Agano Jipya 2023
Januari 16–22. Yohana 1: Tumemwona Masiya


“Januari 16–22. Yohana 1: Tumemwona Masiya,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Januari 16–22. Yohana 1,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi: 2023

mwanamke akishiriki injili kwenye stesheni cha gari moshi.

Januari 16–22

Yohana 1

Tumemwona Masiya

Unaposoma Yohana 1, andika misukumo ya kiroho unayopokea. Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unaweza kukusaidia kuelewa sura hii. Shughuli zifuatazo zilizopendekezwa zinaweza kukupa mawazo kuhusu jinsi ya kuwasaidia watoto kujifunza kanuni katika Yohana 1. Shughuli kwa ajili ya watoto wakubwa zinaweza kutoholewa, kama itahitajika, kwa watoto wadogo.

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwasaidia watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu Yesu, waonyeshe picha Zake akitimiza baadhi ya nafasi Zake zilizoelezwa katika Yohana1 (kama vile kuumba dunia au kufundisha injili). Waombe watoto kueleza kile kinachotokea katika picha.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Yohana 1:1–2

Yesu aliishi na Baba wa Mbinguni kabla hajazaliwa.

Yohana alifundisha kuwa Yesu Kristo aliishi na Mungu kabla ya maisha Yake hapa duniani. Sisi tuliishi na Mungu kabla ya kuzaliwa (ona “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” ChurchofJesusChrist.org). Je, utawafundishaje watoto ukweli huu?

Shughuli Yamkini

  • Elezea kwamba “Neno” katika Yohana1:1 linamaanisha Yesu. Soma mstari huu kwa sauti, na waambie watoto waseme “Yesu” kila wakati unaposoma “Neno.” Onyesha kielelezo chenye jina “Maisha Kabla Kuzaliwa Duniani” (ChurchofJesusChrist.org; ona pia Tazama Wachanga Wenu [2008], 15). Elezea kwamba Yesu Kristo aliishi na Baba wa Mbinguni kabla ya kuja duniani.

  • Chukua kutoka kwenye nyenzo kama hizi ili kuwafundisha watoto kuhusu maisha yetu pamoja na Mungu kabla ya kuja duniani: “Utangulizi: Mpango wa Baba Yetu wa Mbinguni” (katika Hadithi za Agano Jipya, 1–5, au video inayofanana nayo kwenye ChurchofJesusChrist.org) au “Maisha kabla ya kuzaliwa duniani” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org).

  • Mwalike mzazi amlete mtoto darasani. Waulize watoto roho ya mtoto huyu iliishi wapi kabla ya kuzaliwa. Wakumbushe watoto kwamba na wao walikuwa watoto wakati mmoja, na shuhudia kwamba waliishi pamoja na Baba wa Mbinguni kama watoto wa kiroho kabla hawajazaliwa.

Yohana 1:3

Yesu aliviumba vitu vyote.

Kujua kuhusu nafasi ya Kristo kama Muumbaji kunaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuongeza staha yao Kwake.

Shughuli Yamkini

  • Soma Yohana 1:3 pamoja na watoto, na onyesha picha kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Wasaidie watoto kukariri kirai “vitu vyote vilitengenezwa na [Yesu Kristo].”

  • Mwonyeshe mmoja wa watoto picha ya moja ya uumbaji wa Bwana. Mwache aielezee kwa watoto wengine, na waulize kubahatisha kile kinachoelezewa.

  • Muombe kila mtoto ataje kitu kimoja ambacho Yesu Kristo alikiumba. Wasaidie watoto kufikiria njia wanazoweza kuitunza dunia na viumbe vingine vya Bwana.

kuchomoza kwa jua msituni

Yesu Kristo aliumba ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake.

Yohana 1:35–51

Ninaweza kuwaalika wengine kuja kwa Yesu Kristo na kujifunza juu Yake.

Yohana 1 ina simulizi ya wafuasi ambao wakiwaalika watu “njooni muone” kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Hata watoto wadogo wanaweza kufuata mfano huu.

Shughuli Yamkini

  • Elezea jinsi Andrea alivyojua kuhusu Yesu, na simulia jinsi Andrea alivyomfundisha Petro (ona Yohana 1:35–42). Shiriki jinsi ulivyojua kuhusu Kanisa, au mwalike mshiriki mpya kushiriki jinsi yeye alivyojifunza kuhusu Kanisa.

  • Shiriki hadithi ya Filipo akimwalika Natanieli “Njoo na uone” (Yohana1:43–51). Ficha picha ya Yesu kwenye sanduku, na umwalike mtoto mmoja “Njoo uone” na kisha awaambie watoto wengine kuhusu kile alichokiona.

