Agano Jipya 2023
Januari 30–Februari 5. Mathayo 4; Luka 4–5: “Roho wa Bwana Yu juu Yangu”


“Januari 30–Februari 5. Mathayo 4; Luka 4–5: ‘Roho wa Bwana Yu juu Yangu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Januari 30–Februari 5. Mathayo 4; Luka 4–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
Yesu akiwa amesimama nyikani

Nyikani, na Eva Koleva Timothy

Januari 30–Februari 5

Mathayo 4; Luka 4–5

“Roho wa Bwana Yu juu Yangu”

Mwokozi alitumia maandiko kukinza vyote majaribu ya Shetani na kushuhudia juu ya utakatifu wa misheni Yake mwenyewe (ona Luka 4:1–21). Tafakari jinsi maandiko yanavyoweza kujenga imani na dhamira yako ya kupinga majaribu.

Andika Misukumo Yako

Toka ujana Wake, Yesu alionekana kujua kwamba Alikuwa na huduma ya kipekee, takatifu. Lakini Yesu alipokuwa akijiandaa kwa huduma Yake ya duniani, adui alitafuta kupanda shaka katika akili ya Mwokozi. “Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu,” Shetani alisema (Luka 4:3, italiki zimeongezwa). Lakini Mwokozi alikuwa na ushirika na Baba Yake wa Mbinguni. Alijua maandiko, na alijua Yeye alikuwa nani. Kwake Yeye, toleo la Shetani—“Nitakupa wewe enzi hii yote” (Luka 4:6)—lilikuwa la uongo, kwani maandalizi ya maisha yote ya Mwokozi yalimruhusu Yeye kupokea “nguvu za Roho” (Luka 4:14). Hivyo licha ya majaribu, taabu, na kukataliwa, Yesu Kristo kamwe hakutetereka kutoka kwenye kazi Yake teule: “Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu … maana kwa sababu hiyo Nalitumwa” (Luka 4:43).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mathayo 4:1–2

Kuwa na ushirika na Mungu huniandaa mimi kumtumikia Yeye.

Ili kujiandaa kwa huduma Yake, Yesu alienda nyikani “ili kuwa na Mungu” (Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 4:1 [katika Mathayo 4:1, tanbihi b]). Fikiria juu ya nini unafanya ili uhisi kuwa karibu na Mungu. Je, ni kwa jinsi gani hii hukuandaa wewe kwa kazi ambayo Yeye anataka ufanye?

Mathayo 4:1–11; Luka 4:1–13

Yesu Kristo aliweka mfano kwa ajili yangu kwa kushinda majaribu.

Wakati mwingine watu hujiona kuwa wenye hatia wakati wanapojaribiwa kufanya dhambi. Lakini hata Mwokozi, aliyeishi “bila kufanya dhambi” (Waebrania 4:15), alijaribiwa. Yesu Kristo anajua majaribu tunayoyapata na anaweza kutusaidia kuyashinda (ona Waebrania 2:18; Alma 7:11–12).

Unaposoma Mathayo 4:1–11 na Luka 4:1–13, unajifunza nini kinachoweza kukusaidia unapokabiliwa na majaribu? Unaweza kupangilia mawazo yako katika jedwali kama hili hapa:

Yesu Kristo

Mimi

Yesu Kristo

Je, Shetani alimjaribu Kristo afanye nini?

Mimi

Je, Shetani ananijaribu ili nifanye nini?

Yesu Kristo

Je, ni kwa jinsi gani Kristo alijiandaa ili ashinde majaribu?

Mimi

Je, ni kwa jinsi gani mimi ninajiandaa ili kushinda majaribu?

Yesu Kristo

Mimi

Je, ni umaizi gani wa ziada unaoupata kutoka katika Tafsiri ya Joseph Smith ya Mathayo 4? (ona tanbihi kote katika Mathayo 4).

Ona pia 1 Wakorintho 10:13; Alma 13:28; Musa 1:10–22; Mada za Injili, ““Majaribu,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

Luka 4:16–32

Yesu Kristo ndiye Masiya aliyetolewa unabii.

Kama ungeombwa kuelezea Yesu Kristo alitumwa duniani kufanya nini, je wewe ungesema nini? Kwa kunukuu mojawapo ya unabii wa Isaya kuhusu Masiya, Mwokozi alielezea vipengele vya huduma Yake (ona Luka 4:18–19; Isaya 61:1–2). Unajifunza nini kuhusu misheni Yake unaposoma mistari hii?

Ni kwa njia gani Mwokozi anakualika wewe kushiriki katika kazi Yake?

