“Januari 9–15. Mathayo 2; Luka 2: Tumekuja Kumuabudu,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)
“Januari 9–15. Mathayo 2: Luka 2,“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023
Januari 9–15
Mathayo 2; Luka 2
Tumekuja Kumuabudu
Watoto unaowafundisha ni wana na mabinti wa thamani wa Baba wa Mbinguni. Muombe Yeye akusaidie unapotafuta kuwafundisha kutoka katika maandiko. Anaweza kukuongoza kwenye kanuni unazopaswa kuzisisitiza na anaweza kukupa mwongozo wa kiungu juu ya mawazo ya shughuli ambayo itawagusa watoto Wake.
Alika Kushiriki
Waombe watoto wakuambie kile wanachojua kuhusu kuzaliwa kwa Kristo. Je! Ni sehemu gani wanazopenda katika hadithi hii?
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Yesu alizaliwa.
Yesu aliondoka nyumbani kwake na Baba wa Mbinguni kuja kuzaliwa duniani ili apate kuwa Mwokozi wetu. Unawezaje kuwasaidia watoto kukumbuka hadithi ya kuzaliwa kwa Kristo?
Shughuli Yamkini
-
Unaposoma hadithi ya kuzaliwa kwa Kristo, waalike watoto waigize hadithi wenyewe au kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii ili kuipitia tena. (Ona pia “Mlango wa 5: Yesu Amezaliwa,” katika Hadithi za Agano Jipya, 13–15, au video inayofanana nayo kwenye ChurchofJesusChrist.org.)
-
Kama unayo, leta seti ya kuigiza Kuzaliwa kwa Kristo, na waalike watoto waweke vipande hivyo katika sehemu sahihi unapokuwa unawasimulia hadithi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Unaweza kuonyesha picha ya Kuzaliwa kwa Kristo (ona, kwa mfano, muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Onyesha watu tofauti kwenye tukio la kuzaliwa kwa Yesu na waalike watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu kila mtu.
-
Imbeni pamoja nyimbo zipendwazo na watoto kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Unapofanya hayo, angalia kwa ajili ya fursa ya kutoa ushuhuda wako juu ya Mwokozi. Waalike watoto kushiriki kwa nini wanampenda Yesu.
Ninaweza kutoa zawadi nzuri kwa Yesu.
Mamajusi walimtolea Yesu zawadi za dhahabu, uvumba na manemane. Unawezaje kutumia hadithi hii kuwafundisha watoto kwamba wanaweza kutoa zawadi kwa Yesu pia—zawadi kama upendo, huduma, na utii?
Shughuli Yamkini
-
Onyesha picha ya Mamajusi mnaporejelea hadithi yao, inayopatikana katika Mathayo 2:1–12, pamoja na watoto. Unaweza kuonyesha picha Mamajusi Wakitoa Zawadi (ChurchofJesusChrist.org).
-
Picha za zawadi zilizofungwa kwa karatasi za kufungia zawadi au vitu ambavyo vinawakilisha zawadi tunazoweza kumpa Yesu. Waalike watoto kukusaidia kufungua zawadi hizo na kujadili jinsi tunavyotoa zawadi hizi kwa Mwokozi.
-
Msaidie kila mtoto kuchora au kuandika orodha ya zawadi wanazoweza kutoa kwa Yesu, kama vile “kuwa rafiki mwema” au “kusali.” Waalike watoto kushiriki orodha zao pamoja na darasa na kuchagua “zawadi” moja watakayompa Yesu leo.
Yesu wakati mmoja alikuwa mtoto kama mimi.
Kujifunza kuhusu utoto wa Mwokozi kunaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kujifananisha Naye. Waulize watoto kile wanachoweza kujifunza kutokana na mistari hii kuhusu jinsi wanavyoweza kuwa kama Yesu sasa.
Shughuli Yamkini
-
Mwalike mmoja wa vijana katika kata ili kutembelea darasa lako na kushiriki hadithi ya Yesu Akifundisha katika hekalu wakati Alipokuwa kijana.
-
Waombe watoto kadhaa kabla ya muda kuleta picha zao wenyewe wakiwa watoto wachanga za kushiriki. Waulize jinsi walivyokua. Shiriki baadhi ya njia ambazo Yesu alikua (ona Luka 2:40, 52). Imba pamoja na watoto “Jesus Once Was a Little Child” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 55) au wimbo mwingine kuhusu Mwokozi.
