Agano Jipya 2023
Februari 20–26. Mathayo 6–7: “Aliwafundisha kama Mtu Mwenye Amri”


“Februari 20–26. Mathayo 6–7: ‘Aliwafundisha kama Mtu Mwenye Amri’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Februari 20–26. Mathayo 6–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
Yesu Akifundisha kando ya ufukwe wa bahari

Yesu Akifundisha Watu Pwani, na James Tissot

Februari 20–26

Mathayo 6–7

“Aliwafundisha kama Mtu Mwenye Amri”

Tunaposoma maandiko tukiwa na swali akilini na nia ya dhati kuelewa kile ambacho Baba wa Mbinguni anatutaka tujue, tunamualika Roho Mtakatifu ili atupe mwongozo. Unaposoma Mathayo 6–7, zingatia misukumo hii.

Andika Misukumo Yako

Mahubiri ya Mlimani ni mojawapo ya mahubiri yanayojulikana vizuri zaidi katika Ukristo. Mwokozi alifundisha kwa mifano mingi, kama vile mji juu ya kilima, maua ya mashamba, na mbwa mwitu waliojigeuza kondoo. Lakini Mahubiri ya Mlimani ni zaidi ya hotuba nzuri. Nguvu ya mafundisho ya Mwokozi kwa wafuasi Wake inaweza kubadilisha maisha yetu, hasa kama tunaishi kulingana na mafundisho hayo. Ndipo maneno Yake huwa zaidi ya maneno; yanakuwa msingi wa uhakika kwa maisha ambao, kama nyumba ya mtu mwenye busara, inaweza kuhimili pepo na mafuriko ya ulimwengu (ona Mathayo 7:24–25).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mathayo 6–7

Kufuata mfano wa Kristo kunaweza kunisaidia kuwa kama Yeye.

Mahubiri ya Mlimani yana kanuni nyingii za injili. Unapojifunza sura hizi, muulize Bwana kitu ambacho Yeye anataka ujifunze.

Kanuni moja ambayo ungeweza kuipata ni haja ya kuyapa kipaumbele mambo ya Mungu kuliko mambo ya ulimwengu. Ni yapi kati ya mafundisho ya Mwokozi katika Mathayo 6–7 hukusaidia kuzingatia kwenye mambo ya mbinguni? Je, ni mawazo au misukumo gani mingine uliyonayo? Je, unashawishika kufanya nini? Fikiria kuandika misukumo yako. Kwa mfano:

Mathayo 6:1–4

Nataka kujali zaidi kuhusu kile ambacho Mungu anafikiria juu yangu kuliko kile ambacho wengine wanafikiria.

Kanuni nyingine katika Mathayo 6–7 ni sala. Pata muda wa kutathmini maombi yako. Je, wewe unahisi unafanya vipi katika jitihada zako za kumkaribia Mungu kupitia sala? Je, ni mafundisho gani katika Mathayo 6–7 yanayokupa mwongozo wa kuboresha jinsi unavyosali? Andika misukumo unayopokea. Kwa mfano:

Mathayo 6:9

Ninaposali, nataka kulichukulia jina la Baba wa Mbinguni kwa staha.

Mathayo 6:10

Wakati ninaposali, ninapaswa kuelezea hamu yangu kwamba mapenzi ya Bwana yatimizwe.

Unaweza kufikiria kusoma Mahubiri ya Mlimani tena, ukitafuta kanuni au jumbe zingine zinazorudiwa ambazo zinatumika mahususi kwako. Andika katika shajara ya kujifunza kile unachopata, sambamba na fikra na misukumo yako.

Picha
familia ikisali

Tunaweza kusogea karibu zaidi na Mungu kupitia sala.

Mathayo 6:7

Je, inamaanisha nini “kupayuka-payuka” katika sala?

Watu mara nyingi huelewa kuwa “kupayuka- payuka” kunamaanisha kurudia maneno yale yale tena na tena. Hata hivyo, neno bure huweza kuelezea kitu ambacho hakina thamani. Kutumia “kupayuka-payuka” katika sala huweza kumaanisha kuomba bila hisia za dhati, za moyoni (ona Alma 31:12–23).

Mathayo 7:1–5

Ninaweza kuhukumu kwa haki.

Katika Mathayo 7:1, Mwokozi anaweza kuonekana kana kwamba anasema tusihukumu, lakini katika maandiko mengine (ikijumuisha mistari mingine katika sura hii), Anatupatia maelekezo kuhusu jinsi ya kuhukumu. Kama hiyo inaonekana kukanganya, Tafsiri ya Joseph Smith ya mstari huu inaweza kusaidia: “Msihukumu bila haki, msije mkahukumiwa; lakini hukumuni hukumu ya haki” (katika Mathayo 7:1, tanbihi a). Je, unapata nini katika Mathayo 7:1–5, pamoja na sura yote iliyosalia, ambacho kinakusaidia kujua jinsi ya “kuhukumu hukumu ya haki”?

