Agano Jipya 2023
Oktoba 30–Novemba 5 Waebrania 1–6: “Yesu Kristo, ‘Sababu ya Wokovu wa Milele’”


‘Oktoba 30–Novemba 5. Waebrania 1–6: ‘Yesu Kristo,”Sababu ya Wokovu wa Milele,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2021)

‘Oktoba 30–Novemba 5. Waebrania 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Kristo amesimama na msichana mdogo

Zeri ya Gileadi, na Annie Henrie

Oktoba 30–Novemba 5

Waebrania 1–6

Yesu Kristo, “Sababu ya Wokovu wa Milele”

Ni ukweli gani unaupata katika Waebrania 1–6 ambao unahisi kushawishika kuufundisha kwa watoto? Kuwa makini na ushawishi wa Roho ambao unakujia wakati unapojiandaa, na hakikisha unauandika chini.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Je, watoto walikubali mwaliko mwishoni mwa somo la wiki iliyopita la kutafuta mstari wa maandiko wanaoweza kushiriki? Kama ndivyo, wape muda wa kushiriki. Kama sivyo, wasaidie kufikiria kitu kingine walichojifunza kutoka maandiko hivi karibuni ili waweze kushiriki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Waebrania 1:1–10; 2:8–10, 17–18

Ninaamini katika Yesu Kristo.

Mistari hii inaweza kuwasaidia watoto kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo na kuimarisha uhusiano wao na Yeye.

Shughuli Yamkini

  • Pata baadhi ya kweli kuhusu Yesu Kristo katika Waebrania 1:1–10; 2:8–10, 17–18, na ziandike kwenye vipande vya karatasi. Ficha karatasi hizo humo chumbani na waalike watoto wazitafute. Wasaidie watoto kusoma ukweli ulioandikwa kwenye karatasi, na ongelea kuhusu kile kweli hizi humaanisha. Kama inahitajika, eleza kwamba Yesu Kristo anaitwa Mwana wa Mungu kwa sababu Baba wa Mbinguni ni baba wa vyote roho Yake na mwili Wake.

  • Nyanyua juu picha ya Mwokozi na kushiriki kwa nini unayo shukrani kwa ajili Yake. Mwache kila mtoto ashike picha na ashiriki kwa nini yeye anamshukuru kwa ajili ya Yesu Kristo.

Waebrania 3:8

Baba wa Mbinguni anatutaka “tusiifanye mioyo [yetu] kuwa migumu.”

Waebrania 3 inawaelezea Waisraeli wanaifanya mioyo yao kuwa migumu na kukataa baraka za Bwana. Na inaweza kuwa ni onyo kwetu sote tusiifanye mioyo yetu kuwa migumu.

Shughuli Yamkini

  • Leta darasani kitu chenye kufyonza (kama sponji au tambara) na kitu kilicho kigumu (kama jiwe). Waalike watoto kugusa vitu hivyo na kuelezea jinsi wanavyohisi juu ya hivyo vitu. Weka matone machache ya maji juu ya kila kitu, na onyesha kwamba maji yameingia ndani ya kitu chenye kufyonza maji kuliko ndani ya jiwe. Eleza kwamba mioyo yetu inahitajika iwe laini na sio migumu ili kwamba tuweze kukubali ukweli wa Baba wa Mbinguni na upendo Wake.

  • Kata umbo la moyo kutoka kwenye kitu laini, kama vile nguo, na kifaa kigumu, kama vile kadibodi. Jadili na watoto tofauti kati ya kuwa na moyo laini na kuwa na moyo mgumu. Shiriki baadhi ya mifano kutoka kwenye maandiko juu ya watu waliokuwa na mioyo laini au mioyo migumu kama vile Nefi, Lamani, na Lemueli (1 Nefi 2:16–19); Paulo (Matendo 9:1–22); au Joseph Smith (Joseph Smith—Historia ya 1:11–20). Unaposhiriki kila mfano, waalike watoto kuonyesha moyo laini au moyo mgumu.

Picha
Musa akimtawaza Haruni

Haruni alikuwa “ameitwa na Mungu” (Waebrania 5:4). Musa Anamwita Haruni kwenye Huduma, na Harry Anderson

Waebrania 5:4

Wenye Ukuhani wameitwa na Mungu.

Waebrania 5:4 ni mstari muhimu kwa sababu unaeleza wazi kwamba wenye ukuhani—na wengine wanaohudumu katika Kanisa—lazima waitwe na Mungu. Vivyo hivyo ni kweli juu ya kila mtu aliyeitwa kuhudumu katika Kanisa la Bwana.

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto Waebrania 5:4. Muombe mwenye ukuhani kuelezea ukuhani ni nini. Angeweza pia kushiriki jinsi anavyowatumikia wengine anapotimiza wajibu wake. Pia mwombe dada katika kata kushiriki uzoefu wake akiwa anasimikwa katika wito katika Kanisa. Mhimize kuelezea jinsi Bwana alivyombariki kuwa na nguvu za kutimiza wito wake.

