Agano Jipya 2023
Julai 31–Agosti 6. Matendo ya Mitume 22–28: “Mtumishi na Shahidi”


“Julai 31–Agosti 6. Matendo ya Mitume 22–28: ‘Mtumishi na Shahidi’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Julai 31–Agosti 6. Matendo ya Mitume 22-28,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Paulo akiwa gerezani

Julai 31–Agosti 6

Matendo ya Mitume 22–28

“Mtumishi na Shahidi”

Unaposoma maelezo kutoka huduma ya Mtume Paulo katika Matendo ya Mitume 22–28, tafuta kanuni ambazo zitakuwa na maana kwa watoto unaowafundisha.

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha ambazo zinaweza kuwakumbusha watoto hadithi kutoka Matendo ya Mitume 22–28, kama vile chumba cha gereza, boti, na nyoka. Waalike watoto kushiriki hadithi zozote wanazojua kuhusu Paulo zinazohusiana na picha hizi.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Matendo ya Mitume 23:10–11

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanajali kuhusu mimi na watanisaidia wakati wa shida.

Kujifunza kuhusu jinsi Mwokozi alivyomsaidia Paulo kunaweza kujenga imani ya watoto kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanawajali.

Shughuli Yamkini

  • Shiriki hadithi iliyo katika Matendo ya Mitume 23:10–11 ya Mwokozi akimtembelea Paulo gerezani. Au onyesha video “Be of Good Cheer” (ChurchofJesusChrist.org), ambayo inasimulia hadithi hii. Simulia wakati ambapo ulikuwa na majaribu na ukapokea mwongozo na faraja kutoka kwa Mungu. Waombe watoto kushiriki nyakati walipohisi kufarijiwa na Mungu.

  • Wasaidie watoto kukariri kile Yesu alichosema kwa Paulo: “Uwe na moyo mkuu.” Waombe watoto kufikiria juu ya mtu ambaye wanaweza kumwalika kuwa na moyo mkuu—labda mtu fulani ambaye ana huzuni au wasiwasi.

  • Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu kuwa mwenye furaha, kama vile “Smiles” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 267).

msichana akiongea kwenye mimbari kanisani na mwanamke nyuma yake

Kama Paulo, tunaweza kuchagua kutoa shuhuda juu ya Mwokozi.

Matendo ya Mitume 26:1—29

Naweza kushiriki ushuhuda wangu pamoja na wengine.

Kurudia ushuhuda wa Paulo mbele ya Mfalme Agripa kunaweza kuwasaidia watoto kushiriki kile wanachojua kuwa ni kweli.

Shughuli Yamkini

  • Lete taji la karatasi darasani na mwache mtoto aivae na ajifanye kuwa Mfalme Agripa. Mwalike mtoto mwingine asimame mbele ya mfalme kumwakilisha Paulo unapofanya muhtasari wa ushuhuda wa Paulo na majibu ya Mfalme Agripa, yanayopatikana katika Matendo ya Mitume 26:1–29 (ona “Sura ya 63: Paulo Anamaliza Misheni yake,’ katika Hadithi za Agano Jipya, 162—66, au video inayofanana katika ChurchofJesusChrist.org). Elezea kwamba tunaweza kushiriki shuhuda zetu na wengine, kama alivyofanya Paulo.

  • Waombe watoto kusikiliza wakati unaimba au kusoma wimbo kuhusu ushuhuda, kama vile “I Know My Father Lives” (Kitabu cha nyimbo za Watoto, 5). Waalike watoto wainue mikono yao wanaposikia kitu wanachojua kuwa ni kweli. Unaweza kutaka kuimba wimbo mara kadhaa; waalike watoto kujiunga mawe mara wanapoyazoea maneno yake. Wasaidie kufanyia mazoezi kutoa shuhuda zao juu ya mambo wanayojua kuwa ni ya kweli.

  • Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kufikiria kuhusu kitu ambacho wanaweza kusema wanapokuwa wanatoa shuhuda zao (ona Makala ya Imani kwa ajili ya mawazo zaidi). Waalike kutoa shuhuda zao kwa mtu katika familia yao.

Matendo ya Mitume 27

Manabii wananionya juu ya hatari.

Fikiria jinsi hadithi ya Paulo ya kuangamia kwa meli inavyoweza kuwafundisha watoto kwamba manabii wanaona hatari za kimwili na za kiroho ambazo sisi hatuwezi kuziona.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wajifanye wapo ndani ya meli ambayo inaangamia katika dhoruba. Soma onyo la Paulo kwa watu, linalopatikana katika Matendo ya Mitume 27:9–10, na shiriki hadithi ya maangamizi ya meli baharini ambayo yalitokea kwa sababu hawakusikiliza onyo lake (ona Matendo ya Mitume 27, 39–44). Onyesha picha ya Rais wa Kanisa, na toa ushuhuda wako kwamba yeye anaweza kutuonya sisi juu ya hatari za kiroho.

  • Weka picha kadhaa au vitu kote chumba ambavyo vinawakilisha vitu ambavyo manabii wametufundisha kufanya ili kuwa zaidi kama Yesu, kama vile kuwapenda wengine au kubatizwa. Kama darasa, tembeeni kuzunguka chumbani, mkisimama kwenye kila picha au kitu ili kuzungumzia kuhusu jinsi kufuata mafundisho ya nabii kunasaidia kutuweka salama.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Matendo ya Mitume 23:10–11; 27:18–25; 28:1–6

Wakati ninapokabiliana na dhiki Mungu hanitelekezi.

Wakati wote wa majaribu ambayo Paulo alipitia, Bwana alikuwa pamoja naye. Je, unawezaje kuwasaidia watoto kulinganisha uzoefu wa Paulo na maisha yao?

Shughuli Yamkini

  • Ukitumia Matendo ya Mitume 23:10, eleza kwamba Paulo aliwekwa gerezani kwa sababu aliwafundisha watu kuhusu Yesu. Kisha soma Matendo ya Mitume 23:11 pamoja na watoto. Au onyesha video “Be of Good Cheer” (ChurchofJesusChrist.org), ambayo inasimulia hadithi hii. Kwa nini Paulo “angekuwa na moyo mkuu” hata kama alikuwa gerezani?

  • Andika ubaoni Matendo ya Mitume 23:10–11; Matendo ya Mitume 27:18–25; na Matendo ya Mitume 28:1–6. Onyesha picha za gereza, meli, na nyoka, na waalike watoto kurejea mstari hii na kuioanisha na picha. Katika kila moja ya maelezo haya, Bwana alimwoneshaje Paulo kwamba Yeye alikuwa pamoja naye? Elezea tukio ambapo Bwana alikuwa pamoja nawe katika wakati mgumu na jinsi uliimarishwa na ushuhuda wako juu Yake. Waombe watoto pia kuelezea uzoefu wao.

Matendo ya Mitume 26

Ninaweza kushiriki kwa ujasiri ushuhuda wangu juu ya Yesu Kristo.

Ujasiri wa Paulo katika kushiriki ushuhuda wake unaweza kuwasaidia watoto kuwa wajasiri wakati wanaposhiriki shuhuda zao.

Shughuli Yamkini

  • Chagua mistari kutoka katika Matendo ya Mitume 26 ili kusoma na watoto ili iwasaidie wao kuelewa kitu ambacho Paulo alimwambia Mfalme Agripa kuhusu uzoefu wake (kama vile mstari wa 9–16) na kile alichofundisha kuhusu Yesu Kristo (kama vile mstari wa 18, 23). Ungeweza pia kuonyesha sehemu ya video ya “Paul: A Chosen Vessel” (ChurchofJesusChrist.org). Kwa nini ingewezekana ilikuwa ya kuogofya kwa Paulo kushiriki vitu hivi mbele ya Mfalme? Waalike watoto kuorodhesha baadhi ya kanuni za injili wanazojua kuwa za kweli. Waombe wamfikirie mtu wanayemjua anahitaji kusikia ushuhuda wao juu ya kweli hizi.

  • Waalike watoto kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuandika kitu ambacho wangeweza kusema katika shuhuda zao.

Matendo ya Mitume 27

Manabii wananionya juu ya hatari.

Watoto wanaweza kusikiliza jumbe za manabii walio hai na kutambua maonyo yao. Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujifunza jinsi ya kusikiliza maonyo hayo?

Shughuli Yamkini

  • Kata kipande cha karatasi chenye umbo la meli katika vipande vya chemsha bongo. Waalike watoto kuandika maonyo ya Paulo katika Matendo ya Mitume 27:9–11 kwenye vipande hivyo na kuweka chemsha bongo pamoja. Kwa nini watu hawakumsikiliza Paulo? (ona mstari wa 11). Waalike watoto kusoma mstari wa 18–20 na 40–44 ili kupata kile kilichotokea kama matokeo. (Eleza kwamba kwa sababu watu walifuata ushauri wa mwisho wa Paulo kubaki kwenye meli, hakuna hata mmoja aliyekufa katika maangamizi hayo ya meli baharini; ona mstari wa 30—32.) Ni nini tunaweza kujifunza kutoka kwenye uzoefu huu kuhusu kumfuata nabii?

  • Leta ujumbe wa mkutano mkuu wa hivi karibuni wa Rais wa Kanisa na shiriki pamoja na watoto maonyo yo yote au ushauri alioutoa. Waalike watoto kufikiria njia wanazoweza kumfuata nabii.

  • Onyesha video “Blessed and Happy Are Those Who Keep the Commandments of God” (ChurchofJesusChrist.org). Ni kwa jinsi gani manabii ni kama mtu mwenye darubini?

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waombe watoto kutumia kile walichojifunza kuhusu Paulo ili kuzihimiza familia zao kujifunza ujumbe wa nabii wa hivi karibuni na kujadili jinsi wanavyoweza kufuata ushauri wake.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Husisha milango ya fahamu. “Watoto wengi (na watu wazima) wanajifunza vyema zaidi wakati milango mingi ya fahamu inapohusishwa. Tafuta mbinu za kuwasaidia watoto watumie milango yao ya fahamu ya kuona, kusikia, na kugusa wanapojifunza. Katika hali zingine, unaweza hata kupata njia za kujumuisha mlango wa kunusa na kuonja!” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi25).