Agano Jipya 2023
Machi 13–19. Mathayo 11–12; Luka 11: “Nami Nitawapumzisha”


“Machi 13–19. Mathayo 11–12; Luka 11: ‘Nami Nitawapumzisha’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Machi 13–19. Mathayo 11–12; Luka 11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023

Picha
Yesu amesimama miongozi mwa mawingu

Usiogope, na Michael Malm

Machi 13–19

Mathayo 11–12; Luka 11

“Nami Nitawapumzisha”

Rais Dallin H. Oaks alifundisha: “Maandiko, ambayo ni mafunuo ya kale, hayawezi kueleweka pasipo kuwa na uwazi kwa mafunuo ya sasa. … Kujifunza maandiko kunawawezesha wanaume na wanawake kupokea mafunuo” (“Scripture Reading and Revelation,” Ensign, Jan. 1995, 7).

Andika Misukumo Yako

Katika njia nyingi, Mafarisayo na waandishi walikuwa wamefanya kumwabudu Yehova kuwa mzigo. Mara nyingi walisisitizia sheria kali dhidi ya kweli za milele. Sheria kuhusu Siku ya Sabato, ambayo ilikusudiwa kuwa siku ya kupumzika, zilikuwa zenyewe ni mzigo mzito.

Na kisha, Yehova Mwenyewe akaja miongoni mwa watu Wake. Yeye aliwafundisha kwamba madhumuni ya kweli ya dini si kutengeneza mizigo bali kuifanya iwe miepesi. Yeye akifundisha kwamba Mungu anatupatia amri, ikijumuisha ile ya kuiheshimu Sabato, sio kutukandamiza bali kutubariki. Ndio, njia ya kwenda kwa Mungu imesonga na ni nyembamba, lakini Bwana alikuja kutangaza kwamba hatuhitaji kutembea peke yetu. “Njoni kwangu,” Yeye alisihi. Mwaliko wake, kwa wale wote wanaohisi “kulemewa na mizigo” kwa sababu yoyote ile, ni kusimama karibu Naye, kujifunga wenyewe Kwake, na kumuacha Yeye atusaidie mizigo yetu. Ahadi yake ni “Nanyi mtapata raha nafsini mwenu.” Ikilinganishwa na mbadala—kujaribu kubeba peke yetu au kutegemea suluhu za mwanadamu—nira Yake ni laini, na mzigo Wake ni mwepesi. Mathayo 11:28–30.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mathayo 11:28–30

Yesu Kristo atanipa pumziko ninapomtegemea Yeye.

Sote tunabeba mizigo—mingine ikiwa matokeo ya dhambi zetu na makosa yetu wenyewe, mingine ikisababishwa na chaguzi za wengine, na mingine ambayo si kosa la mtu yeyote lakini tu ni sehemu ya maisha ya duniani. Bila kujali sababu za masumbuko yetu, Yesu anatuomba tuje Kwake ili Aweze kutusaidia kubeba mizigo yetu na kupata usaidizi (ona pia Mosia 24). Mzee David A. Bednar alifundisha, “Kufanya na kushika maagano matakatifu hutuunganisha na Bwana Yesu Kristo” (“Walibeba Mizigo Yao kwa Urahisi,” Liahona, Mei 2014, 88). Ukiwa na hili akilini, tafakari maswali kama yafuatayo ili kuelewa vizuri zaidi maneno ya Mwokozi katika mistari hii: “Je, ni kwa jinsi gani maagano yangu huniunganisha nira kwa, na pamoja na Mwokozi?” Je, ninahitajika kufanya nini ili nije kwa Kristo? “Ni kwa namna gani nira ya Mwokozi ni laini na mzigo Wake ni mwepesi?”

Je, ni maswali gani mengine hukujia akilini unaposoma? Yaandike kama kumbukumbu, na tafuta majibu wiki hii katika maandiko na maneno ya manabii. Unaweza kupata majibu kwa baadhi ya maswali yako katika ujumbe wa Mzee David A. Bednar uliorejelewa hapo juu.

Ona pia John A. McCune, “Njoo kwa Kristo—Kuishi kama Mtakatifu wa Siku za Mwisho,” Liahona, Mei 2020, 36–38; Lawrence E. Corbridge, “Njia,” Liahona, Nov. 2008, 34–36.

Picha
wanaume wakiwabeza wanafunzi wanaotembea katika shamba la ngano

Wanafunzi Wanakula Ngano Siku ya Sabato, na James Tissot

Mathayo 12:1–13

“Tenda wema katika siku za Sabato.”

