Agano Jipya 2023
Januari 2–8. Mathayo 1; Luka 1: “Na Iwe Kwangu kama Ulivyosema”


“Januari 2–8. Mathayo 1; Luka 1: ‘Na Iwe Kwangu kama Ulivyosema’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Januari 2–8. Mathayo 1; Luka 1,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023

Picha
Mariamu na Elisabeti

Januari 2–8

Mathayo 1; Luka 1

“Na Iwe Kwangu kama Ulivyosema”

Unaposoma na kutafakari Mathayo 1 na Luka 1, andika misukumo ya kiroho unayopokea. Je, ni kweli gani za kimafundisho ya injili unazozipata? Je, ni ujumbe gani utakuwa wa thamani kubwa kwako na kwa familia yako? Mawazo ya kujifunza katika muhtasari huu yanaweza kukusaidia kugundua umaizi wa ziada.

Andika Misukumo Yako

Kutokana na mtazamo wa maisha ya kidunia, ilikuwa haiwezekani. Bikira hangeweza kupata mimba—wala kwa mwanamke tasa ambaye alipita sana umri wa miaka ya kuzaa mtoto. Lakini Mungu alikuwa na mpango wa kuzaliwa kwa Mwanawe na kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji, hivyo wote wawili Mariamu na Elisabeti, kinyume na uwezekano wote wa kidunia, wakawa mama. Inaweza kusaidia kukumbuka matukio yao ya kimuujiza pale tunapokabiliwa na jambo linaloonekana kutowezekana. Je, sisi tunaweza kuushinda udhaifu wetu? Je, tunaweza kugusa moyo wa mwana familia asiye na mwitikio? Gabrieli kwa urahisi angeweza kuwa anaongea nasi wakati alipomkumbusha Mariamu, “Kwa Mungu hakuna lisilowezekana” (Luka 1:37). Na jibu la Mariamu linaweza kuwa letu wakati Mungu anapofunua mapenzi Yake: “Na Iwe kwangu kama ulivyosema” (Luka 1:38).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Je, Mathayo na Luka walikuwa akina nani?

Mathayo alikuwa mtoza ushuru wa Kiyahudi, au mkusanya kodi, ambaye Yesu alimwita kama mmoja wa Mitume Wake (ona Mathayo 10:3; ona pia Kamusi ya Biblia, “Watoza ushuru”). Mathayo aliandika injili yake hasa kwa Wayahudi wenzake; kwa hivyo, alichagua kusisitiza unabii wa Agano la Kale kuhusu Masiya ambao ulitimizwa kupitia maisha na huduma ya Yesu.

Luka alikuwa Myunani (si-Myahudi) tabibu aliyesafiri pamoja na Mtume Paulo. Aliandika injili yake baada ya kifo cha Mwokozi hasa kwa hadhira isiyokuwa ya Wayahudi. Alishuhudia juu ya Yesu Kristo kama Mwokozi wa wote Wayunani na Wayahudi. Aliandika maelezo ya matukio yaliyoshuhudiwa kwa macho katika maisha ya Mwokozi, na alijumuisha hadithi zaidi zilizohusu wanawake ikilinganishwa na injili zingine.

Ona pia Kamusi ya Biblia, “Injili,” “Mathayo,” “Luka.”

Mathayo 1:18–25; Luka 1:26–35

Yesu Kristo alizaliwa na mama mwenye mwili unaokufa na Baba mwenye mwili usiokufa.

Katika Mathayo 1:18–25 na Luka 1:26–35, tazama jinsi Mathayo na Luka walivyouelezea muujiza wa kuzaliwa kwa Yesu. Je, ni kwa jinsi gani maelezo yao yanaimarisha imani yako katika Mwokozi? Kwa nini ni muhimu kwako kujua kwamba Yesu alikuwa vyote Mwana wa Mungu na mwana wa Mariamu?

Rais Russell M. Nelson alielezea kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo “ulihitaji dhabihu ya pekee kwa kiumbe asiyekufa ambaye hayuko chini ya mauti. Tena Yeye alilazimika kufa na kuchukua tena mwili Wake. Mwokozi alikuwa ni mtu pekee ambaye angeweza kutimiza hili. Kutoka kwa mama yake alirithi uwezo wa kufa. Kutoka kwa Baba yake Yeye alipata uwezo juu ya kifo” (“Constancy amid Change,” Ensign, Nov. 1993, 34).

Luka 1:5–25, 57–80

Baraka za Mungu huja kwa wakati Wake mwenyewe.

Kama ukijikuta unasubiri baraka, au kama inaonekana kwamba Mungu hasikii maombi yako, hadithi ya Elisabeti na Zakaria yaweza kuwa ukumbusho kwamba Mungu hajakusahau. Kama Mzee Jeffrey R. Holland alivyoahidi: “Wakati tukifanya kazi na kusubiri kwa pamoja majibu kwa baadhi ya maombi yetu, ninawapeni ninyi ahadi yangu ya kitume kwamba yamesikika na yanajibiwa, ingawa pengine sio kwa wakati ule, au katika njia tuliyotaka sisi. Lakini daima yanajibiwa katika wakati na katika njia ya mzazi mjua yote na mwenye huruma anavyopaswa kuyajibu” (“Kumsubiria Bwana,” Liahona, Nov. 2020, 115–16). Je, ni kwa jinsi gani Zakaria na Elisabeti walibaki waaminifu? (ona Luka 1:5–25, 57–80). Je, unajikuta katika hali ya kusubiria baraka? Je, unahisi Bwana anatarajia nini kutoka kwako wakati ukisubiri?

