Agano Jipya 2023
Novemba 6–12. Waebrania 7–13: “Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo”


“Novemba 6–12. Waebrania 7–13: ‘Kuhani mkuu wa Mambo Mema yatakayokuwapo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2021)

“Novemba 6–12. Waebrania 7–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Melkizedeki akimbariki Abramu

Melkizedeki Akimbariki Abramu, na Walter Rane Kipaji cha msanii

Novemba 6–12

Waebrania 7–13

“Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo”

Unapopitia tena na kutafakari muhtasari huu, sikiliza kwa makini vishawishi unavyopokea kuhusu watoto unaowafundisha. Roho atakusaidia kupata jumbe kwa ajili yao katika Waebrania 7–13.

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waombe watoto kushiriki vitu wao na familia zao wanafanya ili kujifunza injili nyumbani. Waombe kushiriki baadhi ya matukio yao pendwa ya kujifunza injili pamoja na familia zao.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Waebrania 7:1–6

Ukuhani unaweza kutusaidia katika njia nyingi.

Waebrania 7:1–6 inaweza kutoa fursa ya kutambulisha kwa watoto baraka za ukuhani.

Shughuli Yamkini

  • Kwa ufupi elezea Ibrahamu alikuwa nani, na kisha tumia Waebrania 7:1–6 kufundisha kwamba Ibrahimu alilipa zaka kwa Melkizedeki (ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:36–40 [katika kiambatisho cha Biblia]). Eleza kwamba Melkizedeki alishikilia ukuhani, ambao ni nguvu ya Mungu, na Melkizedeki aliutumia kumbariki Ibrahimu. Watoto wanaweza kufurahia kuigiza hadithi kwa ‘vitu rahisi vya kubeba’ kama taji na bahasha ya zaka.

  • Waalike wenye ukuhani wa Haruni na wa Melkizedeki watembelee darasa na kuwaelezea watoto jinsi walivyotumia ukuhani kubariki wengine. Kisha waoneshe watoto picha tofauti za ibada za ukuhani (kwa mfano, ona Picha 103–8 katika Kitabu cha Sanaa za Injili). Wasaidie watoto kuamua ukuhani gani unahitajika kwa kila ibada na toa picha ile kwa mwenye ukuhani anayefaa kuishikilia.

Waebrania 11:1–32

Imani ni kusadiki katika mambo ambayo hatuwezi kuyaona.

Ingawa hatuwezi kuwaona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, sisi tunaweza kukuza imani yetu kwao na katika ahadi Zao tukifuata mifano ya watu walio waaminifu wanaoelezwa katika Waebrania 11.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya Yesu. Weka kote chumbani vitu kadhaa kuwakilisha “ushahidi” kwamba Yeye ni halisi hata kama hatuwezi kumwona (kama vile maandiko, picha ya Ono la Kwanza, na picha ya dunia). Waombe watoto kuonyesha vitu hivi, na kisha shiriki pamoja nao jinsi kila kitu kinavyotusaidia kuwa na imani kwamba Yesu yu hai.

  • Leta feni ya karatasi, na waache watoto kuchukua zamu kuhisi feni ikipuliza hewa kwenye nyuso zao. Wafundishe kwamba hatuwezi kuona hewa, lakini tunaweza kuihisi. Vilevile, hatuwezi kumwona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, lakini tunaweza kuhisi upendo wao na kuwa na imani kwamba Wao ni halisi.

  • Shiriki hadithi za mmoja au zaidi za watu waliotajwa katika Waebrania 11:4–32. Unaweza pia kupata hadithi za watu hawa katika Hadithi za Agano la Kale. Watu hawa walifanya nini kuonyesha walikuwa na imani katika kitu wasichoweza kukiona? Shiriki baadhi ya baraka ulizopokea kwa sababu ya imani yako.

Waebrania 13:5–6

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo watatusaidia sisi na kamwe hawatatuacha.

Ni majaribu gani watoto wanaweza kuwa wanayapitia? Ni kwa jinsi gani ujumbe wa Waebrania 13:5–6 unaweza kuwasaidia wao?

Shughuli Yamkini

  • Rudia tena baadhi ya hadithi za Agano Jipya ambazo watoto wamejifunza mwaka huu ambapo Mwokozi aliwasaidia wengine, kama vile wakati alipomponya mtu wenye kifafa (ona Luka 5:18–26) au kuwalisha watu 5,000 (ona Mathayo 14:15–21). Wasaidie watoto kujifunza kirai “Bwana ndiye anisaidiaye” (Waebrania 13:6).

