Agano Jipya 2023
Disemba 26–Januari 1 Tunawajibika kwa Kujifunza Kwetu Wenyewe


Disemba 26–Januari 1. Tunawajibika kwa Kujifunza Kwetu Wenyewe,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

Disemba 26–Januari 1. Tunawajibika kwa Kujifunza Kwetu Wenyewe,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
familia ikitazama picha kwenye albamu

Disemba 26–Januari 1

Tunawajibika kwa Kujifunza Kwetu Wenyewe

Unaposoma maandiko katika muhtasari huu, andika misukumo yo yote ya kiroho unayopokea. Utagundua kwamba kila muhtasari katika kitabu hiki cha kiada una shughuli za watoto wadogo na watoto wakubwa, lakini unaweza kutohoa shughuli yo yote kwa ajili ya darasa lako.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Mwanzoni mwa kila darasa, wape watoto nafasi za kushiriki yale wanayojifunza kuhusu injili. Kwa mfano, wiki hii unaweza kuwaalika wao kushiriki hadithi wanazozipenda kuhusu Yesu Kristo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Yesu Kristo anataka nimfuate Yeye.

Wewe na watoto mtasoma hadithi nyingi kutoka katika maisha ya Yesu Kristo mwaka huu. Wasaidie watoto kuelewa kwamba sababu ya kujifunza kwetu hadithi hizi ni ili kwamba tuweze kufuata vyema mfano kamili wa Yesu Kristo.

Shughuli Yamkini

  • Waambie watoto kuhusu mwaliko wa Mwokozi, “Nifuate,” unaopatikana katika Mathayo 4:18–22. Cheza mchezo ambapo mtoto mmoja anafanya kitendo na kisha anawaambia watoto wengine, “Nifuateni.” Waalike watoto wengine kurudia kitendo hicho.

  • Onyesha picha za watu wakimfuata Mwokozi katika njia tofauti, wakati wa huduma Yake akiwa duniani na katika siku yetu. Unaweza kuzipata picha katika Kitabu cha Sanaa za Injili au katika Magazeti ya Kanisa. Unaweza pia kuonyesha video “ “Light the World” (ChurchofJesusChrist.org). Waache watoto watambue jinsi watu wanavyomfuata Mwokozi.

  • Wasaidie watoto kufikiria juu ya vitu wanavyofanya kumfuata Mwokozi. Kuimba “Seek the Lord Early” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 108) kungeweza kuwapa baadhi ya mawazo. Waache wachore picha zao wenyewe wakifanya mambo haya.

Picha
mvulana anasoma maandiko

Watoto wanaweza kupata ushuhuda wao wenyewe wa kweli za kiroho.

Maandiko ni ya kweli.

Watoto wanaweza kupata ushuhuda kwamba maandiko ni ya kweli hata kabla hawajaweza kuyasoma. Unaposoma maandiko na watoto mwaka huu, unaweza kuwasaidia kujua wao wenyewe kwamba maandiko ni ya kweli.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kueleza kuhusu zawadi wazipendazo walizopokea kwa ajili ya siku za kuzaliwa au matukio mengine. Leta nakala ya maandiko iliyofungwa kama zawadi, mwachie mtoto aifungue, na kushuhudia kwamba maandiko ni zawadi kwetu kutoka kwa Baba wa Mbinguni.

  • Onyesha watoto baadhi ya vitabu vyenye hadithi za kutunga, na uwaulize kuhusu hadithi wazipendazo. Waonyeshe maandiko, na shuhudia kwamba maandiko yana neno la Mungu kwa ajili yetu sisi. Yanazungumza juu ya watu ambao waliishi kweli na mambo ambayo kweli yalitokea.

  • Shiriki jumbe zipatikanazo katika 2 Timotheo 3:15 na Moroni 10:3–4, ukiwasaidia watoto kurudia virai vichache. Wasaidie kuelewa kwamba wao nao wanaweza kujua maandiko ni ya kweli wao wenyewe.

  • Ficha picha ya Mwokozi, na wape watoto vidokezo vya kuwasaidia kuipata. Wasaidie watoto kuelewa jinsi kupekua maandiko kunavyoweza kutusaidia sisi kumjua Yesu Kristo. Waache watoto wafiche kwa zamu picha na kutoa vidokezo kwa watoto wengine.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu kujifunza injili, kama vile “Search, Ponder, and Pray” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109), na uwasaidie watoto kubuni matendo yanayoendana na maneno hayo. Shiriki na watoto andiko moja au mawili uyapendayo, na kuwaambia jinsi wewe ulivyokuja kujua maandiko ni ya kweli. Kama watoto wana maandiko wayapendayo au hadithi za maandiko, waalike kushiriki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Yesu Kristo anataka nijifunze kumhusu Yeye na nimfuate Yeye.

