Agano Jipya 2023
Agosti 14–20 Warumi 7–16: “Uushinde Ubaya kwa Wema”


“Agosti 14–20. Warumi 7–16: ‘Uushinde Ubaya kwa Wema’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Agosti 14–20. Warumi 7–16.“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Magofu ya Roma ya kale

Agosti 14–20

Warumi 7–16

“Uushinde Ubaya kwa Wema”

Unaposoma Warumi 7–16, andika misukumo yoyote unayopokea kuhusu jinsi gani unavyoweza kuwafundisha watoto ukweli uliomo katika sura hizi.

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Siku chache kabla, mwalike mtoto mmoja au zaidi kutafuta mstari katika Warumi 7–16 ambao wataweza kushiriki pamoja na darasa. Unaweza kuwaalika wazazi wao kusaidia ikibidi.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Warumi 8:35–39

Baba yangu wa Mbinguni ananipenda.

Unawezaje kutumia maneno ya Paulo kuwafundisha watoto kwamba Baba wa Mbinguni daima atawapenda?

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kukariri kirai “[Hakuna] kinachoweza kututenganisha sisi na upendo wa Mungu” (Warumi 8:39). Fikiria kuhusu njia za kuelezea ukweli huu. Kwa mfano ungeweza kuleta mbao mbili ulizozipigilia msumari pamoja, moja imewekewa lebo ya “sisi” na nyingine “upendo wa Mungu.” Waache watoto waone kama wanaweza kutenganisha hizo mbao.

  • Onyesha picha ya jua, au waalike watoto kutazama nje ya dirisha na waone mwangaza wa jua. Ni kwa jinsi gani jua linafanana na upendo wa Baba wa Mbinguni? Wasaidie watoto kuona kwamba ingawa jua liko mbali sana, linaweza kutusaidia kuhisi joto. Tunaweza kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni wakati wote, ingawa hayupo nasi kimwili. Imbeni pamoja wimbo kuhusu upendo wa Baba wa Mbinguni, kama vile “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29).

Yesu na watoto

Watoto wanaweza kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu Mwokozi na kuwa na imani katika Yeye. Wakati wa hadithi huko Galilaya, na Del Parson

Warumi 10:17

Imani huja kwa kusikia neno la Mungu.

Watoto wanaposikia neno la Mungu na kulisikiliza kwa makini imani yao katika Mungu itakua.

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto Warumi 10:17 na uwaonyeshe picha za hali ambazo wanaweza kusikia neno la Mungu (kama vile kujifunza maandiko kifamilia, madarasa ya kanisa, au mkutano mkuu; ona ukurasa wa shughuli za wiki hii). Waulize watoto ni lini walisikia neno la Mungu.

  • Simulia hadithi kuhusu mtoto anayesikiliza neno la Mungu katika njia mbalimbali. Wakati unaposimulia hadithi, puliza puto kidogo kidogo kuonyesha jinsi imani ya mtoto inavyokua kila wakati anaposikia neno la Mungu.

  • Kuwasaidia watoto kuelewa kwamba imani yao inaweza kukua, wasaidie kuimba “Faith” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96–97). Wanapoimba, waombe wajifanye kuwa mbegu kwa kuchuchumaa chini. Kila wakati wanapoimba neno imani, waambie wainuke kidogo kama mmea unaokua.

  • Ficha darasani seti ya maandiko, picha ya Rais wa Kanisa, na nakala ya gazeti la Rafiki. Waombe watoto watafute vitu hivi na kushiriki jinsi kila kimoja kinavyofanya iwezekane kwetu sisi kusikia neno la Mungu.

Warumi 16:1–4

Ninaweza kusema asante kwa wale wanaonisaidia.

Paulo alikuwa na shukrani kwa watu waliomsaidia. Unaweza kuwasaidia watoto kutambua mambo ya ukarimu watu wengine wanayofanya kwa ajili yao na kukumbuka kuwashukuru.

Shughuli Yamkini

  • Eleza kwamba Paulo alikuwa na shukrani kwa msaada alioupata kutoka kwa mwanamke aliyeitwa Fibi na wanandoa walioitwa Prisila na Akila (ona Warumi 16:1–4). Waombe watoto wachore picha za Paulo na watu hawa watatu unaposhiriki maneno na virai kutoka kwenye mistari hii.

  • Muombe kila mtoto ashiriki kitu fulani kizuri ambacho mtu fulani alikifanya kwa ajili yake hivi karibuni. Wasaidie watoto kutengeneza kadi za asante sana kwa ajili ya watu hao.

  • Wasaidie watoto kujifunza jinsi ya kusema asante sana katika lugha tofauti. Wimbo “Children All Over the World” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 16–17) unaweza kusaidia.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Warumi 8:16–18

Baba wa Mbinguni ananitaka mimi kujiandaa kupokea vyote ambavyo Yeye anavyo.

Mpango wa Baba wa Mbinguni unafanya iwezekane kwa ajili yetu kuwa kama Yeye na kurithi vyote ambavyo Yeye anavyo. Ukweli huu unaweza kuvutia watoto unaowafundisha kuishi injili kwa uaminifu zaidi.

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Warumi 8:16–18. Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu sisi ni kina nani na tunaweza kuwa nani? Eleza kwamba “mrithi” ni mtu anayerithi, au kupokea, kile wazazi wake walichonacho. Andika ubaoni Tunahitaji kufanya nini ili kurithi vyote ambavyo Baba yetu wa Mbinguni anavyo? Imbeni pamoja wimbo kuhusu utiifu, kama vile “I will Follow God’s Plan for Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 164–165), mkitafuta majibu. Ni majibu gani mengine watoto wanaweza kufikiria?

  • Waombe watoto kufikiria kuhusu mfalme anayetaka wana na mabinti zake kutawala katika himaya yake siku moja. Elezea kwamba Baba wa Mbinguni ni kama mfalme, na sisi ni wana na mabinti zake wa kifalme. Unaweza kushiriki hadithi ya mwana wa Mfalme Louis wa XVI wa Ufaransa, inayopatikana katika hotuba ya Dada Elaine S. Dalton “Kumbuka Wewe ni Nani!” (Liahona, Mei 2010, 121). Je, kwa nini ni muhimu kukumbuka kwamba sisi ni watoto wa Baba wa Mbinguni na tumezaliwa ili siku moja tuwe kama Yeye? Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinashawishi chaguzi tunazofanya hapa duniani?

Warumi 10:17

Imani huja kwa kusikia neno la Mungu.

Watoto wana fursa nyingi za kusikia neno la Mungu. Wasaidie kuona namna gani kusikia neno la Mungu kunaweza kuimarisha imani yao.

Shughuli Yamkini

  • Andika sentensi zifuatazo ubaoni: huja kwa , na kwa ya . Waombe watoto wajaze mapengo baada ya kusoma Warumi 10:17. Shiriki muda ambapo mtu fulani alipofundisha ukweli wa injili ambao ulisaidia kuimarisha imani yako—labda ungeshiriki maandiko unayoyapenda au nukuu kutoka mkutano mkuu. Waalike watoto kushiriki uzoefu wao wenyewe.

  • Mpe mtoto mmoja picha ya Mwokozi akimponya mtu na mwambie yeye hasiruhusu watoto wengine kuona picha hiyo. Muombe mtoto kutoa vidokezo kuwasaidia watoto wengine kukisia picha inaonyesha nini. Tunawezaje kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu Mwokozi ili waweze kuwa na imani katika Yeye?

Warumi 14:10, 13

“Acha tusizidi … kuhukumiana.”

Wakati watoto wanaongea na wengine wanaofanya chaguzi tofauti kuliko wanavyofanya wao, wanaweza kushawishiwa kuwa watoa hukumu. Fikiria jinsi ushauri wa Paulo kwa Warumi unavyoweza kuwasaidia kuepuka hukumu kama hiyo.

Shughuli Yamkini

  • Mwalike mtoto asome Warumi 14: 10,13. Waombe watoto wengine kuhesabu ni mara ngapi Paulo alitumia neno hukumu. Nini maana ya kumhukumu mtu? Kwa nini tunapaswa kuepuka kuwahukumu wengine?

  • Onyesha picha ya mtu, na waulize watoto sisi tunajua nini kuhusu mtu huyu kwa kutazama picha yake tu. Je, mambo gani mengine ambayo sisi hatuyajui kuhusu yeye? Kwa nini Bwana ni mtu sahihi zaidi kumhukumu mtu huyu? (Ona 1 Samweli 16:7).

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waombe watoto wachague shughuli moja mliyofanya kama darasa na waifanye pamoja na familia zao. Waambie kwamba wiki ijayo wanaweza kushiriki kile walichofanya.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wape fursa watoto ya kutembea tembea. Mara nyingi ni vigumu kwa watoto kukaa kwa utulivu kwa vipindi vya muda mrefu. Baada ya muda mfupi, waalike watoto kusimama kwa sehemu ya darasa au kukaa sakafuni kuliko kukaa kwenye viti vyao.