Agano Jipya 2023
Januari 23–29. Mathayo 3; Marko 1; Luka 3: “Andaeni Njia ya Bwana”


“Januari 23–29. Mathayo 3; Marko 1: Luka 3: ‘Andaeni Njia ya Bwana’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Januari 23–29. Mathayo 3; Marko 1: Luka 3.“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Yohana Mbatizaji Anambatiza Yesu

Dirisha-lenye kioo kilichotiwa rangi za kuona katika Hekalu la Illinois, na Tom Holdman

Januari 23–29

Mathayo 3; Marko 1; Luka 3

“Itengenezeni Njia ya Bwana”

Unaposoma kuhusu Yohana Mbatizaji na ubatizo wa Yesu Kristo, andika msukumo wo wote wa kiroho unayopokea. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa haya maandiko, na itakusaidia wewe kuunga mkono mafunzo ambayo watoto wanafanya nyumbani.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwapa watoto nafasi ya kushiriki kile walichokwisha kusoma, onyesha picha ya Yesu akibatizwa. Waombe wao wakuambie kile kinachotendeka katika picha na jinsi wanavyojisikia kuhusu kubatizwa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mathayo 3:13–17

Ninaweza kubatizwa kama Yesu alivyobatizwa.

Unawezaje kutumia hadithi ya ubatizo wa Yesu ili kuwasaidia watoto kujiandaa kubatizwa?

Shughuli Yamkini

  • Fanya muhtasari wa hadithi ya ubatizo wa Mwokozi (ona Mathayo 3:13–17; ona pia “Sura 10: Yesu Anabatizwa,” katika Hadithi za Agano Jipya, 26–29, au video inayofanana nayo katika ChurchofJesus Christ.org). Elezea kwamba Yesu alibatizwa kwa kuzamishwa na mtu aliyekuwa na mamlaka ya ukuhani. Rudia hadithi hii mara kadhaa na waalike watoto kushiriki taarifa wanazokumbuka.

  • Onyesha picha ya Yesu akibatizwa na ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Waache watoto waonyeshe mifanano kati ya hizi picha mbili. (Kuna picha ya Yesu akiwa anabatizwa katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.)

  • Rejelea ahadi ambazo watoto watazifanya wakati wanapokuwa wanabatizwa (ona Mosia 18:8–10; Mafundisho na Maagano 20:37; Mada za Injili, “Ubatizo,” topics.ChurchofJesusChrist.org). Waulize watoto kipi kati ya vitu hivi ambacho tayari wanafanya.

  • Mwalike mshiriki wa uaskofu kuwaambia watoto kuhusu mahojiano ya ubatizo ambayo watakuwa nayo kabla ya kubatizwa.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu ubatizo, kama vile “Ubatizo” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 100–101). Fikiria kumwomba mtoto kuongoza watoto wengine wakati wanaimba

Picha
msichana akibatizwa

Tunaweza kufuata mfano wa Yesu kwa kubatizwa.

Mathayo 3:11, 16

Roho Mtakatifu hunisaidia mimi.

Mbali na kujiandaa kwa ajili ya ubatizo, watoto pia wanajiandaa kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Unawezaje kuwasaidia?

Shughuli Yamkini

  • Tumia Mathayo 3:11, 16 ili kuwafundisha watoto kwamba Roho Mtakatifu alimshukia Yesu wakati alipokuwa akibatizwa (njiwa alitokea kama ishara kuonyesha kwamba hii imetendeka) Onyesha picha Kipawa cha Roho Mtakatifu (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.105), na elezea kwamba tunapokea kipawa cha Roho Mtakatifu wakati tunapothibitishwa.

  • Lete sanduku lenye vitu kama vile picha ya Yesu, blanketi lenye kutia joto, na dira au ramani. Waalike watoto kuchagua kitu, na acha waelezee jinsi kitu kinawakilisha njia ambayo kwayo Roho Mtakatifu anavyoweza kutusaidia sisi—Yeye anashuhudia juu ya Yesu (ona Yohana 15:26), anatufariji (ona Yohana 14:26), kinatuonyesha njia sahihi ya kuenenda (ona 2 Nefi 32:5).

  • Shiriki uzoefu wako mwenyewe wa kupokea msaada kutoka kwa Roho Mtakatifu.

  • Waalike watoto kusikiliza njia ambazo Roho Mtakatifu hutusaidia wanapoimba kuhusu Yeye, kama vile “The Holy Ghost” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,105).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mathayo 3

Nimebarikiwa na ibada za Ukuhani wa Haruni.

