Agano Jipya 2023
Februari 6–12. Yohana 2–4: “Lazima Mzaliwe Mara ya Pili”


“Februari 6–12. Yohana 2–4: ‘Lazima Mzaliwe Mara ya Pili’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Februari 6–12. Yohana 2-4,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Yesu anazungumza na Nikodemo

Februari 6–12

Yohana 2–4

“Lazima Mzaliwe Mara ya Pili”

Unaposoma Yohana 2–4, Roho atakufundisha mambo kuhusu uongofu wako mwenyewe. Andika minong’ono Yake. Unaweza kupata umaizi wa kiroho wa ziada kutoka kwenye mawazo ya kujifunza katika muhtasari huu.

Andika Misukumo Yako

Katika karamu ya harusi huko Kana, Kristo aligeuza maji kuwa divai—tukio ambalo Yohana aliliita “mwanzo wa ishara” (Yohana 2:11). Hiyo ni kweli kwa zaidi ya dhana moja. Wakati huo ulikuwa ni muujiza wa kwanza Yesu alioutenda hadharani, unaweza pia kuashiria mwanzo mwingine wa kimiujiza—mchakato wa mioyo yetu kugeuzwa tunapokuwa zaidi kama Mwokozi wetu. Muujiza huu wa maisha yote unaanza na uamuzi wa kumfuata Yesu Kristo, kubadilika na kuishi maisha bora zaidi kupitia Yeye. Muujiza huu unaweza kuwa wa kubadilisha maisha kiasi kwamba “kuzaliwa mara ya pili” ni mojawapo ya njia bora za kuuelezea (Yohana 3:7). Lakini kuzaliwa tena ni mwanzo tu wa njia ya ufuasi. Maneno ya Kristo kwa mwanamke Msamaria pale kisimani hutukumbusha kwamba kama tukiendelea katika njia hii, mwishowe injili itakuwa “chemchemi ya maji” ndani yetu, “yakibubujikia uzima wa milele” (Yohana 4:14).

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Yohana 2:1–11

Miujiza ya Yesu Kristo “ilidhirihisha utukufu Wake.”

Unaposoma kuhusu Mwokozi akibadilisha maji kuwa divai katika Yohana 2:1–11, unaweza kupata umaizi wa ziada kwa kukumbuka mitazamo ya watu tofauti waliokuwepo pale, ikijumuisha Mariamu, wale wanafunzi, pamoja na watu wengine. Kama ungekuwa umeshuhudia matukio yaliyoelezewa hapa, nini ingekuwa misukumo yako juu ya Yesu? Muujiza huu unakufundisha nini kuhusu Bwana?

Yohana 3:1–21

Sina budi kuzaliwa mara ya pili ili kuingia ufalme wa Mungu.

Wakati Nikodemo alipomjia Yesu kwa siri, alikuwa mchunguzi makini. Baadaye, hata hivyo, alimtetea Yesu hadharani (ona Yohana 7:45–52) na aliungana na waaminio katika mazishi ya Mwokozi (ona Yohana 19:38–40). Ni mafundisho gani unapata katika Yohana 3:1–21 ambayo yalimshawishi Nikodemo kumfuata Yesu na kuzaliwa mara ya pili?

Nabii Joseph Smith alifundisha, “Kuzaliwa mara ya pili, huja kwa Roho wa Mungu kupitia ibada” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 95). Ni jukumu gani ubatizo wako na kuthibitishwa kwako—yaani “kuzaliwa kwa maji na kwa Roho” (Yohana 3:5)—unalo katika wewe kuzaliwa mara ya pili? Unafanya nini ili kuendeleza mchakato huu wa kubadilika? (Ona Alma 5:11–14).

Ona pia Mosia 5:7; 27:25–26; David A. Bednar, “Lazima Uzaliwe Upya,” Liahona, Mei 2007, 19–22.

Yohana 3:16–17

Baba wa Mbinguni huonyesha upendo Wake kwangu kupitia Yesu Kristo.

Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha, “Ule ukweli mkuu wa kwanza wa milele yote ni kwamba Mungu anatupenda sisi kwa moyo Wake wote, akili, na nguvu” (“Kesho Bwana Atafanya Maajabu miongini Mwenu,” Liahona, Mei 2016, 127). Ni kwa jinsi gani umehisi upendo wa Mungu kupitia zawadi ya Mwanawe?

Sakramenti hutoa muda wa kutafakari juu ya upendo wa Mungu na zawadi ya Mwanawe. Nyimbo zipi za sakramenti hukusaidia kuhisi upendo huu? Unaweza kufanya nini kufanya sakramenti iwe na maana zaidi?

