Agano Jipya 2023
Januari 2–8. Mathayo 1; Luka 1: “Na Iwe Kwangu kama Ulivyosema”


“Januari 2–8. Mathayo 1: Luka 1: ‘Na Iwe Kwangu kama Ulivyosema ’’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Januari 2–8. Mathayo 1: Luka 1 “ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Mariamu na Elisabeti

Januari 2–8

Mathayo 1; Luka 1

“Na Iwe Kwangu kama Ulivyosema”

Anza kwa kusoma Mathayo 1 na Luka 1. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa sura hizi, na muhtasari huu unaweza kukupa mawazo ya kufundisha. Kama utahitaji msaada wa ziada kuwafundisha watoto wadogo, ona “Kukidhi Mahitaji ya Watoto Wadogo” mwanzoni mwa nyenzo hii.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waombe watoto kukaa katika duara, na kisha muulize mtoto mmoja kushiriki kitu alichojifunza kutoka katika maandiko hivi karibuni. Mtoto huyo anaweza kubingirisha mpira au kumuonyesha kidole mtoto mwingine katika duara, ambaye atachukua zamu ya kushiriki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mathayo 1:18–25; Luka 1:26–38

Malaika walitangaza kuzaliwa kwa Yesu.

Mariamu na Yusufu walitembelewa kila mmoja na malaika aliyetangaza kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Matukio haya yanaweza kuwasaidia watoto kuona jinsi kuzaliwa kwa Kristo kulivyokuwa muhimu.

Shughuli Yamkini

Picha
Gabrieli akimtokea Mariamu

Upashaji Habari,, na John Scott

Luka 1:5–25, 57–63

Baba wa Mbinguni hujibu sala zangu.

Zakaria na Elisabeti pengine walikuwa wakiomba kupata mtoto kwa miaka mingi. Hatimaye Baba wa Mbinguni alijibu sala zao kwa kuwapatia mtoto wa kiume, Yohana Mbatizaji. Unawezaje kutumia hadithi hii kuwafundisha watoto kwamba Baba wa Mbinguni hujibu sala?

Shughuli Yamkini

  • Kwa maneno yako mwenyewe, simulia hadithi kutoka Luka 1:5–25, 57–63. Unaweza kutaka kurudia hadithi hii mara kadhaa. Wapange watoto kucheza nafasi za Zakaria, Elisabeti, na malaika na waigize hadithi hiyo. Sisitiza maneno ya malaika kwa Zakaria: “Maombi yako yamesikilizwa” (Luka 1:13). Shiriki uzoefu ambapo Baba wa Mbinguni alijibu sala zako.

  • Tumia “We Bow Our Heads” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 25) au wimbo mwingine kuwafundisha watoto jinsi ya kusali. Kila wakati watoto wanapoimba maneno “sali” au “sala,” waalike wao kuinamisha vichwa vyao na kukunja mikono yao.

  • Muombe kila mtoto afanye vitendo vinavyowakilisha kitu ambacho anaweza kukisalia. Waache watoto wengine wabahatishe vitendo vinawakilisha nini. Wanaweza kupata mawazo kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki hii.

Luka 1:30–35

Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.

Yesu Kristo ni Mwana wa Baba wa Mbinguni na Mariamu. Ni kitu gani unaweza kufanya ili kuwasaidia watoto kujifunza zaidi kumhusu Yeye?

Shughuli Yamkini

  • Waambie watoto kwamba malaika alimwambia Mariamu kwamba mtoto wake angeitwa Mwana wa Mungu (ona Luka 1:35). Wasaidie watoto kurudia msemo “Yesu ni Mwana wa Mungu.” Wasaidie watoto kuelewa wazazi wa Yesu ni nani kwa kuwaalika kuchora picha za wazazi wao wenyewe. Wanapofanya hivyo, waambie kwamba Yesu alikuwa na wazazi pia—Mariamu na Baba wa Mbinguni. Zaidi ya hayo, Yusufu aliombwa kumlinda na kumtunza Yesu wakati anaishi hapa duniani.

  • Toa ushuhuda wako kwamba kwa sababu Yesu alikuwa Mwana wa Mungu, Angeweza kufa kwa ajili ya dhambi zetu na kurudi kuishi tena. Onyesha picha za Kusulibiwa na Ufufuko wa Yesu (ona Kitabu cha Sanaa za Injili,, na. 57, 59).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mathayo 1:18–25; Luka 1:5–37

Kwa Mungu hakuna kitu kisichowezekana.