Yohana Mbatizaji alishikilia Ukuhani wa Haruni, kwa hiyo kusoma kuhusu Yeye katika Mathayo 3 ni fursa nzuri ya kufundisha watoto kuhusu Ukuhani wa Haruni. Wasaidie kutambua baraka na nguvu ambazo huja kwetu kupitia Ukuhani wa Melkizediki?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kutengeneza orodha ya kazi za Ukuhani wa Haruni, ukitumia Mafundisho na Maagano 20:46, 58–60; 84:111. Waombe watoto kuangalia katika Mathayo 3 kwa ajili ya mifano ya Yohana akitimiza baadhi ya kazi hizi. Sisi sote tunawezaje kuwaalika wengine kuja kwa Kristo, kama Yohana alivyofanya?

  • Onyesha baadhi ya picha za wenye Ukuhani wa Haruni wakifanya ibada za ubatizo na sakramenti (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 103–4, 107–8). Jadili jinsi ibada hizi zinavyotuandaa kumpokea Yesu Kristo na baraka za Upatanisho Wake.

  • Someni pamoja Mafundisho na Maagano 13:1, na ueleze kwamba Yohana Mbatizaji alirejesha Ukuhani wa Haruni kwa Joseph Smith. Waulize watoto jinsi walivyoweza kubarikiwa kwa sababu Ukuhani wa Haruni ulirejeshwa.

Mathayo 3:13–17; Marko 1:1–11; Luka 3:2–18

Ninaweza kuyashika maagano yangu ya ubatizo.

Kujifunza kuhusu hadithi ya ubatizo wa Yesu kunatoa fursa nzuri ili kuwasaidia watoto kurejelea maagano yao ya ubatizo kuweka upya dhamira ya kuendelea kuyashika.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wafanye zamu kusoma mistari kutoka Marko 1:1–11. Jadilianeni ni kwa nini, Baba wa Mbinguni anatutaka sisi tubatizwe? Kwa nini Yesu alibatizwa, ingawa hakuhitajika kuoshwa kwa sababu ya dhambi? Wasaidie watoto kupata majibu ya swali hili katika Mathayo 3:13–15 na 2 Nefi 31:6–7.

  • Rejelea maagano ambayo watoto waliyafanya kwenye ubatizo, yanayopatikana katika Mosia 18:8–10 na Mafundisho na Maagano 20:37. Waalike watoto kuandika marejeo haya katika ukurasa wa shughuli ya wiki hii.

  • Andaa jozi kadhaa za kadi na maneno yanayofanana au picha zinazowakilisha maagano yetu ya ubatizo. Ziweke kadi zikiangalia chini. Waalike watoto kuchukua zamu wakizigeuza kadi mbili kwa wakati mmoja, wakitafuta zile zinazofanana. Baada ya muoanisho kufanyika, waalike watoto kushiriki njia walizoshika maagano hayo.

  • Shiriki jinsi kushika maagano yako ya ubatizo kulivyokubariki.

Mathayo 3:11, 16

Roho Mtakatifu anaweza kuniongoza.

Watoto wanajifunza jinsi ya kutambua na kuufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu. Wasaidie kuelewa kwamba kushika maagano yao ya ubatizo kutawasaidia kuwa wenye kustahili kupokea mwongozo Wake?

Shughuli Yamkini

  • Mwombe kila mtoto asome mojawapo ya maandiko na kuelezea yanafundisha nini kuhusu jinsi gani Roho Mtakatifu anavyoongea na sisi: Helamani 5:30; Mafundisho na Maagano 6:23; 8:2–3; 11:12–13.

  • Muombe mtoto asome Mathayo 3:11. Ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu ni kama moto? Kwa mfano, moto unaweza kufariji, na unatupatia nuru ili kutuongoza (ona Yohana 15:26; 2 Nefi 32:5).

  • Waalike watoto kufunga macho yao na kushikilia mikono yao. Kisha taratibu sugua viganja vyao kwa nyoya au kamba. Waalike waseme pindi watakapohisi hivyo. Ni nini shughuli hii inatufundisha kuhusu kutambua misukumo ya Roho Mtakatifu?

  • Waalike watoto kushiriki uzoefu walioupata kwa njia ya Roho Mtakatifu. Kwa nini kushika maagano yetu kunatusaidia kuwa na mwongozo wa Roho Mtakatifu?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Himiza kila mtoto kuwaambia wazazi wake au wanafamilia wengine kuhusu ubatizo wao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tafuta mwongozo wa kiungu wewe mwenyewe. Usichukulie mihutasari hii kama maelekezo ambayo ni lazima kuyafuata unapofundisha. Badala yake, itumie kama mawazo ya kuchochea hisia zako mwenyewe unapotafakari mahitaji ya watoto unaowafundisha. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi7.)

Chapisha