wanachokumbuka kutoka kwenye somo la wiki iliyopita. Waonyeshe picha ili kuwasaidia kukumbuka.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Marko 10:6–8

Baba wa Mbinguni anatutaka sisi kuoana katika hekalu na kuwa na familia za milele.

Ni kwa jinsi gani watoto unaowafundisha wananufaika kutokana na kujifunza kuhusu mafundisho ya ndoa ya milele? Inaweza kuwa msaada kwako kurejelea kweli kuhusu ndoa katika “Familia: Tangazo Kwa Ulimwengu” (ChurchofJesusChrist.org).

Shughuli Yamkini

  • Wasomee Marko 10:6–8 watoto, na uonyeshe picha ya wanandoa. Waombe watoto kuwanyoshea kidole mwanaume na mwanamke wakati wanasikia ukisoma maneno mwanaume na mwanamke. Elezea kuwa Baba wa Mbinguni anataka mwanaume na mwanamke waoane (ona Mwanzo 1:27–28).

  • Onyesha picha za familia na ya hekalu. Waombe watoto wazungumze kuhusu kile wanachoona katika picha. Elezea kwamba Baba wa Mbinguni anatutaka tuunganishwe na familia zetu katika hekalu ili tuweze kuwa pamoja nao milele. Kuwa makini kwa watoto wale ambao wazazi wao bado hawajaunganishwa.

  • Imbeni wimbo kuhusu familia, kama vile “A Happy Family” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 198). Fikiria kuimba wimbo huo mara kadhaa. Waalike watoto kushiriki vitu vya burudani walivyowahi kufanya na familia zao. Kwa nini wanashukuru kwa ajili ya familia zao?

  • Imba wimbo kuhusu hekalu, kama vile “I Love to See the Temple” au “Families Can Be Together Forever” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95, 188). Waache watoto washike picha za mahekalu au familia, na waalike kuzinyanyua picha zao juu wakati wanapoimba “hekalu” au “familia.” Wasaidie watoto kufikiria sababu kwa nini ni muhimu kuoa au kuolewa hekaluni?

Picha
Yesu pamoja na watoto na wazazi.

Yesu anawapenda watoto, kwa maana “kama hawa ufalme wa Mungu ni wao” (Marko 10:14).

Marko 10:13–16

Yesu anataka watoto wadogo waje Kwake ili awabariki.

Simulizi hii inatoa nafasi ya kuwasaidia watoto kujisikia ni kiasi gani Yesu anawapenda.

Shughuli Yamkini

  • Kwa maneno yako mwenyewe, shiriki simulizi kutoka Marko 10:13–16. Unaweza pia kuonyesha video “Suffer the Little Children to Come unto Me” (ChurchofJesusChrist.org). Wasaidie watoto wafikiri nyakati ambapo walihisi upendo wa Yesu kwao. Toa ushuhuda wako kwa watoto kwamba Yesu anawapenda na anataka kuwabariki.

  • Onyesha picha Kristo na Watoto (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 47). Wasaidie watoto kufikiria kuwa ingekuwaje kama wangekuwa mmoja wa watoto aliyekaa pembeni mwa Yesu katika picha. Waalike watoto kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu Yesu.

  • Acha watoto wachore picha za wao wenyewe wakibarikiwa na Yesu (ona Marko 10:16 na ukurasa wa shughuli ya wiki hii).

Marko 10:17–22

Kama ninatii amri, ninaweza kupokea uzima wa milele.

Yesu alimfundisha kijana tajiri kwamba kupata uzima wa milele—maisha kama aliyonayo Baba wa Mbinguni—anapaswa kutiii amri.

Shughuli Yamkini

  • Wasimulie watoto hadithi ya kijana tajiri katika Marko 10:17–22. (Ona pia “Sura ya 42: Kijana Tajiri,” katika Hadithi za Agano Jipya, 105–6, au video inayofanana nayo katika ChurchofJesusChrist.org.) Waombe kusikiliza kile Yesu alichomwambia kijana kufanya na jinsi kijana alivyojibu.

