Agano Jipya 2023
Februari 13–19. Mathayo 5; Luka 6: “Heri Ninyi”


“Februari 13–19. Mathayo 5; Luka 6: ‘Heri Ninyi’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Februari 13–19. Mathayo 5; Luka 6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023

Picha
Yesu akifundisha mlimani

Yesu Akihubiri Mahubiri ya Mlimani, na Gustave Doré

Februari 13–19

Mathayo 5; Luka 6

“Heri Ninyi ”

Kuwa makini kwa misukumo unayopokea unaposoma Mathayo 5 na Luka 6, na uiandike katika shajara ya kujifunza au katika njia nyingine. Muhtasari huu unaweza kukusaidia kutambua baadhi ya kanuni muhimu katika sura hizi, kuwa wazi kwa zingine unazozigundua katika kujifunza kwako mwenyewe.

Andika Misukumo Yako

Katika hatua hii katika huduma Yake, ilikuwa wazi kwamba mafundisho ya Yesu yangekuwa tofauti na kile ambacho watu wa wakati Wake walikuwa wamezoea kusikia. Masikini watapokea ufalme wa Mbinguni? Wapole watairithi nchi? Heri wenye kuteswa? Waandishi na Mafarisayo hawakuwa wakifundisha mambo kama hayo. Na bado kwa wale ambao waliielewa sheria ya Mungu waliutambua ukweli katika maneno ya Mwokozi. “Jicho kwa jicho” na “mchukie adui yako” zilikuwa sheria za chini (Mathayo 5:38, 43). Lakini Yesu Kristo alikuwa amekuja kufundisha sheria ya juu (ona 3 Nefi 15:2–10) iliyosanifiwa ili kutusaidia sisi siku moja kuwa “wakamilifu kama Baba [yetu] aliye mbinguni alivyo mkamilifu” (Mathayo 5:48).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mathayo 5:1–12; Luka 6:20–26, 46–49

Furaha ya kudumu huja kwa kuishi jinsi Yesu Kristo alivyofundisha.

Kila mtu anataka kuwa na furaha, lakini si kila mtu hutafuta furaha katika sehemu hizo hizo. Baadhi huitafuta katika nguvu na vyeo vya ulimwengu, wengine katika utajiri au kwa kutosheleza matamanio ya kimwili. Yesu Kristo alikuja kufundisha njia ya kupata furaha ya kudumu, kufundisha maana halisi ya kuwa mwenye heri. Je, unajifunza nini kuhusu kupata furaha ya kudumu kutoka katika Mathayo 5:1–12 na Luka 6:20–26? Je, ni kwa jinsi gani hii ni tofauti na mtazamo wa ulimwengu juu ya furaha?

Je, mistari hii, pamoja na Luka 6:46–49, inakufundisha nini kuhusu kuwa mfuasi wa Yesu Kristo? Unahisi ushawishi wa kufanya nini ili kukuza sifa zilizoelezewa katika mistari hii?

Ona pia Mwongozo wa Maandiko, “Mahubiri Mlimani,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org; “Sermon on the Mount: The Beatitudes” (video), ChurchofJesusChrist.org.

Mathayo 5:13

“Ninyi ni chumvi ya dunia.”

Chumvi kwa kipindi kirefu imekuwa ikitumika kuhifadhia, kuongeza ladha, na kusafishia. Chumvi pia ilikuwa na maana ya kidini kwa Waisraeli. Ilikuwa ikihusishwa na utamaduni wa kale wa kutoa wanyama kafara chini ya sheria ya Musa (ona Mambo ya Walawi 2:13; Hesabu 18:19). Chumvi ikiwa imepoteza ladha yake, inakuwa haiwezi kukoleza, au “haifai tena kabisa” (Mathayo 5:13). Hii hutokea inapokuwa imechanganywa na au kuchafuliwa na elementi zingine.

Hifadhi hili akilini mwako unapotafakari Mathayo 5:15. Ni kwa jinsi utadumisha ladha yako kama mfuasi wa Yesu Kristo? Ni kwa jinsi gani utatimiza kazi yako ya kuhifadhi na kusafisha kama chumvi ya duniani?

Ona pia Mafundisho na Maagano 103:9–10.

Picha
chumvi

“Ninyi ni chumvi ya dunia” (Mathayo 5:13).

Mathayo 5:17–48; Luka 6:27–35

Sheria ya Kristo huchukua nafasi ya sheria ya Musa.

Wafuasi wanaweza kuwa walishangaa kusikia Yesu akisema kwamba haki yao ilihitaji kuzidi ile ya waandishi na Mafarisayo (ona Mathayo 5:20), ambao walijiinua kwa jinsi walivyotii vyema sheria ya Musa.

Unaposoma Mathayo 5:21–48 na Luka 6:27–35, fikiria kuwekea alama kote tabia zilizohitajika katika sheria ya Musa (“Mmesikia ya kwamba …”) na kile Yesu alichofundisha ili kuziinua tabia hizi. Kwa nini unadhani njia ya Mwokozi ni sheria ya juu?

Kwa mfano, Yesu alifundisha nini katika Mathayo 5:27–28 kuhusu jukumu letu juu ya mawazo yetu? Je, ni kwa jinsi gani unaweza kupata udhibiti zaidi wa mawazo na hisia zinazokujia akilini na moyoni? (Ona Mafundisho na Maagano 121:45).

Ona pia video ya “Sermon on the Mount: The Higher Law” (video), ChurchofJesusChrist.org.

Mathayo 5:48

Je, Baba wa Mbinguni kweli anatarajia mimi niwe mkamilifu?

Rais Russell M. Nelson alifundisha:

“Neno ukamilifu lilitafsiriwa kutoka Kigiriki teleios, ambalo humaanisha ‘timilifu.’ … Kitenzi jina cha tendo ni teleiono, ambacho humaanisha ‘kufika mwisho mrefu, kuwa kikamilifu, kukamilisha, au kumaliza.’ Tafadhali kumbuka kwamba neno halimaanishi ‘uhuru wa kutofanya kosa’; humaanisha ‘kufikia malengo ya mbali.’…

“…Bwana alifundisha, ‘Ninyi hamuwezi kustahimili uwepo wa Mungu sasa … ; kwa hiyo, endeleeni katika uvumilivu hadi mtakapokuwa mmekamilika’ [Mafundisho na Maagano 67:13].

“Hatupaswi kufa moyo kama jitihada zetu za dhati kuelekea ukamilifu sasa zinaonekana kuwa ngumu na zisizo na mwisho. Ukamilifu unasubiri. Unaweza kuja tu kwa ukamilifu baada ya Ufufuko na kupitia kwa Bwana pekee. Unawasubiri wote wampendao, na kutii amri zake” (“Perfection Pending,” Ensign, Nov. 1995, 86, 88).

Ona pia 2 Petro 1:3–11; Moroni 10:32–33; Mafundisho na Maagano 76:69; Jeffrey R. Holland, “Uwe Mkamilifu—Hatimaye,” Liahona, Nov. 2017, 40–42.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mathayo 5:1–9.Ni kanuni zipi zilizofundishwa katika Mathayo 5:1–9 zingeweza kusaidia nyumba yako kuwa mahali pa furaha? Unaweza kuchagua moja au mbili ya zile zinazonekana muhimu hasa kwa familia yako. Kwa mfano, ni mafundisho gani tunayopata ambayo yanatusaidia kuwa wapatanishi? (Ona Mathayo 5:21–25, 38–44). Je, ni malengo gani tunaweza kuweka? Je, ni kwa jinsi gani tutafuatilia?

Mathayo 5:13.Kuleni pamoja chakula kilichotiwa chumvi na chakula hicho hicho bila chumvi. Tumeona tofauti gani? Inamaanisha nini kuwa “chumvi ya dumia”? Je, tunawezaje kufanya hili?

Mathayo 5:14–16.Ili kuisaidia familia wako kuelewa inamaanisha nini kuwa “nuru ya ulimwengu,” unaweza kutafiti baadhi ya vyanzo vya nuru nyumbani mwako, mazingira ya jirani na kwako, na ulimwenguni. Inaweza kusaidia kuonyesha kinachotokea unapoficha nuru. Je, Yesu alimaanisha nini aliposema, Ninyi ni nuru ya ulimwengu”? (Mathayo 5:14). Je, ni nani amekuwa kama nuru kwa familia yetu? Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kuwa nuru kwa wengine? (ona 3 Nefi 18:16, 24–25).

Mathayo 5:43–45.Familia yako inaposoma maneno ya Mwokozi katika mistari hii, ungeweza kuzungumza kuhusu akina nani, hasa, mnahisi mngeweza kuwapenda, kuwabariki, na kuwaombea. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuongeza upendo wetu kwao?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Shine On,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,144.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa makini. Unapokuwa makini kwa kile kinachotokea katika maisha ya [watoto] wako, utapata fursa nzuri sana za kufundisha. … Maoni ambayo [wao] hutoa au maswali ambayo wao huuliza yanaweza kukuongoza kwenye nyakati za kufundisha” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 16).

Picha
mshumaa

“Ninyi ni nuru ya ulimwengu” (Mathayo 5:14).

Chapisha