Picha
Yesu akiwa amesimama ndani ya sinagogi

Japokuwa Wayahudi walikuwa wakisubiri kwa karne nyingi unabii wa Isaya kutimia, wengi hawakukubali kwamba Yesu alikuwa ndiye Masiya wakati alipotangaza, “Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu” (Luka 4:21). Unaposoma Luka 4:20–30 (ona pia Marko 6:1–6), jaribu kujiweka katika nafasi ya watu wa Nazareti. Je, kuna kitu chochote ambacho kinaweza kukuzuia kumkubali kikamilifu Kristo kama Mwokozi wako binafsi?

Ona pia Mosia 3:5–12; “Jesus Declares He Is the Messiah” (video), ChurchofJesusChrist.org.

Mathayo 4:18–22; Luka 5:1–11

Ninapotumaini katika Bwana, Yeye anaweza kunisaidia kufikia uwezo wangu wa kiungu.

Rais Ezra Taft Benson alifundisha, “Wanaume na wanawake wanaompa Mungu maisha yao watagundua kwamba Yeye anaweza kufanya mengi zaidi kutoka katika maisha yao kuliko wao wanavyoweza” (Teachings of the Presidents of the Church: Ezra Taft Benson [2014], 42). Tazama jinsi hili lilivyowatokea Simoni Petro na wavuvi wenzake. Yesu aliona kitu kikuu ndani yao kuliko wao walivyojiona wenyewe. Yeye alitaka kuwafanya wao kuwa wavuvi wa watu (Mathayo 4:19; ona pia Luka 5:1–11).

Unaposoma Mathayo 4:18–22 na Luka 5:1–11, tafakari vile ambavyo Yesu Kristo anakusaidia wewe uwe. Je, ni kwa jinsi gani umehisi Yeye akikuita umfuate? Je, ni kwa jinsi gani unaweza kumwonyesha Bwana kwamba uko tayari kuacha vitu vyote ili kumfuata Yeye? (ona Luka 5:11).

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mathayo 4:1–2; Luka 4:1–2.Je, ni umaizi gani tunaweza kuupata kutoka kwenye maelezo haya kuhusu nguvu ya kufunga? Ili kuisaidia familia yako kujifunza kuhusu kufunga, unaweza kutumia “Kufunga na Matoleo ya Mfungo” katika Mada za Injili (topics.ChurchofJesusChrist.org). Wanafamilia wangeweza kushiriki uzoefu ambao waliweza kuupata kwa kufunga. Pengine mngeweza kwa sala kupanga mipango ya kufunga pamoja kwa lengo mahususi.

Mathayo 4:3–4; Luka 4:3–4.Wakati Shetani alipomjaribu Kristo ili kubadili jiwe kuwa mkate, aliupa changamoto utambulisho mtakatifu wa Kristo kwa kusema “Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu” (Mathayo 4:3, italiki zimeongezwa). Kwa nini Shetani hujaribu kutufanya tutilie shaka utambulisho wetu mtakatifu—na wa Mwokozi? Je, ni kwa namna gani yeye anajaribu kufanya hivi? (Ona pia Musa 1:10–23.)

Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 4:11.Baada ya Yesu kujaribiwa kimwili na kiroho, mawazo Yake yaligeukia mahitaji ya Yohana Mbatizaji, ambaye alikuwa gerezani: “Na sasa Yesu alijua kwamba Yohana alikuwa amefungwa gerezani, na aliwatuma malaika, na, tazama, walikuja na kumtumikia [Yohana]” (Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 4:11 [katika Mathayo 4:11, tanbihi a). Ni kwa jinsi gani tunabarikiwa tunapofuata mfano wa Kristo wa kuwafikiria wengine?

Luka 4:16–21.Je, tunamjua mtu yeyote ambaye amevunjika moyo au anahitaji “kuwekwa huru”? (Luka 4:18). Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wengine kupokea uponyaji na ukombozi wa Mwokozi? Mnaweza pia kujadili jinsi ambavyo kufanya ibada za hekaluni husaidia kuleta “uhuru kwa waliosetwa” (Luka 4:18).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa“Come, Follow Me,” Nyimbo za Kanisa, na. 116

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ishi Injili ya Yesu Kristo. “Pengine kitu cha muhimu zaidi unachoweza kufanya [kama mzazi au mwalimu] ni … kuishi injili kwa moyo wako wote. … Hii ni njia kuu ya kustahili kuambatana na Roho Mtakatifu. Hauhitaji kuwa mkamilifu, jaribu tu kwa bidii—na kutafuta msamaha kupitia Upatanisho wa Mwokozi wakati wowote unapojikwaa” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi13).

Picha
Yesu anawaita Mitume kuwa wavuvi wa watu

Yesu Anawaita Mitume Yakobo na Yohana, Edward Armitage (1817–96)/Sheffield Galleries and Museums Trust, UK/© Museums Sheffield/The Bridgeman Art Library International

Chapisha