Agano Jipya 2023
Januari 30–Februari 5. Mathayo 4; Luka 4–5: “Roho wa Bwana Yu pamoja Nami”


“Januari 30–Februari 5 Mathayo 4: Luka 4–5: ‘Roho wa Bwana Yu pamoja Nami’’’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Januari 30–Februari 5 Mathayo 4: Luka 4–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Yesu amesimama nyikani

Nyikani, na Eva Koleva Timothy

Januari 30–Februari 5

Mathayo 4; Luka 4–5

“Roho wa Bwana Yu juu Yangu”

Anza maandalizi yako ya somo hili kwa kusoma Mathayo 4 na Luka 4–5. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa sura hizi, na muhtasari huu unaweza kukupa mawazo ya kufundisha.

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waombe watoto wapitishe picha ya Yesu kutoka mtoto mmoja hadi mwingine. Kila mtoto anaposhikilia picha, mwalike kushiriki kitu fulani ambacho Yesu alifanya Alipokuwa duniani.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mathayo 4:1–11; Luka 4:1–13

Ninaweza kuchagua kilicho sahihi kama Yesu alivyofanya.

Watoto wadogo “hawawezi kutenda dhambi” (Mafundisho na Maagano 29: 47). Hata hivyo, tukio la Yesu akipinga majaribu ya Shetani linaweza kuwahamasisha watoto kuchagua kilicho sahihi.

Shughuli Yamkini

  • Simulia hadithi ya majaribu ya Yesu kutoka Mathayo 4:1–11. (Ona pia “Sura 11: Yesu Akijaribiwa”,” Hadithi za Agano Jipya, 30–31, au video zinazoambatana katika ChurchofJesusChrist.org.) Katika sehemu inayofaa katika hadithi, uliza, “Unafikiri Yesu Anapaswa kufanya nini?”

  • Onyesha picha ya Yesu Kristo, na halafu elezea chaguzi ambazo mtoto mdogo anaweza kufanya. Waombe watoto kupiga hatua moja kuelekea kwenye picha kila wakati unapoelezea uchaguzi ulio mzuri. Waambie wapige hatua moja mbali nayo kila wakati unapoelezea uchaguzi mbaya.

  • Wasaidie watoto kujifunza maneno ya wimbo kuhusu kufanya chaguzi nzuri, kama vile “Choose the Right Way” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,160–61). Tumia picha, vitu, au visaidizi vya kuona vingine ambavyo vinahusiana na mashairi hayo.

Luka 4:18–19

Yesu Kristo ni Mwokozi wangu.

Luka 4: 18–19 inaelezea juu ya misheni ya Yesu. Unawezaje kuwasaidia watoto kuthamini alichokifanya kwa ajili yao?

Shughuli Yamkini

  • Wasomee Luka 4:18–19 watoto, na ueleze ni kitu gani Yesu Kristo alitumwa kukifanya duniani (kutufundisha sisi jinsi ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni, kutufariji, na kuponya watu). Shiriki jinsi alivyofanya vitu hivi kwa ajili yako.

  • Waalike watoto wachache wajifanye wamechanganyikiwa, wanasikitika, au wagonjwa. Waombe watoto wengine kuigiza kile ambacho wangefanya ili kuwasaidia. Shuhudia kwamba Yesu Kristo alikuja kufundisha, kufariji, na kutuponya na kwamba tunatakiwa kufuata mfano Wake.

  • Onyesha picha ya Yesu akitimiza misheni Yake (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili). Waombe watoto wakuambie Yesu anafanya nini katika kila picha. Pia onyesha picha za watu wakijaribu kuwa kama Yesu (unaweza kuzipata baadhi kwenye magazeti ya Kanisa).

Mathayo 4:18–22; Luka 5:1-11

Yesu Kristo anatualika sisi tuwe “wavuvi wa watu”.

Wito wa Mwokozi, “Nifuate, na nitawafanya wavuvi wa watu” (Mathayo 4:19), inatumika kwa kila mtu, hata watoto.

Shughuli Yamkini

  • Alika watoto wawili kujifanya kuwa Simoni Petro na Andrea unaposoma Mathayo 4:18–22. Wasaidie watoto kutambua wanaume hawa waliacha nini ili kumfuata Yesu.

  • Waache watoto wachukue zamu kusimulia hadithi kutoka kwenye mistari hii wakitumia picha kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Nifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu kumfuata Yesu Kristo, kama vile “I Will Follow God’s Plan” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 164). Wasaidie watoto kutafuta vitu vilivyotajwa katika wimbo ambavyo wao wanaweza kufanya ili kumfuata Yesu.

  • Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kujadili na watoto jinsi wanavyoweza kuwa “wavuvi wa watu” kwa kumfuata Yesu. Ungeweza kucheza mchezo unaofanana na ule wa ukurasa wa shughuli. Kata nakala mbili za kila samaki, ziweke zikiangalia chini, na alika watoto kuchukua zamu kuzigeuza moja baada ya nyingine ili kuoanisha.