Mafundisho ya Mafarisayo yalitofautiana na ya Mwokozi katika njia nyingi, lakini hasa katika jinsi ya kuheshimu siku ya Sabato. Unaposoma Mathayo 12:1–13, unaweza kufikiria jinsi gani mitazamo na matendo yako kuhusu Sabato yanaendana na mafundisho ya Mwokozi. Ili kufanya hili, unaweza kutafakari maelezo kama haya:

Je, ni kwa jinsi gani mafundisho haya yanashawishi jinsi unavyoichukulia Sabato?

Ona pia Marko 2:233:5; Mada za Injili, “Siku ya Sabato,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

Mathayo 12:34–37; Luka 11:33–44

Maneno na matendo yangu huakisi kile kilicho katika moyo wangu.

Mojawapo ya ukosoaji muhimu wa Mwokozi kwa Mafarisayo ilikuwa kwamba walijaribu kuonekana kuwa wenye haki lakini dhamira zao hazikuwa safi. Unapojifunza maonyo ya Mwokozi kwa Mafarisayo katika Mathayo 12:34–37 na Luka 11:33–44, tafakari muuanganiko kati ya mioyo yetu na matendo yetu. Kishazi “mtu mwema katika akiba njema” kina maanisha nini kwako? (Mathayo 12:35). Ni kwa jinsi gani kwa maneno yetu tunahesabiwa haki au kuhukumiwa? (ona Mathayo 12:37). Ingeweza kumaanisha nini kwa jicho lako kuwa “safi”? (Luka 11:34). Tafakari jinsi unavyoweza kuwa “mwanga ulioenea” (Luke 11:36) kupitia nguvu za Mwokozi.

Ona pia Alma 12:12–14; Mafundisho na Maagano 88:67–68.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mathayo 11:28–30.Unaweza kuisaidia familia yako kupiga taswira kichwani ya mafundisho ya Mwokozi katika mistari hii kwa kuwafanya wapeane zamu kujaribu kuvuta kitu kizito, kwanza wao peke yao na kisha kwa usaidizi. Je, ni ipi baadhi ya mizigo tunayoibeba? Je, inamaanisha nini kujitia nira ya Kristo juu yetu? Picha iliyo mwisho wa muhtasari huu ingeweza kukusaidia kuelezea nira ni nini.

Mathayo 12:10–13.Mnaposoma kuhusu Yesu akimponya mtu siku ya Sabato, familia yako ingeweza kuzungumza kuhusu jinsi tunavyofanywa “kuwa wazima” na Mwokozi. Ni kwa jinsi gani Sabato inaweza kuwa siku ya uponyaji kwetu?

Mkiongozwa na mfano wa Mwokozi katika mistari hii, familia yako ingeweza kutengeneza orodha ya njia mnazoweza “kutenda wema siku ya Sabato” (mstari wa 12). Hakikisheni mnajumuisha fursa za kuwatumikia wengine. Inaweza kuwa msaada kutunza orodha yenu na kuirejelea Jumapili zijazo.

Luka 11:33–36.Tafakari jinsi unavyoweza kuifundisha familia yako kile inachomaanisha kuwa “mwanga ulioenea” (mstari wa 34, 36). Je, somo la vitendo litasaidia? Mngeweza pia kujadili njia za kuleta nuru ya Mwokozi katika maisha yetu, nyumbani kwetu, na ulimwenguni. Kwa mawazo, ona video “The Light That Shineth in Darkness,” ChurchofJesusChrist.org.

Luka 11:37–44.Pengine familia yako ingejadili mistari hii mnapoosha vyombo pamoja. Mngeweza kuzungumza kuhusu kwa nini ingekuwa wazo baya kuosha nje tu ya vitu kama bakuli na vikombe. Mngeweza kuhusisha hilo na haja ya kuwa wema si tu katika matendo yetu ya nje bali pia katika mawazo na hisia zetu za ndani.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa “How Gentle God’s Commands,” Nyimbo, na. 125.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Kuwa na msimamo. Unaweza kuwa na siku ambapo kujifunza maandiko kunaonekana kuwa vigumu au kuwa na matokeo kidogo kuliko ulivyotumainia. Usikate Tamaa. Mzee David A. Bednar alifundisha, “Msimamo wetu katika kufanya mambo yanayoonekana kuwa madogo unaweza kusababisha matokeo ya kipekee ya kiroho” (“Bidii Zaidi na Kujali Nyumbani,” Liahona, Nov. 2009, 20).

Picha
ng’ombe dume wawili waliofungiwa nira

“Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo: nanyi mtapata raha nafsini mwenu;” (Mathayo 11:29). Picha © iStockphoto.com/Amphotora

Chapisha