Picha
Elisabeti na Zakaria pamoja na mtoto Yohana.

Baada ya kusubiri kwa uaminifu, Elisabeti na Zakaria walibarikiwa kuwa na mtoto wa kiume.

Mathayo 1:18–25; Luka 1:26–38

Walio waaminifu kwa hiari hujiweka chini ya mapenzi ya Mungu.

Kama Mariamu, wakati mwingine tunakuta kwamba mipango ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu ni tofauti na kile tulichopanga. Je, unajifunza nini kutoka kwa Mariamu kuhusu kukubali mapenzi ya Mungu? Katika majedwali yafuatayo, andika kauli kutoka kwa malaika na kwa Mariamu (ona Luka 1:26–38), sambamba na ujumbe unaoupata katika kauli zao:

Maneno ya malaika kwa Mariamu

Ujumbe kwa ajili yangu

Maneno ya malaika kwa Mariamu

“Bwana yu pamoja nawe” (mstari wa 28).

Ujumbe kwa ajili yangu

Bwana anajua hali na masumbuko yangu.

Maneno ya malaika kwa Mariamu

Ujumbe kwa ajili yangu

Maneno ya malaika kwa Mariamu

Ujumbe kwa ajili yangu

Majibu ya Mariamu

Ujumbe kwa ajili yangu

Majibu ya Mariamu

“Litakuwaje neno hili?” (mstari wa 34).

Ujumbe kwa ajili yangu

Ni SAWA kuuliza maswali ili kuelewa vyema mapenzi ya Mungu.

Majibu ya Mariamu

Ujumbe kwa ajili yangu

Majibu ya Mariamu

Ujumbe kwa ajili yangu

Unaposoma kuhusu mfano wa uadilifu wa Yusufu katika Mathayo1:18–25, unajifunza nini kuhusu kukubali mapenzi ya Mungu? Je, ni umaizi gani wa ziada unaojifunza kutoka katika uzoefu wa Zakaria na Elizabeti? (ona Luka1).

Ona pia Luka 22:42; Kamusi ya Biblia, “Gabrieli.”

Luka 1:46–55

Mariamu alishuhudia kuhusu huduma ya Yesu Kristo.

Maneno ya Mariamu katika Luka 1:46–55 yalitabiri vipengele vya huduma ya Mwokozi. Je, unajifunza nini kuhusu Yesu Kristo kutokana na maelezo ya Mariamu? Ungeweza kulinganisha mistari hii na maneno ya Hana katika 1 Samueli 2:1–10 na Mahubiri ya Mlimani ya Yesu katika Mathayo 5:3–12. Je, Roho anakufundisha nini unapotafakari mistari hii?

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mathayo 1:1–17.Familia yako inaposoma nasaba ya Yesu, mnaweza kujadili historia ya familia yako mwenyewe na kushiriki baadhi ya hadithi kuhusu mababu zenu. Je, ni kwa namna gani kujua kuhusu historia ya familia yako huibariki familia yako? Kwa shughuli zaidi za historia ya familia, ona FamilySearch.org/discovery.

Mathayo 1:20; Luka 1:11–13, 30Je, ni kwa nini watu katika mistari hii wamekuwa wenye woga? Je, ni kitu gani hutusababisha kusikia woga? Je, ni kwa namna gani Mungu ametualika sisi “tusiogope”?

Luka 1:37.Ili kuisaidia familia yako kujenga imani kwamba “kwa Mungu hakuna lisilowezekana,” mngeweza kupekua Luka 1 pamoja na kutafuta mambo ambayo Mungu aliyafanya ambayo yangeweza kufikiriwa kama yasiyowezekana. Je, ni hadithi gani zingine tunazoweza kushiriki—kutoka kwenye maandiko au maisha yetu wenyewe—ambapo Mungu alifanya mambo yaliyoonekana kutowezekana? Kupekua katika Kitabu cha Sanaa ya Injili kunaweza kutoa mawazo fulani.)

Luka 1:46–55.Ni yapi baadhi ya “mambo makuu” ambayo Mwokozi ametutendea? Je ingeweza kumaanisha nini kwa nafsi zetu “kumtukuza Bwana”?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa “He Sent His Son,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fanyia kazi maandiko katika maisha Yako. Baada ya kusoma kifungu hiki cha maandiko, waalike wanafamilia kukifanyia kazi katika maisha yao (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi21). Kwa mfano, ni kwa jinsi gani wanafamilia wanaweza kukifanyia kazi kile wanachojifunza kutoka katika Mathayo 1 na Luka 1 kuhusu kujibu wito wa Bwana?

Picha
Gabrieli akimtokea Mariamu

Umebarikiwa Wewe kati ya Wanawake, na Walter Rane

Chapisha