Yesu anawaita wafuasi

Kristo Akiwaita Wafuasi Wawili,, na Gary Ernest Smith

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mathayo 4:1–11; Luka 4:1–13

Kristo aliweka mfano kwa ajili yangu kwa kushinda majaribu.

Hata Yesu Kristo alijaribiwa na Shetani, lakini Yeye hakukubali. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kufuata mfano Wake?

Shughuli Yamkini

  • Tengeneza chati kwenye ubao iliyoandikwa Majaribu ya Shetani na Majibu ya Yesu. Wasaidie watoto kujaza chati wakitumia Mathayo 4:1–11 na Luka 4:1–13. Uliza watoto jinsi wanavyoweza kufuata mfano wa Yesu.

  • Andika baadhi ya matukio ambapo mtoto angeweza kujaribiwa kufanya chaguo baya. Mwache mtoto achague moja la kusoma, na waombe watato kuzungumza jinsi ambavyo wangeweza kupinga majaribu katika hali hiyo.

Mathayo 4:1–2

Kufunga kunaweza kunisaidia kuhisi niko karibu na Baba wa Mbinguni.

Kabla ya kuanza huduma Yake, Yesu alifunga na “kuwasiliana na Mungu” (Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 4:2 [katika Mathayo 4:2, tanbihi c]). Wasaidie watoto kuona jinsi kufunga kunavyoweza kuwapatia nguvu ya kiroho na kuwasaidia kuhisi kuwa karibu na Baba wa Mbinguni.

Shughuli Yamkini

  • Alika mtoto asome Mathayo 4:1–2 akitumia Tafsiri ya Joseph Smith ya marekebisho yanayopatikana kwenye tanbihi. Yesu alifanya nini ili “kuwa na Mungu”? Shiriki jinsi kufunga kumekusaidia wewe kuhisi kuwa karibu zaidi na Baba wa Mbinguni.

  • Alika watoto ambao wamewahi kufunga kushiriki uzoefu wao. Wanawezaje kuelezea kuhusu kufunga kwa mtu ambaye hajawahi kufunga hapo awali?

  • Andika maswali kuhusu kufunga (kama vile kwa nini, wakati gani, au jinsi gani tunafunga) kwenye vipande vya karatasi na uviweke kwenye bakuli. Alika watoto waokote swali na kujaribu kulijibu. Ni uzoefu gani wewe au watoto mnaweza kushiriki kuhusu kufunga?

Luka 4:16–22, 28–30

Yesu Kristo ni Mwokozi wangu.

Tafakari jinsi ambavyo Mwokozi amebariki maisha yako. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuthamini vyema ushawishi Wake katika maisha yao?

Shughuli Yamkini

  • Mwalike mtoto kuja darasani akiwa amejiandaa kushiriki hadithi katika Luka 4:16 –30. Yawezekana ikasaidia kutumia “Sura ya 17: Watu Waliokasirika huko Nazareti” (katika Hadithi za Agano Jipya, 42–43, au video inayofanana nayo katika ChurchofJesusChrist.org). Ungeweza pia kuonesha video “Jesus Declares He Is the Messiah” (ChurchofJesusChrist.org).

  • Soma Luka 4:1 kwa sauti wakati watoto wanafuatilia. Waombe watengeneze orodha ya vitu ambavyo Mwokozi alisema amekuja kuvifanya. Waalike watoto kushiriki mifano ya nyakati ambapo Kristo alitenda vitu hivi, aidha kwenye maandiko au kwenye maisha yao.

  • Andika kwenye mikanda ya karatasi maneno “Kwa sababu ya Yesu Kristo …” Mpe karatasi kila mtoto, na ninawaalika kuandika jinsi ambavyo wangekamilisha kirai hiki. Waache washiriki kile walichoandika.

Mathayo 4:18–22; Luka 5:1–11

Yesu Kristo anatualika tumfuate na tuwe “wavuvi wa watu.”

Kuna njia nyingi ambazo watoto wanaweza kumfuata Mwokozi na kuwa “wavuvi wa watu” (Mathayo 4:19). Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wao kuona ushawishi mzuri wanaoweza kuwa nao kwa wengine?

Shughuli za Yakini

  • Alika watoto wasome Mathayo 4:18–22 na Luka 5:1–11. Ni kwa jinsi gani wanafunzi wa Yesu waliitikia wito wa kumfuata Yeye? Tunaweza kufanya nini ili kufuata mfano wao?

  • Onyesha watoto baadhi ya vifaa vya uvuvi au picha ya mvuvi. Inamaanisha nini kuwa “mvuvi wa watu”? Zana gani tulizonazo za kutusaidia kuwa wavuvi wa watu?

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki na familia zao kile ambacho wamejifunza kuhusu kuwa wavuvi wa watu.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto wanaweza kutambua ushawishi wa Roho. Wafundishe watoto kwamba hisia za amani, upendo, na amani walizonazo wakati wanaongea au kuimba kuhusu Yesu Kristo na injili Yake zinatoka kwa Roho Mtakatifu. Hisia hizi zinaweza kujenga shuhuda zao.