Unaposoma endelea kujifunza kuhusu mafundisho na huduma ya Mwokozi, jiulize mwenyewe jinsi ambavyo vitu unavyosoma vinakusaidia kuelewa na kuhisi upendo wa Mungu.

Yohana 4:24

Je, Mungu ni roho?

Baadhi wanaweza kukanganywa na kauli ya Yesu kwamba Mungu ni roho. Tafsiri ya Joseph Smith ya mstari huu hutoa ufafanuzi muhimu: “Kwani kwa hao Mungu ameahidi Roho wake” (katika Yohana 4:24, tanbihi a). Ufunuo wa nyakati hizi pia hufundisha kwamba Mungu ana mwili wa nyama na mifupa (ona Mafundisho na Maagano 130:22–23; ona pia Mwanzo 5:1–3; Waebrania 1:1–3).

Yohana 4:5–26

Yesu Kristo hunipatia maji Yake ya uzima.

Yesu alikuwa akimaanisha nini wakati Yeye alipomwambia mwanamke Msamaria kwamba yeyote anywaye maji ampayo hataona kiu kamwe? Ni kwa jinsi gani injili ni kama maji ya uzima?

kijito cha maji

Injili ya Kristo ni maji ya uzima ambayo hurutubisha nafsi zetu.

Mojawapo ya ujumbe wa Mwokozi kwa mwanamke Msamaria ilikuwa kwamba jinsi tunavyoabudu ni muhimu zaidi ya wapi tunapoabudu (ona Yohana 4:21–24). Je! Unafanya nini ili “kumwabudu Baba katika roho na kweli”? (Yohana 4:23).

Ona pia Mwongozo wa Maandiko, “Abudu,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org; Dean M. Davies, “Baraka za Kuabudu,” Liahona, Nov. 2016, 93–95.

ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Yohana 2–4.Familia yako inaposoma sura hizi wiki hii, kuwa makini na jinsi Mwokozi alivyotumia mambo ya kila siku—kuzaliwa, upepo, maji, na chakula—ili kufundisha kweli za kiroho. Ni vitu gani unaweza kutumia nyumbani kwako kufundisha kweli za kiroho?

Mnapojifunza sura hizi, fikirieni kutazama video pamoja ambazo zinaonyesha matukio haya: “Jesus Turns Water into Wine,” “Jesus Cleanses the Temple,” “Jesus Teaches of Being Born Again,” na “Jesus Teaches a Samaritan Woman” (ChurchofJesusChrist.org).

2:26
1:34
6:4
4:11

Yohana 2:13–17.Ni ushawishi gani usio safi familia yako inahitaji kuondoa nyumbani ili pawe mahali patakatifu—kama hekaluni? Utafanya nini ili kuondoa vitu hivyo?

Yohana 3:1–6.Zungumza na wanafamilia kuhusu muujiza wa ujauzito na kujifungua—mchakato wa kuumba kiumbe hai, kinachotembea, chenye akili. Yesu alifundisha kwamba hatuna budi kuzaliwa tena kabla ya kuingia ufalme wa Mungu. Kwa nini kuzaliwa tena ni sitiari ya badiliko linalohitajika kwetu kabla ya kuweza kuingia ufalme wa Mungu? Ni kwa jinsi gani tunaweza kupata uzoefu wa mchakato wa kuzaliwa tena kiroho?

Yohana 3:16–17.Waalike wanafamilia kusema tena mstari huu kwa maneno yao wenyewe kama vile walikuwa wanauelezea kwa rafiki. Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo alitusaidia sisi kuhisi upendo wa Mungu?

Yohana 4:5–15.Mwokozi alikuwa anatufundisha nini wakati Yeye alipofananisha injili Yake na maji ya uzima? Familia yako ingeweza kutazama maji yakitiririka na kuelezea viwango wa usafi wa maji. Kwa nini tunahitaji kunywa maji kila siku? Ni kwa njia gani injili ya Yesu Kristo ni kama “chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele”? (Yohana 4:14).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “God Is Love,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 97.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Tafuta ishara. Maandiko daima hutumia vitu, matukio, au matendo, kuwakilisha kweli za kiroho. Ishara hizi zinaweza kustawisha uelewa wako wa mafundisho yanayofundishwa. Kwa mfano, Mwokozi alifananisha uongofu na kuzaliwa tena.

Yesu na mwanamke Msamaria kisimani

Maji ya Uzima,na Simon Dewey