Kuzaliwa kwa Yesu na Yohana Mbatizaji kuliwezekana tu kupitia nguvu za Mungu. Kujifunza kuhusu miujiza hii kunaweza kuimarisha imani ya watoto kwamba Mungu ana uwezo wa kufanya miujiza katika maisha yao.

Shughuli Yamkini

  • Wewe na watoto mnaporejelea Mathayo 1:18–25 na Luka 1:5–37, waulize watoto maswali kama “Ungesemaje kama wewe ungekuwa Mariamu?” au “Ungejisikiaje kama wewe ungekuwa Zakaria?”

  • Katika maneno rahisi, simulia hadithi zilizoelezewa katika Mathayo 1:18–25 na Luka 1:5–37. Waombe watoto wainue mikono yao wanaposikia kitu ambacho kinaonekana hakiwezekani bila nguvu za Mungu. Ni hadithi zipi zingine watoto wanaweza kushiriki ambazo Mungu alifanya kitu kilichoonekana kuwa haiwezekani?

  • Wasaidie watoto kukariri Luka 1:37. Ili kufanya hivyo, unaweza kuandika aya kwenye ubao na kuwaalika watoto kuisoma mara kadhaa. Baada ya kila wakati, futa neno moja moja.

Mathayo 1:21–25; Luka 1:30–35, 46–47

Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.

Yesu Kristo ni Mwana wa Baba wa Mbinguni na Mariamu. Unawezaje kuwasaidia watoto kujifunza ukweli huu?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wasome Luka 1:30–35, wakitafuta majibu ya maswali haya: “Ni nani mama wa Yesu?” na “Ni nani Baba wa Yesu?” Wasaidie kuelewa kuwa Yesu Kristo ni mtu peke ambaye alikuwa na mama mwenye mwili wenye kufa, Mariamu na Baba aliye na mwili usiokufa, Baba wa Mbinguni (ona pia 1Nefi 11:18–21).

  • Unaposoma aya hizi, waalike watoto kutafuta majina au vyeo vya Yesu Kristo. Majina haya yanamaanisha nini, na yanatufundisha nini kuhusu Yesu?

  • Toa ushuhuda wako juu ya Yesu Kristo, na waalike watoto kutoa shuhuda zao pia.

Luka 1:5–25, 57–66

Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala zangu.

Mungu hujibu sala lakini si daima katika njia ambazo tunatarajia. Unawezaje kutumia hadithi hii ya Zakaria na Elisabeti ili kuwafundisha watoto ukweli huu?

Shughuli Yamkini

  • Waulize watoto kile wanachoweza kumwambia mtu aliyeomba baraka lakini bado hajapokea. Waalike kufikiria juu ya swali hili wanaposoma pamoja Luka 1:5–25, 57–66. (Ona pia “Mlango wa 1: Elisabeti na Zakaria” na “Mlango wa 3: Yohana Mbatizaji Anazaliwa,” katika Hadithi za Agano Jipya, 6–7, 10–11, au video zinazofanana nayo kwenye ChurchofJesusChrist.org.) Je, Zakaria na Elisabeti wangemwambia nini mtu aliyedhani sala zao hazijibiwi?

  • Waalike watoto kadhaa kabla ya wakati kushiriki uzoefu wao wakati Baba wa Mbinguni alipojibu sala zao. Shiriki wakati ulipohisi kwamba sala zako zilijibiwa kwa njia isiyotarajiwa.

  • Waalike watoto wachore picha ya wakati ambapo Baba wa Mbinguni alijibu maombi–hasa yao wenyewe. Waache washiriki michoro yao na darasa.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kushiriki na familia zao picha yo yote waliyochora wakati wa darasa. Watie moyo wawaulize wanafamilia wao kuhusu nyakati ambapo Mungu alijibu maombi yao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto wadogo wajifunze kutoka kwenye maandiko. Ili kuwasaidia watoto wadogo kujifunza kutoka kwenye maandiko, tilia mkazo mstari mmoja wa maandiko au hata maneno muhimu tu. Unaweza kuwaalika watoto kusimama au kuinua mikono yao wakati wanaposikia neno hilo au kirai hicho. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi21.)

Chapisha