-
Soma Luka 2:52, na eleza “hekima” na “kimo” vinamaanisha nini. Unaweza kuwauliza watoto kufanya vitendo vinavyoonyesha kile inachomaanisha kuongezeka katika hekima na katika kumpendeza Mungu na watu wengine. Kwa mfano, wanaweza kuigiza kusoma kitabu au kumsaidia mtu aliye na uhitaji.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Manabii wa kale walitabiri kuzaliwa kwa Mwokozi.
Manabii na waaminio walikuwa wanatarajia kuzaliwa kwa Mwokozi kwa karne nyingi. Kuelewa ukweli huu kunaweza kuwasaidia watoto kupata kuthamini zaidi kwa maisha ya Mwokozi na huduma Yake.
Shughuli Yamkini
-
Waombe watoto kuzungumza kuhusu mambo wanayotarajia, kama siku ya kuzaliwa au sikukuu. Waache watoto wasome Helamani 14:2–5 kupata kitu fulani manabii walichokuwa wanatazamia.
-
Someni pamoja baadhi ya unabii wa kuzaliwa kwa Mwokozi (ona Isaya 7:14; 9:6; 1 Nefi 11:18; Helamani 14:5). Wasaidie watoto kuorodhesha maelezo yaliyomo katika unabii huu na utafute utimilifu wake katika Luka 2:1–21 na Mathayo 2:1–12.
-
Waalike watoto kuchora picha ya kitu fulani kutoka Mathayo 2:1–12 au Luka 2:1–21 na kushiriki kwa nini wao wanashukuru Yesu alizaliwa.
Yesu akazidi kuendelea katika “hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.”
Kama Yesu, watoto unaowafundisha wana misheni muhimu ya kujiandaa kwa ajili yake. Wanaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Yesu?
Shughuli Yamkini
-
Unaposoma Luka 2:40, 52, waambie watoto wasikilize mambo ambayo Yesu alifanya. Waalike watoto kushiriki njia ambazo wamekua tangu walipokuwa wadogo. Shiriki uzoefu wako mwenyewe wa kujifunza injili kidogo kidogo. Toa ushuhuda wako juu ya Mwokozi.
-
Kamilisha shughuli ambazo zinaonyesha virai katika Luka 2:40,52. Kwa mfano, unaweza kupima urefu wa kila mtoto (“Yesu aliongezeka katika … kimo”) au waombe watoto washiriki maandiko yao wayapendayo (“alikua imara kiroho”). Wasaidie watoto kutambua njia wanazokua na kushiriki na familia zao.
-
Baada ya kurejelea Luka 2:40, 52, waalike watoto kushiriki kile wanachofikiria Yesu angelikuwaje Yeye alipokuwa na umri kama wao. Angemtendeaje mama Yake? Kaka na Dada Zake?
Ninaweza kufuata mfano wa Yesu.
Hata alipokuwa kijana, Yesu alikuwa akifundisha hekaluni. Vivyo hivyo, watoto katika darasa lako wana mengi ya kuwafundisha wale wanaowazunguka.
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto kuja wakiwa wamejiandaa kufanya muhtasari hadithi katika Luka 2:41–52. Ili kuwasaidia watoto kuelewa hadithi hii, fundisha “kazi ya Baba” (mstari wa 49) inamaanisha nini. Kwa mfano, unaweza kuwaelezea kile ambacho wewe au wazazi wako mnafanya kama kazi. Je, ni kazi au “shughuli” gani ilikuwa ya Yusufu baba wa Yesu wa duniani? (ona Mathayo 13:55). Je, Ni nini ndiyo shughuli ya Baba Yake wa Mbinguni? (ona Luka 2:46–49; ona pia Musa 1:39).
-
Pamoja na watoto, someni Luka 2:46–49, na uulize, “Je, Yesu Alifanyaje ‘shughuli ya Baba Yake’?” Wasaidie watoto kuorodhesha au kuchora ubaoni njia wanazoweza kusaidia kufanya kazi ya Baba wa Mbinguni pia.
-
Ili kuwasaidia watoto kujenga kujiamini kwamba wao, kama mvulana Yesu, wanaweza kufundisha injili, wasaidie kufanya mazoezi kufundishana wao kwa wao kanuni kutoka Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wahimize watoto kuelezea familia zao kile ambacho wamejifunza kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo.