Agano la Kale 2022
Nyenzo za Ziada kwa ajili ya Kufundishia Watoto


“Nyenzo za Ziada kwa ajili ya Kufundisha Watoto,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Nyenzo za Ziada kwa ajili ya Kufundishia Watoto” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
mwalimu na watoto wadogo katika darasa la kanisa

Nyenzo za Ziada kwa ajili ya Kufundishia Watoto

Nyenzo hizi zinaweza kupatikana katika aplikesheni ya Maktaba ya Injili na kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia

Unaweza kutohoa na kutumia shughuli kutoka Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa ajili ya matumizi katika darasa lako la Msingi. Usihofu kama watoto tayari wamekwisha fanya shughuli hizi pamoja na familia zao nyumbani; marudio husaidia watoto kujifunza. Watoto wanaweza kuhitaji kukuambia jinsi walivyofanya shughuli pamoja na familia zao na kile walichojifunza.

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Muziki mtakatifu humwalika Roho na hufundisha injili katika njia ya kukumbukwa. Katika kuongezea kwenye kutumia toleo lililochapishwa la Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi za sauti na video za nyimbo nyingi za kanisa na nyimbo za watoto kwenye music.ChurchofJesusChrist.org na katika aplikesheni za Sacred Music na Gospel Media.

Kwa ajili ya mawazo mengine, angalia sehemu za “Kutumia Muziki ili Kufundisha Mafundisho” na “Kuwasaidia Watoto Kujifunza na Kukumbuka Nyimbo za Msingi pamoja na Nyimbo za Kanisa” katika “Maelekezo kwa Ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto ya Muziki wa Sakramenti” ndani ya nyenzo hii.

Behold Your Little Ones

Nyingi kati ya mada zilizotajwa katika kitabu cha kiada cha Behold Your Little Ones: Nursery Manual ni sawa na zile utakazofundisha katika Msingi. Hususani kama unafundisha watoto wadogo, fikiria kuangalia katika kitabu cha kiada cha chekechea kwa ajili ya nyimbo za ziada, hadithi, shughuli, na sanaa na kazi za mikono.

Gazeti la Rafiki

Gazeti la Rafiki hutoa hadithi na shughuli ambazo zinaweza kuwa nyongeza ya kanuni unazofundisha kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Hadithi za Agano la Kale

Hadithi za Agano la Kale zinaweza kuwasaidia watoto kujifunza mafundisho na hadithi zilizopatikana katika Agano la Kale. Unaweza pia kupata video za hadithi hizi katika aplikesheni ya Gospel Library na kwenye MediaLibrary.ChurchofJesusChrist.or.

Kitabu Cha Kupaka Rangi cha Hadithi za Maandiko—Agano la Kale

Nyenzo hii ina kurasa za shughuli ya kuburudisha ya kupaka rangi iliyokusudiwa kuongeza kujifunza kwa watoto kutoka kwenye Agano la Kale.

Video na sanaa

Sanaa za kuchora, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa mafundisho na kupata taswira ya hadithi zinazohusiana na maandiko. Tembelea Gospel Media kwenye MediaLibrary.ChurchofJesusChrist.org ili kupitia pitia mkusanyiko wa nyenzo za habari za Kanisa. Gospel Media pia inapatikana kama aplikesheni ya simu ya mkononi. Picha nyingi ambazo unaweza kutumia katika darasa zinapatikana katika Kitabu cha Sanaa ya Injili.

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi inaweza kukusaida kujifunza kuhusu, na kutumia kanuni za kufundisha kama Kristo. Kanuni hizi zinajadiliwa na kutumiwa katika mikutano ya baraza la mwalimu.

Chapisha