Agano Jipya 2023
Machi 6–12. Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9: “Hawa kumi na Wawili Yesu Aliwatuma”


“Machi 6–12. Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9: ‘Hawa kumi na Wawili Yesu Aliwatuma”’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Machi 6–12. Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Yesu anamtawaza Petro

Machi 6–12

Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9

“Hawa kumi na Wawili Yesu Aliwatuma””

Unaposoma Mathayo 9–10; Marko 5; na Luka 9, unaweza ukapokea misukumo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Misukumo hii, sambamba na Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na muhtasari huu, vinaweza kukusaidia kujiandaa kufundisha.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kushiriki kitu walichofanya ili kumsaidia mtu fulani wiki hii. Mwokozi alifanya nini ili kuwasidia wengine?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mathayo 9:18–30; Marko 5:22–43

Yesu anao uwezo wa kuniponya.

Mwokozi kwa kurudia rudia alionyesha nguvu Zake kwa kuwaponya wale waliokuwa na imani kwake Yeye. Unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kujenga imani yao nguvu Yake ya uponyaji.

Shughuli Yamkini

  • Wasimulie watoto hadithi ya binti wa Yairo (ona Marko 5:22–23, 35–43). Katika kituo sahihi katika hadithi hii, soma maneno ya Yesu “Nakuambia, inuka” (mstari wa 41), na waalike watoto kusimama wima. Wasaidie watoto kuelewa kwamba Yesu anao uwezo wa kuponya watu na kutupatia sisi uzima wa milele.

  • Onyesha picha ya hadithi hii katika Mathayo 9:20–22 unapokuwa unasoma mistari hii. Wasaidie watoto kukariri kifungu hiki “Imani yako imekuponya” (mstari wa 22). Ili kufanya hivyo, ungeweza kumpangia kila mtoto neno na kisha watoto waseme maneno yao kimpangilio mara kadhaa. Yule mwanamke alionyeshaje kwamba ana imani katika Yesu Kristo? Tunaweza kufanya nini ili kuonyesha kwamba tunayo imani katika Yesu Kristo?

  • Waombe watoto kufunga macho yao na kusikiliza wakati unaposoma kutoka Mathayo 9:27–30. Wakati unaposoma kuhusu Yesu Akimponya mtu asiyeona, waalike watoto kufungua macho yao. Waalike watoto kuzungumza kuhusu jinsi ambavyo wangejisikia kama Yesu angewaponya wao.

  • Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kujifunza hadithi ya Mwokozi akimponya binti wa Yairo kutokana na mauti.

Picha
mwanamke akisongea kugusa vazi la Yesu

Mtumaini Bwana,na Liz Lemon Swindle

Mathayo 10:1–10

Yesu Aliwaita Mitume Kumi na Wawili na kuwapatia uwezo wa kufanya kazi Yake.

Je, watoto unaowafundisha wanafahamu kwamba tuna Mitume Kumi na Wawili hivi leo? Unawezaje kutumia mistari hii kuwafundisha kuhusu umuhimu wa Mitume wa sasa na kile walichoitwa kufanya?

Shughuli Yamkini

  • Fupisha Mathayo 10:1–10 katika maneno rahisi. Eleza kwamba Yesu huita Mitume ili kumsaidia kujenga Kanisa Lake. Waache watoto wahesabu Mitume katika picha Yesu Akiwatawaza Mitume (Kitabu cha Sanaa ya Injili,, na.38) na katika picha ya hivi karibuni ya Akidi ya Mitume Kumi na Wawili (ona ChurchofJesusChrist.org au toleo la mkutano mkuu la Liahona). Elezea kwamba tunao Mitume kumi na wawili hivi leo, kama tu ilivyokuwa katika wakati wa Yesu. Shiriki ushuhuda wako juu ya Mitume wa Bwana na juu ya kitu fulani walichofundisha hivi karibuni.

  • Ficha picha ya Mitume wa sasa chumbani kote (ili kupata picha, tazama toleo la hivi karibuni la mkutano mkuu la Liahona). Waalike watoto kutafuta picha, na wasimulie kidogo kuhusu kila Mtume (ona “Meet Today’s Prophets and Apostles” katika ChurchofJesusChrist.org).

  • Mwalike mtoto kunyanyua juu picha ya Urais wa Kwanza na picha ya Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Muombe mtoto kuongoza watoto wengine kuzunguka chumbani hadi katika picha ya Yesu. Shuhudia kwamba manabii na mitume hutuongoza kuelekea kwa Kristo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mathayo 9:18–30; Marko 5:22–43

Yesu anao uwezo wa kuniponya.

Kusoma hadithi ya Mwokozi akiwaponya watu inaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kujenga imani katika Yeye. Hadithi hizi zinaweza pia kuwasaidia wao kuona huruma na upendo Wake.

