Agano la Kale 2022
Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi


“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi,Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi,Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
watoto katika darasa la kanisa

Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi

Kujiandaa Kufundisha katika Msingi

Kujifunza binafsi na kifamilia nyumbani kunapaswa kuwa kitovu cha kujifunza injili. Hii ni kweli kwako na kwa watoto unaowafundisha. Unapojiandaa kufundisha, anza kwa kuwa na uzoefu wako mwenyewe katika maandiko. Maandalizi yako muhimu zaidi yatatokea wakati unapopekua maandiko na kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu.

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia pia ni sehemu muhimu kwa kujifunza kwako binafsi na maandalizi yako ya kufundisha. Itakusaidia kupata ufahamu wa kina zaidi wa kanuni za mafundisho zinazopatikana katika maandiko.

Wakati wa maandalizi yako, mawazo na misukumo itakujia kuhusu watoto unaowafundisha. Utapokea utambuzi juu ya jinsi kanuni katika maandiko zitakavyobariki maisha yao. Utaongozwa ili uwahamasishe kugundua kanuni hizo wakati wanapojifunza kutoka katika maandiko wao wenyewe na pamoja na familia zao.

Mawazo ya Kufundisha

Unapojiandaa kufundisha, unaweza kupata mwongozo wa ziada kwa kuchunguza mihutasari ya kufundishia katika nyenzo hii. Usifikirie mawazo haya kama maelekezo ya hatua kwa hatua lakini badala yake kama mapendekezo ya kuchochea kupata mwongozo wako mwenyewe. Unawajua watoto hawa—na utapata kuwajua hata vizuri zaidi pale unapochangamana nao darasani. Bwana anawajua pia, na Atakuongoza kwa njia bora za kuwafundisha na kuwabariki watoto.

Nyenzo zingine nyingi zinapatikana kwa ajili yako ili kuweza kutumia wakati unapojiandaa, ikiwa ni pamoja na mawazo katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na magazeti ya Kanisa. Kwa maelezo zaidi kuhusu nyenzo hizi na zingine, ona “Nyenzo za Ziada za Kufundishia Watoto” katika nyenzo hii.

Picha
mtu akijifunza maandiko nyumbani

Baadhi ya Vitu vya Kukumbuka

  • Kila mara unapokutana na watoto, fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia wahisi upendo wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu.

  • Wazazi wana jukumu la muhimu la kuwafundisha watoto wao. Kama mwalimu, una jukumu muhimu la kusaidia, kuhimiza, na kujenga juu ya kujifunza injili nyumbani. Kuwa mwangalifu kwa watoto ambao wazazi wao hawafundishi injili nyumbani mwao. Jumuisha watoto wote katika majadiliano ya injili, bila kujali mazingira yao ya nyumbani.

  • Kuelewa mafundisho katika Agano la Kale kunaweza kuwa rahisi zaidi kwa watoto wanapokuwa wanajua muktadha wa kihistoria wa mafundisho hayo. Unaweza kupata muktadha wa kihistoria katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na Hadithi za Agano la Kale.

  • Kurudia rudia ni vyema. Watoto hujifunza ukweli wa injili kwa ufanisi zaidi wakati ukweli huo unapofundishwa kwa kurudiwa rudiwa kupitia shughuli mbalimbali. Ikiwa unaona kuwa shughuli ya kujifunza inafaa kwa watoto, fikiria kuirudia, hasa ikiwa unafundisha watoto wadogo zaidi. Unaweza pia kurejelea tena shughuli kutoka kwenye somo lililopita.

  • Baba wa Mbinguni anataka wewe ufanikiwe kama mwalimu. Ametoa nyenzo nyingi ili kukusaidia, ikiwa ni pamoja na mikutano ya baraza la walimu. Katika mikutano hii unaweza kushauriana na walimu wengine kuhusu changamoto zinazokukabili. Unaweza pia kujadili na kufanyia mazoezi kanuni za kufundisha kama Kristo.

  • Kama unafundisha watoto wadogo na unahitaji msaada wa ziada, ona “Kukidhi Mahitaji ya Watoto Wadogo” katika nyenzo hii.

  • Nyenzo hii inajumuisha mihutasari ya kila wiki ya mwaka mzima. Katika Jumapili ambazo darasa la Msingi halipo kwa sababu ya mkutano mkuu, mkutano wa kigingi au sababu nyingine yoyote, familia zinapaswa kuendelea kusoma Agano la Kale nyumbani kulingana na ratiba iliyooneshwa. Usiogope kuhusu masomo uliyokosa; fundisha muhtasari uliopangwa kila wiki.

Chapisha