Agano Jipya 2023
Agosti 7–13 Warumi 1–6: “Uweza wa Mungu uletao Wokovu”


“Agosti 7–13. Warumi 1–6: ‘Uweza wa Mungu uletao Wokovu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Agosti 7–13. Warumi 1–6.” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Paulo anaandika waraka

Agosti 7–13

Warumi 1–6

“Uweza wa Mungu uletao Wokovu”

Je, ni msukumo gani unaupata unaposoma Warumi 1–6? Misukumo hii inaweza kukusaidia kuchagua kutoka kwenye mawazo yafuatayo ya kufundishia au andaa ya kwako mwenyewe.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kushiriki kile walichofanya katika kuitikia mialiko yoyote uliyowapa katika somo la wiki iliyopita.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Warumi 1:16–17

Ninaweza kuonyesha imani yangu katika Yesu Kristo kwa kumfuata Yeye.

Paulo alifundisha kwamba injili ina uwezo wa kuleta wokovu kwa kila mtu ambaye anaishi kwa imani katika Yesu Kristo. Je, unawezaje kuwasaidia watoto kuonyesha imani yao katika Yesu Kristo kwa kumfuata Yeye?

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto Warumi 1:17 na wasaidie kukariri kirai “Wenye haki wataishi kwa imani.” Unaweza kumpangia kila mtoto neno moja katika kirai na uwaombe waseme neno hilo unapowanyoshea kidole. Elezea kwamba kirai hiki kinamaanisha kwamba tunapaswa kuwa na imani katika Yesu Kristo. Waulize watoto kama wanajua imani ni nini. Onyesha picha ya Yesu Kristo na eleza kwamba tunaamini kuwa Yeye yupo kweli hata kama hatujamwona. Hii ni imani—kusadiki katika kitu hata kama hatujakiona.

  • Eleza kwamba tunaonyesha imani yetu katika Yesu Kristo kwa kumtii Yeye. Ficha picha humo chumbani ya watu wakifanya kile ambacho Yesu ametuomba tufanye. Acha watoto wachukue zamu kutafuta na kuelezea picha hizo. Je, tunaweza kufanya nini ili kumfuata Yesu?

  • Mwombe mmoja wa watoto afumbe macho yake, na mwongoze kuvuka chumba kuelekea picha ya Yesu. Kama muda unaruhusu, acha watoto wengine wapate zamu kushiriki. Wasaidie watoto kuelewa kwamba wanaweza kufuata mafundisho ya Yesu kama walivyofuata maelekezo yako.

Warumi 6:1–11

Kubatizwa ni kama kuwa mtu mpya.

Watoto unaowafundisha wanajiandaa kwa ajili ya ubatizo. Je, wanaweza kujifunza nini kuhusu ubatizo kutoka katika Warumi 6?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kurudia kirai “Kuenenda katika upya wa uzima” (Warumi 6:4). Waambie watoto hii ina maana gani kwako. Kwa mfano, ungeweza kushiriki kumbukumbu kuhusu siku uliyobatizwa na zungumzia kuhusu jinsi ubatizo wako ulivyokusaidia wewe kuwa zaidi kama Yesu Kristo. Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwafundisha watoto kwamba ubatizo unatusaidia kuwa mtu mpya.

  • Ikiwa ye yote kati ya watoto hao amewahi kuhudhuria ubatizo, waombe waelezee uzoefu wao. Au onyesha picha ya mtu akibatizwa (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 35, 103–4). Wasaidie watoto kuelewa kwamba kwenye ubatizo tunafanya ahadi ya kuwa kama Yesu. Waalike kuchora picha zao wenyewe wakiwa wanabatizwa na washiriki kile wanachoweza kufanya ili kujiandaa kwa ajili ya ubatizo wao.

  • Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu ubatizo, kama vile “When I Am Baptized” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103). Tunajifunza nini kuhusu ubatizo kutoka wimbo huu?

Picha
mtoto anabatizwa

Ubatizo unaashiria kuanza maisha mapya kama mfuasi wa Kristo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Warumi 1:16–17

Ninaweza kuonyesha imani yangu katika Yesu Kristo kwa kumfuata Yeye.

Paulo alifundisha kwamba injili ina uwezo wa kuleta wokovu kwa kila mtu ambaye anaishi kwa imani katika Yesu Kristo. Imani katika Yesu Kristo ni kanuni ya kwanza ya injili. Inatuhamasisha kutii amri. Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto waelewe vyema imani?

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kutafuta Rumi kwenye ramani. Wasaidie watoto kuelewa kwamba wiki chache zijazo, watajifunza kutoka kwenye barua Paulo alizoandika kwa waumini wa Kanisa katika sehemu mbali mbali, kuanzia na barua yake kwa Warumi.

  • Andika maandishi kutoka Warumi 1:16 ubaoni, ukiacha mapengo ya maneno machache. Waombe watoto kutafuta kwenye maandiko na kujaza mapengo hayo. Waalike watoto kushiriki kile “Siionei haya injili ya Kristo” inamaanisha kwao,

  • Mwalike mtoto kusoma kwa sauti Warumi 1:17, na waombe watoto wengine kusikiliza neno ambalo litarudiwa. Maana ya “kuishi kwa imani” ni nini? Wasaidie watoto kutafuta ufafanuzi wa imani katika nyenzo kama vile Mwongozo wa Maandiko, “Imani” (scriptures.Churchof JesusChrist.org). Je, ni kwa jinsi gani maisha yetu yangekuwa tofauti kama tusingekuwa na imani katika Yesu Kristo?

  • Waonyeshe watoto mmea na mbegu, na waulize jinsi tunavyosaidia mbegu kuwa mmea. Eleza kwamba wakati tunapopanda na kunyunyizia maji mbegu, tunaonyesha kwamba tuna imani kwamba itaota na kukua. Tunaonyeshaje kwamba tuna imani katika Yesu Kristo? Fikiria kuimba wimbo kuhusu imani, kama vile “Faith” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96), kama sehemu ya shughuli hii.

Warumi 3:23–24

Sisi wote tunamhitaji Yesu Kristo ili tusamehewe dhambi zetu.

Paulo aliwataka Warumi waelewe kwamba wokovu unakuja tu kupitia Yesu Kristo na neema Yake. Tafakari jinsi unavyoweza kufundisha ukweli huu kwa watoto.

Shughuli Yamkini

  • Mpe kila mtoto kirai kutoka Warumi 23–24, kilichoandikwa kwenye kipande cha karatasi. Waalike watoto kuweka kirai hicho katika mpangilio sahihi na waisome mistari hiyo pamoja. Waulize watoto wanajifunza nini kutoka kwenye mistari hiyo. Eleza kwamba “neema” katika mstari wa 24 inamaanisha karama ya Mwokozi ya upendo na rehema, inayofanya iwezekane kwetu sisi kupokea msamaha wa dhambi zetu na kuwa bora zaidi.

  • Ning’iniza picha juu kwenye ukuta au sehemu nyingine ambayo watoto hawawezi kufikia wao wenyewe. Waache wajaribu kuifikia, na fananisha hii na kile Paulo alichofundisha katika Warumi 3:23. Kisha wasaidie kuifikia hiyo picha. Mwokozi amefanya nini kwa ajili yetu ambacho hatuwezi kujifanyia wenyewe? Waalike watoto kushiriki jinsi wanavyojisikia kuhusu Mwokozi wakati wanapofikiria kuhusu kile Yeye alichofanya na anachoweza kuwasaidia wao.

Warumi 6:1–11

Kubatizwa ni kama kuwa mtu mpya.

Paulo alifundisha kwamba ubatizo unaashiria kifo na Ufufuko wa Kristo. Pia unaashiria kuinuliwa juu ili “kuenenda katika upya wa uzima” (Warumi 6:4). Tunafanya upya ahadi yetu ya kuenenda katika upya wa uzima kila wakati tunapopokea sakramenti.

Shughuli Yamkini

  • Mwalike mtoto asome Warumi 6:3–6. Je, Paulo alisema ubatizo ni “katika mfano wa”?

  • Jadili ni kwa namna gani ubatizo unaashiria kifo na ufufuko. Inaweza kusaidia kuonyesha picha ya ubatizo au onyesha video kama “The Baptism of Jesus” (ChurchofJesusChrist.org). Je, kwa nini kifo na ufufuko ni ishara nzuri ya kile kinachotokea wakati tunapobatizwa?

  • Someni pamoja sala za sakramenti (ona Mafundisho na Maagano 20:77, 79). Wakumbushe watoto kwamba tunapopokea sakramenti, tunafanya upya ahadi tulizofanya ya kumfuata Yesu Kristo wakati tulipokuwa tunabatizwa. Je, ni kwa jinsi gani sakramenti inatusaidia “kutembea katika upya wa uzima”?

  • Waalike watoto kuchora picha ambazo zinaonyesha inamaanisha nini kwao “kutembea katika upya wa uzima.” Watoto wanaweza kuning’iniza picha hizi katika vyumba vyao ili kuwasaidia kukumbuka kufanya chaguzi nzuri.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Pendekeza kwamba watoto wawaombe wanafamilia wao kuwajulisha wakati wanapoona kuwa watoto wanafanya kitu ambacho kinaonyesha imani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jenga kujiamini kwa watoto. Wasifie watoto wanapokuwa wanashiriki darasani. Hii ni njia mojawapo ya kujenga kujiamini kwao kwamba wanaweza kujifunza injili.

Chapisha