  • Wasaidie watoto kukariri virai kutoka kwenye makala ya tano ya imani. Toa ushuhuda wako kwamba watu wanaoitwa kufanya kazi ya Mungu wanaitwa na Mungu kwa njia ya ufunuo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Waebrania 1:1–10; 2:8–10, 17–18

Ninaamini katika Yesu Kristo.

Waraka wa Waebrania uliandikwa ili kuimarisha imani ya Watakatifu Waebrania katika Yesu Kristo. Inaweza kufanya vivyo hivyo kwa watoto unaowafundisha.

Shughuli Yamkini

  • Mpangie kila mtoto mistari michache katika Waebrania 1:1–10; 2:8–10, 17–18, na waalike watoto kutafuta kweli katika mistari hiyo kuhusu Yesu Kristo. Waache washiriki au kuandika ubaoni kile wanachokipata. Je, ni kitu gani kingine tunachokijua kuhusu Yesu Kristo? Watoto wanaweza kupata baadhi ya mawazo kutoka katika nyimbo kama vile “I Know That My Redeemer Lives” (Nyimboi, na.136) au “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35).

  • Waalike wanafunzi kuchora picha zao wenyewe wakiwa pamoja na wazazi wao. Waombe kushiriki kile walichonacho cha kufanana wao na wazazi wao. Eleza kwamba wakati Waebrania 1:3 inasema kwamba Yesu Kristo ni “sura halisi ya [Mungu] mwenyewe,” ina maana kwamba Yesu na Baba wa Mbinguni wana tabia na sifa zilezile. Zungumza na watoto kuhusu jinsi kumfuata Yesu Kristo kunavyotuleta karibu na Baba wa Mbinguni.

Waebrania 3:7–19

Ili kupokea mwongozo na baraka za Baba wa Mbinguni, lazima “tusiifanye mioyo [yetu] kuwa migumu.”

Katika Waebrania 3, hadithi ya Waisraeli nyikani inatumika katika kufundisha umuhimu wa kutoifanya migumu mioyo yetu. Je, unawezaje kutumia hadithi hii ili kuwafundisha watoto katika darasa lako kanuni hii?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wafikirie juu ya vitu ambavyo ni vigumu na vilivyo laini (Kama inawezekana, leta mifano ya kuwaonyesha.) Someni pamoja Waebrania 3:8. Je, inamaanisha nini kuwa na moyo mgumu? Je, ni kwa nini Mungu anatutaka tuwe na mioyo laini?

  • Katika maneno yako mwenyewe, simulia hadithi ya Waisraeli wakiifanya mioyo yao kuwa migumu dhidi ya Bwana huko nyikani (ona Hesabu 14:1–12; Waebrania 3:7–19). Acha watoto waigize hadithi hii. Je, ni nini kitatokea kama tutaifanya mioyo yetu kuwa migumu dhidi ya Bwana na injili Yake?

  • Waalike watoto wasome Mathayo 13:15; Waebrania 3:15; Mosia 11:29; na Musa 6:27. Waombe wachore ubaoni sehemu zilizotajwa katika mistari hii. Inamaanisha nini kuwa kiroho na masiko mazito, upofu wa macho, na mioyo migumu? Je, sisi tunawezaje kuhakikisha kwamba masikio yetu, macho, na mioyo viko tayari kutambua sauti ya Roho?

Waebrania 5:1–4

Wenye Ukuhani wameitwa na Mungu.

Waebrania 5 inatoa fursa ya kujadili ukuhani ni nini—ni uwezo na mamlaka ya kutenda katika jina la Mungu—na jinsi unavyopokelewa.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha Musa Anampa Haruni Ukuhani (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.15) wakati mtoto akisoma Waebrania 5:4. Eleza kwamba Ukuhani wa Haruni ulipewa jina la Haruni. Wasaidie watoto wafikirie kazi zinazofanywa na wenye ukuhani wa Haruni (kama vile kubatiza, kubariki na kupitisha sakramenti, na kuwaalika wengine kuja kwa Kristo; Mafundisho na Maagano 20:46–48, 59).

  • Wasaidie watoto kufikiria kuhusu njia tofauti ambazo watu hupokea mamlaka. Kwa mfano, jinsi gani mwalimu, daktari, au kiongozi wa kisiasa wanavyopokea mamlaka? Je, ni kwa jinsi gani Mungu anatoa mamlaka Yake? Waalike watoto kufikiria kuhusu swali hili wanapokuwa wanasoma Waebrania 5:4 na makala ya tano ya imani. Wasaidie watoto kuwafikiria watu katika kata walio na mamlaka kutoka kwa Mungu—ikijumuisha wenye ukuhani, vile vile wanaume na wanawake ambao wamesimikwa kuhudumu katika miito maalumu.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki andiko, wimbo, au shughuli waliyojifunza darasani leo pamoja na familia zao wakati wa jioni ya familia nyumbani.

Kuboresha Mafundisho yetu

Watoto wanaweza kutambua ushawishi wa Roho. Wafundishe watoto kwamba hisia za amani, upendo, na utulivu walionao wakati wanapoongea au kuimba kuhusu Yesu Kristo na injili Yake zinatoka kwa Roho Mtakatifu.

Chapisha