Agano Jipya 2023
Februari 6–12. Yohana 2–4: “Hamna Budi Kuzaliwa Mara ya Pili”


“Februari 6–12. Yohana 2–4: ‘Hamna Budi Kuzaliwa Mara ya Pili,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Februari 6–12. Yohana 2–4,“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Yesu anazungumza na Nikodemo

Februari 6–12

Yohana 2–4

“Hamna Budi Kuzaliwa Mara ya Pili”

Katika darasa la muda mfupi la Msingi, hutakuwa na muda wa kufundisha kila kanuni iliyo muhimu katika Yohana 2–4. Tafuta mwongozo wa kiroho kuhusu nini cha kutilia mkazo ili kukidhi vyema mahitaji na mapendeleo ya watoto.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Himiza watoto kushiriki kile wanachosoma na kupitia, waulize ni kitu gani wamefanya hivi karibuni ili kuwa “wavuvi wa watu” (Mathayo 4:19). Unaweza kurejelea somo la wiki iliyopita pamoja nao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Yohana 3:1–10

Ninahitaji kubatizwa na kuthibitishwa ili kurudi kuishi na Baba wa Mbinguni.

Watoto unaowafundisha wanajiandaa kuchukua hatua muhimu kuishi na Baba wa Mbinguni tena kwa kubatizwa (kuzaliwa kwa maji) na kuthibitishwa (kuzaliwa kwa Roho). Unawezaje kuwasaidia waelewe umuhimu wa ibada hizi mbili?

Shughuli Yamkini

  • Fupisha hadithi ya Yesu anamfundisha Nikodemo (ona Yohana 3:1–10). Waahidi watoto kwamba watakapobatizwa, Baba wa Mbinguni Atawapatia kipawa cha Roho Mtakatifu.

  • Waonyoshe watoto ukurasa wa shughuli ya wiki hii, na waombe kuelezea michoro hii. Soma Yohana 3:5, na ushuhudie kwamba tunahitaji kubatizwa na kuthibitishwa ili kuishi na Baba wa Mbinguni tena.

  • Waombe watoto kuzungumza kuhusu wao wanafanya nini ili kuosha mikono yao. Onyesha picha Msichana Akibatizwa (Kitabu cha Sanaa za Injili,, na.104), na wasaidie watoto kulinganisha kuosha mikono yetu kwa maji na kuwa wasafi kiroho kupitia ubatizo.

Yohana 3:16

Baba wa Mbinguni Ananipenda, hivyo Yeye alinipa Mwokozi.

Unawezaje kuwasaidia watoto kujifunza ukweli huu wa thamani?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wakamilishe sentensi kama hii: “Kwa sababu wazazi wangu wananipenda, wao …” Soma Yohana 3:16. Halafu msaidie kila mtoto kurudia Yohana 3:16, kwa kubadilisha neno “ulimwengu” na jina lake mwenyewe. Wasaidie watoto kutambua mstari huu unasema Baba wa Mbinguni alifanya nini kwa sababu Yeye anatupenda sisi. Waalike wanafunzi kuchora picha Yesu. Waache washiriki picha zao pamoja na darasa na kueleza upendo wao kwa Mwokozi.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu Yesu Kristo, kama vile “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,, 34–35). Waache watoto wainue juu picha ya Yesu kila wakati wanapoimba neno kama “Mwana,” “Yesu.” au “Mwokozi.”

Yohana 4:5–15

Yesu Kristo ni “maji yangu ya uzima.”

Watoto katika darasa lako wanaweza wote kujihusisha na kuwa na kiu. Unawezaje kutumia uzoefu huo kuwasaidia watoto kuelewa jinsi gani tunahitaji maji ya uzima Yesu Kristo anayotoa?

Shughuli Yamkini

  • Tumia picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia kusimulia hadithi ya Yesu na mwanamke kisimani (ona Yohana 4:5–15). Waombe watoto wasimulie tena hadithi hiyo.

  • Onyesha glasi ya maji, na uzungumze na watoto kuhusu kwa nini tunahitaji maji. Kwa ufupi fanya muhtasari Yohana 4:5–15, na kushuhudia kwamba Yesu Kristo na Injili Yake huzipa roho zetu uzima, kama vile maji huipa uzima miili yetu.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Yohana 2:1-11

Ninaweza kumheshimu mama yangu kama Yesu alivyofanya.

Katika harusi huko Kana, Mariamu alimwambia Yesu kwamba divai imeisha. Kufuatana na tafsiri ya Joseph Smith, Yesu Alimjibu mama Yake kwa kumuuliza, “Mama, ni kitu gani ungetaka mimi nikifanye kwa ajili yako? ambacho nitafanya” (katika Yohana 2:4. tanbihi a). Yesu ni mfano wa jinsi watoto wanavyopaswa kuwatendea mama zao.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wasome Yohana 2:1–11 na kuchukua zamu kusimulia tena hadithi hii kwa maneno yao wenyewe.

