Agano Jipya 2023
Januari 23–29. Mathayo 3; Marko 1; Luka 3: “Itengenezeni Njia ya Bwana”


“Januari 23–29. Mathayo 3; Marko 1; Luka 3: ‘Itengenezeni Njia ya Bwana’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Januari 23–29. Mathayo 3; Marko1; Luka 3,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
Yohana Mbatizaji Anambatiza Yesu

Dirisha-lenye kioo kilichotiwa rangi katika Hekalu la Illinois, na Tom Holdman

Januari 23–29

Mathayo 3; Marko 1; Luka 3

“Itengenezeni njia ya Bwana”

Anza kwa kusoma Mathayo 3; Marko 1; na Luka 3. Unapoomba ili Roho Mtakatifu akuongoze kuelewa sura hizi, Yeye atakupa umaizi ambao ni mahususi kwa ajili yako. Andika misukumo hii, na weka mipango ya kuifanyia kazi.

Andika Misukumo Yako

Yesu Kristo na injili Yake inaweza kukubadilisha. Luka alinukuu unabii wa kale wa Isaya ambao ulielezea matokeo ambayo ujio wa Mwokozi ungeleta “Kila bonde litajazwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, na palipoparuza patalainishwa” (Luka 3:5; ona pia Isaya 40:4). Huu ni ujumbe kwetu sote, ikijumuisha wale wanaofikiria kuwa hawawezi kubadilika. Kama kitu cha kudumu kama mlima kinaweza kushushwa, basi hakika Bwana anaweza kutusaidia kunyoosha njia zetu zilizopotoka (ona Luka 3:4–5). Tunapokubali mwaliko wa Yohana Mbatizaji wa kutubu na kubadilika, tunaandaa akili na mioyo yetu kumpokea Yesu Kristo ili kwamba nasi pia tuweze “kuona wokovu wa Mungu”(Luka 3:6).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Marko alikuwa nani?

Miongoni mwa waandishi wa Injili, tunajua kidogo tu kuhusu Marko. Tunajua kwamba alikuwa mmisionari mwenza wa Paulo, Petro, na wamisionari wengine kadhaa. Wasomi wengi wa biblia huamini kwamba Petro alimuelekeza Marko kuandika matukio ya maisha ya Mwokozi. Injili ya Marko yawezekana iliandikwa kabla ya hizi zingine tatu.

Ona pia Kamusi ya Biblia, “Marko.”

Mathayo 3:1–12; Marko 1:1–8; Luka 3:2–18

Toba ni badiliko kuu la akili na moyo.

Misheni ya Yohana Mbatizaji ilikuwa ni kuandaa mioyo ya watu ili kumpokea Mwokozi na kuwa zaidi kama Yeye. Alilifanyaje hili? Alitangaza, “Tubuni” (Mathayo 3:2). Alitumia mifano kama vile tunda na ngano kufundisha kuhusu toba (ona Luka 3:9,17).

Je, ni mifano gani mingine unayoipata katika maelezo ya huduma ya Yohana Mbatizaji? (ona Mathayo 3:1–12; Marko 1:1–8; Luka 3:2–18). Fikiria kuiwekea alama katika maandiko yako au kuchora michoro yake. Je, mifano hii inafundisha nini kuhusu mafundisho na umuhimu wa toba?

Toba ya kweli ni “badiliko la akili, mtazamo mpya kuhusu Mungu, kuhusu mtu wenyewe, na kuhusu ulimwengu. … [Humaanisha] badiliko la moyo na mapenzi kwa Mungu” (Kamusi ya Biblia, “Toba”). Katika Luka 3:7–14, ni mabadiliko gani Yohana aliwaalika watu kufanya ili kujiandaa kumpokea Kristo? Je, ni kwa jinsi gani ushauri huu unaweza kutumika kwako? Je, ni kwa namna gani wewe unaweza kuonyesha kwamba umetubu kweli? (ona Luka 3:8).

Ona pia Russell M. Nelson, “Tunaweza Kufanya Vyema na Kuwa Bora zaidi,” Liahona, Mei 2019, 67–69; Dallin H. Oaks, “Kutakaswa kwa Toba,” Liahona, Mei 2019, 91–94.

Mathayo 3:7; Luka 3:7

Mafarisayo na Masadukayo walikuwa akina nani?

Mafarisayo walikuwa waumini wa chama cha kidini ya Kiyahudi waliojiinua kwa kufuata kikamilifu sheria ya Musa na taratibu zake. Masadukayo walikuwa tabaka la Wayahudi matajiri wenye ushawishi wa kidini na wa kisiasa; hawakuamini katika mafundisho ya ufufuko. Makundi yote yalichepuka kutoka kwenye dhamira halisi ya sheria za Mungu.