  • Waalike watoto kuchora picha ya wakati mtu alipowafariji walipokuwa wakiogopa. Wasomee wao Waebrania 13:5–6, na kushuhudia kwamba Baba wa Mbinguni atatusaidia na kamwe hatatuacha. Wasaidie watoto kukata karatasi zenye umbo la moyo mkubwa kutosha kufunika michoro. Ni vitu gani vingine ambavyo vinatusaidia kuhisi kuwa karibu zaidi na Baba wa Mbinguni? Andika baadhi ya mambo haya juu ya huo mioyo.

  • Fundisha watoto wimbo kuhusu jinsi Baba wa Mbinguni na Yesu wanavyotupenda na kutusaidia, kama vile “Tell Me, Dear Lord” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 176). Tunawezaje kujua kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wako karibu nasi? Zungumzia kuhusu wakati ambapo ulihisi “Bwana ndiye alikuwa msaidizi [wako wewe].

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Waebrania 7:1–4

Viongozi wa Kanisa wanamfuata Mwokozi.

Unawezaje kutumia mistari hii kuwasaidia watoto kuelewa kwamba wale walioitwa kuhudumu katika Kanisa la Bwana wanatakiwa wawe waaminifu na kuwahudumia wengine kama Yeye alivyofanya?

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kuorodhesha mambo wanayojua kuhusu viongozi wakuu wawili Ibrahimu na Melkizedeki. Wanaweza kupata msaada katika Waebrania 7:1–4; Ibrahimu 1:1–2; na Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:25–40 (katika kiambatisho cha Biblia). Ni sifa zipi za kama Kristo watu hawa wanazo ambazo ziliwasaidia kuuheshimu ukuhani?

  • Waombe watoto wasome Mathayo 7:1–2 na kutafuta vyeo vilivyotumika kumwelezea Melkizedeki. Je, ni kwa jinsi gani vyeo hivi vinatukumbusha juu ya Yesu Kristo. Wasaidie wao kufikiri juu ya njia ambazo Yesu alikuwa “Mfalme wa amani.” Waalike kuzungumzia kuhusu wenye ukuhani wengine ambao pia ni mfano wa kumfuata Mwokozi.

  • Shiriki uzoefu ambapo imani yako katika Mwokozi iliimarishwa kwa sababu ya huduma ya mwenye ukuhani aliye wenye haki. Wasaidie watoto kufikiri juu ya njia ambazo ukuhani amewabariki.

Waebrania 11

Baba wa Mbinguni huwapa thawabu wale walio na imani.

Waebrania 11 ina mifano mingi ya watu ambao walibarikiwa walipotenda kwa imani. Hadithi zipi zitawavutia zaidi au zenye msaada kwa watoto unaowafundisha?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kutengeneza orodha ubaoni ya mambo wanayojifunza kuhusu imani katika Waebrania 11:1–36. Mpe kila mmojawapo wa watoto jina la mtu fulani aliyetajwa katika Waebrania 11, na waalike wasome mistari inayohusiana na yule mtu. Waombe kushiriki vidokezo kuhusu yule mtu huyo ili kwamba watoto wengine waweze kukisia ni nani huyo. Watu hawa walionyeshaje imani, na jinsi gani Baba wa Mbinguni aliwatuza? (Kwa picha za watu hawa, ona sehemu ya Agano la Kale ya Kitabu cha sanaa za injili).

  • Baada ya kusoma kuhusu baadhi ya mifano ya uaminifu katika Waebrania 11, waombe watoto kuandika kuhusu mtu wanayemjua ambae alionesha imani. Waalike watoto kadhaa kushiriki mifano yao na darasa.

Waebrania 12:5–11

Bwana huwarudi wale anaowapenda.

Mistari hii inaweza kuwasaidia watoto kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni, wazazi wao, na wengine wanawakosoa kwa sababu wanawapenda na wanawataka wajifunze kutokana na makosa yao.

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Waebrania 12:5–11, na uwaombe watoto kutafuta kwa nini Baba wa Mbinguni anaturudi (anatukosoa au kututia nidhamu). Hii inatufundisha nini sisi kuhusu kwa nini wazazi wa duniani pia wanawakosoa watoto wao? Je, ni kwa jinsi gani tunapaswa kukubali ukosoaji wa upendo?

  • Shiriki mifano ya watu katika maandiko waliorudiwa na Bwana na wakatubu (kwa mfano, ona 1 Nefi 16:25–27; Etheri 2:13–15). Je, ni kwa jinsi gani wanakuwa mifano mizuri ya kanuni katika Waebrania 12:5–11?

  • Baada ya kusoma Waebrania 12:5–11, waalike watoto kuandika mambo machache watakayojaribu kukumbuka wakati wanakosolewa kwa ajili ya makosa yao.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto waandike au wachore picha ya kitu walichojifunza darasani. Wahimize kuitumia ili kushiriki walichojifunza pamoja na familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia kurasa za shughuli. Watoto wanapokamilisha kurasa za shughuli wakati wa darasa, tumia muda huo kupitia tena kanuni kutoka katika somo hili.