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja hadithi ya Yesu akiponya watu inayopatikana katika Mathayo 9:20–22, 27–30 na Marko 5:22–23, 35–43 (au onyesha video hizi “Jesus Heals a Woman of Faith” and “Jesus Raises the Daughter of Jairus” kwenye ChurchofJesusChrist.org). Ni kwa jinsi gani watu katika hadithi hizi wanaonyesha imani yao kwa Yesu Kristo? Je, tunajifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka kwenye hadithi hizi?

  • Waalike watoto washiriki uzoefu wakati wao au mtu mwengine wanayemfahamu alipokea baraka ya ukuhani kwa ajili ya uponyaji wa mgonjwa. Ni kwa jinsi gani waliponywa au kubarikiwa? Elezea kwamba nyakati zingine uponyaji wa kimuujiza sio mapenzi ya Bwana, lakini bado tunaweza kubarikiwa kwa upendo Wake na faraja.

Mathayo 10:1–10

Mitume Kumi na Wawili wanaweza kunifundisha kuhusu Yesu.

Ni kwa jinsi gani kujifunza kuhusu Mitume Kumi na Wawili katika siku ya Kristo kunawasaidia watoto kuelewa vyema kile wafanyacho Mitume Kumi na Wawili leo?

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha za Mitume katika wakati wa Yesu na katika siku yetu (ona Kristo Akiwatawaza Mitume [Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 38] na toleo la mkutano wa hivi karibuni la gazeti la Liahona). Waombe watoto wasome Mathayo 10:7 ili kujua kile ambacho Mitume wanafanya (ona pia Luka 9:1–2, 6; Mafundisho na Maagano 107:23).

  • Waalike watoto kuandika ubaoni majina ya Mitume wa mwanzoni kabisa kadiri wanavyoweza kukumbuka. Kisha waombe waorodheshe majina ya Mitume wengi walio hai kadiri wanavyoweza kuwakumbuka. Na wakague orodha zao na Mathayo 10:2–4 na toleo la mkutano wa hivi karibuni la gazeti la Liahona. Mngeweza pia kucheza mchezo wa kulinganisha ambamo watoto wanaweza kulinganisha jina la kila mtume aliye hai na picha yake. Picha zinaweza kupatikana katika ChurchofJesusChrist.org.

  • Siku kadhaa kabla ya darasa, waalike watoto wachache waje wakiwa wamejiandaa kushiriki hadithi iliyosemwa na mmoja wa hao Mitume walio hai (ona matoleo ya gazeti la Liahona kwa ajili ya mawazo). Ni kwa jinsi gani Mtume huyo alitumia hadithi hiyo ili kutushawishi sisi kuwa zaidi kama Mwokozi?

  • Shiriki pamoja na watoto mifano kadhaa ya shuhuda za Mitume wa siku hizi juu ya Kristo (ona jumbe za mkutano mkuu wa hivi karibuni au “Kristo Anayeishi: Shuhuda za Mitume” [ChurchofJesusChrist]).

  • Wasaidie watoto kukariri na kuelewa Makala ya Imani 1:6.

Luka 9:23–25

Kumfuata Yesu Kristo kunahitaji dhabihu.

Utawasaidiaje watoto kuelewa inamaanisha nini “kupoteza” maisha yao wanapomfuata Mwokozi?

Shughuli Yamkini

  • Waambie watoto kuhusu wakati ambapo ulipoacha kitu ili kupata kitu kilicho bora zaidi. Waalike watoto kushiriki mifano yao wenyewe. Kisha someni pamoja Luka 9:23–25. Elezea kwamba Yesu anatuhitaji sisi tuwe radhi kuacha cho chote ili kumfuata Yeye. Wakati yawezekana asituambie kuacha maisha yetu, ni kitu gani basi Yeye anatutaka tutoe? (ona Tafsiri ya Joseph Smith Mathayo 16:24 [katika Mathayo 16:24, tanbihi e]).

  • Andika sifa kadhaa za Kristo kwenye vipande na kinyume cha sifa hizo kwenye vipande vingine vya karatasi (kama vile upendo na uchoyo, unyenyekevu na kiburi na kuendelea). Andika maneno okoa na poteza kama vichwa vya habari ubaoni, na waalike watoto wazichambue sifa hizo na kuziweka kwenye kichwa cha habari kilicho sahihi. Wape watoto muda wa kutafakari sifa hizo za kama Kristo zilizoko ubaoni na kuchagua moja ili kuikuza kikamilifu zaidi.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kufundisha familia zao kuhusu Yesu Kristo akimponya binti wa Yairo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza staha. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kipengele muhimu cha staha ni kufikiria juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Unaweza kuwakumbusha watoto kuwa wenye staha kwa kuimba kimya kimya au kwa mvumo au kuonyesha picha ya Yesu.

Chapisha