Agano Jipya 2023
Machi 6–12. Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9: “Hao Thenashara Yesu Aliwatuma”


“Machi 6–12. Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9: ‘Hao Thenashara Yesu Aliwatuma’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Machi 6–12. Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
Yesu anamtawaza Petro

Machi 6–12

Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9

“Hao Thenashara Yesu Aliwatuma”

Mawazo ya kujifunza katika muhtasari huu yanakusudiwa kukusaidia kupata maana binafsi katika maandiko. Hayapaswi, hata hivyo, kuchukua nafasi ya ufunuo binafsi ambao unaweza kuupokea kuhusu ni vifungu gani vya kujifunza au jinsi ya kuvijifunza.

Andika Misukumo Yako

Habari ya miujiza ya Yesu kuponya ilikuwa ikisambaa kwa kasi. Umati ulimfuata, wakitumainia nafuu kutokana na magonjwa yao. Lakini wakati Mwokozi alipoutazama umati, Aliona zaidi ya maradhi yao ya kimwili. Akijawa na huruma, Aliwaona “kondoo wasio na mchungaji” (Mathayo 9:36). “Mavuno ni mengi, Aligundua, lakini watenda kazi ni wachache” (Mathayo 9:37). Hivyo aliwaita Mitume kumi na wawili, “akawapa amri,” na kuwatuma kufundisha na kuwahudumia “kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” (Mathayo 10:1,6). Leo hii hitaji la watenda kazi zaidi kuwahudumia watoto wa Baba wa Mbinguni bado ni kubwa. Bado kuna Mitume kumi na wawili, lakini kuna wafuasi wengi wa Yesu Kristo kuliko ilivyowahi kuwa hapo mwanzo—watu ambao wanaweza kutangaza ulimwenguni kote, “Ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mathayo 10:7).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mathayo 9:18–26; Marko 5:22–43

“Usiogope, amini tu.”

Wakati Yairo mwanzo alipomuomba Yesu amponye binti yake, ambaye alikuwa “katika kufa,” Yairo alizungumza kwa dharura lakini kwa matumaini: “nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, … apate kuishi” (Marko 5:23). Lakini walipokuwa wakienda, mjumbe akamwambia kwamba wamechelewa sana: “Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kumsumbua Mwalimu?” (mstari wa 35). Vivyo hivyo, ingeweza kuonekana kuchelewa sana kwa mwanamke aliyeelezewa katika Marko 5:25–34, ambaye alikuwa ameugua kwa miaka 12.

Unaposoma maelezo haya, unaweza kufikiria vitu ambavyo ambavyo vinahitaji uponyaji katika maisha yako au ya mwanafamilia wako—ikijumuisha vitu ambavyo vingeweza kuonekana “katika kufa” au vimechelewa sana kuweza kuponywa. Ni kitu gani kinachokupendeza kuhusu maonyesho ya imani katika maelezo haya? Tazama pia kile Yesu anachowaambia mwanamke na Yairo. Je, unahisi Yeye anakuambia nini wewe?

Ona pia Luka 8:41–56; Russell M. Nelson, “Kuvuta Nguvu ya Yesu Kristo kwenye Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2017, 39–42; Teachings of Presidents of the Church: Gordon B. Hinckley (2016), 333–42.

Picha
mwanamke akinyosha mkono kugusa vazi la Yesu

Mtumaini Bwana, na Liz Lemon Swindle

Mathayo 10; Luka 9:1–6

Bwana huwapa watumishi wake nguvu ya kufanya kazi Yake.

Maelekezo ambayo Yesu aliyatoa katika Mathayo 10 kwa Mitume Wake yanatumika kwetu pia, kwa sababu sisi sote tunayo sehemu katika kazi ya Bwana. Ni nguvu gani Kristo aliwapa Mitume Wake ili kuwasaidia kutimiza misheni zao? Je, ni kwa jinsi gani wewe unaweza kufikia nguvu Zake katika kazi uliyoitwa kufanya? (ona 2 Wakorintho 6:1–10; Mafundisho na Maagano 121:34–46).

Unaposoma mamlaka Kristo aliyowapa Mitume Wake, unaweza kupokea misukumo kuhusu kazi ambayo Bwana anakutaka wewe ufanye. Chati kama hii ifuatayo inaweza kukusaidia wewe kuyapanga mawazo yako:

Mathayo 10

Misukumo ninayopokea

Mwokozi aliwapa wanafunzi Wake nguvu.

Mungu atanipatia nguvu ninazohitaji katika kufanya kazi yangu.

