Agano la Kale 2022
Wewe ni Mwalimu wa Watoto


“Wewe ni Mwalimu wa Watoto,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Wewe ni Mwalimu wa Watoto,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Yesu amembeba mtoto

Wewe ni Mwalimu wa Watoto

Umeitwa na Mungu kufundisha watoto Wake katika njia ya Mwokozi. Umesimikwa katika wito huu kwa mamlaka ya ukuhani Wake mtakatifu. Hata kama wewe sio mwalimu mwenye uzoefu, unapoishi kwa kustahili, kusali kila siku, na kujifunza maandiko, Baba wa Mbinguni atakuzawadia ushawishi na nguvu za Roho Mtakatifu ili kukusaidia kufanikiwa (ona 2 Nefi 33:1).

Wale waliowekwa chini ya uangalizi wako ni watoto wa Baba wa Mbinguni, na Yeye anajua kile wanachohitaji na jinsi ya kuwafikia vizuri zaidi. Kupitia Roho Mtakatifu, Mungu atakuongoza wakati wa maandalizi yako na wakati unapofundisha. Atakufunulia kile unachopaswa kusema na unachopaswa kufanya (ona 2 Nefi 32:5).

Dhumuni kuu la kufundisha na kujifunza injili ni kuongeza uongofu kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Lengo lako kama mwalimu ni kuwasaidia wale unaowafundisha kufanya kila wawezalo kuwa waongofu zaidi—juhudi ambayo inaenda zaidi ya muda wa darasani. Waalike wale unaowafundisha kushiriki kwa dhati katika kujifunza kuhusu Yesu Kristo na injili Yake na kutenda juu ya yale wanayojifunza. Wahimize kufanya kujifunza kwao binafsi na kama familia nje ya darasa kuwa kiini cha msingi wa kujifunza kwao injili. Wanapotenda kwa imani kwa kujifunza kama watu binafsi na familia, watamwalika Roho katika maisha yao na ni Roho ndiye aletaye uongofu wa kweli. Kila kitu ufanyacho kama mwalimu hakina budi kuelekeza katika dhumuni hili takatifu.

Fundisha mafundisho pekee ya injili ya urejesho ya Yesu Kristo kama yanavyopatikana katika maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho. Mafundisho safi—ya milele, ukweli usiobadilika uliofundishwa na Mungu na watumishi Wake—humwalika Roho na una uwezo wa kubadili maisha ya watu.

Wito wa kufundisha ni wajibu mtakatifu, na ni kawaida kuhisi kuzidiwa wakati mwingine. Lakini kumbuka kwamba Baba yako wa Mbinguni amekuita, na Yeye hatakuacha kamwe. Hii ni kazi ya Bwana na unapohudumu “kwa moyo wako wote, uwezo, akili na nguvu” (Mafundisho na Maagano 4:2), Yeye ataongeza uwezo, karama na vipaji vyako na huduma yako itabariki maisha ya wale unaowafundisha.

Chapisha