Njoo, Unifuate
Februari 10–16. 2 Nefi 6–10: “Ee Jinsi Gani Ulivyo Mkuu Mpango wa Mungu Wetu”


“Februari 10–16. 2 Nefi 6–10: ‘Ee Jinsi Gani Ulivyo Mkuu Mpango wa Mungu Wetu ’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Februari 10–16. 2 Nefi 6–10,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Yesu Akisali katika Gethsemane

Sio Mapenzi Yangu, Bali Yako,Yafanyike na Harry Anderson

Februari 10–16

2 Nefi 6–10

Ee Jinsi Gani Ulivyo Mkuu Mpango wa Mungu Wetu!

Njia mzuri ya kujitayarisha mwenyewe kufundisha ni kwanza kusoma 2 Nefi 6–10 kwa ajili yako mwenyewe. Andika misukumo unayopokea, na tumia muhtasari huu kutafuta umaizi wa ziada na mawazo ya kufundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni kushiriki

Alika Kushiriki

Yakobo aliwafundisha watu wake kwamba mafundisho ya Isaya “yanaweza kufananishwa na nyinyi”2 Nefi 5:6). Unaweza kuanza kwa kuwataka washiriki wa darasa kushiriki chochote cha mafundisho ya Yakobo katika 2 Nefi 6–10 ambacho wanahisi kinaweza kufananisha na maisha yao. Wanaweza kuelezea kwa nini wanaona mafundisho yana maana.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

2 Nefi 6–8

Bwana ni mwenye huruma kwa watu Wake na atatimiza ahadi Zake.

  • Kutoa kiasi cha muktadha kwa jumbe za 2 Nefi 6–8, inaweza kuwa msaada kwa darasa lako kutengeneza utaratibu wa matukio yaliyoelezwa katika 2 Nefi 6:8–15. Matukio haya yanatoa ushauri gani kuhusu Bwana na hisia Zake kwa watu Wake? (Ona pia 2 Nefi 7:1–3; 8:3). Unaweza kutaka kuelezea kwamba kama washiriki wa Kanisa, sisi ni watu wa agano wa Mungu hivi leo, na tunakusanywa kutoka ulimwenguni kwenda kwenye usalama wa injili. Sura hizi zina jumbe gani kwa ajili yetu sasa?

2 Nefi 9

Kupitia kwa Upatanisho Wake, Yesu Kristo anakomboa watu wote kutokana na kifo cha kimwili na kiroho cha roho.

  • Njia mojawapo ya kuongeza shukrani zetu kwa Upatanisho wa Yesu Kristo ni kufikiria kuhusu nini kingetokea kwetu bila Upatanisho. Washiriki wa darasa wanaweza kutafakari vitu hivi wanapojifunza 2 Nefi 9. Unaweza kuwataka washiriki wa darasa kuanza kwa kujifunza mistari 4–9 na kisha kuorodhesha ubaoni nini kingeweza kutokea bila Upatanisho wa Kristo. Kulingana na mistari 10–14, jinsi gani Mwokozi alituokoa kutoka maangamizi haya? Ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland katika “Nyenzo za Ziada” unaweza kusaidia darasa lako kuelewa hitaji letu la Upatanisho wa Yesu Kristo. Unaweza pia kuonesha video yenye msingi wa ujumbe wake—“Where Justice, Love, and Mercy Meet” (ChurchofJesusChrist.org). Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki mawazo yoyote au hisia kwamba ujumbe wa Mzee Holland unavutia kuhusu Mwokozi.

  • Watake washiriki wa darasa kufikiria jinsi watakavyoelezea upatanisho wa Yesu Kristo kwa mtu fulani ambaye hajui ni nini au kwa nini ni muhimu. Kweli zinazopatikana katika 2 Nefi 9 zinaweza kusaidia kuwatayarisha washiriki wa darasa kwa mazungumzo kama haya. Labda wanaweza kuchunguza mistari 4–12, wakitafuta jinsi upatanisho wa Mwokozi unashinda kifo cha mwili na kiroho. Kutokana na kile tunachojifunza kutoka maandiko haya, kwa nini dhabihu ya Mwokozi inaitwa “upatanisho usio na mwisho”? (2 Nefi 9:7).

  • Yakobo aliingiwa na staha kwa mpango wa Mungu wa wokovu kiasi kwamba alielekezwa kutamka kwa mshangao “Ee jinsi gani ulivyo mkuu” na “Ee ukuu” wakati alipoelezea mpango. Kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa vizuri zaidi hisia hizi kwa Mwokozi na Upatanisho wake, fikiria kuwataka kuchambua 2 Nefi 9 kwani matamko ya Yakobo (mengi yake yanapatikana katika mistari 8–20). Mistari hii inafundisha nini kuhusu Mungu na mpango Wake? Ni uzoefu gani umetusaidia kuhisi kile Yakobo alihisi kuhusu mpango wa Mungu kwa ajili ya watoto wake? Mnaweza pia kuimba wimbo kuhusu ukuu wa Mungu, kama vile “How Great Thou Art” (Nyimbo, na. 86), kuimarisha majadiliano haya.

2 Nephi 9:27–54

Tunaweza kuja kwa Kristo na kupokea baraka tukufu za Upatanisho Wake.