Fikiria kuhusu jinsi wewe ulivyokuja kumjua Yesu Kristo. Ni kitu gani unachoweza kufanya ili kuwasaidia watoto kujifunza kumhusu na kumfuata Yeye?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wazungumze kuhusu rafiki wa karibu wanayemjua na kuelezea jinsi gani mtu huyu amekuja kuwa rafiki. Soma na jadili Yohana 5:39 na Yohana 14:15 ili kupata njia tunazoweza kuhisi tu karibu na Yesu. Waombe watoto waelezee nyakati wao walipohisi kuwa wapo karibu Naye.

  • Wapeleke watoto matembezini kuzunguka jumba la mikutano. Waalike watoto kunyoosha mikono yao watakapoona kitu fulani kwenye matembezi kinachowakumbusha juu ya njia ya wanayoweza kumfuata Mwokozi (kama vile kisima cha ubatizo au picha).

  • Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu kumfuata Yesu Kristo, kama vile “Come, Follow Me” (Nyimbo,, na. 116). Waalike watoto washiriki nyakati wao walipofuata mfano wa Mwokozi.

Ninaweza kujifunza maandiko kwa ajili yangu mwenyewe.

Unaposoma maandiko na watoto na kuwauliza maswali, unaweza kujenga kujiamini kwao kwamba wanaweza kujifunza kutoka katika maandiko na kupata hazina ya maarifa yenye thamani.

Shughuli Yamkini

  • Someni kwa pamoja Yohana 5:39 na Matendo ya Mitume 17:10–11, na waulize watoto ni kitu gani wameelewa kuhusu jinsi ya kujifunza maandiko.

  • Chagua maandiko rahisi machache, yenye nguvu kutoka katika Agano Jipya, andika kila moja kwenye kipande cha karatasi, na uzifiche karatasi hizo. Tengeneza vidokezo vitakavyowaongoza watoto kwenye “kuwinda hazina” ndani ya darasa au jengo la kanisa ili kupata maandiko haya. Baada ya kupata kila andiko, jadili kile andiko linamaanisha na kwa nini ni hazina hasa.

  • Shiriki maandiko machache unayothamini na kuelezea kwa nini yana maana kwako. Kama darasa, wekeni orodha ya maandiko yenye thamani ambayo watoto wamepata katika Agano Jipya mwaka huu—nyumbani au wakati wa Msingi.

  • Kuwa na majadiliano na watoto kuhusu kwa nini wakati mwingine ni vigumu kusoma maandiko. Waombe watoto washiriki ushauri kwa kila mmoja kuhusu kujifunza maandiko. Waombe watoto waelezee uzoefu wowote mzuri waliopata kutokana na maandiko.

  • Wasaidie watoto kutengeneza kalenda rahisi ambazo wanaweza kutumia kuweka alama ya mara ngapi wamesoma maandiko. Kalenda hizi zinaweza kuwakumbusha kusoma maandiko kila siku.

Ninahitaji ushuhuda wangu mwenyewe.

Watoto unaowafundisha watahitaji shuhuda zao wenyewe juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Ni kitu gani unachoweza kufanya ili kuwahamasisha kujifunza ukweli wao wenyewe?

Shughuli Yamkini

  • Simulia hadithi ya wale wanawali kumi (ona Mathayo 25:1–13; ona pia “Mlango wa 47: Wanawali Kumi,” katika Hadithi za Agano Jipya, 118–20, au video inayofanana nayo kwenye ChurchofJesusChrist.org). Waulize watoto maswali kama haya: Je, ni kwa jinsi gani shuhuda zetu ni kama taa? Kwa nini ni muhimu kuwa na shuhuda zetu wenyewe?

  • Jadili tunaweza kufanya nini ili kuimarisha shuhuda zetu. Kwa ajili mawazo, waalike watoto kupekua Yohana 7:17 na Moroni 10:3–5. Waalike wao washiriki mambo wanayojua kuwa ni ya kweli.

  • Waombe watoto kukusaidia kubandika lebo katika matofali ya kujengea zenye kweli ambazo zinatengeneza shuhuda zetu (ona Mada za Injili, “Ushuhuda,” topics.ChurchofJesusChrist.org). Acha watoto watumie matofali hayo ili kujenga jengo linalowakilisha ushuhuda.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Je, unawezaje kuwahimiza watoto na wazazi wao kujifunza kutoka katika Agano Jipya nyumbani? Kwa mfano, unaweza kuwaalika watoto kukariri mojawapo ya maandiko mliyojadili katika darasa (inaweza kusaidia kugawanya maandiko katika virai vifupi) na kushiriki mstari hiyo na familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Badilisha shughuli kulingana na umri na uwezo wa watoto unaowafundisha. Watoto wadogo wanahitaji maelezo ya kina na wanajifunza kutoka mbinu mbalimbali za kufundisha. Watoto wanapokomaa, wanaweza kuchangia zaidi na kuwa mahiri katika kuelezea mawazo yao. Wape fursa za kuelezea, kushuhudia, na kushiriki. Toa msaada unapohitajika (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25–26.)

Chapisha