  • Waulize watoto kuorodhesha vitu ambavyo mama yao anaweza kuhitaji msaada. Waalike wafanyie mazoezi kile wanachoweza kumwambia wakitumia baadhi ya maneno ya Yesu: “Ni kitu gani ungetaka Mimi nifanye kwa ajili yako?” (Yohana 2:4. tanbihi a).

  • Waalike baadhi ya wakina mama kutembelea darasa lako na kushiriki kile watoto wao hufanya ili kuonyesha heshima kwao.

Picha
Yesu akizungumza na Mariamu katika karamu ya harusi

Yesu Alisema kwa mama Yake, “ni kitu gani ungetaka mimi nikifanye kwa ajili yako?” (Tafsiri ya Joseph Smith, Yohana 2:4 [katika Yohana 2:4. tanbihi a]).

Yohana 3:1–8

Kubatizwa na kuthibitishwa ni kama kuzaliwa kwa mara ya pili.

Tunapobatizwa, ambako Yesu aliita “kuzaliwa kwa maji,” tunapokea ondoleo la dhambi zetu na “kuingia katika ufalme wa Mungu” (Yohana 3:5). Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuelewa kuzaliwa kwa mara ya pili inamaanisha nini?

Shughuli Yamkini

  • Tengeneza mishipi ya maneno ya karatasi ikionyesha maneno ya Mwokozi katika Yohana 3:3, na waache watoto wayaweke katika utaratibu sahihi. Ni kwa jinsi gani kubatizwa na kuthibitishwa ni kama kuzaliwa kwa mara ya pili?

  • Onyesha picha ya mtoto mchanga aliyezaliwa na mtu mwingine akibatizwa na kuthibitishwa (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.104–5). Ni kwa jinsi gani sisi tunakuwa kama mtoto mchanga baada ya kuwa tumebatizwa na kuthibitishwa? (ona Yohana 3:3–5).

  • Waalike watoto kushiriki kumbukumbu za ubatizo wao. Soma Mosia 18:8–10 na Mafundisho na Maagano 20:37 ili kurejelea agano la ubatizo. Wafundishe watoto kwamba kupokea sakramenti kwa umakini kila wiki ni njia ya kuendelea na mchakato wa kuzaliwa tena.

  • Wasaidie watoto kukariri Makala ya Imani 1:4.

Yohana 3:16–17

Baba wa Mbinguni Ananipenda, hivyo Yeye alimtuma Mwanawe.

Unawezaje kuwasaidia watoto kujua kwamba Yesu Kristo alitumwa duniani kama kielelezo cha upendo wa Baba wa Mbinguni?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kuchora picha ya zawadi waipendayo na mtu aliyewapatia hiyo zawadi. Halafu muuliza mtoto asome Yohana 3:16. Ni zawadi gani Baba wa Mbinguni Ametupatia? Ni kwa jinsi gani zawadi hii inaonyesha upendo Wake?

  • Waombe watoto kutafuta majibu ya maswali “Kwa nini baba wa Mbinguni alituletea Yesu Kristo?” wanaposoma Yohana 3:16–17 au imbeni au sikilizeni “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35).

Yohana 4:5–23

Yesu Kristo ananipa “maji ya uzima.”

Kama Yesu Alivyotumia maji kumfundisha mwanamke wa Samaria, unaweza kutumia maji kuwafundisha watoto kwa nini tunahitaji injili ya Yesu Kristo.

Shughuli Yamkini

  • Kutumia Yohana 4:5–23, andika muhtasari wa mistari hii kutokana na hadithi ya yule mwanamke kisimani. Waombe watoto kurejelea mistari hii ili kuweka sentensi hizi katika utaratibu sahihi. Yesu alikuwa anajaribu kumfundisha nini yule mwanamke?

  • Wapeni watoto kinywaji cha maji, na waombe washiriki uzoefu wao wakati walipokuwa na kiu. Zungumza kuhusu jinsi ulivyojisikia hatimaye kupata maji ya kunywa. Waalike watoto kutaja vitu ambavyo, kama kikombe cha maji, huturidhisha kwa muda. Ni vitu gani kama “maji ya uzima” ambavyo vinaweza kuturidhisha milele?

  • Andika ubaoni Ni kwa namna gani injili ni kama maji? Uliza watoto kufikiria kuhusu jinsi ambavyo wangeweza kujibu hili swali wanaposoma katika Yohana 4:5–23.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Fikiria kuwaomba watoto kuwapatia wanafamilia wao kinywaji cha maji watakapofika nyumbani. Wanapofanya hivi, wanaweza kushiriki kile walichojifunza kuhusu maji ya uzima.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia kurasa za shughuli. Watoto wanapokamilisha kurasa za shughuli, tumia muda kupitia kanuni kutoka katika somo hili.

Chapisha