Ona pia Mada za Injili, “Kuwahukumu Wengine,” topics.ChurchofJesusChrist.org; Lynn G. Robbins, “Mwamuzi wa Haki,” Liahona, Nov. 2016, 96–98.

Mathayo 7:21–23

Napata kumjua Yesu Kristo kwa kufanya mapenzi Yake.

Kirai “sikuwajua ninyi kamwe” Mathayo 7:23 kilibadilishwa katika Tafsiri ya Joseph Smith kuwa “Hamkunijua mimi kamwe” (Mathayo 7:23, tanbihi a). Je, ni kwa jinsi gani badiliko hili hukusaidia kuelewa vizuri zaidi kile ambacho Bwana alifundisha katika mstari wa 21–22 kuhusu kufanya mapenzi Yake? Je, unahisi unamjua Bwana vizuri kiasi gani? Je, unaweza kufanya nini ili kumjua vizuri zaidi?

Ona pia David A. Bednar, “Kama Mngalinijua Mimi,” Liahona, Nov. 2016, 102.

Mathayo 7:24–27

Kutii mafundisho ya Mwokozi hujenga msingi imara wa maisha yako.

Kuishi injili hakuondoi dhiki katika maisha yetu. Nyumba zote mbili katika fumbo la Mwokozi katika Mathayo 7:24–27 zilipatwa na dhoruba ile ile. Lakini nyumba moja iliweza kustahimili. Ni kwa jinsi gani kuishi mafundisho ya Mwokozi kumejenga msingi imara kwako? Unahisi kushawishika kufanya nini ili kuendelea kujenga “nyumba yako juu ya mwamba? (ona mstari wa 24).

Ona pia Helamani 5:12.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mathayo 6–7.Njia mojawapo ya kujifunza kutoka katika Mathayo 6–7 kama familia ni kuangalia video “Sermon on the Mount: The Lord’s Prayer” na “Sermon on the Mount: Treasures in Heaven” (ChurchofJesusChrist.org). Wanafamilia wanaweza kufuatilia kwenye maandiko yao na kusimamisha kwa muda video wanaposikia jambo wanalotaka kujadili. Shughuli hii inaweza kudumu kwa siku kadhaa, kama itahitajika.

Mathayo 6:5–13.Je, tunaweza kujifunza nini kuhusu sala kutokana na jinsi Mwokozi alivyosali? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia sala Yake kama mfano wa kuiga ili kuboresha sala zetu binafsi na za familia? (Ona pia Luka 11:1–13.) Kama una watoto wadogo, mnaweza kufanya mazoezi ya kusali pamoja.

Mathayo 6:33.Inamaanisha nini “kutafuta … kwanza ufalme wa Mungu”? Je, ni kwa jinsi gani tunafanya hili kama mtu binafsi na kama familia?

Mathayo 7:1–5.Ili kupata taswira ya mafundisho katika mistari hii, familia yako inaweza kutafuta kibanzi (kipande kidogo cha mbao) na boriti (kipande kikubwa cha mbao). Je, kufananisha vitu hivi viwili kunatufundisha nini kuhusu kuwahukumu wengine? Kama ungependa kuchunguza mada hii zaidi, unaweza kutumia baadhi ya taarifa katika “Kuwahukumu Wengine” (Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org).

Mathayo 7:24–27.Ili kusaidia familia yako kuelewa vizuri zaidi fumbo la Mwokozi juu ya mtu mwenye busara na mtu mpumbavu, unaweza kuwafanya wamwage maji kwenye mchanga na kisha juu ya mwamba. Je, tunawezaje kujenga misingi yetu ya kiroho juu ya mwamba?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Imbeni pamoja “The Wise Man and the Foolish ManKitabu cha Nyimbo za Watoto, 281.

Kuboresha Kujifunza Binafsi.

Shiriki umaizi. Kujadili kanuni unazojifunza kutoka katika kujifunza kwako binafsi sio tu njia nzuri ya kuwafundisha wengine; husaidia pia kuimarisha uelewa wako wewe mwenyewe. Jaribu kuelezea kanuni uliyojifunza wiki hii na mwanafamilia au katika madarasa yako ya Kanisani.

Picha
Yesu akisali

Nimesali kwa Ajili Yenu, na Del Parson

Chapisha