  • Unaweza kuanza kujadili juu ya mafundisho ya Yakobo katika mistari hii kwa kuwataka washiriki wa darasa kufikiria jinsi ya kumtaka mtu fulani kutubu na kuja kwa Kristo. Yakobo aliwezaje kufanya hivi katika 2 Nefi 9:50–53? Ni baraka gani alizosema zitatujia katika maisha yetu tunapokubali mialiko hii?

  • Katika 2 Nefi 9, Yakobo alitumia vishazi viwili vyenye nguvu na vinavyotofautiana: “mpango wa huruma wa Muumbaji mkuu” na “mpango ule wa hila wa yule mwovu” (2 Nefi 9:6 28). Kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kutoka tofauti hizi, unaweza kuchora njia ubaoni na kuiwekea alama Mpango wa Baba wa Mbinguni. Watake washiriki wa darasa kuchambua 2 Nefi 9:27–52, wakitafuta ushauri Yakobo alitoa kutusaidia kufuata mpango wa Baba wa Mbinguni. Watake waandike kile wanachokipata karibu na njia. Yakobo alifundisha nini kuhusu jinsi Shetani anavyotuvuta mbali kutoka mpango wa Baba yetu wa Mbinguni? Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu wapi kufuata mpango wa Baba yetu wa Mbinguni utatupeleka na wapi kumfuata Shetani atatupeleka? (Ona 2 Nefi 9:9, 18.) Kulingana na mistari hii, tunaweza kufanya nini tufuate kikamilifu zaidi mpango wa Baba yetu wa Mbinguni?

  • Katika 2 Nefi 9:28–38, Yakobo alionya dhidi ya baadhi ya fikra na tabia ambazo zinatuzuia kufuata mpango wa Mungu kwetu. Fikiria kuwataka washiriki wa darasa kuzitafuta. Ni misimamo na tabia zipi zinaonekana hususani kuenea leo? Nini inazifanya ziwe hatari sana? Tunajifunza nini kutoka 2 Nefi 9:50–53 kuhusu jinsi ya kuepuka hatari hizi?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kuwasaidia washiriki wa darasa kujihisi kujiamini kuhusu kusoma maandiko ya Isaya yaliyonukuliwa na Nefi katika 2 Nefi 11–24, unaweza kuwaeleza kwamba Nefi aliyaweka ndani ya maandiko haya kuimarisha imani ya watu wake katika Yesu Kristo. Watake washiriki wa darasa kutazamia usomaji wa wiki ijayo kama nafasi ya kujenga imani yao wenyewe Kwake.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Hitaji letu la Mwokozi

Mzee Jeffrey R. Holland alisimulia hadithi ya mpanda milima aliyekuwa akinin’ginia kwa hatari kwenye ukingo wa korongo ulioinuka ghafla, bila chochote cha kumzuia asianguke na kufa. Wakati ambapo mshiko wake ulipoanza kuteleza kwenye uso wa mchanga wa mwamba, alihisi mikono wa ndugu yake mdogo ikishika viganja vyake na kumvuta kwenye usalama. Mzee Holland alifananisha uzoefu wa mpandaji na hali yetu katika ulimwengu huu ulioanguka:

“Kulikuwa na Adamu na Hawa halisi ambao walianguka kutoka Edeni halisi, pamoja na matokeo yote anguko lile yaliyochokuliwa pamoja nalo. … Kwa sababu hiyo basi tunazaliwa katika dunia iliyoanguka na kwa sababu nasi pia tungevunja sheria za Mungu, nasi pia tulihukumiwa katika adhabu ambazo Adamu na Hawa walikuwa wanakabiliwa nazo.

Ni taabu ya jinsi gani! Wanadamu wote wakiwa katika kuanguka kusikozuilika—kila mwanaume, mwanamke, na mtoto, wote wakiwa ndani ya mporomoko kwa vurumai kwenye kifo cha kudumu, kiroho wakitumbukia kwenye machungu ya milele. Je, hivyo ndivyo maisha yalitakiwa yawe? Je, haya ndiyo matokeo ya mwisho ya uzoefu wa mwanadamu? Sisi sote tunaning’inia kwenye korongo baridi katika sehemu fulani ya ulimwengu usiojali, kila mmoja wetu akitafuta sehemu ya kushikilia, kila mmoja wetu akitafuta kitu chochote cha kushikilia—bila chochote isipokuwa hisia ya mchanga ukiteleza chini ya vidole vyetu, bila cha kutuokoa, bila cha kushikilia, na kwa hakika bila chochote cha kutushikilia sisi? …

Jibu kwa maswali haya ni la hasha, ya milele bila kusita! … Upatanisho huo ungefanikisha ushindi kamili dhidi ya kifo cha mwili, na kutoa bila masharti uwezo wa kufufuka kwa kila mtu aliyezaliwa na yule atakayezaliwa katika ulimwengu huu. Kwa rehema pia utatoa msamaha wa dhambi binafsi kwa watu wote kutoka kwa Adamu hata mwisho wa ulimwengu, kwa masharti ya toba na utii kwa amri takatifu” (“Where Justice,Love, and Mercy Meet,” Ensign au Liahona, Mei 2015, 105–6).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa ushuhuda wako kila mara. Ushahidi wako rahisi, wa kweli kuhusu ukweli wa kiroho unaweza kuwa na ushawishi wenye nguvu kwa wale unaowafundisha. Hauhitaji kuwa wa kushawishi au mrefu. Fikiria kushiriki ushahidi wako binafsi wa Mwokozi unapojadili 2 Nefi 9.

Chapisha