Njoo, Unifuate
Februari 3–9. 2 Nefi 1–5: “Tuliishi kwa Furaha”


“Februari 3–9. 2 Nefi 1–5: ‘Tuliishi kwa Furaha,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020.)

“Februari 3–9. 2 Nefi 1–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Adamu na Hawa wakiondoka katika Bustani ya Edeni

Adamu na Hawa, na Douglas Fryer

Februari 3–9

2 Nefi 1–5

“Tuliishi Kwa Furaha”

Anza maandalizi yako ya kiroho kwa kusoma 2 Nefi 1–5 na kurekodi misukumo yako. Kuna kanuni zaidi katika sura hizi kuliko ulivyo na muda kujadili katika kipindi kimoja cha darasa, kwa hiyo mfuate Roho katika maandalizi yako na kuzingatia umaizi ulioshirikiwa na washiriki wa darasa kukusaidia kuamua kanuni gani za kulenga na jinsi ya kuongoza mazungumzo.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni kushiriki

Alika Kushiriki

Inawezekana kwamba washiriki wa darasa lako wameweka alama au angalizo angalau mstari mmoja katika 2 Nefi 1–5. Kwa kuanza darasa, unaweza kuwataka washiriki wa darasa kushiriki mistari ambayo ilikuwa yenye maana kwao. Litake darasa kufanya muhtasari wa kanuni ya kimafundisho wanayojifunza kutoka mistari waliyoshiriki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

2 Nephi 2:11–30

Tuko huru kujitendea wenyewe.

  • Mara kwa mara, watu hutumia uhuru wao wa kuchagua kusababisha mateso mengi kwa wengine. Kwa nini uhuru wa kuchagua ni muhimu kwa Baba wa Mbinguni? Pengine unaweza kuandika swali hili ubaoni, na washiriki wa darasa wanaweza kutafuta majibu katika 2 Nefi 2:11–30 na andika majibu yao ubaoni. Je, ni kwa namna gani adui anajaribu kudhoofisha uhuru wetu wa kuchagua? Je, ni kwa namna gani Mwokozi anatusaidia “kuchagua uhuru na maisha ya milele”? (2 Nefi 2:27) Fikiria kuimba pamoja wimbo kuhusu uhuru wa kuchagua, kama vile “Know This, That Every Soul is Free” (Nyimbo, na. 240), na watake washiriki wa darasa waongeze kwenye orodha yao utambuzi mwingine wanaoupata kutoka kwenye wimbo

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unatambua hali nne muhimu ambazo zinafanya uhuru wa kuchagua kuwezekana. Hapa ni moja wapo ya njia unayoweza kuijenga kwenye kile washiriki wa darasa waliweza kujifunza nyumbani: Andika hali hizo ubaoni. Kisha watake washiriki wa darasa kushiriki kauli kutoka 2 Nefi 2 ambazo zinafundisha kwa nini hali hizi ni muhimu kufikia kuweza kuwa na utakatifu wetu.

2 Nephi 2:15–29

Anguko na Upatanisho wa Yesu Kristo ni sehemu muhimu za mpango wa Baba wa Mbinguni.

  • Wakristo wengi wanaamini kwamba anguko lilikuwa ni tanzia na kwamba Hawa alifanya kosa baya. Mistari hii katika 2 Nefi 2 inabainisha kweli kuhusu anguko la Adamu na Hawa, na inashuhudia kwamba Yesu Kristo anatukomboa kutoka kwenye Anguko. Njia moja ya kujadili mawazo haya ni kuwataka washiriki wa darasa kuchunguza 2 Nefi 2:15–25 na kutengeneza orodha ya kweli wanazojifunza kuhusu nini kilichotokea katika Bustani ya Edeni. Ni umaizi gani mwingine wanaoupata katika nukuu kutoka Rais Dallin H. Oaks katika “Nyenzo za Ziada”? Jinsi gani Yesu Kristo alitukomboa kutoka kwenye Anguko? (Ona 2  Nefi 2:6–8, 26–29.

  • Baada ya kufanya shughuli kama iliyopita, unaweza kuonesha maswali kadhaa kama yafuatayo na watake washiriki wa darasa kushiriki umaizi wao:

    • Jinsi gani mafundisho ya Lehi katika mistari hii yanaunganisha baadhi ya sintofahamu kuhusu Anguko?

    • Ni kwa njia zipi Anguko ni baraka?

    • Kuelewa Anguko kiusahihi kunatusaidiaje kuelewa vyema haja yetu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake?

    • Nini ni sababu moja wewe una shukrani kwa uchaguzi wa Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni?

    • Jinsi gani uamuzi wako kuja duniani unafanana na uamuzi wa Adamu na Hawa kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na uovu?

    • Je, Madhumuni ya maisha ni nini? Kwa nini Anguko lilikuwa muhimu kufanikisha azma hii?

2 Nephi 4:15–35

Tunaweza kumgeukia Mungu katika udhaifu wetu.