Ona pia Mathayo 23:23–28; Kamusi ya Biblia, “Mafarisayo,” “Masadukayo.”

Mathayo 3:11, 13–17; Marko 1:9–11; Luka 3:15–16, 21–22

Yesu Kristo alibatizwa ili “kutimiza haki yote.”

Wakati wewe ulipobatizwa, ulifuata mfano wa Mwokozi. Linganisha kile unachojifunza kutoka kwenye hadithi hizi za ubatizo wa Mwokozi na kile kilichotokea wakati wa ubatizo wako.

Ubatizo wa Mwokozi

Ubatizo Wangu:

Ubatizo wa Mwokozi

Je, ni nani alimbatiza Yesu, na alikuwa na mamlaka gani?

Ubatizo Wangu:

Je, ni nani alikubatiza wewe, na alikuwa na mamlaka gani?

Ubatizo wa Mwokozi

Je, Yesu Kristo alibatiziwa wapi?

Ubatizo Wangu:

Je, wewe ulibatizwa wapi?

Ubatizo wa Mwokozi

Je, Yesu Kristo alibatizwaje?

Ubatizo Wangu:

Je ,wewe ulibatizwaje?

Ubatizo wa Mwokozi

Kwa nini Yesu alibatizwa?

Ubatizo Wangu:

Kwa nini wewe ulibatizwa?

Ubatizo wa Mwokozi

Je, ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni alionyesha kwamba Yeye alipendezwa na Yesu?

Ubatizo Wangu:

Je, ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni alionyesha kwamba alipendezwa wakati wewe ulipobatizwa? Je, ni kwa jinsi gani Yeye ameonyesha idhinisho Lake tangu wakati huo?

Ona pia 2 Nefi 31; Mosia 18:8–11; Mafundisho na Maagano 20:37, 68–74; “The Baptism of Jesus” (video), ChurchofJesusChrist.org.

Mathayo 3:16–17; Marko 1:9–11; Luka 3:21–22

Washiriki wa Uungu ni viumbe watatu tofauti.

Biblia ina ushahidi mwingi kwamba washiriki wa Uungu ni viumbe watatu tofauti. Hadithi za ubatizo wa Mwokozi ni mfano mmoja. Unaposoma hadithi hizi, tafakari kile ambacho unaweza kujifunza kuhusu uungu. Kwa nini mafundisho haya ni muhimu kwako?

Ona pia Mwanzo 1:26; Mathayo 17:1–5; Yohana 17:1–3; Matendo 7:55–56; Mafundisho na Maagano 130:22.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mathayo 3.Yohana Mbatizaji alikuwa na Ukuhani wa Haruni. Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Yohana kuhusu madhumuni ya Ukuhani wa Haruni? Ni baraka gani tunazipokea kwa sababu ya Ukuhani wa Haruni? Kama una mvulana katika familia yako, unaweza kumpatia msaada wa kuelewa jinsi anavyoweza kutumia Ukuhani wa Haruni kuwabariki wengine. (Ona pia Mafundisho na Maagano 13:1; 20:46–60.)

Picha
kijana akimbatiza kijana mwenzake.

Tunapobatizwa, dhambi zetu zinaoshwa kabisa.

Mathayo 3:11–17; Marko 1:9–11; Luka 3:21–22.Je, wanafamilia yako wameshamuona mtu akibatizwa au kuthibitishwa kuwa muumini wa Kanisa? Wanafamilia walijisikiaje? Pengine ungeweza kuwafundisha kuhusu ubatizo na uthibitisho ni ishara za nini. Ni kwa jinsi gani kubatizwa na kuthibitishwa ni kama kuzaliwa upya? Kwa nini tunazamishwa kabisa ndani ya maji wakati tunapobatizwa? Kwa nini tunavalia mavazi meupe wakati tunapobatizwa? Kwa nini kipawa cha Roho Mtakatifu huelezewa kama “ubatizo wa moto”? (Mafundisho na Maagano 20:41; ona pia Kamusi ya Biblia, “Ubatizo,” “Roho Mtakatifu”).

Mathayo 3:17; Marko 1:11; Luka 3:22.Je, ni wakati gani tumehisi kwamba Mungu amependezwa nasi? Tunaweza kufanya nini kama familia ili kumpendeza Mungu?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Baptism,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 100–101.

Kuboresha Kujifunza binafsi.

Muombe Bwana msaada. Maandiko yalitolewa kwa ufunuo, na ili kuyaelewa vyema tunahitaji ufunuo binafsi. Bwana ameahidi “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa” (Mathayo 7:7).

Picha
Yohana akimbatiza Yesu

Yohana Mbatizaji Akimbatiza Yesu, na Greg K. Olsen.

Chapisha