Ona pia Marko 6:7–13; Makala ya Imani 1:6; Kamusi ya Biblia, “Mtume”; “Jesus Calls Twelve Apostles to Preach and Bless Others” (video), ChurchofJesusChrist.org.

Mathayo 10:17–20

Ninapokuwa katika huduma ya Bwana, Yeye atanishawishi kitu cha kusema.

Bwana aliona mapema kabla kwamba wanafunzi Wake wangeteswa na kuulizwa kuhusu imani yao—kitu ambacho ni sawa sawa na kile ambacho wanafunzi leo wanaweza kupitia. Lakini aliwaahidi wanafunzi wale kwamba wangejua kupitia Roho nini cha kusema. Je, umewahi kupatwa na matukio ambapo ahadi hii takatifu ilitimizwa katika maisha yako, pengine wakati ulipotoa ushuhuda wako, ulipotoa baraka, au ulipokuwa na mazungumzo na mtu? Fikiria kushiriki uzoefu wako na mpendwa wako au uandike kama kumbukumbu katika shajara. Je, unahisi kuongozwa kufanya nini ili kwamba uweze kuwa na uzoefu kama huo kila mara?

Ona pia Luka 12:11–12; Mafundisho na Maagano 84: 85.

Mathayo 10:34–39

Je, Yesu alimaanisha nini kwa kusema “Sikuja kuleta amani, bali upanga”?

Mzee D. Todd Christofferson alifundisha: “Nina uhakika kwamba wengi wenu mmekataliwa na kutengwa na baba na mama, akina kaka na akina dada mlipokubali injili ya Yesu Kristo na kuingia katika agano Lake. Kwa njia moja au nyingine, upendo wenu mkuu kwa Kristo umehitaji kuacha mahusiano ambayo yalikuwa ya thamani kwenu, na mmedondosha machozi mengi. Bado kwa upendo wenu usiopunguka, mnashikilia kwa uthabiti chini ya msalaba huu, mkijionyesha kutomuonea haya Mwana wa Mungu” (“Kupata Maisha Yako,” Ensign, Machi 2016, 28).

Utayari huu wa kupoteza uhusiano mliouenzi kwa upendo mkubwa kwa ajili ya kumfuata Mwokozi huja na ahadi kwamba “mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona” (Mathayo 10:39).

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Marko 5:22–43.Familia yako inaposoma hadithi pamoja, unaweza kutulia kidogo ili kuwauliza wanafamilia jinsi ambavyo wangeweza kuhisi kama wangekuwa Yairo, yule mwanamke, au watu wengine katika hadithi hii. Pengine unaweza kuonyesha picha za hadithi, kama vile zile zilizopo katika muhtasari huu. Je, ni kwa jinsi gani picha zinaonyesha imani ya watu katika hadithi hizi? (Ona pia video “Jesus Raises the Daughter of Jairus” na “Jesus Heals a Woman of Faith” kwenye ChurchofJesusChrist.org.) Unaweza pia kufikiria changamoto zinazoikabili familia yako. Tunawezaje kutumia maneno Yake, “Usiogope, amini tu”? (Marko 5:36).

Mathayo 10:39; Luka 9:23–26Inaweza kumaanisha nini kwa “kupoteza” maisha yako na “kuyaona”? (Mathayo 10:39) Pengine wanafamilia wangeweza kushiriki uzoefu walio nao ambao unaonyesha mafundisho ya Yesu katika mistari hii.

Mathayo 10:40Je, wewe na familia yako mnaendeleaje katika kupokea na kufuata ushauri wa Mitume wa siku za leo? Je, ni kwa jinsi gani utiifu wetu kwa ushauri wao hutuleta karibu zaidi na Yesu Kristo?

Luka 9:61–62.Je, inamaanisha nini kuangalia nyuma baada ya kuweka mkono kwenye jembe? Je, kwa nini mtazamo huu hutufanya sisi tusifae kwenye ufalme wa Mungu?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa“When Faith Endures,” Nyimbo za Kanisa, na. 128.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Msikilize Roho. Unapojifunza, kuwa makini na mawazo na hisia zako (ona Mafundisho na Maagano 8:2–3), hata kama vinaonekana havihusiani na kile unachosoma. Mawazo hayo yanaweza kuwa ndiyo mambo hasa Mungu anakutaka uyajue na uyafanye.

Picha
Yesu akimwinua msichana kutoka kitandani

Talitha Cumi, na Eva Koleva Timothy

Chapisha