  • Simulia hadithi moja au zaidi kuhusu watoto ambao wanaomba ushauri au maelekezo kutoka kwa wazazi wao lakini hawafuati au kutii. Ni baadhi ya vitu gani Baba wa Mbinguni anatuambia tufanye? Tunajisikiaje tunapotii amri Zake?

  • Shiriki uzoefu wako wakati ulipokea misukumo binafsi ya kufanya kitu ili kuwa bora.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Marko 10:6–8

Baba wa Mbinguni anatutaka sisi kuoa au kuolewa hekaluni na kuwa na familia za milele.

Vitu ambavyo Yesu alifundisha kuhusu ndoa vinaweza kuwasaidia watoto watazamie kuoa au kuolewa hekaluni na kulea familia ya milele.

Shughuli Yamkini

  • Muombe mtoto mmoja asome Marko 10:6–8 kwa sauti. Eleza kwamba ambatana inamaana “kushikilia kwenye” au “kuendelea hadi mwisho” wa jambo. Kwa nini ni muhimu kwamba waume na wake waungane pamoja, wapendane, na kufanya kazi kama wabia?

  • Waombe watoto wakusaidie wewe kufikiria majibu ya swali kama “Kwa nini familia ni muhimu katika Kanisa?” au “Kwa nini ni muhimu kwako wewe kufunga ndoa katika hekalu?” Wasaidie kutafuta majibu katika nyenzo kama Marko 10:6–8; 1 Wakorintho 11:11; Mafundisho na Maagano 42:22; 131:1–4; Musa 3:18, 21–24; na “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.”

  • Imbeni pamoja wimbo unaoelezea baraka za hekaluni, kama vile “Families Can Be Together Forever” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188). Shiriki ushuhuda wako juu ya ndoa ya milele na familia pamoja na watoto. Waalike kushiriki shuhuda zao pia.

Marko 10:17–22

Yesu anaweza kunisaidia kujua kile ninachohitaji kufanya ili kuendelea.

Kijana tajiri alimtafuta Yesu na kupokea maelekezo maalumu ambayo yaliyokusudiwa hususani kwa ajili yake. Unawezaje kuwashawishi watoto kutafuta mwongozo kama huo katika maisha yao wenyewe?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kutafuta mstari katika Marko 10:17–22 ambao unaielezea picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Nifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Eleza kwamba ushauri wa Yesu alioutoa kwa kijana ulikuwa binafsi, na sisi sote tunaweza kupokea mwongozo binafsi kutoka kwa Bwana kupitia Roho.

  • Someni pamoja Marko 10:17–22. Waalike watoto kuandika katika ubao amri ambazo Mwokozi alimwambia kijana tajiri kuzitii (ona mstari wa 19). Je, ni kitu gani kingine Yesu alimtaka akifanye? (ona mstari wa 21). Wahimize watoto kufikiria kuhusu mambo wanayoweza kuhitajika kuanza kuyafanya au kuacha kuyafanya ili kumfuata Yesu vizuri zaidi. Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kujua kile Yesu anachotutaka tufanye.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuonyesha familia zao kwamba wanawapenda, pengine kwa kuandika ujumbe mfupi au kufanya tendo la ukarimu la huduma.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa makini na watoto. Ni kwa jinsi gani watoto katika darasa lako wanaitikia shughuli za kujifunza? Kama hawaonyeshi kushiriki, inaweza kuwa ni wakati mwafaka wa kujaribu shughuli nyingine au kufanya matembezi mafupi, ya utulivu. Kwa upande mwengine, kama unagundua kwamba watoto wanashiriki na wanajifunza kutoka kwenye sehemu fulani ya somo, usijisikie kushinikizwa kuendelea mbele ili kuhakikisha unapitia taarifa zote za somo.

Chapisha