  • Waache watoto wapake rangi ukurasa wa shughuli ya wiki hii, na wahimize kuitumia kumwalika mtu kujifunza kuhusu Yesu.

  • Muombe mtoto kusimulia kuhusu kipindi ambacho yeye alishiriki kitu, kama vile mwanasesere au zawadi, na mtu mwingine. Ni kwa jinsi gani tunaweza kushiriki injili? Simulia hadithi ya mtoto ambaye alishiriki injili na rafiki yake, kama vile “Rafiki na Mmsionari,” Rafiki, Julai 2018, 12–13; Liahona, Julai 2018, 70–71.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Yohana 1:1–5

Yesu aliishi pamoja na Baba wa Mbinguni kabla ya kuzaliwa.

Hata kabla ya kuzaliwa, Yesu Kristo alitekeleza wajibu katika mpango wa Baba wa Mbinguni. Unaposoma Yohana 1:1–5, ni nini kinachokuvutia kuhusu kazi ya Kristo kabla kuzaliwa duniani.

Shughuli Yamkini

  • Waulize watoto kama wanajua chochote kuhusu kitu ambacho Yesu alifanya kabla hajazaliwa. Waalike watafute majibu katika Yohana 1:1–5. Inaweza kusaidia kuangalia katika Tafsiri ya Joseph Smith, Yohana1:1–5 (katika kiambatisho cha Biblia).

  • Shiriki sehemu za “Utangulizi: Mpango wa Baba Yetu wa Mbinguni” (katika Hadithi za Agano Jipya, 1–5, au video inayofanana nayo kwenye ChurchofJesusChrist.org). Waulize watoto kile wanachojifunza kuhusu Yesu Kristo.

  • Siku chache kabla, waalike baadhi ya watoto kuja darasani wakiwa wamejiandaa kuonyesha au kuelezea kitu walichounda. Onyesha baadhi ya picha za uumbaji wa Bwana, na tumia Yohana 1:3 kuelezea kwamba Yesu aliumba nchi na kila kitu kilichopo ndani yake.

Yohana 1:4–9

Yesu Kristo ni nuru yangu.

Mfano wa nuru unaweza kuwasaidia watoto kumuelewa Mwokozi na injili Yake. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwahamasisha watoto kutafuta nuru ya Mwokozi wakati dunia inapoonekana giza?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kusoma Zaburi 27:1; Yohana 1:4–9; Mosia 16:9; na Mafundisho na Maagano 39:1–2, wakiangalia maneno ambayo yanalingana kwenye maandiko haya. Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo ni kama nuru?

  • Onyesha picha ya Mwokozi na baadhi ya vitu ambavyo hutoa nuru kama vile tochi. Ni kwa njia gani Yesu Kristo ni kama vitu hivi? Ni kwa jinsi gani tunaweza kushiriki nuru Yake na wengine? Imbeni pamoja “The Lord Is My Light” (Nyimbo, na. 89) au wimbo mwingine kuhusu nuru ya injili.

  • Waulize watoto kile wanachofanya wanapokuwa gizani na wanapohisi na uoga. Shuhudia kwamba kila wakati wanaweza kumgeukia Mwokozi wanapokuwa na woga.

Yohana 1:35–51

Kama mfuasi wa Yesu Kristo, ninawaalika wengine kumfuata Yeye.

Fikiria jinsi unavyoweza kutumia mifano katika Yohana 1:35–51 kuwahimiza watoto kuwaalika wengine kujifunza kuhusu Mwokozi.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kupekua Yohana 1:35–51 ili kutafuta vitu ambavyo watu walisema kuwaalika wengine kujifunza kuhusu Mwokozi. Waache wafanyie mazoezi kile wanachoweza kusema ili kumwalika rafiki kujifunza kuhusu Yeye.

  • Waombe watoto watumie ukurasa wa shughuli ya wiki hii kutengeneza mwaliko wanaoweza kutumia kumwalika rafiki au mmoja wa familia kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo.

  • Wape watoto nafasi kuelezea kwa darasa kuhusu kitu ambacho wanakipenda. Wasaidie watoto kuona jinsi kushiriki injili kunavyoweza kuwa kama kushiriki vitu vingine tunavyovipenda (kwa mfano, ona video “Good Things to Share” kwenye ChurchofJesusChrist.org).

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Himiza watoto kumwalika mtu fulani wanayependa ajifunze zaidi kuhusu Yesu Kristo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia visaidizi vya kuona. Tafuta njia za kuwasaidia watoto kuona kile wanachojifunza katika maandiko. Unaweza kufanya hivyo kwa sanaa za injili, michoro, video, vikaragosi, au vichekesho.