  • Maandiko ya Nefi katika 2 Nefi 4:15–35 yanaweza kutuletea matumaini na faraja tunapohisi kuzidiwa na mapambano na udhaifu wetu. Pengine washiriki wa darasa wanaweza kurejea mistari hii katika jozi na kutafuta vifungu ambavyo wanaweza kutumia kumfariji mtu fulani anayehisi kuzidiwa na mzigo wa mateso yake. Kisha kila jozi linaweza kushiriki vifungu hivi pamoja na darasa. Labda mtu fulani katika darasa anaweza kushiriki uzoefu ambao yeye alipata faraja kwa kumgeukia Mungu, kama alivyofanya Nefi.

  • Njia ingine ya kurejea 2 Nefi 4 inaweza kuwa kuwataka washiriki wachache wa darasa kabla ya muda kuja wamejiandaa kushiriki mistari na vishazi kutoka sura hii ambavyo vilikuwa na maana kwao. Waombe kushiriki kile wanachofanya wakati wanapohisi kuzidiwa na udhaifu wao. Wimbo kuhusu faraja na matumaini, kama vile “Where Can I Turn For Peace?” (Nyimbo, na. 129), inaweza kuongezwa katika majadiliano haya. Kwa mfano, washiriki wa darasa wanaweza kushiriki jinsi wimbo unaimarisha mfano wa Nefi wa kumtegemea Bwana katika wakati wa kukata tamaa.

2 Nefi 5

Furaha inapatikana katika kuishi injili.

  • Licha ya changamoto Nefi na watu wake zilizowakabili, waliweza kuijenga jamii kwenye msingi wa kanuni ambazo zinaongoza kwenye furaha. Ni kanuni gani walizozipata washiriki wa darasa katika mafunzo yao ya 2 Nefi 5 ambazo zilichangia kwenye furaha iliyowapa uzoefu Wanefi? Unaweza kutoa kipande cha karatasi kwa washiriki wa darasa na watake kuchunguza 2 Nefi 5 kanuni ambazo zinazongoza kwenye furaha na ziandike. Jinsi gani njia ambazo ulimwengu unatafuta furaha ni tofauti kutoka kile tunachopata katika 2 Nefi 5? Ni malengo gani washiriki wa darasa wanaweza kuweka kutumia mojawapo ya kanuni hizi?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waambie washiriki wa darasa kwamba 2 Nefi 6–10 ina mojawapo ya mahubiri mazuri sana kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo katika maandiko yote. Unaweza pia kushiriki mstari unaoupata katika sura hizi ambao unakufanya usisimke kuusoma.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Anguko lilikuwa sehemu ya mpango wa Mungu.

Rais Dallin H. Oaks alifundisha:

“Wakati Adamu na Hawa walipopokea amri ya kwanza, walikuwa kwenye hali ya mpito, hawapo tena katika ulimwengu wa kiroho bali wakiwa na miili ya asili bado haijatawaliwa na kifo na bado hawana uwezo wa kuzaa. Hawakuweza kutimiza amri ya kwanza ya Baba bila kuvunja kizuizi kati ya furaha kamili ya Bustani ya Edeni na majaribu ya kutisha na nafasi za ajabu za maisha ya kufa. …

“… Nabii Lehi alieleza kwamba ‘Kama Adamu hangevunja sheria hangeanguka’ (2 Ne. 2:22). Bali angebaki katika hali ileile ambayo alikuwa ameumbwa.

“… Anguko lilipangwa, Lehi anahitimisha, kwa sababu ‘vitu vyote vimetendwa kwa hekima ya yule ajuae vitu vyote’ (2 Ne. 2:24).

“Ilikuwa Hawa aliyevunja sheria ya mipaka ya Edeni kwanza ili kuanzisha hali za maisha ya kufa. Kitendo chake, vyovyote vile asili yake, ilikuwa hapo mwanzo ni uvunjaji wa sheria lakini daima ni utukufu muhimu kufungua mlango kuelekea maisha ya milele. Adamu alionesha busara yake kwa kufanya vilevile. Na ndivyo Hawa na ‘Adamu alianguka ili wanadamu wawe’ (2 Ne. 2:25).

“Baadhi ya Wakristo wanamshutumu Hawa kwa kitendo chake, wakimalizia kwamba yeye na mabinti zake wana mapungufu kwa ajili hiyo. Si Watakatifu wa Siku za Mwisho! Tukijulishwa na ufunuo, tunashangilia kitendo cha Hawa na kuheshimu busara yake na ujasiri katika tukio kubwa lililoitwa Anguko. …

“Ufunuo wa kisasa unaonesha kwamba wazazi wetu wa kwanza walielewa umuhimu wa Anguko. Adamu alitangaza, ‘Na libarikiwe jina la Mungu, kwani kwa sababu ya uvunjaji wangu wa sheria macho yangu yamefunguliwa, na katika maisha haya nitakuwa na shangwe, na tena katika mwili nitamwona Mungu’ (Musa 5:10)” (“The Great Plan of Happiness,” Ensign, Nov.1993, 72–73).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Waendee wale ambao hawahudhurii. Kufundisha ni zaidi ya kuongoza majadiliano siku ya Jumapili; inahusisha kuhudumia kwa upendo na kuwabariki wengine kwa injili. Huenda unaweza kumfikiria mtu fulani ambaye hahudhurii na kumpa mwaliko maalumu kushiriki katika somo lijalo. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 8–9.)

Chapisha